Kazi za Mtandaoni Zinazolipa

Tafsiri:
amen_US

Kazi za kwenye intaneti (online jobs) ni fursa nzuri ya kujipatia mapato na kukuza ujuzi wako katika uchumi wa kidijitali. Kuna kazi nyingi za mtandaoni kwa nchi za Kiafrika kwa wanaofanya kazi wakati wote (full-time) na wale wa muda (part-time). Leo tutaangalia kazi za kufanya mtandaoni zinazolipa.

Soma makala haya kwa Kiingereza: Online jobs that pay in Africa

Kuhusu Kazi za Kulipwa Mtandaoni

Zifuatazo ni baadhi ya kazi za online ambazo unaweza kuzianzisha.

Uuzaji kwa ushirikishi (Affiliate Marketing)

‘Affiliate marketing’ au uuzaji wa ushirikishi ni mbinu maarufu ya kujipatia riziki kwa wanablogu wengi na ‘influencers’ (washawishi wa mitandao ya kijamii). Kupitia uuzaji huu, huduma au bidhaa zinazouzwa na maduka ya mfumo wa kielektroniki (ecommerce) zinatambulishwa na hawa bloggers na influencers ambao hulipwa kila wanapofanikisha mauzo yoyote. Unaweza kuanzisha blogu na kutolea maoni baadhi ya bidhaa unazozifahamisha kwenye tovuti yako. Baadhi ya programu za mauzo kwa njia hii ni pamoja na Amazon, Jumia na Fiverr.

Ufanyakazi huria (Freelancing)

Ufanya kazi huria ni miongoni mwa kazi maarufu sana za online barani Afrika. Ni njia nzuri ya kujipatia riziki Afrika. Hufanya kazi huria ni neno linalotumiwa kuwarejelea watu waliojitegemea kikazi bila kujihusisha na mwajiri maalum wa muda mrefu. Ili kuanzisha shughuli za ufanyakazi huria Afrika, unahitaji kufungua akaunti kwenye ulingo wa ufanyakazi huria ili uweze kujiunga na freelancers wengine wengi wa Afrika.

Ulingo wa ufanyakazi huria kama vile Upwork huleta pamoja vipaji na waajiri. Ikiwa una ujuzi kama wa kutafiti au kuhariri; unaweza kuuuza kupitia majukwaa haya. Unahitaji kuandika pendekezo la kuvutia zaidi na kuwatumia waajiri watarajiwa. Ikiwa mwajiri atapendezwa na pendekezo lako, basi atakushirikisha kuifanya kazi hiyo. Kisha, unahitaji kukamilisha na kuwasilisha kazi hiyo ili uweze kupokea malipo. Waajiri hulipa tu iwapo kazi imefanywa kwa kiwango cha kuridhisha.

Jiunge na Ajira Digital Kenya. The Ajira Digital Program ni mpango wa serikali nchini Kenya unaoendeshwa na Wizara ya ICT, Ubunifu na Vijana wene nia ya kuwawezesha zaidi ya vijana milioni moja kupata fursa za kazi za kidijital

YouTube

Unaweza kujichumia mapato kwa kuandaa maudhui (content) na kuziweka YouTube. Kisha unahitaji kutayarisha na kuzipakia video hizo zenye ujumbe na maswala ya thamani ambayo yanavutia watazamaji kwenye chaneli yako ya YouTube. Unaweza kujipatia malipo kwa kuweka matangazo au hata kwa kutoa huduma na kuuza bidhaa hapo YouTube. Watu wengi hupokea pesa kutoka YouTube kupitia matangazo.

Uza Bidhaa (Drop Shipping na Ecommerce)

Unaweza kupata mapato mtandaoni barani Afrika kwa kuuza bidhaa na kutoa huduma kupitia biashara mtandaoni na ‘drop shipping.’ Dropshipping ni njia nzuri ya kupata riziki kwa njia ya rejareja bila kuwa na bidhaa zinazouzwa. Mfumo huu unahusisha ununuzi wa bidhaa kutoka kwa watu wengineo ambao kisha huwasafirishia moja kwa moja waununuaji. Wewe kama mmiliki wa duka hutajishughulisha na bidhaa, lakini utakuwa unazitambulisha na kuuza kwa niaba ya (supplier) wasambazaji. Wakati mteja ananunua, utapeleka agizo la ununuzi (order) kwa muuzaji. Msambazaji huyo atapeleka bidhaa kwa mteja huyo moja kwa moja. Unaweza kutumia mifumo kama vile Shopify katika biashara ya aina hii.

Kutafsiri

Unaweza kujipatia pesa mtandaoni kwa kutafsiri makala, machapisho ya blogu, maelezo ya bidhaa, na kadhalika. Unahitaji tu kuwa na ugwiji katika lugha ya asilia (ya ujumbe) na lugha unayolenga kutolea tafsiri. Tafsiri ni sekta yenye ushindani mkubwa sana, kwa hiyo unahitaji kuwa na subira na ukakamavu. Baadhi ya mitandao ambapo unaweza kufanya kazi ya online translation ni:

Mbali na tovuti hizi za kutafsiri zilizotajwa hapo juu, unaweza pia kutafuta kazi za kufanyia tafsiri kwenye website zinazolipa kama vile Upwork, Fivver, Guru, PeoplePerHour na Freelancer.

Uandishi wa blogu (Blogging)

Tovuti na blogu ni njia nzuri ya kujipatia mapato kwa kuwapa watu habari muhimu. Blogging ni miongoni mwa kazi za mtandaoni ambazo zina fursa nyingi. Ili kuanzisha blogu, unahitaji kutaitambua mada ambayo unaweza kuiblogu kuhusu. Ni bora kwamba ujitafutie kitengo na mada ambayo unapenda sana. Kwa mfano, inaweza kuwa kuhusu fedha, afya, bima, kazi na hata jinsi ya kujijenga mwili na umbo (fitness).

Kwa kutumia blogu, unaweza kupata mapato kupitia affiliate marketing, kwa kuweka matangazo kwenye tovuti yako, au kwa kuuza bidhaa na kutoa huduma. Baadhi ya kampuni za matangazo ambazo unaweza kutumia ni pamoja na Google AdSense na MediaVine. Unaweza kuunda tovuti kwa kutumia:

  • WordPress
  • Blogger
  • Medium
  • Wix

Uuzaji kupitia Facebook

Facebook ni sehemu mojawapo nzuri ya kuuza bidhaa na huduma. Facebook ni mtandao wa kijamii ambako wengi wa Waafrika wamejiunga. Ili uweze kuanza kuuza kwenye Facebook, unahitaji kuunda profile yako ya Facebook halafu utoe maelezo ya bidhaa au huduma unazouza. Unaweza kujiunga na Facebook groups ambapo unaweza kuchapisha picha za bidhaa zako za na kama watu watazipenda, watawasiliana nawe ili waweze kuzinunua. Baadhi ya bidhaa ambazo unaweza kuuza kwenye Facebook ni pamoja na nguo, viatu, samani, magari na vifaa vya kielektroniki.

Mauzo ya Kidijitali

Biashara nyingi na makampuni yanatumia ‘digital marketing’ kwa sababu zinalenga wateja na ni za gharama nafuu ikilinganishwa na njia za zamani za kuendesha mauzo.

Baadhi ya mikakati ya kufanya mauzo kidijitali ni pamoja na Search Engine Optimization (SEO), Search Engine Marketing (SEM), kuuza kupitia mitandao ya kijamii, kuwatumia influencer kuuza bidhaa, uuzaji kupitia barua pepe na matangazo ya mtandaoni kupitia Google au Facebook.

Ajira kupitia Uandishi

Ikiwa unapenda kuandika au una ujuzi huo wa kuandika, unaweza kujipatia pesa  kupitia uandishi wa mtandaoni (online writing). Unaweza kuandika makala kwa ajili ya vyombo vya habari au kwa kushiriki katika uandishi wa kiubunifu au kuandika makala ya kiakademia (essay writing). Unaweza pia kuandikia websites ambazo zinafanyia bidhaa maoni (reviews). Unachohitaji ni kuchagua kitengo ambacho unataka kuandika na kisha umtafute mwajiri. Unaweza kuwapata waajiri wanatafuata waandishi kupitia tovuti za kazi mtandaoni. Unaweza pia kutuma sampuli za kazi yako kwa wachapishaji kama vile kampuni za habari na iwapo wataipenda kazi yako, watakuajiri kama mwandishi wa habari mtandaoni.

Kazi ya Umbali (Remote Working)

Unaweza kufanya kazi bila kutoka nyumbani au popote ulipo kwa muda mfupi au wakati wote huku ukijipatia riziki. Kutokana na kuzuka kwa covid-19, kampuni nyingi zinawashauri wafanyakazi wao kufanya kazi kwa mbali. Unahitaji tu kuwa na kompyuta, simu na intaneti sawa. Hii itakuwezesha kufanya kazi kutoka mahali popote na kisha uwasilishe kazi hiyo mtandaoni kwa malipo.

Baadhi ya maeneo ambapo unaweza kupata kazi za umbali (website zinazolipa) ni pamoja na:

Pata maelezo zaidi kuhusu kazi za mtandaoni kwa Waafrika

Tulizoziorodhesha hapo juu ni baadhi ya kazi za kufanya mtandaoni. Kazi ya mtandaoni Tanzania, Kenya na nchi nyingine ni mbinu rahisi ya kujipatia pesa kwa kuwa unaweza kufanya kazi ukiwa tu  nyumbani mwako na kuiwasilisha kazi hiyo ili uyapokee malipo. Unaweza kufanya kazi mtandaoni wakati wote au kwa muda mfupi tu kwa siku. Isitoshe, unaweza pia kuiwekea ratiba ya kazi hizi za online kwa kutegemea wakati unaofaa zaidi hasa ikiwa umejiriwa tayari. Hii ina maana kuwa unaweza kufanya kazi za mtandaoni hata bila kuacha au kujiuzulu kazi yako nyingine.