Ni Wapi Unaweza Kutumia Bitcoin Barani Africa?

Tafsiri:
en_USsw

Matumizi ya Bitcoin yanaendelea kukua kwa taratibu barani Afrika. Je ni wapi watumiaji wa Bitcoin Waafrika au wasafiri wa nje wanaweza kutumia Bitcoin?

Katika makala hii, FiFi inatazama biashara zinazokubali matumizi ya Bitcoin Afrika.

Ni Wapi Unaweza Kutumia Bitcoin Afrika?

Mahali Usipotarajia

Mgahawa wa Nyama Choma

Betty’s Place ni mgahawa unaomilikiwa na Betty Wambugu, ulioko Nyeri, mji ulioko Kenya vijijini. Anauza chakula maarufu Afrika Mashariki, nyama choma. Anakubali malipo ya Bitcoin.

Stan Williams, the Sculptor

Stan Williams ni mchonga vinyago wa Zimbabwe anayekubali malipo ya Bitcoin toka kwa wanunuzi wa vinyago vyake.

Kenya

Mamamikes

Mamamikes ni duka la zawadi la rejareja na biashara ya mtandaoni.

Healthland Spa

Healthland Spa ni sehemu ya kuimarisha afya na uzuri iliyoko jijini Nairobi.

Boxlight Electronics

Boxlight Electronics ni duka la jumla na rejareja linalojihusisha na bidhaaa za elektroniki.

Nigeria

Sungrowmall

Sungroowmall ni duka la mtandaoni ambapo unaweza kununua bidhaa kwa kutumia Bitcoin.

Minku

Minku ni duka linalouza bidhaa za ngozi na nguo mtandaoni.

South Africa

White Dog Taproom

White Dog Taproom ni mgahawa na uwanja wa kucheza gofu.

Bidorbuy

Bidorbuy ni soko la mnada mtandaoni.

Fines4U

Fines4U ni kampuni ya usimamizi wa faini za makosa ya barabarani. Toka mwaka 2017, kampuni hii imekuwa ikipokea malipo ya Bitcoin kwa wateja wao.

Ashworth Africa

Ashworth Africa ni kampuni ya utalii ya Afrika Kusini.

TakeAlot

TakeAlot ni duka la rejareja la mtandaoni.

Duka kubwa la rejareja la Afrika Kusini, Pick n Pay, lilifanya jaribio fupi ya malipo ya Bitcoin mwaka 2017.

Cape Coffee beans

Cape coffee beans ni duka la mtandaoni linalouza kahawa iliyochomwa.

Bankymoon

Bankymoon ni kampuni iliyoanzisha mfumo wa kununua umeme kwa kutumia Bitcoin.

Red & Yellow Creative School of Business

Red & Yellow Creative School of Business ni chuo cha biashara ambacho kinakubali malipo ya ada ya Bitcoin.

Sapphire Corporate Solutions

This South African company ni kampuni inayotoa huduma mbalimbali ikiwemo sare za kazini.

Nigeria iliongoza duniani kwa utafutaji wa neno Bitcoin kwenye Google Trends tarehe 12 August, 2019.

Hitimisho

Kukubalika kwa Bitcoin kunaonyesha kuwa fedha za "crypto" zitaendelea kuwepo na matumizi yake kuongezeka. Kwa mfano, kwa mujibu wa the Blockchain Association of Kenya, jumla ya transaction za Bitcoin nchini Kenya mwaka 2018 ni zaidi ya dola za Kimarekani milioni 1.5. Kenya ni nchi ya 25 duniani kwenye soko la Bitcoin ikiwa nyuma ya Nigeria na Afrika Kusini.

Soma zaidi