Jinsi ya Kufungua Akaunti ya Benki Nchini Kenya

Tafsiri:
en_US

Ikiwa unafikiria kuishi nchini Kenya, ni muhimu kufungua akaunti ya benki. Ni jambo la kushukuru kwamba Kenya tuna benki nyingi za kuchagua, benki za Kenya na za kigeni. Hapa utapata muhtasari juu ya benki za Kenya na mwongozo mfupi wakati wa kufungua akaunti ya benki.

Kenya inajulikana kwa fukwe zake nzuri na hifadhi za wanyama wa pori. Kenya inayo uchumi unaonawiri kwa haraka sababu ya kuongezeka kwa viwanda. Sababu hizi zinavutia wataalamu wa kigeni kujiunga na watalii nchini Kenya. Watu wengine wanahamia Kenya kwa madhumuni ya ajira ili wajikimu maishani.
Kenya also has the cooperative bank.

Stakabadhi Muhimu Wakati wa Kufungua Akaunti ya Benki

Baadhi ya stakabadhi ambazo unahitaji kuwasilisha wakati wa kufungua akaunti ya benki nchini Kenya ni pamoja na kitambulisho cha kitaifa cha Kenya au pasipoti na picha ya pasipoti. Benki zingine zina kamera za kidijitali ambazo unaweza kutumia kuchukua picha ya pasipoti. Mbali na hayo, unahitaji pini ya Mamlaka ya Kodi ya Kenya ili kudhibitisha kuwa unalipa ushuru.

Zaidi ya hayo unahitaji kutoa uthibitisho wa anwani yako ya nyumbani na benki chache zitakuhitaji kuwa na nambari ya simu ya Kenya. Benki chache zitahitaji vipendekezo vya mtu aliyekuwasilisha kwa benki hiyo.

Je Unaweza Kufungua Akaunti Kama Wewe Si Mkaaji?

Ndio. Benki za Kenya zina huduma tofauti za kifedha kwa wasio wakaaji. Kwa mfano, benki za Standard Chartered ina akaunti kwa wasio wakaaji kwa muda mrefu kama unaweza kutoa uthibitisho kwa anwani yako ya nyumbani na kushikilia nambari ya simu ya Kenya. Benki za Barclays inahitaji wasio wakaaji kuwa na pini za Mamlaka ya Kodi ya Kenya na kitambulisho cha picha.

Ugumu Katika Kufungua Akaunti za Benki Nchini Kenya

Idadi kubwa ya Wakenya hawana akaunti za benki. Hata wale ambao wana akaunti za benki, chini ya asilimia kumi wana zaidi ya shilingi milioni moja katika akaunti zao. Mojawapo ya tatizo kubwa ni kwamba benki nyingi ziko katika vituo vya mji. Kwa hivyo, wanashindwa kuitumikia jamii walio vijijini.

Kwa kubuniwa kwa benki ya rununu nchini Kenya kama vile Mpesa, Wakenya wengi wanaoishi vijijini wamehimiza utumiaji wa benki ya M-Pesa . Miongoni mwa faida za M-Pesa ni kuwa watu wengi vijijini wana simu za rununu; kwa hivyo, wanaweza kuweka na kutoa pesa kwa urahisi. Pia, wanaweza kupata mikopo ya M-Pesa kwa urahisi. M-Pesa haina ada ya hifadhi mbali na ada ya kutuma pesa na ada ya uondoaji. Kwa hivyo, akaunti za benki zimebadilishwa na utumiaji wa M-Pesa.

Je Inawezekana Kufungua Akaunti ya Benki Ukiwa Nje ya Kenya?

kwa hali nyingi, utahitaji kujiwasilisha kwa benki kufungua akaunti ya benki isipokuwa unapofungua akaunti ya benki ya rununu. Walakini, unaweza kuanza maombi ya kufungua akaunti ya benki mtandaoni na kisha utembelee benki kuhakikisha stakabadhi zako ili akaunti yako iamilishwe.

Benki Bora Nchini Kenya

Kenya ina benki za humu nchini na za kigeni. Baadhi ya benki za kigeni ni pamoja na Benki ya Standard Chartered na Benki ya Barclays. Baadhi ya benki unaweza kufungua akaunti ni:

1. Benki ya Equity

Benki ya Equity ina matawi 173 na 38 kati yao yako katika jiji kuu la Nairobi. Baadhi ya huduma kwa wateja wake ni pamoja na akaunti ya akiba, akaunti za sasa, akaunti za amana zilizohifadhiwa na akaunti za sarafu. Pia hutoa mikopo kwa wateja wake kwa sababu tofauti. Inatoa Visa, MasterCard na kadi ya mkopo ya Amex na ukopaji.

2. Benki ya Standard Chartered.

Baadhi ya huduma kwa wateja wake ni pamoja na akaunti za akiba, akaunti za amana zilizohifadhiwa na akaunti za sasa. Inayo akaunti za akiba za sarafu za kigeni na inatoa huduma ya kutumia fedha usiowekeza kwenye benki kwa akaunti kadhaa. Mbali na hayo, inatoa kadi za mkopo na deni kwa wateja wake.

3. Benki ya Kenya Commercial (KCB)

KCB inayo mtandao mkubwa wa ATM nchini Kenya. Inayo zaidi ya matawi 250 na inafanya kazi karibu kila mahali nchini. Zaidi ya watu milioni saba wamefungua akaunti ya benki na KCB. Baadhi ya huduma wanazo kwa wateja wake ni pamoja na akiba na akaunti za sasa, kadi za mkopo na deni na huduma zote za mtandaoni na za programu za simu.

4. Benki ya Barclays

Benki ya Barclays nchini Kenya ni kampuni ndogo ya Barclays Bank inayopatikana nchini Uingereza. Unaweza pata huduma chache za benki ya Barclays Bank kupitia ofisi ya posta. Wana mpango mkubwa wa matawi na mifumo ya ATM nchini Kenya. Huduma chache wanayotoa ni pamoja na mikopo na bima, akaunti ya mkondoni na akaunti maalum kwa wanafunzi na wafanyabiashara.

5.Benki ya Cooperative

Benki ya Cooperative ni kati ya benki kongwe nchini Kenya. Inayo mtandao mpana wa matawi na ATM zinapatikana katika miji mikubwa. Benki hii inatoa huduma za akaunti za sasa na akaunti za akiba. Pia hupea wateja wake aina tofauti za mikopo.

sending money to Kenya
Kutuma fedha Kenya kwenye akaunti ya benki ni rahisi na haraka ukifuata mwongozo wetu.

Utumaji wa Pesa Nje ya Mipaka

Kutuma pesa hadi nchi za kigeni kunaweza kuwa kwa hali ngumu au rahisi kulingana na njia unachochagua kutuma. Unaweza kuchagua kutuma pesa kwa kutumia benki ambayo ni ghali au kutumia TransferWise. Mabenki hutumia viwango vya soko la kati wakati wa kutuma fedha kwa wenyewe ili kuongeza faida.

Ikiwa unataka kutuma fedha kupita mipaka, unaweza kupata mbadala ya bei rahisi kwa kutumia TransferWise. TransferWise inatoa njia bora na salama ya kuhamisha fedha kutoka akaunti moja hadi nyingine. TransferWise hutumia kiwango cha katikati cha soko, ambacho ni bei nafuu ukulinganisha na njia zingine.

Ada ya Benki

Mabenki hutoza ada tofauti kwa huduma mbali mbali. Kwa hivyo, ni muhimu kuzingatai benki husika na malipo yake. Miongoni mwa ada ya benki ni pamoja na ada ya kukimu, ada ya ATM kama vile malipo ya kuondoa pesa kwa kutumia ATM na pia malipo ya kawaida kama vile malipo ya uondoaji wa pesa kwa kutumia Keshia ndani ya benki husika.