Jinsi Ya Kujipatia Pesa Kupitia ‘Affiliate Marketing’

Tafsiri:
amen_USes_ESnl_NL

Je, unaweza kupata pesa kupitia uuzaji wa kushirikishwa (affiliate marketing kwa Kiswahili)? Uuzaji wa ushirikishi ni mojawapo ya biashara online unayoweza kutumia kujipatia pesa hasa kama wewe ni mwanablogu au unamiliki tovuti. Unapotafiti kuhusu mada hii, utapata watu wengi wenye vidokezo na miongozi kuhusu jinsi inavyofanya kazi. Utawaona pia baadhi ya ‘mamilionea’ wakizungumzia jinsi walivyojipatia utajiri wao kama washirika. Licha ya kuifanya shughuli hii kuonekana rahisi, ukweli ni kwamba si rahisi hivyo! Makala haya yatakuelezea jinsi ya kufanya biashara online kupitia uuzaji kwa ushirikishi (affiliate marketing).

Ilani kuhusu Kujipatia Pesa Kupitia ‘Affiliate Marketing’

Kabla ya kukuelezea jinsi unaweza kuanza, hapa ni tahadhari chache ambazo unahitaji kujua.

  • Uuzaji kwa ushirikishi si mpango wa kujiharakishia utajiri.
  • Inaweza kukuchukua muda mrefu kabla ya kuanza kupata pesa kupitia uuzaji kwa ushirikishi
  • Inaweza kuchukua kiasi kikubwa cha rasilimali kama vile muda au pesa kabla uanze kuchuma kutokana na uuzaji kwa ushirikishi
  • Watu wengi ambao wanaanza katika shuguli za masoko ya ushirikishi hushindwa. Ili kufanikiwa, kidokezo muhimu ni kujikakamua na kuwa mbunifu.

‘Affiliate Marketing’ ni nini?

Kampuni zina mbinu tofauti za kutambulisha na kuuza bidhaa zao mtandaoni. Kwanza, wanaweza kutumia matangazo kupitiaa kampuni kama Google, Twitter, na Facebook. Vinginevyo, wanaweza kushirikiana na wamiliki wa tovuti na ‘influencers’ ili kujipatia wateja. Wamiliki wa tovuti hawa wanaweza kulipwa kiasi fulani maalum au wanaweza kupata kiwango fulani cha malipo kutokana na mauzo ya bidhaa. Kwahiyo, faida ya affiliate marketing ni gawio (commission) unayopata toka kwa kampuni unazotangaza biashara zao. Huu ndio mkakati unaojulikana kama Affiliate Marketing (Uuzaji wa kushirikishwa).

Affiliate Marketing Tanzania

  • Kampuni unazoweza kupata pesa kwa kutangaza biashara zao kwenye blogu yako au tovuti yako ni pamoja na Kariakoo Mart, Travelstart, n.k. Unaweza pia kujiunga na mitandao ya affiliate marketing (affiliate networks) kama hii iliyoorodheshwa hapa.

Zifuatazo ndizo hatua unazohitaji kufuata ili kujipatia pesa kupitia ‘affiliate marketing’.

Jenga mwonekano wa mtandaoni

Jambo la kwanza unalohitaji kufanya kujipatia pesa kupitia affiliate marketing ni kujijengea uwepo wako wa mtandaoni. Kuna njia mbili kuu unazoweza kufanya hivyo:

  • Unaweza kuunda tovuti yako ya kibinafsi ambapo utakuwa unachapisha maudhui mbalimbali kama vile soka, muziki, elimu, siasa, sayansi, mitindo, teknolojia, n.k. Lengo ni kujijengea ufuasi mkubwa. Unaweza kutangaza tovuti yako kupitia mitandao ya kijamii au kuweka mkakati wa Search Engine Optimization (SEO).
  • Unaweza pia kutumia mitandao ya kijamii kama vile Twitter, YouTube, Facebook, Snapchat, Instagram na Tiktok kama ‘influencer’ (mshawishi) katika taaluma yako. Sababu ya kujenga mwonekano huu ni kwa kuwa haiwezekani kufanikiwa kama muuzaji wa ushirikishi (affiliate marketer) mtandaoni ikiwa huna wafuasi.

Vidokezo vya kujenga tovuti ya kibinafsi ya kushirikiana

Ni vigumu sana kufanikiwa wakati wa kujijengea tovuti bora ya kushirikiana. Ili kufanikiwa, unahitaji kuhakikisha kwamba tovuti hiyo ni rahisi kwa watumiaji. Kwa hivyo, tunapendekeza kutumia majukwaa ya kawaida kama vile SquareSpace na WordPress. Majukwaa haya yatahakikisha kwamba tovuti yako ni rahisi kwa watumiaji.

Tovuti hii pia inahitaji kuwa imeandaliwa ifaavyo kwa ajili iweze kupatikana kwa urahisi katika injini za utafutaji (search engines) kama Google. Kufanikiwa katika hili, unahitaji kutumia mbinu iitwayo SEO (Search Engine Optimization). Tovuti ambayo imeboreshwa vizuri kwa ajili ya injini za utafutaji ni rahisi kupatikana na itakuokoa pesa nyingi katika mauzo. Mkakati mzuri wa SEO pia utakupa mamlaka katika kitengo/eneo unalolenga.

Search Engine Optimization (SEO) nzuri

SEO nzuri haimaanishi tu kwamba robots za utafutaji kama za Google au Yahoo zina uwezo wa kuchambua mada zako kwa urahisi, ila pia ina maana kwamba unajua jinsi ya kuwapa wasomaji wake kile wanachokitaka. Jambo la muhimu ni: fahamu nini wageni wa tovuti yako wanatafuta na uhakikishe kuwa wanaweza kupata kile wanachotafuta kupitia kwako. Unapowatumikia wageni wako vizuri, ‘search rankings’ yako itaimarisha kwa sababu injini za utafutaji huangazia jinsi wasomaji wanavyofurahia maudhui yako.

Licha ya kuwa inawezekana kujichumia pesa kwa kuuza bidhaa za kiteknolojia kama vile simu za mkononi, nafasi za kufanikiwa ni nadra sana. Hii ni kwa sababu bidhaa hizi tayari zina washawishi (influencers) wa kuaminika ambao huuza bidhaa hizi kwa niaba ya kampuni hizi. Badala yake, unaweza kuzingatia nyanja ndogo kama vile visu vya jikoni au hata bidhaa za mitindo na mapambo. Unapojijengea umaarufu wako katika nyanja hizi, utavutia idadi ndogo ya wateja, ambao wataishia kununua zaidi.

Vidokezo vya kuwa mshawishi (Influencer)

Ikiwa unapenda mambo ya kiteknolojia, huenda umetazama video za Linus Tech Tips, MKBHD, na Unbox Therapy. WanaYouTube hawa wana mamilioni ya wafuasi na hujipatia mamilioni ya dola kila mwaka kutokana na mapato ya YouTube. Pia, wanashirikiana na mashirika mengine ili kuwauzia bidhaa zao. Baadhi ya bidhaa za simu kama OnePlus zimeongeza mauzo kutokana na ushawishi wa washawishi hawa. Wewe pia unaweza kuwa mwenye mvuto katika nyanja yako. Ili kufanya hivyo, fuata vidokezo vifuatavyo:

  • Unda video bora zinazoongeza thamani kwa watazamaji.
  • Wekeza katika vifaa bora za video na sauti.
  • Kuwa na uthabiti. Hakikisha kwamba unapakia video angalau mara moja kwa wiki.
  • Wakumbushe watazamaji wako wakufuate kwenye mitandao ya kijamii uliyoko.
  • Waulize YouTubers wengine maarufu ili wazungumzie au kutaja video zako na mada unazoshughulikia.

Nini kinachofuata?

Baada ya kujua jinsi ya kuwa affiliate na kujijenga kama ‘brand’, ili uweze kujipatia pesa kupitia ‘affiliate marketing’, sasa unahitaji kutafuta kampuni ambazo hulipa kupitia masoko ya washirika. Njia rahisi ya kuanza ni kutumia mipango ya washirika (affiliate programs) ya kampuni za kimataifa kama Amazon, 24Monetize au affiliate Tanzania (affiliate marketing in Tanzania) kama Travelstart Tanzania, Kariakoo Mart, na nyingine zilizoorodheshwa hapa.

Kuna kampuni nyingi ambazo hutoa mipango ya washirika. Mbali na kampuni kubwa kuwa na mipango yao ya washirika moja kwa moja, unaweza pia kupata majukwaa mengineyo ya washirika ambayo yanafanya kazi kwa niaba ya kampuni mbalimbali. Katika majukwaa haya unaweza kupata maelfu ya kampuni, kubwa na ndogo. Una uhuru wa kutuma maombi kwenye programu yoyote na kuuza bidhaa hizo.

Njia nyingine ni kuwasiliana mwenyewe na wenye bidhaa katika sekta yako. Kupitia njia hii unapaswa kuwasiliana na meneja wa mauzo wa kampuni unayolenga kufanya kazi nayo na kuwawasilishia blogu yako au akaunti zako za mitandao ya kijamii kama jukwaa lao la mauzo.

Hitimisho Kuhusu ‘Affiliate Marketing’

Masoko ya Washirika yanakupa fursa ya kuvutia ya kukuza biashara yako. Ni mojawapo ya njia bora mbadala za kujichumia pesa. Hata hivyo, kama tulivyoelezea, kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio ni safari. Safari ambayo itachukua miezi au hata miaka ili ufanikiwe. Ikiwa utaweka jitihada za kutosha, utakuwa umejiweka katika nafasi nzuri ya kujipatia pesa hatimaye.