Kutafsiri Ebola

FiFi ni tovuti ya masuala ya fedha. Lengo letu ni kuboresha maarifa ya fedha ili fedha zimsaidie kila mtu. Tovuti yetu ni ya lugha mbalimbali na inalenga ulimwengu mzima. Tunaamini kwa dhati uwezo wa Africa na Amerika ya Kusini. Lengo letu linajumuisha FiFi kwa Kiswahili, ambayo huenda ndio tovuti ya kwanza maalum kwa masula ya fedha.

Madaktari wakimtibu mgonjwa wa Ebola.

Ebola ni ugonjwa hatari sana ambao umeua watu wengi Afrika. Kutokuwepo kwa taarifa na pia habari za uongo mtupu kuhusu ugonjwa huu ni tatizo kubwa. Tunataka kutatua tatizo kama hili kwa kutafsiri habari bora na sahihi kwa lugha ya Kiswahili na baadaye lugha nyingine za Afrika.

Kwanini

Mwaka 2005 Kasper alianzisha juhudu za kuandika Wikipedia kwa lugha za Afrika Magharibi (hasa Bambara na Peul). Ilikuwa ni kazi ngumu lakini inayowezekana. Kulipa watu dola 1 ya Marekani kwa makala moja ya Wikipedia ilikuwa ndio njia yenye ufanisi. Leo hii mwaka 2019 Wikipedia hizi bado zipo. Hata hivyo, zinakuwa polepole. Wikipedia ya Kiswahili ni kubwa zaidi, lakini hata kwenye Wikipedia hiyo, makala muhimu kama Ebola ina mambo ya msingi tu.
Mwaka 2019, Kasper alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa FiFi, tovuti ya lugha mbalimbali ya masuala ya fedha na kwa asili alitaka pia kuwa na FiFi kwa lugha za Afrika. Na kama mfumo wa Google wa kuwapa wafanyakazi wake muda asilimia 20 kujihusisha na miradi yao binafsi, FiFi inawapa waajiriwa wake uhuru wa kuboresha Wikipedia za lugha za Afrika kama moja ya kazi zao kwa Fifi.

Tunaweka juhudi kwenye FiFi Afrika na lugha za Afrika kwasababu tunaamini uwezo wa Afrika kwa muda mrefu. Tunaamini pia kuwa upatikanaji wa habari kwa lugha za Afrika utakuwa na wajibu wa kuiendeleza Afrika. Hatutarajii mradi wetu wa Afrika utakuwa na faida peke yake.

Tunataka kujenga nguvu kazi kubwa katika nchi mbalimbali za Afrika ili kuandika habari kwa lugha za Afrika na pia lugha za kikoloni kama Kiingereza na Kifaransa. Tunataka pia kuhamasisha ujasiriamali, hasa mtandaoni.

Kwahiyo, kuboresha Wikipedia kwa lugha za Afrika ni moja ya malengo ya FiFi.

Jinsi Gani

Tafsiri Makala ya Ebola ya Kiingereza Kwa Kiswahili

  • Kupitia Twitter tumepata watu wengi ambao wako tayari kutafsiri makala ya Ebola toka Wikipedia ya Kiingereza.
  • Tutawatumia sehemu za makala hii wazitafsiri.
  • Ndesanjo atazichambua, kama ni nzuri basi tutaziweka kwenye Wikipedia ya Kiswahili.

Tutaajiri watafsiri watakaofanya kazi nasi kwa muda mrefu.

Rekodi Maka ya Kiswahili

Baada ya makala za Kiingereza kutafsiriwa, tutatumia Twitter kutafuta watu wenye ujuzi wa kurekodi sauti ili wasome makala hizi.

Kusambaza Rekodi Kwenye Vituo vya Redio

Redio bado ni chombo muhimu sana cha kusambaza habari muhimu barani Afrika.

Tutaandaa orodha ya vituo vya redio vya Kiswahili na kuwatumia makala zilizorekodiwa.

Nani

  • Kasper aliishi Mali mwaka 2005 na anazumzumza Bambara. Ni mmoja wa waanzilishi wa FiFi Finance.
  • Ndesanjo anafanya kazi FiFi, Kiswahili ni lugha yake ya asili na ni mmoja wa wakabidhi wa Wikipedia ya Kiswahili walioisaidi kufikisha makala 1,000. Hadi September 2019, Wikipedia ya Kiswahili ina makala 54,000. Ndio Wikipedia kubwa Afrika ya lugha za Niger–Congo au Nilo-Sahara.