Jinsi ya Kupata Pesa Ukiwa Chuoni Bila Kupitwa na Masomo

Tafsiri:
amen_US

Chuo kinaweza kuwa kipindi cha kufurahisha katika maisha ya mtu. Binafsi, wakati nikiwa chuoni ulikuwa ni muda bora zaidi wa maisha yangu. Kuwepo kwa uhuru, muda mwingi, na watu ambao unakutana nao hapo chuoni wanaweza kusaidia kuyaunda maisha yako. Maisha ya chuoni pia yanaweza kuwa yenye shughuli nyingi sana haswa ikiwa unasomea kozi ngumu kama vile uhandisi na utabibu. Hata hivyo, chuo bado kinaweza kuunda maisha yako. Katika makala haya, tutaangalia njia bora za kupata pesa ukiwa chuoni na bila kukosa darasa. Baadhi ya njia hizi zinaweza kukuzalishia pesa kila mwezi.

Ukufunzi (Tutoring)

Kwa kuwa uko katika chuo kikuu, pana uwezekano kwamba wewe ni mjuzi katika uwanja fulani. Unaweza kuwa na ujuzi katika nyanja kama uhandisi wa programu, coding, na hisabati. Ikiwa hii ndio hali, basi haifai kupoteza ujuzi wako kwa sababu ujuzi wako unahitajika na unaweza kuwa mkufunzi wa mtandaoni. Kuna njia kadhaa ambazo unaweza kufanya hivyo. Kwanza, unaweza kuunda wavuti wako wa kutolea mafunzo mtandaoni na kuwafikia wateja wako. Ukiwa na mfumo huu, utajipatia faida asilimia mia ya shughuli unazoziendesha. Pili, unaweza kutumia majukwaa anuwai ya kufundisha mtandaoni ambayo yapo tayari na uyatumie kuzindua kazi yako ya kutoa mafunzo. Kwa mfano, unaweza kutuma kozi zako kwenye jukwaa la Udemy na hivyo kuwavutia wanafunzi. Faida ya kutumia jukwaa kama Udemy ni kwamba lina watumiaji wengi ulimwenguni. Changamoto kuu ni kwamba utalazimika kugawanya faida unayopata na kampuni hii.

Kazi ya ufundi / Sanaa

Ikiwa wewe ni msanii, njia nzuri ya kupata pesa ni kuandaa mchoro na vitu vinginevyo vya kisanaa na kuviuza. Kwa bahati nzuri, hauhitajiki kuwa na duka la kuuza vitu hivi. Kwa vile watumiaji wengi huwa mtandaoni, njia bora ya kupata pesa kwa kutumia mbinu hii ni kuziuza bidhaa zako za sanaa mtandaoni. Unaweza kuunda tovuti yako mwenyewe ya sanaa na ufundi, uitambulishe, na kuwauzia bidhaa wateja wako mtandaoni. Njia bora zaidi ni kutumia kwa pamoja wavuti wako mwenyewe na mitandao ya kijamii na maduka makubwa ya e-commerce duniani kama vile Etsy na Amazon. Unaweza pia kutumia maduka ya ecommerce Tanzania au maduka ya ecommerce Kenya (makala ya Kiingereza) na nchi nyinginezo.

Uandishi wa kitaaluma na huria (Academic and freelance writing)

Njia nyingine ya kujipatia pesa ukiwa chuoni ni kupitia uandishi wa makala. Kuna njia kadhaa kuafikia mbinu hii. Kwanza, unaweza kuzingatia uandishi wa kitaaluma/kiakademia, ambapo unawasaidia wanafunzi wengine katika kazi zao. Ili kufanya hivyo, unaweza kuunda wavuti wako wa academic writing. Ikiwa hutaweza kuunda wavuti wako, unaweza kutumia masoko anuwai yanayochapisha kazi hizi za uandishi. Ikiwa wewe ni mwandishi mzuri, unaweza pia kujitafutia kazi za kuandika kutoka mtandaoni. Siku hizi, mahitaji ya uandishi wa makala yanaongezeka haraka sana kwani kampuni nyingi zinahamishai shughuli zao mtandaoni. Unaweza kutumia masoko ya kisasa kama Fiverr na Upwork kupata wateja. Tafadhali soma makala hii itakuonyesha kwa undani jinsi ya kupata pesa kupitia uandishi mtandaoni.

Ubunifu wa picha na wavuti (Graphic and website design) na SEO

Hizi ni njia tatu maarufu unazoweza kutumia kupata pesa na kuboresha ujuzi wako. Ubunifu wa picha ni mchakato wa kutumia programu kama vile Photoshop, Illustrator, na InDesign kuunda bidhaa muhimu kama vipeperushi, nembo, na brochures. Mahitaji ya bidhaa hizi za picha daima huongezeka kadiri kampuni nyingi zinavyoanzishwa.

Kadiri idadi ya watumiaji wa mtandao inavyoongezeka, ndivyo mahitaji ya wavuti (website) za kitaalamu yanaongezeka. Kwa hivyo, unaweza kuanzisha kampuni inayounda tovuti na kuziboresha kwa mujibu wa injini za utaftaji (Search Engine Optimisation – SEO). Kutokana na umuhimu wa kuongezeka kwa mauzo ya kidijitali, kampuni nyingi zina uwezo wa kukulipa maelfu ya pesa kila mwezi ili ubuni au kuzikarabati tovuti zao.

Drop Shipping

Drop Shipping ni mchakato ambao unahusisha kuunda wavuti na kisha uanze kuuza bidhaa kwa niaba ya watengenezaji, wasambazaji au wauzaji wa jumla wa bidhaa hizo. Mtu anapotoa oda ya kununua bidhaa, utamjulisha muuzaji, msambazaji au mtengenezaji wa bidhaa hizo kisha yeye ndiye atamtumia mnunuzi. Unaweza kufanya hivyo kwa njia tofauti. Kwanza, unaweza kuunda tovuti nyingi za bidhaa mbalimbali. Pili, unaweza kuunda wavuti moja ambapo unauza bidhaa zote. Faida mojawapo ya Drop Shipping ni kwamba unaweza kuunda wavuti kwa urahisi kwa kutumia Shopify. Faida nyingine ni kwamba hauhitajiki kuwekeza katika vifaa na miundomsingi sana. Unayohitaji tu ni wavuti, picha nzuri za bidhaa, na muuzaji mzuri unayeweza kumtegemea.

Kazi za Mitaani/Nyumbani

Njia nyingine ya kujipatia pesa chuoni ni kufanya kazi za kawaida hapo mtaani. Kwa mfano, unaweza kutumia gari lako la kibinafsi kuendesha shughuli kupitia app za taxi kama vile TanTaxi na QTaxi nchini Tanzania and Uber na Bolt nchini Kenya. Unaweza pia kutumia app kama TaskMate na Remote Tasks kujitafutia shughuli ambazo unaweza kufanya na kulipwa.

Blogu za video (Video blogging) na michezo ya kidijitali

Katika enzi hizi za YouTube na Twitch, wanafunzi wengi wa vyuoni wanajipatia pesa kwa kufanya kile wanachokipenda. Baadhi ya superstars wanaojulikana zaidi kwenye YouTube na Twitch ni wanafunzi wa vyuoni. YouTubers hulipwa na Google kulingana na idadi ya watu ambao hutazama video zao. Pia wao hutayarisha video zilizodhaminiwa, ambapo wanapata endorsements kutoka kwa kampuni kubwa. Wachezaji wa Twitch kwa upande mwingine hulipwa na wadhamini na watu ambao hutazama video zao. Soma makala hii ujue jinsi ya kupata pesa kupitia YouTube.

Hitimisho

Chuoni ndipo unapounda maisha yako. Ukiwa huko, unapaswa kutumia wakati wako mwingi darasani kusikiliza wahadhiri wako. Katika wakati wako wa mapumziko, unapaswa kufanya vitu ambavyo vinaongeza thamani kwenye maisha yako. Baadhi ya shughuli ambazo tumetaja hapa zitakusaidia kupata pesa na pia kukusaidia kupata uzoefu unaofaa unapoelekea kwenye soko la ajira.

Soma Zaidi