Jinsi ya Kuwekeza Katika Mikopo ya Sarafu za Kidijitali Kwa kutumia CoinLoan

Tafsiri:
de_DEsw

CoinLoan ni kampuni ya mikopo ambayo husaidia wamiliki wa sarafu za kidijitali kupata mikopo bila kuathiri thamani ya sarafu zao. Kwa kufanya hivi, wawekezaji hupata fedha wanazohitaji papo kwa papo na bado kusalia na sarafu zao wakiwa na matumaini kuwa bei itaongezeka. Nunua na Hifadhi ni mojawapo ya mikakati tanzu ya uwekezaji katika soko la crypto. Kampuni hii pia huwasaidia wakopeshaji kutoa mikopo kwa wakopaji duniani kote. CoinLoan imepokea zaidi ya dola milioni 3.1 katika ufadhili wa miradi ya uwekezaji.

Tutaangazia jinsi ya kuwekeza katika CoinLoan na mambo mengineyo unayohitajika kujua.

Sababu za Kuanzishwa kwa CoinLoan

Mikopo miongoni mwa wenza (peer to peer) imeshuhudia ukuaji mkubwa katika miaka michache iliyopita. Kufikia sasa, kampuni kama Lending Club ina thamani zaidi ya $ bilioni 1.4. Imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 40 na ina zaidi ya wawekezaji laki moja. Kampuni nyingine, Prosper, nayo ina thamani ya zaidi ya dola nusu bilioni.

Kampuni za jadi (asilia) za mikopo kama vile Lending Club zimekabiliwa na changamoto kadhaa. Kwanza, ni kujizuilia kwao kwa sehemu moja ndogo ya kijiografia. Kutokana na mifumo yao ya kifedha, kampuni hizi huwa na zimekabwa kwa ajili ya kujitanua. Pili, shughuli zake zimejikita kwa msingi wa uaminifu. Fedha hutolewa kwa wakopaji bila kuambatana na dhamana yoyote. Hali hii huibua uwezekano wa watu wendi kushindwa kulipa madeni.

Hapa ndipo kampuni za mikopo kama CoinLoan zinapoafiki. Kampuni kama hii huazimia kuondoa vikwazo ambavyo Lending Club na Prosper hukumbwa navyo kwa njia kadhaa. Ni kampuni ya kimataifa inayowezesha mtu yeyote kutoa mikopo na kukopa fedha. Pia, fedha zote zilizokopwa zinawekewa dhamana na crypto, ambayo inaweza kubadilishiwa fedha iwapo waliokopa watashindwa kulipia.

Jinsi ya Kuwekeza Katika CoinLoan

Investing in CoinLoan
Kuwekeza katika CoinLoan.

Kama mkopeshaji, unahitajika kujiunga kwa kufungua akaunti bila malipo kwa kutembelea tovuti yao. Utahitajika kutumia anwani ya barua pepe na maelezo mengineyo ya kibinafsi kufungua akaunti yako. kampuni itaweza kuthibitisha maelezo yako ya kibinafsi na mahali pako pa makazi ili kuweza kuzingatia sheria.

Kisha, itakupasa kuweka pesa kwenye ulingo huo wa kifedha. Unaweza kutumia kadi ya benki au kutumia njia ya uhamisho kwa benki ili kuhamisha fedha hizo. Unaweza pia kuweka amana ya sarafu za kidijitali ukitumia mkoba wako uupendao.

Baadaye, unahitaji kutambulisha hali mwafaka ya mkopo. Hapa, utaweza kujijengea akiba ya mikopo yako, masharti utakayo, mipaka ya viwango vya mkopo, na viwango vya riba. Hatimaye, unapaswa kuwasilisha ombi la kutoa mkopo. Unaweza kufanya hivyo kwa kusakura wakopeshaji tofauti na kukubali maombi ya mikopo.

Baada ya kuwekeza, waliopata mikopo wataanza kulipia fedha kwa awamu kulingana na kigezo chako cha masharti.

Jinsi ya Kukopa Kutumia CoinLoan

Borrow using CoinLoan
Kukopa kwa kutumia CoinLoan.

Kukopa kwa kutumia CoinLoan ni rahisi sana. Kama ilivyo kwa ajili ya mikopo, unahitaji kufungua akaunti yako bila malipo. Unahitaji tu anwani ya barua pepe au nambari ya simu kufungua akaunti. Baada ya hayo, unahitaji kuweka amana ya sarafu za kidijitali ukitumia mkoba wako uupendao. Hatimaye, unaweza kuomba mkopo kutoka kwa wakopeshaji wa kimataifa na kuipata haraka iwezekanavyo. Inachukua chini ya siku ili mkopo wako uweze kuchunguzwa. Tofauti na mifumo mingine ya ukopeshaji, hutahitajika kukaguliwa kwa misingi ya mikopo yako ya awali.

Kiasi cha chini unachoweza kukopa ni dola 100. Hakuna kiwango cha juu unachoweza kukopa. Muda wa chini sana unaoweza kulipia mkopo ni siku saba, wakati upeo mrefu ni miezi 36. Pia, hakuna riba inayoamuliwa kabla. Viwango hivi vimewekwa na kukubaliana baina ya wakopeshaji na wakopaji.

Faida za Kuwekeza katika CoinLoan

Kuna faida kadhaa unazopata kwa kuwekeza katika CoinLoans:

  • Mikopo huwekewa dhamana kwa kutumia sarafu imara za kidijitali.
  • Kampuni hizi huwa zimewekeza katika teknolojia ya uhafidhi ili kukuhakishia usalama.
  • Mikopo kuvutia viwango vya juu vya riba.
  • Upatikanaji wa wakopaji wengi wa kimataifa.

Hatari ya Kuwekeza katika CoinLoan

Faida kuu ya kuwekeza katika CoinLoan ni kwamba mikopo huwekewa dhamana kwa kutumia sarafu imara za kidijitali. Hata hivyo, kuna hatari kadhaa ambazo hutokana na kuwekeza katika mifumo hii:

  • Utete katika sekta hiyo. Sarafu za kidijitali ni bidhaa tete sana kwani bei hubadilika mara kwa mara. Kuna uwezekano kuwa thamani ya dhamana inaweza kupungua kwa kiasi kikubwa.
  • Hatari ya mfumo wa mawasiliano. CoinLoan ni kampuni ya kidijitali. Hii ina maana kwamba kuna uwezekano wa mfumo wa mfumo huo kuathirika.
  • Hatari ya kutokuwepo kwa pesa tasilimu. Kuna changamaoto ya kutokuwepo kwa pesa tasilimu, ambayo inafanya kuwa vigumu kujiondoa kwa baadhi miradi iliyowekezwa. Hii ni kwa sababu hakuna soko mbadala.
  • Hatari ya Kampuni. CoinLoan inapata ushindani mkubwa. Kuna uwezekano kwamba kampuni hii haitaweza kudumu.

Nchi CoinLoan Inakubali Wakopaji na Wakopeshaji

CoinLoan inapatikana duniani kote. Wakopaji na wakopeshaji wanaweza kushiriki bila kujali wanaishi wapi.

Muhtasari

CoinLoan ni mojawapo ya kampuni nyingi zinatotoa mikopo baina ya wenza. Pia, ni moja ya kampuni kadhaa ambazo zinazouunganisha ulimwengu wa fedha za kidijitali. Kampuni nyinginezo zinazotoa huduma kama hiyo ni OkEx na Nexo. Kwa kutumia ulingo kama huu ni jambo zuri kwani unaweza kuimarisha vyanzo mbalimbali vya mapato yako. Hata hivyo, unapaswa kuhakikisha kiwano kikuba cha fedha zako zipo katika fedha zilizofaharisishwa (index funds), dhahabu, Bitcoin na hisa.