Benki ya M-Pesa Ni Nini?

Tafsiri:
en_US

M-Pesa ni njia ya ubunifu wa kuhifadhi na kuhamisha pesa kwa kutumia simu ya mkononi. Ina wateja wengi na taratibu imeingia hadi nchi nyingine. Ilianzishwa rasmi na Vodafone mwaka 2007 nchini Kenya. Kwa sasa, imesambaa nchi nyingine kama Tanzania, Afghanistan, Afrika Kusini, India na Romania. Kampuni ya mawasiliano ya mkononi ya Safaricom, inasimamia shughuli za kila siku za M-Pesa nchini Kenya.

M-Pesa ni uhamishaji wa fedha kwa njia ya simu ya mkononi, huduma ya fedha na mikopo midogo midogo. M-Pesa inamwezesha mtumiaji kuweka fedha, kutoa, kuhamisha na kufanya malipo ya huduma na bidhaa.

M inasimama badala ya neno ‘mobile’ (inayotembea) wakati pesa ni neno la Kiswahili kumaanisha fedha.

M-Pesa Inakuwezesha Kuhifadhi Fedha Kwenye Simu Yako

Watumiaji wanaweza kuhifadhi fedha kwenye simu zao, kutuma au kutoa kwa gharama kidogo kupitia menu ya M-Pesa. Kuongeza salio kwenye simu yako au ya mtu mwingine, ni bure. Kuweka fedha kwenye M-Pesa, pia ni bure. M-Pesa ina mawakala wengi na ni huduma ya benki isiyo na matawi. M-Pesa yaweza kutumiwa kuweka fedha, kutoa, kuhamisha , kuongeza salio kwenye simu na pia kulipia huduma na bidhaa kwa kutumia simu ya mkononi.

kiwango cha mwisho mpesa
Mchoro wa kitakwimu kuonyesha hali ya M-Pesa baada ya kufanya kazi kwa miaka 10.

M-Pesa kwa Biashara

Huduma hii inatumika pia kwenye biashara kwa vile watu wengi walio na biashara rasmi na zisizo rasmi, wanatumia M-Pesa kununua bidhaa na kutoa huduma. Pia wanatumia M-Pesa kuifadhi pesa wazipatazo kutokana na shughuli zao za kila siku. Sanjari na hilo, M-Pesa imetoa ajira kwa mamilioni ya wakenya wanaofanya kazi kama mawakala wa M-Pesa na huduma zake tanzu.

Idadi ya Wateja wa M-Pesa

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007, M-Pesa imekua kwa kiasi kikubwa sana. Kufikia mwaka 2012, akaunti zaidi ya milioni 17 za M-Pesa, zilikuwa zimesajiliwa na akaunti milioni 31 kwa mwaka 2018- Kuna miamala ya M-Pesa zaidi ya milioni tano kila siku. Miamala hiyo ni pamoja na kuongeza salio, kuhamisha fedha, kutoa na kuhamisha fedha kwenda benki au kutoka benki kwenda M-Pesa.

M-Pesa inapatikana kwenye simu zote za aina ya Adroid na zile za aina ya iPhone. Sambamba na hilo, waweza pia kutumia program ya mySafaricom ambayo pia inapatikana kwenye simu za aina ya iOS na Android. Kwa kutumia program ya mySafaricom, waweza kutuma pesa kwenda kwenye namba yako ya simu ya nchini Kenya, kuhamisha fedha, kuongeza salio na kulipia bidhaa na huduma.

Watu wengi wanaihusudu M-Pesa kwa vile mawakala wake wametapakaa nchi nzima ya Kenya. Watu waishio sehemu za mbali na mijini, hawahitaji tena kusafiri kwenda mijini kuweka pesa zao benki. Kwa M-Pesa, waweza kununua au kuuza bidhaa kutoka mahali popote nchini Kenya.

Faida za Kutumia M-Pesa

  • M-Pesa imeshirikiana na benki kadhaa nchini Kenya. Hivyo waweza kuweka fedha kwenye akaunti yako ya benki kwa kutumia M-Pesa au kutoa fedha kutoka benki. Kampuni ya Safaricom imeanzisha namba za bili za malipo ya biashara na mashirika au vyombo vya kisheria vya kushughulikia mambo yanayohusiana na umiliki wa mali ambapo waweza kutumia kulipia huduma na bidhaa.
  • Pia waweza kukopa mikopo kwa muda wa sekunde chache kutoka M-Pesa. M-Pesa ina huduma zijulikanazo kama M Shwari na KCB M-Pesa ambazo waweza kuzitumia kuombea mkopo.
  • Waweza pia kuhifadhi pesa zako kwenye M Shwari na KCB M-Pesa na kujipatia gawio. Mawakala wa M-Pesa wanapatikana hadi sehemu zilizo mbali na mijini. Hivyo huhitaji kusafiri ili kwenda kuweka au kutoa pesa.
  • Miongoni mwa faida za M-Pesa ni kupatikana kwake hadi sehemu za mbali na mijini, gharama nafuu ya miamala, waweza kuongeza salio kwenye simu yako, kutuma na kupokea pesa kutoka kwa watumiaji wengine wa M-Pesa.
  • Iwapo umetuma pesa kimakosa kwa mtu mwingine, waweza kuusitisha muamala na kuzirudisha pesa hizo kwenye simu yako.

Hata hivyo, nyakati fulani, japo ni mara chache, mifumo ya M-Pesa hukwama. Hii hutokea wakati Safaricom inapohuisha mfumo. Kwa bahati nzuri, Safaricom huwataarifu wateja marekebisho ya mfumo yanapotarajiwa kufanyika ili kuepusha usumbufu. Hili huchukua muda mfupi sana na mara nyingi, hufanyika usiku.

Gharama za Kutoa na Kutuma Pesa

Gharama za M-Pesa hubadilika mara kwa mara. Hili linatokea hasa kutokana na sera za serikali kuhusu kodi. Kwa mfano, mwaka 2018, kulikuwa na ongezeko dogo kwenye gharama kutokana na kupanda kwa kima cha kodi ya serikali. Hata hivyo, hizi ni gharama mpya kwa mwaka 2019:

Kiwango cha chini (Kwa shilingi ya Kenya)Kiwango cha juu (kwa shilingi ya Kenya)Hamisho kwenda watumiaji wengine wa M-PesaGharama za hamisho wa watumiaji wasiosajiliwaGharama za kutoa M-Pesa toka kwa wakala
149BureHaihusikiHaihusiki
50100BureHaihusiki10
101500114527
5011,000154928
1,0011,500265928
1,5012,500417428
2,5013,5005611250
3,5015,0006113567
5,0017,5007716684
7,50110,00087205112
10,00115,00097265162
15,00120,000102288180
20,00135,000105309191
35,00150,000105Haihusiki270
50,00170,000105Haihusiki300

Waweza hamisha fedha kutoka akaunti yako ya M-Pesa kwenda akaunti yako ya benki ya nchini au mahali ulipo au kuhamisha kutoka akaunti yako ya benki kwenda akaunti yako ya M-Pesa. Baadhi ya Benki za nchini Kenya ambazo waweza kutumia M-Pesa kufanya miamala ni pamoja na Benki ya Barclays, Benki ya KCB, Benki ya Equity pamoja na Benki ya Ushirika.

Kiwango cha mwisho kuweka M-Pesa Kenya ni shilingi 300,000.

M-Pesa Kwenda Benki ya Barclays


1. Kutoka kwenye menyu yako ya M-Pesa, chagua Lipa na M-Pesa
2. Chagua ‘lipa bili’
3. Chagua ‘ingiza namba ya kampuni, kisha ingiza ‘303030’ ambayo ni namba ya kampuni ya Barclays na ubonyeze ‘OK’
4. Ingiza namba ya akaunti ya Barclays unayotaka kuitumia pesa na ubonyeze ‘OK’
5. Ingiza kiasi unachoweka
6. Ingiza nywila yako ya M-Pesa na ubonyeze ‘OK’
7. Hakiki taarifa zako ulizoingiza na ubonyeze ‘OK’
8. Utapokea ujumbe mfupi wa uthibitisho kutoka M-Pesa na benki ya Barclays

M-Pesa Kwenda Benki ya KCB


1. Kutoka kwenye menyu yako ya M-Pesa, chagua Lipa na M-Pesa
2. Chagua Paybill
3. Chagua Ingiza Nambari ya Biashara na uingie 522522 ambayo ni nambari ya biashara ya Benki ya KCB na ubonyeze OK
4. Ingiza nambari ya Akaunti ya Benki ya KCB unayotaka kuhamisha kwa na bonyeza OK
5. Ingiza kiasi unachopenda unachoweka
6. Ingiza M-Pesa PIN yako na ubonyeze OK
7. Thibitisha maelezo uliyoingiza na bonyeza OK
8. Utapokea ujumbe wa uthibitisho kutoka kwa M-Pesa na Benki ya KCB

M-Pesa Kwenda Benki ya Equity


1. Kutoka kwa menyu yako ya Mpesa, chagua Lipa na M-Pesa
2. Chagua Paybill
3. Chagua Ingiza Nambari ya Biashara na uingie 247247 ambayo ni nambari ya biashara ya Benki ya Equity na bonyeza OK
4. Ingiza nambari ya Akaunti ya Benki ya Usawa ambayo unataka kuhamisha kwa na bonyeza OK
5. Ingiza kiasi unachopenda unachoweka
6. Ingiza M-Pesa yako na bonyeza OK
7. Thibitisha maelezo uliyoingiza na bonyeza OK
8. Utapokea ujumbe wa uthibitisho kutoka M-Pesa na Benki ya Equity

M-Pesa Kwenda Benki ya Ushirika


1. Kutoka kwa menyu yako ya M-Pesa, chagua Lipa na M-Pesa
2. Chagua Paybill
3. Chagua Ingiza Nambari ya Biashara na uingie 400222 ambayo nambari ya biashara ya Benki ya Ushirika na bonyeza OK
4. Ingiza nambari ya akaunti ya Benki ya Ushirika unayoweza kuhamisha kwa na bonyeza OK
5. Ingiza kiasi unachopenda unachoweka
6. Ingiza M-Pesa PIN yako na ubonyeze OK
7. Thibitisha maelezo uliyoingiza na bonyeza OK
8. Utapokea ujumbe wa uthibitisho kutoka M-Pesa na Benki ya Ushirika

Hamisho kwenda Airtel, PayPal na Skrill

Waweza pia kuhamisha pesa kutoka M-Pesa kwenda kwenye mitandao mingine ya kifedha kama Airtel, PayPal na Skrill.

Mpesa Kwenda Airtel


1. Piga *234#
2. Chagua bidhaa za M-Pesa
3. Ingiza 98 kwenda chaguzi zaidi
4. Chagua M-Pesa tuma pesa popote
5. Ingiza nambari ya Airtel unayopeleka pesa
6. Ingiza Pini yako ya M-Pesa

M-Pesa Kwenda PayPal


1. Ingia akaunti yako ya PayPal
2. Bonyeza Anza wwenye akaunti yako ya PayPal
3. Chagua tuma fedha akaunti ya PayPal
4. Piga hesabu kiasi cha Dola za Amerika unazotaka kuweka kwenye PayPal
5. Utaona kiasi cha Shilingi za Kenya kuweka amana kwa kutumia M-Pesa
6. Fungua Mpesa na uchague Lipa na M-Pesa na Paybill
7. Ingiza 800088 kama nambari ya biashara na nambari yako ya simu kama nambari ya akaunti
8. Thibitisha maelezo na ubonyeze OK

M-Pesa Kwenda Skrill


1. Nenda kwa M-Pesa na uchague Paybill
2. Ingiza 640057 kama nambari ya malipo
3. Nambari ya akaunti itatolewa moja kwa moja na Eastpesa
4. Ingia kwa akaunti yako ya Skrill
5. Lipa kiasi na tuma
6. Utapokea ujumbe wa uthibitisho wa kiwango chako cha Skrill kinachopatikana

Kutumia M-Pesa Kwa Njia ya Tovuti

Waweza kuunganisha tovuti yako na M-Pesa. Waweza kuijaribu huduma hii kwa kutumia msimbo mfupi wa majaribio. Baadhi ya vitu unavyopaswa ili kuunganisha tovuti yako na M-Pesa ni pamoja na kuunda akaunti yako kwenye mtandao wa Safaricom. Utahitajika kuandika jina lako la kwanza, la mwisho, aina ya akaunti, jina la utumizi, anuani ya barua pepe, jina la kampuni, nchi na namba ya simu.

Historia ya M-Pesa

M-Pesa ilikuwa ni njia ya kwanza ya uhamishaji wa fedha kwa njia ya simu ambayo iligunduliwa duniani mwaka 2007. Inamilikiwa na Safaricom, Kampuni ya mawasiliano ya Kenya. Safaricom inatumia menyu ya STK ambapo kila laini ya simu iliyoko sokoni, lazima iwe pia na menyu ya M-Pesa.

Kiasili, M-Pesa iligunduliwa na mwanachuo ambaye wakati huo, alikuwa akifanya kazi mradi kwenye chuo kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta. Aliikabidhi kazi mradi hiyo kwa Safaricom na alituzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom wa wakati huo Michael Joseph.

Mwanafunzi huyo hakutumia muda wake mwingi katika kuwekeza kwenye wazo lake, Hivyo Safaricom wakapata umiliki wote wa teknolojia hiyo. Utata uliibuka baadaye juu ya nani hasa ni mmiliki halali wa wazo la M-Pesa. Hata hivyo, Safaricom wana umiliki wote kihalali na kiteknolojia wa wazo la M-Pesa.

Mnamo mwezi Mei mwaka 2019, Safaricom na Vodacom (mwendeshaji wa M-Pesa nchini Tanzania) walitangaza mipango ya kutumia dola za Kimarekani milioni 13.4 ili kununua haki miliki kutoka Vodafone. Mpango huo utapelekea uhifadhi mkubwa wa fedha kwa mirahaba iliyolipwa kwa Vodafone na kutanua huduma kwenye masoko mapya barani Afrika.