Jinsi Ya Kujipatia Pesa Kupitia Youtube

Tafsiri:
amen_USuk

Mojawapo ya mfumo wa kidijitali ambao inaruhusu watu kujipatia pesa ni YouTube. Tangu kuzinduliwa mwaka wa 2005 na hatimaye kupokelewa na Google mwaka wa 2006, ulingo huu umekua kwa kasi sana na kuishia kuwa mfumo wa pili bora wa kidijitali baada ya Google. Makala haya yatakupa maelezo muhimu ya jinsi ya kujipatia pesa mtandaoni kupitia YouTube.

Kuhusu YouTube

  • Kwa kila dakika, kuna zaidi ya masaa 500 ya video iliyopakiwa kwenye YouTube.
  • Takriban watumiaji bilioni 1.9 huingia kwenye tovuti hii kila mwezi.
  • Wakati watu wengine wanaona YouTube kama njia ya kupata habari na burudani, kuna wengine ambao wamefanya tovuti hii kuwa kazi yenye malipo.
  • Baadhi ya YouTubers, ambao wameishia kuwa celebrities, hujipatia hadi dola milioni 20 kila mwaka kupitia mfumo huu wa kupata pesa kidijitali.
make money on youtube
YouTubers tano bora kimapato.

Kati ya njia kuu za kujipatia fedha kupitia tovuti ya YouTube ni hizi zifuatazo:

Uza Bidhaa Zako

Kuna makundi mawili ya watu wanaojipatia pesa kupitia YouTube: wajasiriamali ambao hutumia jukwaa hili ili kuuza bidhaa zao na wabunifu wanaotumia umaarufu wao ili kuanzisha miradi yenye faida.

Ili kupata fedha kupitia YouTube kwa kuuza bidhaa zako, utahitajika:

  • Uwe na bidhaa inayowakilisha chaneli yako. Usiwachoshe watazamaji wako na bidhaa nyingi mara moja.
  • Kupata wasambazaji au watengenezaji wa bidhaa wa kuaminika.
  • Kuunda tovuti itakayofanya kazi kama duka lako. Weka kiungo cha tovuti yako kwenye video zako ili iwe rahisi kwa watazamaji wako kuipata.
  • Kujiunga na YouTube Partner Program ili kufaidika kutokana na kipengele cha rafu ya bidhaa.
  • Kukuza na kuitambulisha zaidi bidhaa kwa kuitumia kwenye video zako na hata kushirikiana na watu wengine wenye ushawishi ambao wanatumia bidhaa zako.

Tengeneza Maudhui Yaliyodhaminiwa

Kama una hadhira kubwa, unaweza kuandaa video zinazoshawishi watu kununua bidhaa mbalimbali ambapo wamiliki wa bidhaaa hizo wanakulipa. Hii ni mojawapo ya njia nzuri za kujipatia pesa kupitia YouTube kwa sababu hutahitajika kugawanya mapato yako na mtu yeyote.

Unachohitaji ni kuwa na chaneli ya YouTube yenye watazamaji wengi. Kwa mfano, video za Maasaiboys zinatazamwa na watu wengi sana kutokana na maudhui yake. Tazama moja ya video yao hapo chini.

Kuuza Maudhui za Video kwa Vituo Vya Habari

Vyombo vya habari kama vile vituo vya televisheni daima hutafuta video mpya kwa watazamaji wao. Kupitia soko la haki za video kama Jukinmedia, video zako zitaweza kufikia vituo maarufu kwa urahisi kama vile CNN, BBC, na MTV. Fanya utafiti wa vyombo vipi vya habari nchini mwako vinavyoweza kununua maudhuo yako ya video.

 

Uchangishaji Fedha wa Halaiki (Crowdfunding)

Kuna tovuti mbalimbali za ‘crowdfunding’ zilizoidhinishwa na YouTube. Tovuti hizi zinakuwezesha kuchangisha pesa toka kwa watu mbalimbali duniani ambao hata hamjuani. Inaweza kuwa kampeni moja tu kwa ajili ya mradi au mwito wa kuchangisha fedha wa mara kwa mara. Unaweza kutumia chaneli yako ya YouTube pamoja na mitandao mingine ya kijamii kwa kutangaza kampeni yako ya kuchangisha pesa.

Tovuti za kuchangisha pesa za halaiki ni pamoja na hizi:

Kujiunga na programu ya YouTube Partner Program

Unaweza pia kupata pesa kutoka kampuni ya YouTube kwa kupitia YouTube Partner Program. Kwa mfano ukiwa mshirika wa programu hii, YouTube itakuwa inaweka matangazo yake kwenye video zako kisha inakulipa. Ili uweze kuwa mshirika wa YouTube, unapaswa kukidhi sera zote zilizotolewa.

Maombi yako ya kujiunga na programu hii yakikubaliwa, utakuwa na uwezo wa kupata pesa kupitia vipengele mbali mbali ikiwa ni pamoja na:

  • Super chat na stickers. Watazamaji hulipia ili ujumbe wao uweze kuonekana kwenye mkondo wa mazungumzo.
  • Uanachama wa Chaneli. Wanachama wa chaneli yako ya YouTube wanaweza kulipa ada ya kila mwezi ili kufurahia matoleo maalum kutoka kwako.
  • Mapato ya YouTube Premium9. Unapata sehemu ya malipo yaliyofanywa na waliojisali kwa mpango wa YouTube Premium kila wakati wanatazama video zako.
  • Mapato ya matangazo. Hii ni pamoja na mapato kutoka kwa video, video za kiziada ndani ya video zako zinazoonyesha matangazo.
  • Rafu ya bidhaa (Merchandise shelf). Kipengele hiki kinawawezesha wafuasi (followers/subscribers) wako kuangalia na kununua bidhaa zilizowekwa kwenye kurasa zako.

Jinsi ya kupata watazamaji wengi kwenye YouTube

Kitu cha msingi cha kukuwezesha kupata pesa kwenye YouTube ni kuwa na idadi kubwa ya watazamaji na wanachama (subscribers). Ni lazima usome makala mbalimbali zinazotoa ushauri wa jinsi ya kuongeza subscribers YouTube. Hata ikiwa ni mapato kutokana kwa utazamaji wa video zako YouTube au mikataba ya udhamini, YouTubers wenye watazamaji na wanachama wengi wana uwezo wa kupata pesa nyingi kutoka kwenye jukwaa hili la kidijitali.

Ili kufikia kiwango kilicholengwa cha utazamaji kwenye video fulani, fikiria mikakati ifuatayo:

  • Wahimize wafuasi wako wasubscribe kwenye chaneli yako. Kwa njia hii, wanachama wako wanaweza kuona video zako za baadaye.
  • Waulize watazamaji wako wapendekeze aina ya video na maudhui ambayo wangependa uwaandalie.
  • Unda orodha ya video ili uweze kufaidika na kipengee cha auto-play.
  • Andaa video za mada na maudhui mahsusi badala ya kuunda video kuhusu kitu chochote na kila kitu.
  • Tumia maneno muhimu na yanayoweza kuwa rahisi kutafutwa na watazamaji katika majina yako na maelezo.
  • Tumia picha za kuvutia.
  • Kuwa na maingiliano mazuri na wafuasi wako na YouTubers wengine.
  • Tumia majukwaa mengine ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, na Twitter ili kuongeza utazamaji kwenye chaneli yako ya YouTube.

Hitimisho

Mifumo ya kidijitali kwa kiwango kikubwa imebadilisha ulimwengu. YouTube ni mojawapo ya njia za mtandaoni ambapo mtu anaweza kupata habari na pia kujijengea taaluma. Jambo la msingi ni kuandaa video na maudhui ambayo yatawafurahisha wafuasi wako walengwa. Utahitaji pia kutumia mikakati ya kiziada ili kupata watazamaji wengi ili uweze kuwa influencer anayejulikana.