Je unatarajia kutuma fedha Kenya? Unaweza kuwa na jamaa au rafiki nchini Kenya. Unaweza pia kuwa ni mfanyabiashara anayetaka kutuma fedha kwa kampuni yako Kenya au mfadhili anayetaka kutuma fedha kwa Shirika Lisilo la Kiserikali nchini humo. Kawaida, ungependa kutuma kwa kutumia njia ambayo ni ya haraka na rahisi.
Nafuu na haraka
- Kuna njia mbalimbali za kutuma fedha Kenya. Chagua njia ambayo ni nafuu kwako na kwa mpokeaji, na iwe ni ya haraka na ya ufanisi.
- Katika njia zote, tunashauri utumie Transferwise, World Remit, au kutuma kwa benki. Hata hivyo, ni vyema umuulize mpokeaji aliyeko Kenya ni njia gani anayopendelea kwakuwa inawezekana akapendelea hata Bitcoin.
Transferwise
Transferwise ni kampuni ngeni katika nyanja hii. Ilianzishwa London na kuweza kuchangisha fedha zaidi ya dola za Kimarekani milioni 770 na thamani yake hivi sasa ni dola bilioni 3.5. Lengo la kampuni hii ni kufanya utumaji wa fedha kuwa wa ufanisi, nafuu na haraka. Kufanikisha lengo lao, kampuni hii imefungua mamia ya akaunti za benki duniani. Kwahiyo, ukimtuma fedha Kenya, kampuni hii itatumia akaunti yake ya benki nchini Kenya ili mpokeaji aweze kupewa fedha zake kwa haraka.
Jinsi ya Kutuma Fedha Kenya Kwa Kutumia Transferwise
- Tazama kiwango cha kubadilisha fedha. Unaweza kutumia Google kutazama kiwango cha sasa. Tofauti na kampuni nyingine, Transferwise inatumia kiwango cha kubadilisha fedha kama kinachoonyeshwa kwenye Google.
- Anzisha akaunti kwenye Transferwise kisha chagua nchi unayotaka kutuma fedha, hii itamaanisha Kenya.
- Weka maelezo ya akaunti ya benki nchini Kenya ya mpokeaji. Unahitaji wastani wa saa moja kumaliza utaratibu wa kutuma. Unaweza pia kutuma fedha moja kwa moja kwenye akaunti ya M-Pesa.
World Remit
World Remit ni kampuni ya kimataifa ya kutuma fedha yenye wateja zaidi ya milioni 4 duniani. Tofauti kubwa kati yake na Transferwise, mpokeaji anaweza kutumia wakala wa World Remit kupokea fedha zake.
Kutuma fedha Kenya kwa kutumia World Remit, fuata hatua zifuatazo.
- Nenda kwenye tovuti ya WorldRemit ambapo unaweza kutumia “app” au tovuti.
- Weka kiwango cha fedha na nchi unayotuma fedha (Kenya). Utaona kiasi cha fedha ambacho mpokeaji atapewa.
- Weka maelezo binafsi ya mpokeaji kisha tuma. Mpokeaji atapokea fedha chini ya saa moja. Kwa kutumia tovuti utaweza kuona kama mpokeaji amepewa fedha au la.
Kuponi ya World Remit
Kuponi hii inamalizika muda wake September 30, 2019. Tuma fedha kwa WorldRemit kwa kutumia neno fupi ‘3FREE’ ambapo hutalipa gharama ya kutuma fedha kwa mara tatu za mwanzo. Kuponi ya WorldRemit ya kutuma fedha bure.
Faida za Kutumia World Remit
1. Mpokeaji hahitaji akaunti ya benki.
2. Mara ya kwanza unapotuma fedha gharama yake ni bure. Na ukitumia neno fupi ‘3FREE’ utatuma fedha bure mara tatu.
3. Unaweza kufuatilia fedha kwa kutumia “app”.
4. Kiwango cha kubadilisha fedha kinaonyeshwa wazi kabla ya kutuma.
5. Ni njia ya haraka.
Kutuma fedha Kenya kwa kutumia benki yako pia ni njia rahisi ingawa kwa ujumla ni ya gharama zaidi. Inabidi uiruhusu benki yako kutuma fedha kwenye akaunti ya benki nchini Kenya. Unaweza kutuma kwa kwenda kwenye tawi la benki yako au kutumia intaneti. Kutumia njia hii unahitaji vitu vifuatavyo:
- Namba ya akaunti ya benki ya mpokeaji.
- Jina na anuani ya benki ya mpokeaji.
- Namba ya Swift ya benki ya mpokeaji.
Utaratibu huu unaweza kuchukua dakika chache na mpokeaji atapata fedha kwa si zaidi ya siku saba. Kwa kawaida, huchukua chini ya siku mbili fedha kuingia kwenye akaunti ya mpokeaji.
Tazama jinsi ya kufungua akaunti ya benki Kenya.
PayPal
PayPal ni kampuni kubwa kabisa duniani yenye thamani ya dola bilioini $140 billion. Kwa kutumia PayPal, unaweza kutuma fedha Kenya na mpokeaji akazipata kwa sekunde chache. Lakini, mpokeaji lazima awe na anuani ya PayPal. Unachohitaji ni kuweka anuani ya barua pepe ya mpokeaji na kiasi cha fedha. Mpokeaji anaweza kupokea fedha hizo kwa kutumia M-Pesa. Kutegemea na kiwango cha fedha hizo, inaweza kuchukua sio zaidi ya masaa 5. Njia nyingine ya kutuma fedha hizo toka PayPal kwenda kwenya akaunti yake ya benki. Kwa hivi sasa, hii inawezekana kwa kutumia tu Benki ya Equity.
Tumia PayPal iwapo mpokeaji amesisitiza utumie njia hii maana ina kasoro kadhaa . Kwanza, itachukua siku tatu kwa fedha kuingia kwenye akaunti ya mpokeaji (iwapo atataka kupokea fedha hizi kwa njia ya benki). Pili, kuna malipo mengi unapotumia PayPal. Kwa mfano, ukituma dola 300, mpokeaji atapata dola 288. Halafu kutakuwa na gharama za benki anapotoa fedha hizo.
Western Union
Western Union ni kati ya njia zee kabisa za kutuma fedha. Kampuni hii ina thamani ya zaidi ya dola bilioni 8 na inapatikana karibu nchi zote ulimwenguni. Kutuma fedha kwa kutumia Western Union ni rahisi. Unaweza kutuma kwa njia mbili. Unaweza kutumia tovuti ya kampuni hii au unaweza kwenda kwa wakala wa kampuni.
Ukitumia tovuti, utalipa kwa kutumia kadi. Kama unataka fedha hizo ziende kwenye akaunti ya benki ya mpokeaji, utaweka maelezo ya akaunti yake. Kama utataka mpokeaji achukue fedha zake toka kwa wakala, itabidi umpe namba, MTCN, utakayopewa baada ya kumaliza kutuma.
Kuna faida kadhaa za kutumia Western Union kutuma fedha Kenya:
- Ni njia ya haraka.
- Kuna mamia ya mawakala ambapo mpokeji anaweza kuchukua fedha zake.
- Mpokeaji hahitaji akaunti ya benki.
Badala ya kutumia Western Union, unaweza kutumia MoneyGram, ambayo utaratibu wake hautofautiana sana na Western Union.
Bitcoin
Unaweza pia kutuma fedha Kenya kwa kutumia Bitcoin. Kutuma kwa Bitcoin unahitaji kuwa na Bitcoins kwenye mkoba wako. Na mpokeaji anatakiwa kuwa na anuani ya kupokea. Kujua kwa undani juu ya Bitcoin nchini Kenya, soma makala hii ya Kiswahili kuhusu Bitcoin.
Tumeona kuna njia mbalimbali za kutuma fedha Kenya. Ni vyema unapochagua njia ya kutumia uangalie ni njia ipi ni nafuu kwako na kwa mpokeaji na pia njia ambayo ni ya haraka. Katika njia tulizozungumzia tunashauri utumie Transferwise, World Remit, au benki. Lakini ni vyema pia kumuuliza mpokeaji njia anayoipenda maana anaweza hata kuchagua Bitcoin.
This post is also available in en_US.