Wakati Bitcoin inaendelea kupata umaarufu barani Afrika, tunapenda kukusaidia kujua wapi unaweza kununua au kuuza Bitcoin ikiwa unaishi nchini Tanzania.

» Bitcoin ni fedha dijitali isiyosimamiwa na benki kuu au msimamizi mmoja ambayo inaweza kutumwa kutoka kwa mtumiaji mmoja hadi mwingine kwenye mtandao wa Bitcoin.
» Bitcoin ilianzishwa mnamo 2008 na mtu asiyejulikana au kikundi cha watu kwa kutumia jina la Satoshi Nakamoto na ilianza mnamo 2009.
» Bitcoins huundwa kama malipo kwa mchakato unaojulikana kama “uchimbaji wa Bitcoin”. Bitcoin huweza kubadilishwa kwa sarafu zingine, au kununua bidhaa na kulipia huduma.

Jinsi Bitcoin Inavyofanya Kazi

  • Bitcoin huhifadhiwa kwenye mkoba wa dijiti kwenye kompyuta au simujanja yako.
  • Unaweza pia kutumia mkoba wa kifaa au mkoba wa karatasi, ambayo ni kifunguo cha umma na kibinafsi kilichochapishwa kwenye karatasi.
  • Ununuzi wako wote huandikwa kwa wazi na kudumu daima kwenye daftari la hesabu la umma linaloitwa blockchain.

Unachohitaji Kabla ya Kununua au Kuuza Bitcoin

Kama ilivyoelezwa hapo juu, shughuli za Bitcoin zinahitaji mkoba wa Bitcoin. Ununuzi wako, hata hivyo, utafanyika katika soko la ubadilishaji wa Bitcoin, soko la dijiti ambalo wafanyabiashara wanaweza kununua na kuuza Bitcoin au kwenye soko ambalo ambapo mnunuzi hulipa moja kwa moja kwa muuzaji.

Kisha utahitaji fedha za kawaida (ikiwa unataka kununua) au Bitcoin (ikiwa unataka kuuza). Kama shughuli zingine za jadi za kifedha, lazima uchague njia yako ya malipo unayopendelea kama vile kadi ya benki, uhamishaji fedha kwa kutumia benki, Western Union, Moneygraph, Transferwise, kadi za zawadi, fedha taslimu, au kwa kutumia M-Pesa.

Grafu ikionyesha mabadilisho ya Bitcoin 1 na shilingi ya Tanzania, tazama kiwango cha kubadilisha cha sasa.

Vitu vya Kuzingatia Kabla ya Kununua au Kuuza Bitcoin

Unapotaka kununua au kuuza Bitcoin, unahitaji kuzingatia mambo kadhaa muhimu. Wakati wa kuchagua soko la Bitcoin, hakikisha unafanya bidii inayofaa ili kujua, kwa mfano, sifa yake katika tasnia ya Bitcoin, ni lini ilisajiliwa, ni nani watendaji wae, jiulize kama imekata bima, nk.

Sehemu nyingine muhimu ya habari unayohitaji kujua ni ada zao. Angalia ada zao za biashara, ada ya uondoaji wa Bitcoin toka kwenye akaunti, ada ya amana, nk. Zaidi ya hayo, ni vyema ujue kikomo cha kiwango cha Bitcoin unachoweza kununua au kuuza. Kiwango hutofautiana kati ya soko na soko.

Ikiwa unaamua kutumia soko linalowawezesha watu kununua na kuuziana Bitcoin moja kwa moja, unahitaji kuwa mwangalifu zaidi kwa sababu kwa chaguo hili utakuwa unafanya biashara yako na mtu usiyemjua. Tafuta ikiwa mtu huyo maelezo yake binafsi yamethibitishwa, jinsi gani anaaminika kwenye soko hilo, ikiwa amezuiliwa na baadhi watumiaji kwenye soko hilo, nk Ikiwa lazima ukutane naye ana kwa ana, chagua mahali pa umma na uombe rafiki au jamaa aende nawe.

Wakati wa kuchagua mkoba, unahitaji kuzingatia mambo kama usalama wake, ufikiaji wa funguo za kibinafsi, unganisho la moba na la programu ya simujanja, uwezo wa mkoba kuficha taarifa zake (ikiwa unataka kufanya biashara ya Bitcoin bila kujulikana) na masoko ambapo mkoba huo unaweza kutumika. Soko la kununua au kuuza Bitcoin utakalochagua linaweza pia kupendekeza mkoba wa kutumia.

Masoko ya Bitcoin hutoa njia tofauti za malipo. Chagua soko ambalo hutoa njia ya malipo ambayo ni rahisi na inapatikana kwako. Kumbuka kuwa muda wa kununua na kuuza Bitcoin hadi kukamilika utategemea njia ya malipo uliyochagua.

Bei ya Bitcoin inatofautiana ulimwenguni. Unahitaji kulinganisha viwango kutoka masoko makubwa ya Bitcoin na soko ulilochagua. Unaweza kutumia CoinDesk kufanya ulinganisho.

Masoko ya Kununua na Kuuza Bitcoin Nchini Tanzania

Kenya ni kiongozi katika tasnia ya Bitcoin katika Afrika Mashariki. Ikiwa na makao yake makuu jijini Nairobi, Kenya, BitPesa ni jukwaa la ubadilishanaji wa fedha za dijiti na malipo. Kampuni hii soko la Bitcoin la BFX.

KuBitx) ni soko la Bitcoin toka nchini Kenya. Mbali na kushughulika na Bitcoin na fedha zingine za dijiti, ina fedha yake yenyewe inayoitwa KubitCoin (KBX).

Ikiwa unataka kufanya biashara na soko la Bitcoin lililoko nchini Tanzania, basi unaweza kuchagua Cryptocurrency International Tanzania Limited (CITL), kampuni ya kibinafsi ya Kitanzania inayoshughulika na mifumo ya malipo ya kimataifa kupitia teknolojia ya fedha dijiti na teknolojia ya Blockchain.

Unaweza pia kuchagua kwenda na kampuni ya Shelisheli inayoitwa Remitano. Inatoa soko la Bitcoin ambalo watu hununua na kuuza Bitcoin nchini Tanzania.

Kwa kushirikiana na BitPesa, kampuni ya Bitbond inaruhusu watumiaji nchini Tanzania kubadilishana Bitcoin zao. Kampuni mpya katika soko la Bitcoin ni Totalcoin, kampuni ya ya Estonia inayofanya kazi katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki pamoja na Tanzania.

Ikiwa unakusudia kununua au kuuza moja kwa moja Bitcoin toka kwa muuzaji au mnuzuzi binafsi, unaweza kutumia LocalBitcoins).

Hitimisho

Wakati wa kuandika makala hii, Bitcoin 1 ililingana na shilingi 19,242,413.93 za kitanzania.
Tanzania haijazuia rasmi Bitcoin. Walakini, benki kuu haidhibiti shughuli za fedha dijiti kama Bitcoin.