Jinsi ya Kununua na Kuuza Bitcoin Kwa M-Pesa

Kuwekeza kwenye sarafu za kidijitali, hakuhitaji mtu kuwa na fedha nyingi. Kwa bahati nzuri, hata kwa dola moja, bado waweza kununua sarafu za kidijitali. Sarafu za kidijitali ni fedha zenye thamani sawa na fedha za kawaida. Hivyo, kwa kuanzia, inakubidi ubadili fedha kwa sarafu za kidijitali.

Tunawashauri sana wasomaji wetu kutowekeza kiasi cha fedha wasichopenda kukipoteza kwenye bitcoin. Uwekezaji huu una hatari kama uwekezaji mwingine wowote. Kwahiyo mtu aweza akapata faida au hasara. Ukosefu wa pesa usikuzuie kufanya biashara ya sarafu za kidijitali kwa vile waweza kupata faida kwenye uwekezaji huu. Lakini ni kwa vipi waweza kuuza na kununua bitcoin kwa M-Pesa?

Kununua Bitcoin kwa M-Pesa

Yakubidi ufuate hatua zifuatazo ili kununua sarafu mtandao kwa M-Pesa:

  • Tembelea duka la kubadilisha fedha za kidijitali unazotaka kubadili, jisajili bure na unda akaunti.
  • Angalia barua pepe yako kuthibitisha taarifa za usajili ulizotoa.
  • Kwenye kubadili, chagua mfanyabiashara anayekidhi matakwa yako, kwa mfano baadhi ya wauzaji wana wastani wa chini wa shilingi 1,000 za Kenya, wakati wengine wana wastani wa chini wa shilingi 10,000 za Kenya. Kisha angalia sifa za muuzaji huyo kabla hujanunua. Hakikisha unafanya biashara na wafanyabiashara wenye asilimia alama mia moja ya mrejesho.
  • Pindi umuaminipo muuzaji, bonyeza ‘buy Bitcoin’ mbele ya jina lake ili kununua. Tovuti itakuelekeza kwenye ukurasa wenye vigezo na masharti. Soma vigezo na masharti ya mfanyabiashara huyo.
  • Baada ya kukubaliana na vigezo na masharti ya mfanyabiashara, ingiza kiasi unachotaka kubadili kuwa Bitcoin kwa shilingi ya Kenya. Utaziona namba za Bitcoin utakazopokea.
  • Kisha fanya malipo kwa kutumia M-Pesa na kisha thibitisha kiasi. Mara utapokea Bitcoin.

Hakikisha unafanya biashara na wafanyabiashara wenye asilimia alama mia moja ya mrejesho (feedback).

jinsi ya kununua na kuuza bitcoin

Jinsi ya Kutoa (Withdraw) Bitcoin kwa M-Pesa

Inawezekana kutoa Bitcoin kwa kutumia M-Pesa. Hii ndiyo njia rahisi ya kufanya. Mtambue muuzaji wa Bitcoin anayeaminika na anayejishughulisha na utoaji wa Bitcoin kwa M-Pesa. Mtumie Bitcoin unayotaka kuitoa. Wao watakutumia pesa taslimu kwenye M-Pesa inayowiana na Bitcoin uliyotuma. Hapo waweza kutoa pesa hiyo kwa M-Pesa.

Ni lazima ujifunze mambo muhimu ya sarafu mtandao ambayo mara kwa mara utakuwa unayatumia.

  • Mkoba wa bitcoin: Mkoba wa Bitcoin ni mfuko wa kidijitali kwa utunzaji wa sarafu mtandao. Mfuko huo una chaguo la kutuma, kupokea na kuhuisha (backup) sarafu zako. Ili kupokea fedha kwenye mfuko wako, unahitaji kumpa mtumaji anuani ya mfuko wako. Anuani ya mfuko wako ni kama namba ya akaunti ya benki au namba ya M-Pesa. Chukua tahadhari kuhuisha usiri wa mfuko wako pamoja na vibonye umma nje ya mtandao kwa usalama.
  • Badilisho: Hili ni soko eneo ambapo watu huuza na kununua bitcoin mtandaoni. Watu hawahitaji kuonana kwa vile wanaweza kubadilishana fedha za kidijitali kwa njia ya mtandao. Nchini Kenya na Tanzania, kuna masoko mengi ya kuuza na kununua fedha ambayo mtu aweza kuyatumia.

Maduka ya Kuuza na Kununua Fedha za Kidijitali

Soma makala yetu kuhusu jinsi ya kujiunga na Bitcoin Tanzania. Makala hii itakuonyesha jinsi ya kununua Bitcoin Tanzania.

Kuna masoko maarufu ambayo mtu aweza kununua na kuuza sarafu za kidijitali kwa kutumia M-Pesa. Hayo ni pamoja na:

Paxful

Paxful ni duka maarufu ambalo mtu aweza moja kwa moja kununua fedha za kidijitali kwa kutumia M-Pesa nchini Kenya. Pindi ujisajilipo, waweza kununua au kubadilisha Bitcoin kwa kutumia M-Pesa. Lina mchakato rahisi na wa haraka wa kujiisajili. Ni sehemu nzuri zaidi ya biashara ya fedha za kidijitali, kwa vile ina sehemu ya huduma ya msaada kwa wateja na pia uwepo wa jumuiya ya watumiaji wa Bitcoin barani Afrika.

LocalBitcoins

LocalBitcoins ni eneo linaloshughulika na sarafu za kidijitali aina ya Bitcoin pekee. Unahitajika kujisajili kwanza na kuamilisha akaunti kwa kupitia kiungo kinachotumwa kwenye barua pepe yako ili kuanza. Ukimaliza hayo, waweza kuabiri na kutafuta nyasifu za wafanyabiashara ambao utafanya nao biashara.

Pursa

Pursa ni kati ya masoko ya kununua na kuuza bitcoin. Kwenya soko la Pursa, unaweza kununua na kuuza kwa kutumia njia mbalimbali za maliko ikiwemo M-Pesa.

LocalCryptos

LocalCryptos ni duka ambalo hapo nyuma lilikuwa likiitwa Localethereum. Kwenye eneo hili, waweza fanya biashara ya kununua na kuuza bitcoin kwa kutumia M-Pesa. Kwa bahati nzuri, kuna huduma ya utawala wa kifedha wa mtu wa tatu iitwayo escrow ambayo inatumika kuhakikisha fedha muuzaji wa bitcoin hatoweki na fedha zako baada ya kulipa.

Hitimisho Kuhusu Jinsi ya Kununua na Kuuza Bitcoin

Fedha za kidijitali ni tete. Inakubidi uzinunue baada ya utafiti yakinifu na kwa tahadhari. Kumbuka kutowekeza kiasi cha fedha usichopenda kukipoteza.