Mkataba wa Biashara Huru Katika Bara la Afrika: Faida na Changamoto

Mkataba wa Biashara Huru Katika Bara la Afrika (AfCFTA) ni makubaliano ya kibiashara ambayo yanazingatiwa miongoni mwa nchi 27 za Jumuiya ya Afrika. Ulitiwa sahihi jijini Kigali, Rwanda manmo tarehe 21 Machi 2018.

Ramani ikionyesha nchi zilizotia sahihi ya mkataba huu.
» Kufikia Julai 7, 2019, mataifa 27 yametia sahihi makubaliano hayo. Kuidhinishwa kwa mwafaka huu, mataifa 22 ilihitajika ili AfCFTA liweze kufanikiwa.
» Utendaji wa biashara chini ya AfCFTA utaanza Julai 1, 2020.
» Taifa la Ghana ndipo makao makuu ya AfCFTA barani Afrika.
» ulai 7 itaadhimishwa rasmi kama Siku ya Ushirikiano wa Afrika katika kumbukumbu ya uzinduzi wa kihistoria wa utekelezaji wa AfCFTA.

Makubaliano hayo yamekusudiwa kuhusisha soko la watu bilioni 1.2 katika mataifa 55 zenye mazao ya ndani (GDP) ya jumla ya $2 trilioni. Ikiwa itatekelezwa kikamilifu, itafanya Afrika kuwa eneo kubwa la biashara ya huru ulimwenguni. Licha ya hayo inaaminika kuwa makubaliano hayo yataleta faida kadhaa za kiuchumi na kijamii kwa bara la Afrika na wakaji wake.

Zifuatazo ni faida na changamoto ambazo zinatarajiwa iwapo biashara chini ya makubaliano haya itaanza mnano Julai 1, 2020.

Faida

Mseto wa Biasahara

Asilimia 85 ya bidhaa zinazokwenda nje toka Zambia ni shaba.

Makubaliano hayo yanalenga kukabadilisha mauzo ya nje ya nchi, kupunguza utegemezi kwenye tasnia ya ziada kwa bidhaa na huduma zilizoongezwa thamani. Kati ya 1990 na 2014, mataifa yaliyoendelea yalifanya uchumi wao kuwa mseto wakati nchi nyingi za Kiafrika zilitegemea sekta ya mali asili kama vile madini, mafuta, n.k. Mafuta iliwakilisha zaidi ya nusu ya usafirishaji wa bidhaa Afrika kwa nchi zisizo za Kiafrika kutoka 2010 hadi 2015, wakati bidhaa za viwandani zilikuwa asilimia 18 tu ya mauzo kwenda kwa ulimwengu wote.

Vera Songwe, katibu mkuu wa Tume ya Uchumi ya Afrika, anaamini kwamba AfCFTA itahimiza mseto wa biashara kwa sababu mauzo ya nje ambayo yatapata faida zaidi ni yale yenye kuhitaji nguvu kazi nyingi kama utengenezaji na usindikaji wa mazao ya kilimo, badala ya biashara ya mafuta na madini inayohitaji rasilimali nyingi.

Mbali na mseto wa bidhaa na huduma, AfCFTA itaruhusu biashara, hususan biashara ndogo na za kati kuwa na fikio mbalimbali ndani ya bara la Afrika. Hii itawezesha biashara ndogo na za kati kuingia katika masoko mapya na kupanua wigo wao wa wateja.

Ufunguaji wa Mipaka

Ufunguaji wa mipaka kupitia AfCFTA unatarajiwa kuongeza fursa za ajira kwa vijana wa Afrika na akina mama ambao hujumuisha asilimia 70 ya biashara ndogo ndogo mipakani.

Licha ya hayo, soko moja la Kiafrika litatoa suluhisho kwa mojawapo ya vizuizi vikubwa zaidi ambalo likabili bara la Afrika: uhamaji wa kitaalamu na uwezo wa kutumia ujuzi katika nchi mbalimbali. Wahamiaji wengi wa Kiafrika huchagua kukaa barani Afrika na 70% ya wahamiaji wa Kusini mwa Jangwa la Sahara huzunguka ndani ya Afrika.

Kugharimu visa na vigezo vya kustahiki ni moja ya vizuizi vikuu kwa uhamaji barani Afrika. Nchini Nigeria, kwa mfano, vigezo vya kustahiki visa kwa mfanyakazi mwenye ujuzi huzingatiwa kuwa na mahitaji mengi sana, kuzingatia viwango rasmi ya elimu badala ya uzoefu uliopatikana kupitia kazi.

Mseto wa kazi utaimarishwa na mipango mingine ya Bara kama Itifaki ya Huru wa Watu Kusafiri na Haki ya Makazi.

Asilimia 70 ya wahamiaji wa Kusini mwa Jangwa la Sahara huzunguka ndani ya Afrika.

Biashara Ndani ya Kikanda

AfCFTA itafungua uwezo wa kiuchumi wa Afrika kwa kuongeza biashara ndani ya kikanda. Biashara ndani ya kikanda ya Kiafrika ilichangia asilimia 17 tu ya mauzo ya nje mnamo 2017 dhidi ya 59% huko Asia na 69% huko Uropa. Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa ya Afrika inakadiria kuwa utekelezaji wa makubaliano hayo yanaweza kuongeza biashara ya ndani na Afrika kwa asilimia 52 ifikapo 2022.

Ukoloni ulileta hali ambayo majirani waliacha kufanya biashara miongoni mwao. Njia kuu ya biashara ilikuwa kati ya nchi za Kiafrika na nchi za Ulaya na kati ya nchi za Kiafrika na Amerika. – anasema David Luke, mratibu wa Kituo cha Sera ya Biashara ya Afrika.

Kuondolewa Kwa Ushuru

Mojawapo ya sehemu muhimu ya makubaliano ni upunguzaji wa ushuru wa bidhaa za kuuza nje ya nchi. Wanachama wataondoa ushuru kwa bidhaa nyingi, ambayo itaongeza biashara katika kanda kati ya asilimia 15-25 kwa muda wa kati.

Idadi kubwa ya wanachama watafaidika kutokana na kupunguzwa kwa ushuru kutoka asilimia 90 katika kipindi cha miaka mitano. Tarehe ya mwisho ya kupunguzwa ni miaka kumi kwa nchi zilizoorodheshwa kama “Nchi Zilizoendelea Kwa Kiwango cha Chini” na Umoja wa Mataifa. Nchi zingine kama Msumbiji, Niger na Malawi, zilipata nyongeza ya miaka 15.

Kuondolewa kwa ushuru kunatarajiwa kuongeza biashara ndogo na za kati, ambazo zina jumuisha zaidi ya asilimia 80 ya ajira Afrika na asilimia 50 ya Pato la Taifa.

Kwa kuongezea, makubaliano hayo pia yataondoa vizuizi vingine visivyo vya ushuru kwa biashara kama vile upendeleo wa kuingiza bidhaa nchini, kucheleweshwa kwa forodha kwa muda mrefu kwenye mipaka na ruzuku.

Biashara ndogo na za kati hujumuisha asilimia 80 ya ajira Afrika na asilimia 50 ya Pato la Taifa.

Kupunguza Gharama ya Uekezaji

Mchakato wa kuagiza malighafi kutoka nchi zingine utarahisishwa. Biashara ndogo na za kati zitaweza kuanzisha vitengo vya uzalishaji katika nchi zingine za Afrika ili kupata njia za uzalishaji wa bei rahisi.

Viwango Vilivyoboreshwa na Viwango Mwafaka

AfCFTA limetambua ubora na kufuata mitindo mwafaka kama jambo la msingi katika biashara. Hii itahusisha viwango vinavyohusu afya, usalama, na mazingira, na kuhakikisha viwango vya ubora katika bara la Afrika.

Changamoto

Kuna changamoto ngumu zilizo mbele ambazo zinahitaji kushughulikiwa kwa bara la Afrika ili kupata faida zilizoainishwa hapo juu. Zifuatazo ni changamoto kadhaa zinazotarajiwa.

Hatuna nguvu ya umeme; watengenezaji wetu bado wanajitahidi kunawiri. Kampuni zitaenda kwa mazingira salama zaidi ambapo gharama ya uzalishaji itakuwa rahisi kutengeneza na kuileta katika soko kubwa la Nigeria kuuza bila malipo. Tutapoteza kazi nyingi. – Mwandishi wa Nigeria, Umeh Chidozie akiandika kwenye ukurasa wa Facebook wa DW Africa.

Kutofautiana Kwa Maendeleo

Afrika Kusini ndio kati ya uchumi mkubwa Afrika.

Viwango vya maendeleo kwenye bara hutofautiana sana. Mfano, zaidi ya asilimia 50 ya pato la bara la Afrika linachangiwa na Misri, Nigeria na Afrika Kusini, wakati mataifa sita ya visiwa vya Afrika kwa pamoja huchangia 1% tu.

Mashindano mMiongoni mwa Jamii za Biashara

Hivi sasa, Afrika ina jamii 8 za biashara zinazoshindana. Kulingana na ripoti ya Tume ya Uchumi kwa Afrika, kizuizi muhimu cha kujumuika barani Afrika kimekuwa ni wingi wa jamii za kiuchumi za kikanda zinazochangiana wanachama na hivyo kusababisha kurudiwa kwa juhudi na upotezaji wa rasilimali ndogo barani Afrika. Kati ya nchi 53 za Kusini mwa Jangwa la Sahara, ni 6 tu ambao ni wanachama wa jamii moja ya kiuchumi, 26 ni wanachama wa jamii zaidi ya moja na 20 ni wanachama wa angalau jamii tatu.

Kwa hivyo, jamii chache za kikanda zingepunguza gharama za kiutawala na kutoa pesa za kuboresha shughuli za kila siku na kukimu miradi.

Msuko Huru wa Kazi

Wakfu ya Mo Ibrahim inabainisha kuwa kuna mfumo mdogo au dhaifu wa kutambuliwa na utangamano wa ujuzi, miundo ya masomo na uzoefu katika ya nchi na nchi. Hii inazuia uwezo wa wahamiaji kuingia na kushiriki kikamilifu katika masoko ya bara.

Sheria za Asili
Jammie de Melo anasisitiza kuwa biashara ya huru itahitaji pia kuoanisha sheria za asili (vigezo vinavyohitajika kuamua bidhaa linatoka taifa gani) katika kiwango cha bara kwani nchi nyingi bado zinadumisha sera mbalimbali za biashara na washirika wa kigeni.

Kuongezeka Kwa Mkazo wa Ushindani

Uchumi mdogo katika bara la Afrika utakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa uchumi ulioendelea katika bara la Afrika. Kwa mfano, nchi za Kiafrika ambazo zinategemea kilimo cha kiwango cha chini hazitaweza kushindana na biashara kubwa za kilimo katika nchi zenye mapato makubwa barani Afrika kama Afrika Kusini, Kenya, Ethiopia, Misri na Nigeria.

Kuharibiwa Kwa Mazingira

Ushindani mgumu unaweza kusababisha kampuni zingine kupuuza mazingira kuweza kushindana. Biashara nnyingi ndogo na za kati zina uwezekano wa kupunguza gharama, pamoja na zile zinazohusiana na utengenezaji na utupaji sahihi wa taka.

Hitimisho

Ukiangalia makubaliano ya zamani ya bara la Afrika, mafanikio ya AfCFTA yatategemea neema za kisiasa, kujitolea kwa dhati na utekelezaji mzuri. Shida za kawaida za kijamii, kisiasa na kiuchumi kwenye bara la Afrika kama vile ufisadi, migogoro, na utawala duni zinahitaji kushughulikiwa haraka ili faida ya AfCFTA ihimizwe.