Taarifa 21 za Kufurahisha Upaswazo Kuzijua Kuhusu Bitcoin

Tafsiri:
en_US

Sarafu mtandao iliyokasimiwa madaraka Bitcoin, ina habari nyingi za kuvutia na kufurahisha. Tumechagua habari 21 za kufurahisha ambazo wapaswa kuzijua.

1. Nimehamia Kwenye Mambo Mengine

Nani aliiumba Bitcoin? Hili yawezekana ni fumbo kubwa zaidi kuliko yote katika kipindi cha kidijitali. Mtu atumiaye jina Satoshi Nakamoto, aliunda Bitcoin mwaka 2008. Kisha mwaka 2010. Satoshi akatoweka . Mara ya mwisho Satoshi kusikika ni mwaka 2011 pale alipotuma barua pepe akisema “nimehamia kwenye mambo mengine”.

Hakuna mtu aliyewahi kumuona kwa macho, kuisikia sauti yake au kuiona picha yake. Bitcoins zake ambazo sasa zimefikia thamani ya dola bilioni 19.4, hazijaguswa tangu ‘ahamie kwenye mambo mengine’. Mwaka 2017, Satoshi alikuwa ni mtu wa 44 tajiri zaidi duniani.

Mada kuhusu Bitcoin iliyochapishwa na Satoshi Nakamoto mwaka 2008.

2. Anayedhaniwa Kuwa Satoshi Nakamoto

Msako wa utambulisho halisi wa Satoshi Nakamoto umeendelea kwa miaka mingi. Baadhi ya watu katika jamii ya Bitcoin ambao wanedhaniwa kuwa Satoshi Nakamoto ni pamoja na Adam Black, Nick Szabo, Wei Dai, Dorian Nakamoto and Hal Finney.

Mwezi Aprili mwaka huu, mvumbuzi wa programu za tarakilishi na mfanyabiashara John McAfee alidai kwamba anamfahamu Satoshi Nakamoto na kwamba ameongea naye. Japo sio watu wengi wanaochukulia kwa uzito dai hili.

3. Bitcoin “Inachimbwa” Lakini Sio Kama Dhahabu

Bitcoin inaumbwa kwa “kuchimbwa” kwa kutumia teknolojia ya Blockchain. Kwa kupitia uchimbaji, miamala ya Bitcoin inahalalishwa. Baada ya hapo tarakilishi kwenye mtandao hupambana kutatua milinganyo migumu ya kihesabati. Tarakilishi inayowezesha kutatua milinganyo, inazawadiwa Bitcoin mpya zilizoundwa. .

4. Mashine Za Kutolea Bitcoin Barani Afrika

Katika Bara ambalo nchi kama Elitrea haina mashine za kutolea hela wakati Somalia ilifungua mashine ya kwanza ya kutolea hela mwaka 2014, inafurahisha kuona kwamba kuna mashine kumi za kutolea Bitcoins katika Afrika ambazo ziko Kenya Nigeria, Afrika Kusini, Uganda, Zimbabwe, Botswana na Djibouti.

5. Tukio La Kuongezeka kwa Thamani na kuumbwa Bila Kutarajiwa Kwa Bitcoins Bilioni 184

Mwaka 2010, pasi kusudiwa, kirusi kiliunda Bitcoins bilioni 184. Kosa hilo lilisababishwa na msimbo unaotumika kuangalia miamala inayozalishwa. Kirusi hicho kinajulikana kama ‘tukio la kuongezeka kwa thamani’.

6. Idadi ya Juu ya Bitcoins ni Milioni 21

Kuna Bitcoin milioni 21 tu kwa ujumla ambazo zaweza ‘kuchimbwa’. Hii ni kwa sababu itifaki ya Bitcoin inafafanua kuwa ijara ya kuongeza ‘block’, itagawanywa mara mbili kwa kila ‘block’ 210,000, takribani kila miaka minne. Kima cha mwisho cha Bitcoin milioni 21 kitafikiwa mwaka 2140, rekodi ya utunzaji itazawadiwa kwa adaya miamala.

7. Mnufaika Wa Kwanza Wa Bitcoin

Hal Finney alikuwa ni mnufaika wa kwanza wa muamala wa kwanza wa Bitcoin mwezi Januari mwaka 2009. Utajiri wake mkubwa kutoka Bitcoin unalipia mwili wake uliohifadhiwa kwa matarajio ya kufufuka. Alifariki mwaka 2014 kutokana na maradhi yatokanayo na misuli kushindwa kufanya kazi (ALS).

8. ‘Uchimbaji’ Wa Bitcoins Unatumia Umeme Linganishi kwa Australia

Kutokana na Digiconomist, Bitcoin kwa sasa inatumia terawati 73.12 kwa saa kwa mwaka. Hii ni kulinganisha na matumizi yote ya nishati ya Australia, nchi yenye watu milioni ishirini na tano. Sababu ya kutumia kiasi kikubwa hivyo cha raslimali nishati ni kwamba wachimbaji wanatumia nguvu ya kukokotoa ili kuhalalisha miamala ya data na kutatua mafumbo magumu ya hisabati kwenye blockchain.

Chanzo: digiconomist.net

9. Chuo Kikuu Cha Kwanza Kukubali Bitcoin

Chuo kikuu cha Nikosia nchini Cyprus, ni chuo kikuu cha kwanza duniani kuzikubali Bitcoin kwa malipo ya ada ya taaluma. Shule ya biashara na ubunifu ya Red and Yellow ni chuo cha kwanza barani Afrika kukubali Bitcoin kuwa malipo kwa stashahada, cheti na kozi za mtandaoni.

10. Jenga Na Bitcoin

Mwaka huu, Paxful, soko la sarafu za kidijitali, ilijenga shule ya pili nchini Rwanda kama sehemu ya mpango wa #BuildWithBitcoin. Paxful inakusudia kujenga shule 100 barani Afrka. Mpango wa #BuildWithBitcoin umekusanya zaidi ya dola laki moja za Bitcoin na kwenye sarafu nyingine za kidijitali ili kusaidia ujenzi.

11. Muamala wa Kwanza Wa Bitcoin Kurekodiwa ulikuwa ni wa Ununuzi Wa Piza

Tarehe 22 Mei mwaka 2010, Laszlo Hanyecz alifanya muamala wa kwanza halisi duniani kwa kununua piza mbili katika mji wa Jacksonville, Florida kwa Bitcoin 10,000. Kiasi hicho kingeweza kuwa karibu ya dola 750,000 za Kimarekani kwa mwaka 2013. Alituma Bitcoin kwa mfanyakazi wa kujitolea nchini Uingereza ambaye alitumia dola 25 kumuagizia Hanyecz piza toka mgahawa wa Papa John’s pizzas.

Laszlo Hanyecz aliweka picha hii ya piza mtandaoni kama ushahidi wa muamala huo.

12. Muamala Mkubwa Zaidi wa Bitcoin Kufanywa

Muamala mkubwa zaidi kufanywa umefanyika mwaka huu ukihusisha sarafu za kidijitali zenye thamani ya dola bilioni moja. Wachambuzi wa sarafu za kidijitali wameshindwa kubaini mtu au kundi lililohusika kwenye muamala huo.

13. Kuishikilia Bitcoin Kwa Miaka Mitatu Na kuiuza Kwa Faida:

Kufikia sasa, kwenye historia ya Bitcoin hakujawa na muda ambapo ungeweza kuinunua na kuiuza baada ya miaka mitatu na kutoweza kuiuza kwa faida. Katika kipindi cha miaka mitatu, faida zitakuwa kubwa.

14. Bitcoin Kwa Malipo Ya Taarifa Zilizodukuliwa (Ransomware)

Makampuni nchini Marekani yananunua Bitcoin ili kujiandaa kwa malipo ya taarifa au habari zilizodukuliwa (hacked). Wadukuzi wengi huhitaji fidia kwa malipo ya Bitcoin.
.

15. Ukipoteza Ufunguo Wako Binafsi Wa Bitcoin, Unapoteza Bitcoins Zako Zote

James Howells alipoteza Bitcoin 7,500 mwezi Novemba mwaka 2013. Alikitupa kiendeshi kikuu (hard disk) chake kilichokuwa na funguo (passcode) zake binafsi wakati akisafisha nyumba yake. Bitcoin 7,500 ni sawa na dola milioni 56 za Kimarekani. Inakisiwa kuwa karibu asilimia ishirini na tano ya Bitcoin zote tayari zimeshapotea.

16. Satelaiti ya Blockstream Inaitangaza Bitcoin Blockchain kwa Ulimwengu Wote kwa Kupitia Setalaiti

Mtandao wa setalaiti ya Blockstream unaitangaza bure Bitcoin blockchain ulimwenguni kote kwa siku na muda wote wa wiki, ili kuzuia kukatika kwa matangazo na kumpa fursa mtu yeyote duniani kuitumia bitcoin.

Mtandao wa satelaiti ya Blockstream.

17. Wapi Bitcoin ni Haramu?

Bitcoin imepigwa marufuku kwa sasa nchini Namibia, China, Kyrgyzstan, Bolivia, Vietnam, Ecuador, Bangladesh na Kolombia.

18. Watu Maarufu Wanaoihusudu Bitcoin

Bitcoin imehusudiwa na watu wenye sifa kubwa kwenye biashara, burudani na michezo duniani kama vile Gwyneth Paltrow, Paris Hilton, Snoop Dogg, Ashton Kutcher, Hugh Laurie, Mike Tyson, na Pitbull.

19. Bitcoin ni Miongoni Mwa Bidhaa za Kifedha Zinazofanya Vizuri Zaidi

Thamani ya Bitcoin imepanda zaidi ya asilimia elfu mbili katika miaka mitano iliyopita. Ufanisi wake ni mzuri zaidi kuliko faida iliyopatikana kwenye hisa na dhahabu.

Bitcoin vs Stocks

20. Bitcoin Itagota Dola Milioni Moja Mwaka 2020

John McAfee anabashiri kuwa kila kipande cha Bitcoin kitakuwa na thamani ya dola milioni moja kufikia mwishoni mwa mwaka 2020. Anasema “kimahesabu, ni vigumu kwa Bitcoin moja kuwa chini ya dola milioni moja mwishoni mwa mwaka 2020”. Lakini McAfee amewahi kukiri hapo awali kuwa anapenda kuustaajabisha umma.

21. Shimo la Sungura ni Refu Sana

Yapo mengi ya kujifunza kuhusu Bitcoin: kifedha, uchumi, siasa, historia, kihisabati, usalama wa habari na mengine. Kama taarifa hizi za kufurahisha, zinakufanya kutaka kujifunza zaidi, tembelea Bitcoin-resources.com.