Yellow Card ni wakala wa bitcoin Tanzania na Kenya. Unaweza kununua bitcoin kupitia kampuni hii kwa kutumia pesa za rununu kama vile Mpesa, akaunti ya benki na kadi za benki (debit au credit). Zaidi ya kuuza na kununua crypto, na akaunti ya Yellow Card ina mkoba wa kidijitali wa Bitcoin (Bitcoin Wallet.)
Soma makala hii ya Yellow Card App kwa Kiingereza: Yellow Card Review 2022
Mambo Muhimu Kuhusu Wakala wa Bitcoin Yellow Card
- Wakati wa kuandika makala haya, Yellow Card inafanya kazi katika nchi zaidi ya 15 za Afrika ikiwa ni pamoja Tanzania, Zambia, Nigeria, Ghana, Kenya, na Afrika Kusini.
- Jukwaa la bitcoin la Yellow Card linapatikana kwa lugha zifuatazo za Kiafrika: Kiswahili, Kiausa, Igbo, Luganda, Kisomali, Kixhosa, Kiyoruba na Kizulu.
Yaliyomo
- 1 Jinsi Ya Kufungua Akaunti Ya Yellow Card
- 2 Jinsi Ya Kununua Bitcoin Kupitia Yellow Card
- 3 Mkoba wa Yellow Card
- 4 Jinsi Ya Kuuza Sarafu za Kidijitali Kupitia Yellow Card
- 5 Nchi Yellow Card Inapopatikana
- 6 Sarafu Zinazokubalika
- 7 Njia za Malipo za Yellow Card Zinazokubalika
- 8 Mpango wa VIP wa Yellow Card
- 9 Mipaka ya Yellow Card
- 10 Yellow Card Fees
- 11 Je Yellow Card ni Salama? Je, Yellow Card ni Halali?
- 12 Msaada kwa Wateja wa Yellow Card
- 13 Majukwa mbadala ya Yellow Card
- 14 Mawazo ya Mwisho Kuhusu Wakala wa Bitcoin Yellow Card
- 15 Pata maelezo zaidi
Jinsi Ya Kufungua Akaunti Ya Yellow Card
Ili kununua na kuuza sarafu za kidijitali kwenye soko la bitcoin la Yellow Card, utahitaji kwanza kujiandikisha kwenye tovuti ya Yellow Card au kupakua programu ya Yellow Card ya Android au iOS na ubonyeze ‘Sign Up’. Jaza maelezo yako katika maeneo yaliyohitajika na bofya ‘Ingia’ (‘Sign Up’). Utatumiwa msimbo wa kuthibitisha kwenye nambari yako ya simu. Ingiza msimbo huo na bofya ‘Thibitisha’ (‘Confirm’)’. Wakati mwingine, ujumbe mfupi ulio na msimbo unaweza kuchelewa. Katika hali kama hii, unaweza kuchagua ‘Pata msimbo kupitia WhatsApp’ au ‘Pata msimbo kupitia USSD’. Kisha, thibitisha anwani yako ya barua pepe kwa kubonyeza kiungo kilichotumwa. Hatimaye, jiwekee PIN yako, uihakikishe na kisha ubonyeze ‘Next’ na akaunti yako itakuwa imeshafunguliwa.
Jinsi Ya Kununua Bitcoin Kupitia Yellow Card
Kununua Kutoka Jukwaa la Yellow Card
Utahitaji kwanza kufungua akaunti na Yellow Card na uingie kwenye akaunti yako. Kisha, utaweka fedha ndani ya mkoba wako wa kidijitali halafu bonyeza ‘Buy Cryptocurrency’. Weka kiasi unachotaka kununua na bofya ‘Review and Confirm’. Angalia muhtasari wa shughuli yako na bonyeza ‘Pay’ na Wallet yako ya Bitcoin itapokea fedha hizo.
Mkoba wa Yellow Card
Yellow Card hutoa mkoba wa bitcoin ambao unaweza kutumia kutuma, kupokea, na kuhifadhi cryptocurrency. Unapojiandikisha kwa akaunti ya Yellow Card, unajipata ruhusa ya kupata mkoba wako binafsi wa crypto.
Tunakushauri sana kuhifadhi bitcoin zako katika mkoba wako mwenyewe, na wala si mkoba unaomilikiwa na kampuni zinazojishughulisha na ubadilishanaji wa sarafu za kidijitali. Hii inamaanisha kuwa, pindi tu umenunua Bitcoin, unaweza kuziondoa kwa urahisi kutoka kwenye mkoba wa Yellow Card hadi kwenye mkoba wako mwenyewe. Mikoba ya crypto au pochi ya crypto salama ya kutumia ni pamoja na Muun, BlueWallet, Samourai, nk.
Jinsi Ya Kutuma Sarafu za Kidijitali Kutoka Mkoba Wako wa Yellow Card
Kwanza, ingia kwenye akaunti yako ya Yellow Card na kisha chagua sarafu ya kidijitali unayotaka kutuma. La sivyo, nenda kwenye ‘Wallets’ na uende chini kwenye sarafu za kidijitali unayotaka kutuma. Kisha, chagua kule unakotaka kutuma crypto zako. Unaweza kuchagua kutuma crypto kwa mtumiaji mwingine wa Yellow Card kwa kutumia nambari yake ya simu au anwani ya barua pepe au unaweza kutumia chaguo la ‘Wallet Address’. Baada ya kuchagua kunapotumwa sarafu hizo, jaza maelezo ya anayetumiwa (nambari ya simu, anwani ya mkoba, au anwani ya barua pepe) na uweke kiasi cha crypto unayotaka kutuma. Hatimaye, thibitisha maelezo haya na kisha tuma.
Jinsi Ya Kupokea Sarafu za Kidijitali Katika Mkoba Wako wa Yellow Card
Baada ya kuunda akaunti yako ya Yellow Card, mkoba maalum utatayarishwa kwa kila sarafu za kidijitali zinazoweza kupokelewa. Unaweza kutumia mkoba huu kupokea Crypto iliyotumwa kwako kutoka kwa mikoba mingineyo ya nje au kutoka kwa watumiaji wengine wa Yellow Card. Ili kupokea Crypto, ingia kwanza kwenye akaunti yako, nenda kwenye dashibodi yako na uchague sarafu za kidijitali unayotaka kupokea, au uende kwenye ‘Wallets’ halafu uichague. Kisha, bonyeza kwenye kifungo cha ‘Receive’. Baada ya hapo, utaona screen itakayokuonyesha maelezo yako ya anwani. Fanya nakala ya anwani ya mkoba na umtumie anayepokea sarafu za kidijitali. La sivyo, unaweza kutuma msimbo wa QR (QR code) moja kwa moja kutoka kwa mkoba wako. Crypto yako itaonekana katika mkoba wako mara tu cryptocurrency imetumwa na kuthibitishwa.
Jinsi Ya Kuuza Sarafu za Kidijitali Kupitia Yellow Card
Ili kuuza Crypto kwenye Yellow Card, unahitaji kuingia kwa akaunti ya Yellow Card na uende kwenye dashibodi yako. Ukiwa hapo, bofya kwenye ‘Sell Cryptocurrency’ na uweke kiwango cha Bitcoin unachotaka kuuza. Kisha, bofya ‘Review and Confirm’. Hakikisha maelezo yako ya shughuli hiyo na ubonyeze ‘Sell’ na kiwango sawia cha pesa za kawaida cha bitcoin yako kitatumwa kwenye mkoba wako.
Nchi Yellow Card Inapopatikana
Nchi ambazo shughuli za Yellow Card zinapatikana ni pamoja na
App ya bitcoin ya Yellow Card inapatikana katika lugha 14 ikiwa ni pamoja na lugha 3 za Ulaya, lugha 8 za Kiafrika (ikiwemo Kiswahili), Kiarabu na Mandarin.
Sarafu Zinazokubalika
Yellow Card inaruhusu matumizi ya sarafu zifuatazo TZS, KES, UGX, USD, Zar, NGN, GHS, BWP, ZMW, XAF, na sarafu za kidijitali (Bitcoin, Ethereum, na Tether).
Njia za Malipo za Yellow Card Zinazokubalika
Yellow Card inayawezesha malipo kupitia njia za malipo kupitia simu kama vile MPESA, Tigo Pesa, Airtel Money, Kadi za benki, uhamisho wa benki, vyeti vya papo (instant voucher) na pesa tasilimu. Njia za malipo zinazopatikana na unazoweza kuzitumia zinategemea nchi yako.
Mpango wa VIP wa Yellow Card
Yellow Card inatoa mpango maalum wa VIP kama ishara ya kuwashukuru wateja wake waaminifu. Ikiwa utafanya biashara yenye thamani kiasi fulani ya dola za Marekani au kiasi sawa katika sarafu ya nchi yako kwa muda wa siku 30, utakuwa umejisajili moja kwa moja katika programu. Kadri unavyofanya biashara zaidi, ndivyo kiwango chako cha VIP kinaongezeka, na ndivyo unavyopata faida zaidi. Vitengo vya VIP ni;
- Gold VIP. Utajipa kiwango hiki ikiwa utafanya shughuli zenye thamani ya dola elfu 40 au kiwango sawia katika fedha ya nchi yako katika sarafu za kidijitali. Hapa, utapata kwa mapema vipengele vya Yellow Card kabla ya watu wengineo. Pia, utapata msaada wa kipaumbele wa VIP.
- Platinum VIP. Utajifungulia kiwango hiki ikiwa utafanya shughuli zenye thamani ya dola laki moja au kiwango sawia katika fedha ya nchi yako. Unapata msaada wa kipaumbele wa VIP, mialiko ya kipekee ya matukio ya Yellow Card ya VIP, na pia utapata kwa mapema vipengele vya Yellow Card kabla ya watu wengineo.
- Diamond VIP. Unakuwa mwanachama wa Diamond VIP ikiwa utafanya shughuli zenye thamani ya dola elfu 250 au kiwango sawia katika fedha ya nchi yako. Unapata msaada wa kipaumbele wa VIP, upatikanaji wa mapema kwa vipengele vya Yellow Card, na pia utapata kwa mapema vipengele vya Yellow Card kabla ya watu wengineo, na mialiko ya kipekee ya matukio ya Yellow Card ya VIP.
Mipaka ya Yellow Card
Mipaka ya Yellow Card hutegemea nchi maalum na pia kiwango cha uhakiki utakachopokea. Viwango na mahitaji yake ni kama ifuatavyo;
- Tier 1 (Kitengo cha 1). Kwa madhumuni ya kuthibitisha unahitajika kutambulisha jina lako, barua pepe, namba ya simu, na tarehe ya kuzaliwa.
- Tier 2(Kitengo cha 2). Utahitajika kufanya uthibitishaji wa nambari ya benki (Bank Verification Number (BVN)) au uthibitishaji wa hati.
- Tier 3(Kitengo cha 3). Pakia ushahidi wa sehemu yako ya makazi au pakia kitambulisho kilichotolewa na serikali.
Yellow Card Fees
Yellow Card haitozi ada ya kununua au kuuza. Hata hivyo ada ya kudeposit na kuwithdraw, inayotozwa hutegemea nchi mahsusi.
Je Yellow Card ni Salama? Je, Yellow Card ni Halali?
Ndiyo. Yellow Card inadhibitiwa na FinCEN nchini Marekani na katika kila nchi ambapo Yellow Card inafanya kazi. Hata hivyo, Yellow Card pia inakabiliwa na mashambulizi kutoka kwa walaghai. Ili kuhakikisha kwamba huhatarishi shughuli zako mikononi mwa walaghai hawa, usitambulishe nenosiri lako la Yellow Card na mtu yeyote kwenye mtandao. Walaghai wengi watajifanya kuwa mawakala wa bitcoin wa Yellow Card, lakini unastahili kufahamu kuwa mawakala wa Yellow Card hawatakuuliza kamwe maelezo yako ya kibinafsi. Pia, usimtumie yeyote fedha zako ili akuwekee kwenye Yellow Card kwa niaba yako.
Kashfa za sarafu za kidijitali zinaongezeka duniani kote ikiwa ni pamoja na nchi za Tanzania, Kenya, Rwanda, n.k. Usipumbazwe na jumbe za mitandao ya kijamii ukishawishiwa “kujiunga na Bitcoin” na kupata utajiri wa haraka. Jihadharini na watu binafsi au makampuni ambayo yanaahidi mapato ya kiwango cha juu sana kutokana na uwekezaji wa Crypto. Jifunze zaidi kuhusu kashfa/ulaghai wa sarafu za kidijitali na jinsi ya kuepuka.
Msaada kwa Wateja wa Yellow Card
Unaweza kuwasiliana na timu ya kutoa msaada kwa wateja wa Yellow Card kupitia barua pepe support@yellowcard.io. Iwapo una maswali yoyote, unaweza kutafuta usaidizi kupitia kituo chao cha usaidizi au kutembelea knowledge base. Vilevile, unaweza kuwasiliana na timu ya usaidizi kupitia WhatsApp, Facebook, Twitter, na Telegram.
Majukwa mbadala ya Yellow Card
Ikiwa unatafuta njia mbadala za Yellow Card, zifuatazo ni njia bora zaidi
Mawazo ya Mwisho Kuhusu Wakala wa Bitcoin Yellow Card
Yellow Card inaendelea kupata umaarufu barani Afrika kwa sababu inatoa njia rahisi ya kununua na kuuza sarafu za kidijitali hata kama huna akaunti ya benki, kwa kutumia pesa rununi. Kwa mfano Yellow Card Tanzania ni moja la soko kubwa la bitcoin Tanzania. Lengo kuu la Yello Card ni kufanya sarafu za kidijitali kupatikana kwa urahisi katika nchi mbalimbali za Afrika.
Pata maelezo zaidi
This post is also available in en_US.