Orodha ya Pochi za Bitcoin (Bitcoin Wallet) Salama Zaidi

Tafsiri:

Bitcoin, pesa ya kidijitali iliyoanzishwa mwaka 2009, imeendelea kukua. Kufikia sasa, mtaji wa soko la Bitcoin ni kubwa kuliko kampuni nyingi kubwa kama vile Nike, IBM, Disney, na kadhalika. Katika makala haya, tutaangalia wallet (pochi za bitcoin) salama ya Bitcoin ambayo unaweza kutumia ili kuhifadhi safaru zako kwa njia salama.

Je, Pochi ya Bitcoin ni nini? (Bitcoin Wallet)

“Seed phrase,” “seed recovery phrase” au “backup seed phrase” ni orodha ya maneno ambayo huhifadhi habari zote zinazohitajika ili kurejesha fedha za bitcoin. Programu ya Wallet itazalisha vifungu hivi vya maneno na kumwelekeza mtumiaji kuyaandika kwenye karatasi. – Bitcoin Wiki

Bitcoin iliundwa na lengo la kuchukua nafasi ya sarafu ya zinazotumia katika nchi mbalimbali kama vile shilingi ya Tanzania au dola ya Marekani. Satoshi Nakamoto, mwanzilishi wa Bitcoin (ambaye hadi leo hii hakuna mtu anayefahamu kama ni mwanaume, mwanamke, mtu mmoja au ni kikundi cha watu) aliamini kuwa benki kuu na serikali zilikuwa na udhibiti mkubwa juu ya maisha yetu. Kwa hivyo, alifikiri kuwa sarafu isiyodhibitiwa mahali pamoja inaweza kuwa huru kutokana udhibiti wa serikali.

Kama zilivyo sarafu nyinginezo, bitcoin inahitaji kuhifadhiwa. Hapa ndipo mikoba hii ya kidijitalia inahitajika. Mkoba huu unaweza kuwa wa kihalisia ama wa kidijitali ambapo mtu anaweza kuhifadhi fedha zake. Kwa fedha za kawaida kama vile shilingi, mkoba wake unaweza kutengenezwa kutokana na ngozi. Mkoba wa bitcoin ni tofauti. Ni mkoba wa kidijitali ambapo unaweza kuhifadhi pesa zako. Mifano ya mikoba mingine ya kidijitali ni kama Google Pay, PayPal, na Apple Pay.

Wallet ya bitcoin inatumiwa kuhifadhi bitcoin na pia kutuma bitcoin kwa wallet za watu wengine. Kwa hiyo, mkoba huo unahitaji kuwa rahisi kutumiwa na salama.

Mkoba wa kukodisha (Custodial wallet) na Mkoba usio wa kukodisha (Non custodial wallet)

  • Mkoba wa kukodisha ni wallet ya kidijitali inayohifadhiwa na mshirika wa tatu (third party). Mshirika huyu, ambaye sio mmiliki wa sarafu hizo, ana funguo za faragha na ana udhibiti kamili wa fedha zilizohifadhiwa humo. Kutokana na hili, kwa vile humiliki funguo zako za siri, pana uwezekano wa pesa zako kutokuwa salama. Hii ndiyo sababu haipaswi kuhifadhi cryptos zako kwa kubadilishana, kuondoa fedha zako mara tu unapozinunua. Binance, Coinbase na Bitfinex ni baadhi ya mifano ya wallet za kukodishwa.
  • Wallet isiyo ya kukodisha ni mkoba wa crypto ambapo mmiliki / mtumiaji ana funguo zake za faragha na ana udhibiti kamili wa fedha. Huu ndio mkoba salama zaidi kwa bitcoin yako na crypto nyinginezo kwa vile hakuna mtu anayeweza kuzifikia fedha zako bila funguo za faragha. Mifano ya wallet zisizo za kukodisha ni Samourai, Exodus, Muun, na vifaa vya kuhifadhia kama vile Trezor (ambayo ni “hardware wallet”).

Aina ya Wallet za Bitcoin

Hot wallets (Mikoba Moto) na cold wallets (Mikoba Baridi)

  • Hot wallets ni mikoba ambayo inahitaji kuunganishwa na mtandao kupitia kompyuta, simu, au vifaa vingine vya intaneti ili kuweza kufanya kazi huku cold wallets zinafanya kazi bila kuunganishwa kwenye mtandao. Kwa hiyo,mikoba baridi ni salama zaidi kuliko mikoba moto.

Kuna aina kadhaa za mikoba ya bitcoin. Mikoba hii ina sifa tofauti na viwango tofauti vya usalama na hutumiwa kwa sababu mbalimbali.

  • Mikoba Tamba. Hizi ni wallet za bitcoin ambazo zinaweza kutumika kupitia vifaa vya simu na vinaendana na mifumo tofauti kama iOS na Android. Mifano ya wallet tamba za bitcoin ni Samourai, Exodus, Muun, BlueWallet na Mycelium.
  • Mikoba ya Vifaa (Hardware Wallets). Hii inafanana kidogo na mkoba wa ngozi wa pesa za kawaida kama vile shilingi. Ni vifaa vidogo, vyenye ukubwa wa flash disk, ambapo unaweza kuhifadhi sarafu zako. Inachukuliwa kuwa aina salama zaidi ya mkoba wa bitcoin. Mifano ya aina hii ya mikoba ya Bitcoin ni KeepKey, Trezor, Ledger na Coldcard.
  • Mikoba ya Kiprogramu (Desktop wallets). Hii ni programu ambayo inapakuliwa kwenye kompyuta. Inaweza kuwekwa kwenye Windows, Mac, Linux au mfumo wowote ule. Mifano yake ni pamoja na Wasabi, Electrum, BlueWallet na Exodus.
  • Mikoba ya Wavuti (Web wallets). Hii ni mikoba ambayo inaweza kupatikana tu kwenye wavuti kupitia Chrome au Firefox. Wallet za wavuti sio salama sana hivyo hatukushauri kuhifadhi bitcoin yako katika mkoba wowote wa wavuti.

Kibeti cha Karatasi (paper wallet) ni jina ambalo linatokana na njia ya zamani na isiyo salama ya kuhifadhi Bitcoin ambayo ilikuwa maarufu kati ya mwaka wa 2011 na 2016. Inafanya kazi kwa kuwa na ufunguo wa kibinafsi na anwani ya kibinafsi ya bitcoin. Anwani hii na ufunguo huzalishwa kwenye tovuti, na kisha kuchapishwa kwenye karatasi. Njia hii ina uwezekano mkubwa wa kutokuwa salama na haipaswi kutumiwa.

bitcoin wallet
Trezor, mkoba wa kifaa (hardware wallet) wa bitcoin.

Mikoba Tamba Bora ya Crypto

Kuna matoleo mengi ya bandia ya mikoba ya bitcoin. Hakikisha unapata mkoba kutoka kwenye tovuti ya kweli na kuaminika. Watu wengi wamepoteza pesa kwa walaghai wa bitcoin.

Samourai Wallet

Mkoba maarufu wa Samourai Wallet ni mkoba wa mtandaoni na pia nje ya mtandao ambao hutoa vipengele muhimu vya kuhifadhi bitcoin. Unaweza kupakua Samourai Wallet kwenye kifaa chako cha Android na iOS bila malipo. Unaweza pia kupakua na kuiweka kwenye kompyuta. Mkoba huu una vipengele vya pekee ambavyo mikoba mingine haina:

  • Uwezo wa kutumika kikamilifu nje ya mtandao (Offline). Hii ina maana kwamba unaweza kulinda bitcoin yako kwa ku kutounga kwenye intaneti.
  • Segregated witness. Samourai ni miongoni mwa mikoba ya kwanza inayowezesha kugawanyika kwa mchakato wa kuhakikisha shughuli za bitcoin, kipengele kinachosaidia kupunguza gharama za shughuli hizo.
  • Ada ya mchimbuaji (Smart miner fees). Hiki ni kipengele kinachojulikana kwa wachimbuaji. Inasaidia kukadiria kiasi cha fedha kitakacholipwa kwa shughuli ya uchimbaji. Bitcoin huzalishwa kwa kuchimbwa kidijitali (bitcoin mining).
  • Dojo. Samourai inakuwezesha kuendesha nodi (node) yako mwenyewe kwenye mtandao wa bitcoin.
  • Stonewall. Hii hukupa ulinzi dhidi ya mashambulizi ya kianwani na pia kutokana na uvamizi usiotambulishwa.
  • PayNym. Hiki ni kipengele kinachokinga dhidi ya kufuatilia na kampuni za ujasusi

Mbali na yote haya, mkoba wa Samourai hutumia teknolojia ya encryption ya AES-256 ambayo inakukinga kutokana na mashambulizi. Pia inatumia teknolojia ya passphrase encryption ya BIP 39. Hii ni pamoja na PIN na nenosiri (password) unayopaswa kutumia.

BlueWallet

BlueWallet ni mkoba wa bitcoin wa bure unaoweza kutumiwa kwenye simu ya mkononi na kompyuta na ulizinduliwa mwaka 2017. Unaweza kutumia mkoba huu kwa pamoja na ColdCard Hardware Wallet na hata unaweza pia kutumia na mkoba wa Electrum. Kampuni iliyounda BlueWallet pia imezindua aina ya kwanza ya saa ya mkononi ya Apple ya bitcoin, ambayo inaruhusu watumiaji kupokea au kutuma malipo moja kwa moja kutoka kwa saa zao.

Baadhi ya vipengele vingine vya kuvutia vya BlueWallet ni uwezo wa kuona tu (watch-only) bitcoin bila kuweza kuziuza au kuhamisha na Lightning Network (teknolojia kwa ajili ya kunua bitcoin bei nafuu na haraka).

Muun Bitcoin Wallet

Muun ni mkoba wenye uwazi wa Bitcoin na pia teknolojia ya Lightning Network uliotengenezwa nchini Argentina. Ni mkoba bora kwa watu wasio wazoefu wa bitcoin na kwa malipo ya haraka na ya bei nafuu. Mkoba huu una mfumo wa kiusalama wa 2-of-2 multi-signature, unoinafanya kuwa moja ya mikoba ya Bitcoin salama zaidi kwani shughuli zako zote zinahitaji kusainiwa na funguo 2 badala ya 1. Ikiwa simu yako imevamiwa (hacked), hakuna njia ambayo hacker ataweza kuzifikia bitcoin zako kwa sababu kuna ufunguo mmoja tu katika mkoba wako. Na kama simu yako itaibiwa, utakuwa na uwezo wa kuufunga mkoba wako mpaka upate simu mpya.

Mkoba wa Muun unakuja na Kifaa cha dharura, ambacho kinahakikisha kuwa pana usalama wa kujitegemea kwa kuhifadhi funguo zako za faragha hata bila kujiunganisha kwenye intaneti.

Kifaa cha dharura (Emergency Kit)ni maandishi kwa PDF yenye habari na maelekezo yanayohitajika kwa shughuli za matumizi ya fedha zako kwa kujitegemea. Hakuna haja ya kulazimisha au kubahatisha data yoyote kwani kila kitu kiko pale, ikiwa ni pamoja na funguo zako binafsi na maelezo yake. Funguo zako za faragha zinawekwa salama na pia njia ya kizipata tena ukisahau au ukipoteza. Hii inafanya Emergency Kit yako iwe salama: unaweza hata kuweka nakala nyingi, na unaweza hata kuihifadhi salama mtandaoni.

Wallet ya Exodus

Exodus ni mojawapo ya mikoba bora ya Bitcoin kwa wale wanaoanza shughuli za sarafu za kidijitali. Ni mkoba wa simu na kompyuta ambao unaingiliana na Trezor hardware wallet. Exodus Wallet haitozi gaharama yoyote na inaweza kutumika kuhifadhi sarafu za kidijitali (cryptocurrencies) zaidi ya 100. Baadhi ya faida zake ni pamoja na msaada kutoka kwa wasaidizi na wahudumu kila saa, wiki nzima, uwezo wa kubadilishana kwa sarafu tofauti. Aidha, Exodus inawaruhusu watumiaji wake kupata kipato cha ziada kutokana na riba inayotozwa kwenye crypto zao. Hata hivyo, ni programu funge isiyowezwa kubadilishwa kwa urahisi.

Mycelium

Mycelium ni mkoba huria usiotoza gharama unaohifadhi bitcoin tu. Ni mkoba unaowafaa watumiaji wale waliobobea katika shughuli za sarafu za kidijitali. Mycelium ina uwezo wa kindani wa ubadilishji sarafu na mikoba ya vifaa na hivyo kuwaruhusu wenye bitcoin kuhifadhi bitcoin zao kwenye hardware wallet kama Trezor, Ledger na KeepKey .

Ili kutumia Mycelium, hakuna kitambuliso kinachohitajika au data nyingine yoyote ambayo inaweza kutoa utambulisho wako. Aidha, mkoba huu hutumia teknolojia ya TOR ili kuficha anwani yako ya IP mtandaoni na eneo ulipo. Wallet hii pia ina mode ya kusoma tu, ambayo inakuwezesha kufuatilia shughuli zako au kuangalia sawio lako. Mycelium inawaruhusu wamiliki wa wallet kuweka ada maalum ya kufanya shughuli zao. Ada unayoweka itaamua muda gani utachukuliwa ili shughuli yako kukamilika.

Hatukushauri kutumia mikoba ya Crypto inayowezesha altcoins kama vile Coinbase na bitcoin.com, ambayo inajihushisha na fedha za bitcoin ila si Bitcoin halisi.

Programu Bora za Wallet za Kidijitali (Desktop Wallets)

Wasabi

Wasabi ni mkoba huria unaohifadhi Bitcoin kupitia kompyuta na unatumia mkakati wa CoinJoin. Ili kuhakikisha kutokujulikana, trafiki zote za mtandao wa Wasabi hupitia teknolojia ya Tor. Wasabi hufuata falsafa ya Bitcoin kwa kufanya programu ya wazi (open soure).

Kwa kuwa mkoba wa Bitcoin wa desktop, Wasabi inaendeshwa katika operating systems nyingi za 64-bit. Inaweza kutekelezwa kupitia Windows 10 1607 + (isipokuwa 1703), MacOS 10.13+, Ubuntu 20.10, 20.04 (LTS), 18.04 (LTS), 16.04 (LTS), Fedora 32+, na Debian 9+.

 

Electrum

Electrum ni mkoba wa kidijitali kupitia programu za kompyuta. Inajishughulisha tu na Bitcoin. Unaweza kudownload Electrum kwenye Windows (7 na ya juu), MacOS (10.13 na ya juu) na Linux.

Aina za Elecrum zaidi ya 3.3.4 zinaweza kupatwa na uharibifu wa rahis mtandaoni. Usidownload Electrum kutoka mtandao tofauti isipokuwa electrum.org, na ujifunze kuthibitisha saini za GPG.

Mikoba ya Vifaa (Hardware Wallets) ya Cryptocurrency

Trezor

bitcoin wallet
Trezor, mkoba wa kifaa (hardware wallet) wa bitcoin.

Trezor ni kampuni inayotengeneza vifaa hivi vya mikoba. Kampuni hutoa aina mbili za mikoba. Trezor One ni vifaa vya dola 59 ambavyo husaidia kuhifadhi bitcoin yako na sarafu nyingine hata nje ya mtandao. Trezor Model T ni vifaa vya dola 179, vyenye ukubwa wa ufunguo wa gari ambapo unaweza kuhifadhi sarafu zako. Tofauti kati ya hizo mbili ni kwamba Trezor Model T ina uwezo wa ziada wa usalama. Vifaa vinginevyo vya Trezor kama vile mfuko ya Trezor (Trezor case) ni dola 15 na Trezor Lanyard ni dola 3.50.

Ledger

Ledger wallet huwawezesha watumiaji kuhifadhi, kutuma, na kupokea Bitcoin na sarafu nyingine za kidijitali. Wallet hii inapatikana katika mifano miwili; Ledger Nano S na Ledger Nano X. Ledger Nano S itakugharimu dola 59 huku Ledger Nano X itakugharimu dola 119.

Coldcard

Coldcard ni vifaa vya Bitcoin vinavyoweka salama mikoba kwa njia ya cold storage. Mikoba ya Coldcard huweka vifungu na taarifa nyingine nyeti ambazo huwezi kuziweka kwenye hot wallet. Mikoba kadhaa ya bitcoin kama vile Electrum vina uwezo tayari wa kindani unaolenga kusaidia Coldcard. Wallet hii huruhusu watumiaji wake kujifanyia shughuli za nje ya mtandao kupitia Coldcard. Coldcard Mk3 itakugharimu dola 119.97.

Promo Code ya Coldcard: Tumia CKBTC kama Promo code ili uweze kupunguziwa 5% ya ununuzi wako wakati unapolipa ukitumia Bitcoin.

Mawazo ya Mwisho Kuhusu Wallet bora za Bitcoin

Mkoba mzuri wa bitcoin unapaswa kukidhi sifa tatu kuu. Kwanza, unahitaji kuwa salama. Mikoba ambayo tumeelezea hapa yote ni salama. Pili, inahitajika kuwa rahisi kutumia. Hatimaye, mkoba wa Bitcoin unapaswa kutekeleza majukumu mengi. Tunaamini kwamba mifano tuliyoorodhesha inakidhi mswada huu. Hata hivyo, tunapendekeza kuijaribu na kuifanya utafiti wako wa kina kabla ya kutumia kati ya mikoba hii.

This post is also available in en_US.