Pata Kazi Mtandaoni

Tafsiri:
en_US

Mojawapo ya changamoto kubwa zinazokabili mataifa ya Afrika ni ukosefu wa ajira, hasa miongoni mwa vijana. Ni kwa sababu hii ndio maana Waafrika wamechangamkia ufanyakazi huria (gig economy) ili kupata kazi na kupata mapato.

Kulingana na utafiti wa 2018 wa Payoneer wa Mapato ya Wafanyakazi Huria, Afrika inachangia asilimia 10.1 ya soko la ufanyakazi huria duniani kote. Takwimu za Rockefeller Foundation zinaonyesha kuwa soko hili liliingizia bara la Afrika dola bilioni 5 kufikia 2016.

Hebu tuangalie baadhi ya mitandao ya Kimataifa na ya Kiafrika inayohusisha ufanyakazi huria na jinsi ya kujiunga na kutuma maombi ya kazi.

Ulingo wa Kiafrika

Kuhustle

Kuhustle ni jamii ya kimtandao ya wafanyakazi huria nchini Kenya inayounganisha biashara na wafanyakazi huria wenye ujuzi Afrika ambao wananuia kufanya kazi ya hali ya juu. Mifano ya makundi ya kazi ambazo zinapatikana kwenye ulingo huu ni maendeleo ya programu, utoaji wa mafunzo, mauzo, usanii na ubunifu.

Inavyofanya Kazi

Kuanza kazi katika Kuhustle ni rahisi, bonyeza “Start Working” ili kujisajili.

Kwa Wateja

 1. Lazima ujiunge kwa kutumia Gmail, Twitter au Facebook ili uweze kutumia Kuhustle.
 2. Bonyeza sehemu ya maelezo yako binafsi na uyajaze. Maelezo yako yanahusisha sehemu za lazima yaani ujuzi, tajiriba na habari za kibinafsi. Habari hizi za kibinafsi hukutambulisha kwa kutoa utangulizi kukuhusu.
 3. Bonyeza “Post a job” kwenye tovuti na utoe maelezo na mahitaji mahsusi ya kile unachotaka kufanyika na unachonuia kupata.
 4. Wateja wenye kampuni zinazotafuta wafanyakazi wanaweza kufanya kazi pamoja na meneja wa bidhaa wa Kuhustle ili kuweza kuchangia mawazo na pia kupata nafasi ya kuteua timu ya kufanya kazi nayo.

Kwa Washauri

 1. Lazima ujiunge kwa kutumia Gmail, Twitter au Facebook ili uweze kutumia Kuhustle.
 2. Bonyeza sehemu ya kuhusu maelezo yako binafsi na uyajaze. Maelezo yako yanahusisha sehemu za lazima yaani ujuzi, tajiriba na habari za kibinafsi. Habari hizi za kibinafsi hukutambulisha kwa kutoa utangulizi kukuhusu.
 3. Nunua muamana wa Kuhustle ambao unahitaji wakati wa kuwasilisha kidondoa (tazama Uzabuni mdogo). Wafanyakazi huria wanaweza kununua miamana 3 kwa $3 au miamana 12 kwa $10, au miamana 24 kwa $20. Miamana haina muda wa kuharibika ila haiwezi kubadilishwa kwa fedha taslimu.
 4. Tafuta ajira ambayo inafaa ujuzi wako na kuwasilisha kidondoa.
 5. Iwapo itakuwia vigumu kuwasilisha bei yako, unaweza kuwaandika Kuhustle ili waweze kukuongoza katika shughuli hii.
 6. Wakati kazi mpya inabandikwa ambayo inahitaji ujuzi unaolingana na wako, utajulishwa kupitia barua pepe.

Njia ya Malipo


– Nchini Kenya, Kuhustle hutumia M-Pesa na malipo ya kadi (Visa na Mastercard).
– Katika nchi nyinginezo, Kuhustle hutumia tu kadi ya malipo (Visa na Mastercard).

Uzabuni mdogo

Kuhusutle hutumia hatua za zabuni ili kuhakikisha ubora wa zabuni hizo. Baadhi ya faida ya kutumia mbinu ya kuzabuni ni:
1. Huweka mipaka ya zabuni hadi 5: Wateja wanaweza kupata zabuni stahilifu 5 tu ambazo ni rahisi kukagua.
2. Hubadili maombi ya zabuni kuwa uzabuni mdogo: ili kuongeza ubora wa zabuni kutoka wafanyakazi huria, Kuhustle hutoza ada ndogo ya kuzabuni ya miamana 3 ($ 3) kwa kila ombi la zabuni. Hii ni kuhakikisha kwamba wafanyakazi huria wanatia makini maombi ya wateja na kuchukua muda kuangazia mapendekezo yenye thamani kwa mujibu wa muda na juhudi za mteja.
3. Huwakinga wafanyakazi huria: Baadhi ya wateja hutaka tu kujua gharama au wakati mwingine hubadilisha mawazo yao. Ili kutatua tatizo hili, Kuhustle inaruhusu mteja kuchapisha kazi mbili tu (kuchapisha kazi kupitia Kuhustle ni bure), kama wateja watachapisha kazi zaidi ya 2 bila kuajiri mfanyakazi huria yaani wakitupilia mabali kazi hiyo au kumalizika (baada ya siku 30), mteja atatakiwa kulipa $15 kabla ya kuchapisha kazi yoyote mpya katika siku zijazo.

Ajira ya kudumu

Ikiwa mteja anataka kuajiri wafanyakazi huria wa kudumu, Kuhustle itakuuganisha na watu binafsi kutoka kwa kundi la wataalam waliokaguliwa ili waweze kujiunga na timu yako.


 

Onesha

Onesha ni ulingo wa Kiafrika unaotilia makini kuwaunganisha wateja kutafuta huduma za ubunifu na wataalamu katika sekta ya ubunifu. Onesha huwahusisha wafanyakazi huria wa Kiafrika waliokaguliwa na wakapangwa kwa mujibu wa vipaji vyao.

Makundi maarufu ya ajira kwenye Onesha ni pamoja na sanaa na ufundi, maendeleo ya mtandao na simu, filamu na usanii wa uhaishaji, urembo na upodozi, biashara na matangazo, upigaji picha na uanamitindo.

Inavyofanya kazi

Kwa wateja

 1. Baada ya kujisajili, unaweza kuomba kazi kutumia Kielelezo hiki cha Kuomba kazi au kwa kuwasiliana na Onesha moja kwa moja ili kupata usaidizi wa kipekee kupitia 0708533383/0712983630.
 2. Wateja wanaweza kuzitafuta kazi katika nyanja mbalimbali na kusakura maelezo zaidi kuwahusu waubunifu wengineo kupitia ulingo huu. Mara tu baada ya mteja kumpata yule anayemwajiri, anaweza kutuma ombi kwa kuteua sehemu ya Kuajiri ili aweze kupata huduma kutoka kwa mfanyakazi huria huyo.
 3. Utakuwa na mapitio 3 ya rasimu ya kazi hiyo kabla ya toleo la mwisho kufanywa na mtunzi huyo. Ni wakati huu wa marekebisho hayo ndipo mabadiliko yanaweza kufanywa.

Kwa watunzi

 1. Baada ya kujisajili, mbunifu huonyesha wateja wake kile anachoweza kufanya.
 2. Wafanyakazi huria wanaweza pia kuchapisha baadhi ya miradi yao ya awali na pia kutoa orodha ya huduma wanazoweza kutoa kwenye wasifu wao.
 3. Wanaweza pia kuorodhesha ujuzi wao na kudhibiti maelezo yao mafupi.
 4. Mara tu baada ya mteja anapompata mtaalamu anayeafiki, mbunifu huyo atataarifiwa na wao wanaweza kuwasilisha mapendekezo yao ya ada kwa ajili ya kazi hiyo. Pindi mteja anapopokea nukuu hii, kazi inaweza kuanza.

Njia ya malipo

 • Malipo yote ni kufanyika kupitia malipo ya simu (Mpesa, Airtel Money au Eazzy Pay).
 • PayPal, hundi au Wire Transfer kupitia akaunti ya benki ya Onesha.


 

Ulingo wa Kimataifa

Upwork

Upwork, zamani ikijulikana kama Elance-oDesk, ni ulingo wa ufanyakazi huria Marekani ambapo biashara na wataalamu wa kujitegemea huungana na kushirikiana wakiwa maeneo ya mbali kotekote. Upwork ina zaidi ya wafanyakazi huria milioni kumi na mbili ambao wamesajiliwa na wateja milioni tano waliosajiliwa.

Inavyofanya Kazi

Kuanzisha akaunti ya Upwork

 • Kuanzisha akaunti yako kwenye Upwork ni bure.
 • Unahitaji kujisajili na kutayarisha wasifu wako.
 • Tafuta kazi inayokufaa kwa mujibu wa ujuzi wako na kisha tuma maombi

Ada


Upwork hutoza ada za huduma ambazo huchukuliwa kama asilimia ya mapato yako. Ni ada inayokokotolewa kwa kuangazia ujumla wa mapato yako kama ulivyowagharimu wateja wako:

 • asilimia 20 kwa $500 za kwanza unazotoza wteja wako katika mikataba yote na wao.
 • asilimia 10 ya jumla ya gharama ya ada kwa wateja wako kati ya $500.01 na $10,000.
 • asilimia 5 ya jumla ya gharama ya ada unayowatoza wateja wako inayozidi $10,000.

Njia ya malipo

 • Kutumia amana ya benki ya moja kwa moja
 • PayPal (jua ni nchi zipi za Afrika unazoweza kupokea fedha kupitiaa PayPal)
 • Wire Transfer
 • Local Funds Transfer (LFT)
 • Payoneer
 • Skrill


 

 

Freelancer

Freelancer ilianzishwa mwaka 2009. Makao yake makuu yako Sydney, Australia. Waajiri na wafanyakazi huria kwenye tovuti hii wanatoka katika zaidi ya mataifa 200.

Inavyofanya Kazi

Kuanzisha akaunti ya Freelancer

 • Kuanzisha akaunti yako ni ya bure.
 • Unahitajika kujisajili hapa (kwa kutumia jina la mtumizi na nywila au kwa kutumia akaunti yako ya Facebook).
 • Tafuta kazi na kisha uanze kuzizabuni.

Ada

 • Freelancer hulipa baina ya asilimia 10 – 20 na kiwango cha chini cha asilimia $5 kwa gharama ya mradi wowote funge.
 • Usitawashiji wa zabuni wa hiari wa unaweza kununuliwa ili kukuza jitihada zako za uzabuni.

Njia ya malipo

 • Kadi ya Mikopo
 • PayPal
 • Skrill
 • WetMoney

 

Guru

Guru ilianzishwa mwaka 1998 kule Pittsburgh kama eMoonlighter.com. Ni mojawapo ya wavuti maarufu ya ufanyakazi huria.

Inavyofanya Kazi

Kuanzisha akaunti kwenye Guru

 • Kujisajili na kutumia tovuti ni bure.
 • Kujiunga, unahitaji kusajili akaunti.
 • Una chaguo la kusajili akaunti yako kwa kuunganisha na mitandao yako ya kijamii.

Ada

 • Wafanyakazi huria hulipa ada ya kuendeshea biashara kati ya asilimia 5-9.

Njia ya malipo

 • Kutumia amana ya benki ya moja kwa moja
 • PayPal
 • MasterCard
 • Wire Transfer

Fivver

Fivver ilianzishwa mwaka 2010 mjini Tel Aviv, Israel. Fivver ni soko la kitamtandao kwa wafanyakazi huria duniani kote.

Inavyofanya kazi

Kuanzisha akaunti kwenye Fivver

 • Kujiunga na Fivver ni bure, kwani hapana malipo ya usajili.
 • Tayarisha akaunti yako pamoja na maelezo kukuhusu.
 • Unaweza pia kujiunga kwa kutumia akaunti yako ya Google au ukurasa wako wa Facebook.

Ada

 • Fivver huchukua asilimia 20 ya kila kazi unayoikamilisha.
Kunaweza kukawa na ada zaidi kutegemea njia utakayotumia kupokea malipo yako.

Njia za malipo

 • Kadi za Mikopo / Malipo
 • PayPal
Unahitaji kujua ni njia ya malipo inayotumika au kukubalika nchini mwako. Kwa mfano, Payoneer inaweza kutumika kupokea fedha nchini Zambia ilhali PayPall inaweza tu kutumika kwa ajili ya kutuma pesa na si kupokea ukiwa mkaazi wa taifa lilo hilo la Zambia.

Hitimisho

Ni vigumu kupata ajira barani Afrika. Hata hivyo, ufanyakazi huria mitandaoni kupitia mifumo hii tuliyoangazia, hutoa fursa mbadala ya kutarazaki ili uweze kupata mapato na kuboresha kiwango chako cha maisha barani humu.