Sarafu za kidijitali zimekuwa mojawapo ya kikundi bora cha mali imara mwaka huu. Huku Bitcoin ikionyesha ongezeko la thamani kwa zaidi ya asilimia 100, fahirisi kuu nyinginezo ziliashiria ongezeko kwa chini ya asilimia 20.
Kutokana na mabadiliko haya, pamezuka upya hamu kuhusu sarafu hizi miongoni mwa watu kote duniani. Matukio yanayohusiana na sarafu za kidijitali yameendelea kuwavutia watu wengi na hata kuongezeka kwa maneno yanayosakurwa kwenye Google yanayohusiana na kutengeneza pesa kupitia shughuli ya sarafu za kidijitali.
Matumaini haya yamesababisha wachambuzi wengi kutabiri kwamba kusisimka kwa bei ya Bitcoin kumeanza. Mwaanzilishi mashuhuri wa usalama wa kimtandao, John McAfee ametabiri kwamba bei ya Bitcoin inaweza kufikia dola milioni 1 kufikia mwaka 2020. Lakini McAfee amekiri katika hafla za awali kwamba anapenda kuibua matendo yenye umaarufu tu.
Wakati huo huo, watu wengi wanazidi kupoteza fedha kila siku kwa njia ya ulaghai wa sarafu za kidijitali. Katika makala haya, tutaangazia 5 kati ya ulaghai wa sarafu za kidijitali na jinsi ya kuuepuka.
Ulaghai wa OneCoin
- Ulaghai wa OneCoin ni mojawapo ya ulaghai mkubwa wa sarafu za kidijitali katika historia.
- Mwanzilishi wa OneCoin, Ruja Ignatova, alitoweka mwaka wa 2017 wakati kibali cha siri cha Marekani kilifunguliwa kwa kukamatwa kwake.
- Waendesha mashtaka wa Marekani wamedai kuwa ulaghai huo uliwapatia watapeli takriban dola bilioni 4 duniani.
Yaliyomo
1. Utoaji Awali wa Sarafu (Initial Coin Offerings)
Utoaji Awali wa Sarafu (ICOs) ni njia ambayo kampuni nyingi za blockchain hutumia ili kuchanga fedha. Ni mbinu iliyoundwa kuakisi Utoaji wa Awali wa Umma (IPO) kwa mujibu wa soko la hisa. Tofauti na IPOs, ICOs haina udhibiti na huendeshwa kimataifa. Pia, kampuni zinazohusika katika ICOs hazitakiwi kutoa maelezo yoyote ya mapato yao na hali yake ya kibiashara. Nyingi ya kammpuni hizi pia hazina maelezo haya.
Katika miaka michache iliyopita, wawekezaji wameweka takriban dola bilioni 10 kwa ICOs. Katika 2017, Block.one iliweza kuchangisha zaidi ya dola bilioni 4 kutoka kwa wawekezaji. Hii ni robo ya kiasi ambacho Alibaba walizalisha kutokana na IPO yake katika 2014. Telegram, program maarufu ya ujumbe, iliweza kuchangisha zaidi ya dola bilioni 1.7 katika ICO.
Kwa bahati mbaya, watu wengi waliowekeza fedha zao katika baadhi ya ICOs walipoteza fedha hizo. Isitoshe, hivi karibuni kampuni ya Block.one ililazimishwa kutatua maswala na Tume ya Kudhibiti Ubadilishanaji wa Hisa ya Marekani (SEC) kwa kufanya kushiriki mauzo ya hisa bila udhibiti.
Sababu inayofanya ICOs kuwa ulaghai ni kwamba hatua za kuzindua huwa rahisi sana. Mtu yeyote anaweza kutumia vielelezo vingi vya ICO ambavyo vinapatikana mtandaoni na kuwadanganya watu. Kwa sababu hii, mwaka 2017, kampuni iitwayo Useless Coin iliweza kupokea zaidi ya dola elfu 54 kutoka kwa wawekezaji. Katika tovuti yake, kampuni hii ilikuwa iliwaambia wawekezaji kwamba ingetumia mapato hayo “kununua vitu fulani.”
Ili kujikinga na ulaghai wa ICO, tunapendekeza kwamba usijihusishe kabisa na shughuli kama hizo. Puuza mitandao inayoonekana kuvutia, timu ya watu wanaoonekana wema kwenye wavuti wao, na bidhaa bandia wanazouza.
2. Hazina ya Uwekezaji wa Kidijitali
Katika sekta ya jadi ya fedha, mameneja wa uwekezaji wanatakiwa kuwa wamedhibitiwa. Huko Marekani, kila meneja wa hazina lazima awe ameidhinishwa na Tume ya Kudhibiti Ubadilishanaji wa Hisa. Sheria hii husaidia kuweka sekta ya fedha salama kwa kuwazuia wasimamizi laghai kuhusika.
Kama sekta ya kimataifa, sarafu za kidijitali hazionekani kuzingatia kanuni hizi. Hawazingatii kanuni kwani tofauti na sarafu nyinginezo, sarafu za kidijitali haziwezi kugunduliwa na wadhibiti wa kifedha. Kwa sababu hiyo, Wamarekani wengi hupoteza fedha nyingi kwa kuwekeza kupitia mameneja wajanja wa kifedha ambao huahadi mapato makubwa.
Mfano mzuri wa jambo hili ni BitConnect, ambayo ilikuwa imetuhumiwa kuwa mradi wa ponzi. Katika upeo wake, kampuni hiyo ilikadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 2.6. Wawekezaji walikuwa wameahidiwa mapato ya asilimia 40 kila mwezi. Hii ilimaanisha kuwa wawekezaji wa mapema ambao wangewekeza dola 1000 wangetarajia kuwa mamilionea katika kipindi cha miaka mitatu. Kampuni hii ilifungwa mwaka wa 2018.
Ili uweze kujikinga, jiepushe na mikataba ya sarafu hizi inayoonekana kuwa na uhalisia wa kupindukia. Pia, inakupasa kuepuka kuwekeza katika kampuni za kigeni ambazo hazipo katika mamlaka ya wadhibiti wa Marekani.
3. Ulaghai wa Ubadilishanaji wa Sarafu
Kuna mamia ya masoko ya ubadilishanaji saarafu za kidijitali duniani. Umaarufu wa kubadilishana huko kumeongezeka kwa sababu ya jinsi ilivyo rahisi kuzindua ubadilishana. Inawezekana kuzindua ukumbi wa kubadilisha unaovutia kwa chini ya dola 1,000. Mapema mwaka huu, iliripotiwa kuwa mojawapo ya kumbi za ubadilishanaji za sarafu za kidijitali kule Canada ilifungwa baada mwanzilishi wake kufa na nywila. Wakati huo huo, mabilioni ya dola za thamani ya sarafu hizi zimeibiwa kupitia wizi wa kidijitali. Baadhi ya wizi huo hufanyika kwa ushirikiano na wafanyakazi wa ndani.
Kwa mfano, SEC ilifunga 1Broker, kampuni ya kubadilishana kisiwani Marshal iliyokuwa imesajiliwa. SEC na wadhibiti wengine wa kimataifa wameweza kufunga kampuni nyingi za ubadilishanaji na wahusika wake.
Ili uwe salama, tunapendekeza kwamba uweze kuchukua muda na kutafiti kuhusu kampuni hiyo ya ubadilishanaji kabla ya kuwekeza fedha yako. Pia, tunapendekeza kwamba ujihusishe na wabadilishanaji wakubwa wa Marekani kama Coinbase na Kraken. Wabadilishanaji kama hawa wanadhaminiwa na wawekezaji wa kuaminika na pia wanafuatiliwa kwa karibu na kudhibitiwa.
Kuna aina mbili ya masoko ya ubadilishaji ya Bitcoin – zile ambayo tayari zimevamiwa na zile zinazoelekea kuvamiwa.
Usihifadhi Bitcoin yako kwenye sehemu za ubadilishanaji. Kamwe! Hihifadhi tu fedha ambazo unakusudia kutumia kwa biashara. Kama huna udhibiti kwa funguo binafsi za mkoba wako wa Bitcoin, basi hiyo si Bitcoin yako.
4. Utapeli wa Data
Utapeli wa data ni aina ya hadaa amayo imeenea. Ni aina hiyo ya udanganyifu ambayo ilipelekea kutolewa kwa maelfu ya barua pepe kutoka kwa John Podesta, mshauri wa kisiasa wa Marekani, mwaka wa 2016 uchaguzi.
Utapeli wa data hujiri wakati unapokea ujumbe wa barua pepe wenye kiungo. Ujumbe huo huundwa ili uakisi ule wa huduma maarufu kama Google na Amazon. Wakati ukifuata kiungo, utaweza kuulizwa kubadili nywila yako au kutoa maelezo zaidi ya binafsi. Kwa kufanya hivyo, wadanganyifu hawa huwa wanafuatilia na kuiba taarifa zako, ambazo wao huuza kwa ajili ya sarafu za kidijitali.
Ili uwe salama, tunapendekeza kwamba uweze kufikiria mara mbili kabla ya kubonyeza kiungo unachopata katika ujumbe wa barua pepe yako. Ikiwa barua pepe imetoka Google au Amazon, thibitisha kuwa ni kweli imetoka kwa kampuni hiyo. Vilevile, tunapendekeza kwamba kamwe usifichue habari zako za binafsi kwa mtu yeyote.
5. Ulaghai wa Kuchimba Mawinguni (Cloud Mining)
Kusanidi Bitcoin kunahitaji vifaa ghali. Vifaa vipya vya bei vya kusanidi kutoka Bitmain, kwa mfano, hugharimu zaidi ya dola 250. Vifaa ghali vya uchimbaji huuzwa kwa zaidi ya dola 10,000. Kwa kuwa watu wengi hawana uwezo wa kununua mashine hizo, wao kutegemea kampuni zinazotoa huduma hizi mawinguni kidijitali. Wao huishia kulipa kampuni hizi ada na kubadilishiwa kwa Bitcoins. Licha ya kuwepo kwa baadhi ya kampuni za kweli za uchimbaji mawinguni, nyingi kati yazo hufanya hivyo kinyume cha sheria au ni kampuni za ulaghai.
Tunapendekeza kwamba uepuka kuzitumia kampuni za uchimbaji mawinguni. Kama ni lazima, tunapendekeza kwamba utumie kampuni za uchimbaji mawinguni za Marekani. Pia, hakikisha kwamba kampuni hizi zimesajiliwa na zimedhibitiwa na mdhibiti wa kuaminika.
Mawazo ya Mwisho
Ulaghai unaohusiana na sarafu za kidijitali ulipungua mwaka 2018 wakati bei ya sarafu hizo za kidijitali ilikuwa imedidimia. Mwaka huu, ulaghai umerejea tena kwani bei ya sarafu za kidijitali imekuwa ikiimarika. Cha kusikitisha ni kuwa bado watu wengi wanapoteza fedha nyingi kupitia mifumo hii. Tunapendekeza kwamba uweze kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya ulaghai unaohusiana na ulaghai wa sarafu za kidijitali.