Jinsi ya Kuwekeza Kwa Dhamana za Serikali Nchini Tanzania

Tafsiri:
en_US

Uwekezaji kwenye dhamana za serkali nchini Tanzania ni aina ya mikopo, kama vile dhamana ambayo hutolewa kwa kitega uchumi ambacho huambatana na ahadi ya maandishi ya kumlipa mwekezaji kwa muda maalum.

Mikopo hii hutolewa na serkali kwa kubadilishana na fedha zilizokopwa kwa umma. Mwekezaji atajipatia riba pale uwekezaji unapofikia hatua ya malipo.

Serkali ya Tanzania ina mikopo ya dhamana ya aina mbili, hati dhamana (T-Bonds) na hati fungani (T-Bills). Hati dhamana ni mikopo ya muda mrefu ambayo hutoa faida baada ya mwaka mmoja, wakati hati fungani hutoa faida chini ya mwaka mmoja.

hati fungani ni nini

Uwekezaji huu wenye dhamana ya serkali hutolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa niaba ya serkali. Hati dhamana ziko kwenye makundi matano yenye kupevuka miaka miwili, miaka mitano, miaka saba, miaka kumi na miaka kumi na tano. Hati fungani zinatolewa kwa makundi manne yenye kupevuka siku thelathini na tano, siku tisini na moja, siku mia moja themanini na mbili na siku mia tatu sitini na nne.

Mikopo yenye dhamana ya serkali nchini hufanywa kwenye masoko mawili, soko la awali na soko kuu. Mikopo hiyo kwanza huuzwa kwenye soko la awali Benki kuu ya Tanzania kupitia Mfumo Mkuu wa Uhifadhi au kwa Kiingereza Central Depository System (CDS) na kisha kuandikishwa kwenye Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE) kwa soko linalofuatia baada ya kununuliwa kwenye soko la awali. CDS ni mfumo unaodumisha na kuchakata miamala ya hati fungani na hati dhamana kupitia Mfumo wa Mikopo Yenye Dhamana ya Serkali au kwa Kiingereza Government Securities System (GSS).

Hati fungani hutolewa kwa mara ya kwanza kwa mtindo wa wiki mbili mbili na hati dhamana hutolewa kwa mtindo wa mwezi mmoja mmoja.

Faida za Mikopo Yenye Dhamana ya Serkali

Uwekezaji wenye dhamana ya serkali humpa mwekezaji faida kadhaa kama vile:

  • Hakuna hatari yoyote kwa vile inatolewa na serkali.

  • Uahamishika na unaruhusu mazungumo ya makubaliano.

  • Unaweza kuahidiwa kama dhamana ya mkopo kwa vile ni mikopo yenye hatari ndogo sana.

  • Kiwango cha rejesho kina ushindani.

  • Wawekezaji wanapatiwa uthibitisho wa kiwango cha rejesho lenye ushindani kwa punguzo la bei ya uwekezaji.

    dhamana za serikali
    Fomu ya maombi ya dhamana.

Inavyofanya Kazi

  • Inabidi mtu afungue akaunti ya mfumo mkuu wa uhifadhi wa uwekezaji wenye dhamana ya serkali kupitia benki kuu au kutoka kwa dalali yoyote ili kuwekeza kwenye mikopo hii ya serkali.

  • Picha tatu ndogo za pasipoti, nakala tatu za kitambulisho halali kinachotambulika na nakala tatu za namba ya usajili wa utambulisho wa biashara zinahitajika.

  • Mfumo mkuu wa uhifadhi ulioko benki kuu unadumisha na kuchakata uwekezaji wenye dhamana ya serkali.

Uwekezaji Wenye Dhamana ya Serkali Huuzwaje?

Mwekezaji atawekeza fedha ya kitega uchumi kwa dalali ampendaye. Dalali huyo atashiriki kwenye mnada wa Benki Kuu ya Tanzania kwa niaba ya mwekezaji huyo ili kununua hati dhmana kwenye soko la awali au DSE ili kunua hati dhamana kwenye soko kuu. Kiwango cha chini cha kuwekeza kwenye uwekezaji wenye dhamana ya serkali ni Shilingi milioni moja za Kitanzania kwa hati dhamana na shilingi laki tano kwa hati fungani.

Nani Aweza Kununua Hati Hizi za Serkali?

Watu waishio Afrika Mashariki, wanaruhusiwa kushiriki. Kufuatana na mabadiliko ya sheria ya masoko yaliyoorodheshwa ya mitaji ya nje ya mwaka 2014, mfanyabiashara ni mtu yeyote aliyeishi mfululizo miezi kumi na mbili na zaidi au ambaye haja yake kuu ya mwanzo ya kiuchumi ni Tanzania.

Wakazi wote wa Jumuia ya Afrika Mashariki pia wanaweza kushiriki. Hii ni kwa sababu mabadiliko ya udhibiti yanafafanua kuwa mwananchama wa eneo maalum ni mwanachama wa Afrika Mashariki. Lakini hata hivyo, kutokana na mabadiliko hayo ya udhibiti, mwananchama wa eneo maalum aweza kuwekeza kwenye uwekezaji wa dhamana ya serkali kama atakidhi vigezo vifuatavyo:

  • Jumla ya mapato yaliyopatikana kwenye uwekezaji wenye dhamana ya serkali kwa wakazi wa eneo maalum hayazidi asilimia arobaini ya fedha ya uwekezaji iliyotolewa.

  • Uwekezaji wenye dhamana ya serkali uliopatikana hautohamishwa kwenda kwa mkazi mwingine ndani ya kipindi cha miezi kumi na mbili ya tarehe ya kuanza kwa uwekezaji huo.

Jinsi Umma Unavyojulishwa Kuhusu Mnada

Taarifa kwa umma inatolewa siku tano kabla yam mnada kupitia magazeti na mtandao wa CDS.

Baada ya taarifa kutolewa, washiriki waliosajiliwa wa Uhifadhi Mkuu (CDPs), pamoja na wateja wao, wanahitajika kuomba kwa kutumia fomu za zabuni CDS/FORM/03 (Annex 1). Fomu hii yaweza kupatikana kutoka matawi ya Benki Kuu, tovuti ya Benki Kuu na kutoka ofisi za CDP.

Kima cha chini cha kiasi cha zabuni kwa hati fungani ni shilingi laki tano za Kitanzania huku thamani kamili ikiwa katika mafungu ya shilingi elfu kumi. Wazabuni wanaruhusiwa kuwasilisha maombi mengi ya zabuni kila pale faida inapopevuka sehemu mbali mbali. Benki kuu ya Tanzania ina haki ya kukubali au kukataa fomu yoyote ya uzabuni iliyowasilishwa kwa ajili ya mnada. Benki kuu inafanya kitarakilishi mnada ili kupanga fedha kwa wazabuni walioshinda. Kila mzabuni aliyeshinda, atalipa bei kadri alivyotamka.

hati fungani za serikali
Mfano wa taarifa kwa umma kuhusu mnada.

Kutangazwa Kwa Matokeo na Utoaji wa Misimbo ya Zabuni

Matokeo ya mnada yanapatikana kwenye tovuti ya Benki Kuu mara baada ya mnada. CDP pia huonesha matokeo kwenye ofisi zao. Wazabuni walioshinda wanahitaji kuchukua taarifa za matokeo ya zabuni (misimbo zabuni) kutoka kwa CDPs wao. Misimbo zabuni ni ya kutumika kama kielelezo cha malipo ya hati fungani kupitia mfumo wa mabenki nchini Tanzania au kwa Kiingereza Tanzania Inter-bank Settlement System (TISS).

Malipo ya Mzabuni Aliyeshinda

Wazabuni walioshinda watalipia hati fungani siku moja baada ya mnada kupitia benki zao za ukazi.

Malipo Kwa Mwekezaji (Ugombozi)

Kama mwekezaji, utapokea asilimia mia ya malipo ya deni ambayo yanajumuisha thamani ya gharama na kiasi cha riba.
Kipato kitokanacho na uwekezaji kinapswa kulipiwa kodi ya mapato yalipwayo na mlipaji ambapo kodi hiyo hukatwa moja kwa moja kwenye mapato hayo. Iwapo umesamehewa kulipa kodi hii, utatakiwa uoneshe cheti cha msamaha kutoka mamlaka ya mapato Tanzania (TRA).

Hitimisho

Uwekezaji wenye dhamana ya serkali nchini Tanzania, unatoa huduma ya kuaminika na ya usalama sana kwa faida kwa vile unaungwa mkono na serkali. Hata hivyo, itakubidi utafiti kiasi cha sasa cha riba kutoka kwa dalali wako.
Kalenda ya mwaka 2019/2020 ya utoaji wa mikopo yenye dhamana ya serkali:

Soma Zaidi

This post is also available in en_US.