Kadri umaarufu wa Bitcoin unavyozidi kuongezeka, watu wengi wamekuwa wakijiuliza jinsi ya kupata Bitcoin. Basi usiwe na shaka, tutakonyesha jinsi ambavyo unaweza kupata Bitcoin. Kwa kufuata njia tulizoorodhesha hapo chini pamoja na utafiti wa kutosha, utaweza kupata Bitcoin.
Jinsi ya Kupata Bitcoin
Kununua Bitcoin
Njia maarufu ya kupata Bitcoin ni kununua kwenye masoko ya Bitcoin kama vile Yellow Card. Tofauti na masoko mengine ya Bitcoin ambayo yapo mtandaoni na ofisi zao ziko nchi nyingine, Yelow Card ina ofisi zake Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, n.k. Kununua Bitcoin sio shughuli ngumu kwani unaweza hata kununua Bitcoin kwa Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money, n.k.
Soma pia: Jinsi ya Kununua Bitcoin Tanzania, Jinsi ya Kununua Bitcoin Kenya, na Jinsi ya Kununua Bitcoin kwa Mpesa.
Kwakuwa Bitcoin sio fedha kama vile Shilingi za Tanzania bali ni fedha dijitali. Hivyo huwezi kuhifadhi Bitcoin kwenye mkoba wa mfukoni, mfuko wa suruali, au chini ya mto kitandani! Unahitaji mkoba wa Bitcoin (Bitcoin wallet). Mkoba huu ndio utakaotumia kuhifadhi Bitcoin zako.
Fanya Kazi Zinazolipa kwa Bitcoin
Siku hizi kuna kazi nyingi mtandaoni ambazo zinalipa kwa Bitcoin. Kuna tovuti nyingi ambazo zinakutanisha watu wanaotafuta kazi na waajiri ambao wanalipa kwa Bitcoin. Tovuti ambazo unaweza kupata kazi na kisha ukalipwa na Bitcoin ni pamoja na hizi.
Unaweza pia kupata malipo kwa fedha za kawaida kama vile dola, euro au shilingi kisha ukatumia kampuni kama vile Bitwage kubadilisha mshahara wako kwa Bitcoin.
Kufanya Kazi Ndogo Ndogo Za Kifedha (Bitcoin Micro Jobs)
Hii ni kazi ya ndogo (micro job), mara nyingi hupatikana kupitia mtandao wa intaneti. Zipo tovuti nyingi ambazo zinalipa kwa Bitcoin kwa kazi rahisi kama kujibu barua pepe, kubonyeza kwenye tangazo, kukamilisha utafiti wa mtandaoni, kuangalia video, nk. Mitandao kama Earn, waweza kupata Bitcoin kwa kujibu barua pepe na kukamilisha kazi fulani. Hakikisha umefanya utafiti wa kutosha kujiridhisha kuwa eneo unalotaka kutumia ni halali.
Tovuti ambazo unaweza kuzitumia kupata kazi ndogo (micro jobs) ni pamoja na:
Kujipatia fedha za kutosha kwa kufanya kazi ndogo ndogo ni vigumu, kunachosha na kunatumia muda mwingi.
Pata Bitcoin kwa Kucheza Michezo ya Kompyuta
Unaweza kupata Bitcoin kwa kucheza michezo mbalimbali mtandaoni. Jua kuwa baadhi ya michezo inakuhitaji kutumia muda mwingi sana kucheza ili kuweza kupata mapato ya kuridhisha. Baadhi ya michezo unayoweza kujiunga nayo na kupata malipo ya Bitcoin ni pamoja na hii:
Andika Kuhusu Bitcoin
Waweza kujitengenezea fedha kwa kuandika kuhusu Bitcoin. Bitcoin ni dhana mpya na ya kuvutia, ndio maana tovuti nyingi zinatafuta waandishi. Tovuti mbalimbali hulipa waandishi waandikao makala zihusianazo na Bitcoin. Kwenye tovuti hizo waweza kulipwa kwa kuwa bloga mwalikwa au mwandishi wa habari za Bitcoin analiyelipwa.
Kati ya tovuti unazoweza kulipwa kwa kuandika makala za kuhusu Bitcoin ni hizi (makala za Kiingereza):
Washirika Wa Bitcoin (Bitcoin Affiliate)
Soko shirikishi (Affiliate marketing) ni aina ya soko tendaji ambapo biashara inakuzawadia kwa kila mgeni au mteja anayeletwa na vyanzo vyako. Unapokuwa muuzaji shirikishi, unapata kiunganishi ambacho waweza kushea kwenye tovuti yako au kwenye mitandao ya kijamii. Waakati ununuzi unapofanyika kutokana na juhudi zako za kuitangaza biashara, unalipwa kwa kamisheni.
Kampuni ambazo hulipa kamisheni kwa Bitcoin unapotangaza biashara zao ni pamoja na hizi:
Kukubali Bitcoin Kama Njia Ya Malipo
Waweza kuuza bidhaa na huduma kwa kubadilisha na Bitcoin. Kuikubali Bitcoin kwaweza kuleta wateja wapya kwenye biashara yako. Kuna biashara na watu binafsi wengi wanaokubali Bitcoin kama njia ya malipo barani Afrika. Kwa mfano, Betty’s place, mgahawa unaomilikiwa na Betty Wambugu, ulioko Nyeri, nchini Kenya. Betty anauza nyama ya kuchoma na anapokea malipo kwa Bitcoin hasa kutoka kwa watalii.
Kama una biashara kwa mfano ya utalii (hoteli, mgahawa, duka la vinyago, kampuni ya usafiri, n.k.), ni rahisi kupokea malipo ya Bitcoin kwakuwa utakuwa unapokea watalii toka nchi mbalimbali zikiwemo nchi zenye watu wengi wanaotumia Bitcoin safarini.
Vimotisha Vidogovidogo Vya Bitcoin
Kuna maeneo mitandaoni ambapo waweza kupewa Bitcoin kama sehemu ya kukumotisha kwa ulichokifanya mtandaoni. Yaweza kuwa ni kwa jambo ulilolianzisha mtandaoni au kwa kumsaidia mtu. Sehemu ambazo wanatoa motisha hizi ni pamoja na hizi:
Bilula Za Bitcoin (Bitcoin Faucets)
Bilula ya Bitcoin ni mfumo wa zawadi kwa njia ya tovuti au programu ambayo inasambaza zawadi ya satoshi, ambayo ni sehemu mamia ya mamilioni ya Bitcoin, kwa watembeleao tovuti ya bilula na kuweza kujibu swali maalum la kirakilishi au kazi kama ilivyobainishwa na tovuti. Matangazo ni chanzo kikuu cha mapato cha bilula hizi. Hii ina maana kwamba utalipwa kwa kuangalia matangazo au kujibu tafiti za mitandaoni.
Kwa ujumla, bilula za Bitcoin zinakuja na hatari na kazi zinazochosha. Baadhi ya bilula zinaiteka kompyuta yako na kuitumia kwenye kazi za ‘kuchimba’ Bitcoin. Kumbuka kutotumia pochi za bilula kuifadhi bitcoin zako.
Uchimbaji Wa Bitcoin
Wachimbaji wa Bitcoin wanalipwa kama tuzo kwa kuthibitisha miamala ya Bitcoin kwenye mtandao wa Blockchain. Tuzo kwa uchimbaji wa Bitcoin hugawanywa mara mbili kwa miaka minne. Wakati Bitcoin ilichimbwa kwa mara ya kwanza mwaka 2009, uchimbaji kwenye ‘block’ moja, ungeweza kukupatia Bitcom 50. Mwezi Novemba mwaka 2009 ungeweza kupata Bitcoin 12.5 kwa kumaliza block moja.
Sehemu unakoweza kupata huduma ya “kuchimba” Bitcoin na kulipwa ni pamoja na hizi:
- NiceHash
- Slushpool
- CryptoTab Browser (it allows you to mine while browsing)
- Ecos
- Bitfly
Hitimisho Kuhusu Jinsi ya Kupata Bitcoin
Ili kutumia njia mojawapo kati ya tulizozitaja hapo juu, unahitaji kutumia muda wa kutosha kutafiti tovuti unazotaka kutumia na kuelewa hatari zilizopo na jinsi ya kuzitatua.
This post is also available in en_US.