Jinsi ya Kununua na Kuuza Bitcoin Nchini Kenya

Bitcoin ni mfumo wa kwanza wa malipo ya dijitali usio na msimamizi ulioanzishwa mwaka 2009. Hata hivyo, kutokana na kutoeleweka kwa urahisi kwa mfumo wa sarafu kama huu, Wakenya walichukua muda mrefu kujihusisha na biashara ya bitcoin. Miaka ya hivi karibuni idadi ya Wakenya wanaojihusisha na biashara ya sarafu ya bit imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Barani Afrika, Kenya ni moja ya nchi zinazoongoza kwa biashara ya sarafu ya mtandaoni.

Soma makala haya kwa Kiingereza: [How to Buy Bitcoin in Kenya[(https://fififinance.com/bitcoin-kenya)

Sifa za sarafu ya bitcoin

  • Hazina msimamizi yeyote (kama vile Benki Kuu)
  • Ni rahisi kubadilishana kati ya mtu na mtu toka sehemu tofauti duniani
  • Ni za bei nafuu. Unaweza kubadilisha sarafu za bit kwa thamani ya senti chache.
  • Ni rahisi kuhamisha. Kuhamisha bitcoin huchukua sekunde chache tu tofauti na benki ambapo kuhamisha fedha huweza kuchukua siku kadhaa.

Jinsi ya kununua bitcoin Kenya

Unaweza kununua bitcoin nchini Kenya kwa kutumia mifumo ya malipo kama vile PayPal, Transferwise, M-Mpesa na benki. Baadhi ya fedha unazoweza kutumia kununua sarafu ya bit Randi ya Afrika Kusini, Euro, Pauni ya Uingereza, Dola ya Australia na nyinginezo.

Bitcoin exchange rate with Kenya Shillings

Kima cha mabadilishano ya bitcoin na Shilingi ya Kenya, tazama kima cha mabadilishano cha sasa.

Unahitaji vifuatavyo ili kuuza na kununua bitcoin

1. Fedha

Bitcoin ni fedha digitali yenye thamani. Huhitaji kuwa na fedha nyingi ili kunuua bitcoin. Unahitaji dola kadhaa na pia utazame bei yake maana hubadilika mara kwa mara. Kuanza, unahitaji kubadilisha fedha taslimu na bitcoin. Tazama bei ya bitcoin kwenye masoko mbalimbali. Chukua tahadhari kwa kununua bitcoin ya thamani ndogo ambayo haitakuathiri kama ukiipoteza. Uwekezaji kwenye bitcoin ni kama uwekezaji mwingine wowote ambapo kuna faida na hasara.

2. Mkoba

Unahitaji kuwa na mkoba wa dijitali wa kuhifadhi bitcoin. Mkoba unaweza kutumika kutuma, kupokea na kuhifadhi bitcoin. Nchini Kenya, unaweza kutumia M-Pesa. Kutuma, unahitaji kuwa na anuani ya mkoba wa unayemtumia kama vile akaunti ya benki au namba ya M-Pesa. Hakikisha unatumza ufunguo wa dijitali wa mkoba wako mahali salama na sio mtandaoni.

3. Mabadilishano

Kuna majukwa ya mtandaoni ambayo wanunuzi na wauzaji wanaweza kubadiishana bitcoin kwa fedha taslimu. Hawahitaji kukutana ili kubadilishana. Nchini Kenya, kuna majukwaa mengi mtandaoni ambao mtu anaweza kutumia. Kati ya hayo ni pamoja na yafuatayo:

  • Mabadilishano ya wanunuaji
  • Mabadilishano ya wauzaji

Mabadilishano ya wanunuaji

Mahali watu wanaweza kununua bitcoin kwa kutumia M-Pesa ni pamoja na:

  • Paxful: Ni rahisi kununua bitcoin hapa kwa kutumia M-Pesa. Paxful inatumiwa na watu wengi toka nchi mbalimbali barani Afrika.
  • Localbitcoins: Unachohitaji kufanya na kujiandikisha na baadaye unaweza kutafuta mtu anayenunua bitcoin.

Jinsi ya kuuza bitcoin

Unaweza kuuza fedha za kawaida kwenye soko la fedha dijitali kutegemea na nchi husika. Unaweza kuuza bitcoin ndani ya Kenya au kwa mtu aliyeko nje ya nchi.

Mabadilishano ya wauzaji

Wakenya wanaweza kuuza bitcoin kwa kutumia: