Jinsi ya Kulipwa Pesa Mtandaoni

Tafsiri:
en_US

Kazi za kujitegemea mtandaoni ni moja ya njia mpya ya kujipatia ajira na kipato. Je ukifanya kazi za mtandaoni, utalipwaje pesa? Makala hii inonesha njia mbalimbali za malipo kwa wafanyakazi wa kujitegemea online barani Afrika.

Njia za Kutuma Pesa Rahisi na ya Haraka Zaidi

  • Kati ya njia bora za kupokea pesa toka nje ya nchi, tunapendekeza TransferWise, WorldRemit au kutuma kwa benki (wire transfer). Hata hivyo, unapaswa kumuuliza anayekutumia njia anayoipendelea.

WorldRemit

WorldRemit, iliyoanzishwa mwaka 2010, ni huduma ya mtandaoni inayotoa chaguo rahisi la kulipa wafanyakazi wanaojitegema barani Afrika. Kufuatana na uzoefu wetu, hii ni njia mojawapo rahisi mno ya kutuma pesa Tanzania, Kenya, n.k. Kama gawio la ziada, waweza pia ukapata hadi mahamisho matatu bla malipo kama unatumia msimbo kuponi 3FREE hadi tarehe 31, mwezi Machi mwaka 2020.

Machaguo ya malipo yanayopatikana ni pamoja na hamisho la benki, kadi ya Debit, kadi ya Credit, wakati machaguo ya upokeaji wa fedha yanajumuisha hamisho la benki (kwa baadhi ya nchi), kupokea fedha taslimu, salio kwenye simu ya mkononi na pochi ya simu ya mkono kama vile M-Pesa. Mara nyingi pesa zitumwazo, hupokelewa ndani ya dakika chache tu.

Ofa Maalum ya WorldRemit

Ofa maalum ya kutuma fedha bure. Tuma pesa kwa WorldRemit kwa kutumia msimbo 3FREE na hakuna malipo kwa mahamisho matatu ya kwanza. Msimbo kuponi WorldRemit kwa mahamisho ya bure.

 

PayPal

PayPal ni mwanzilishi wa malipo ya mtandaoni. Ni njia ya kawaida zaidi inayotumiwa na wafanyakazi wanaojitegemea kutoka zaidi ya nchi mia mbili tangu mwaka 2002. Unatakiwa kuunganisha akaunti yako ya benki na akaunti ya PayPal, kisha thibitisha akaunti hiyo.

Kutuma pesa kutoka akaunti moja ya PayPal kwenda nyingine ni papo hapo, wakati inachukua siku za kazi tatu kutuma pesa toka akaunti ya PayPal kwenda akaunti ya benki.

Kwa kawaida PayPal inatoza gharama kwa miamala yake yote. Mfanyakazi wa kujitegemea akipokea pesa zake za kwanza, ada ni asilimia 2.9 ya muamala uliofanyika na ongezeko la dola ya kimarekani 0.30. Wafanyakazi wa kujitegemea walioko nje ya Marekani wanatozwa asilimia 2.5 kwa ubadilishaji wa fedha. Kando ya hilo, wakati wa kupokea malipo kutoka PayPal kwenda akaunti ya benki, mabenki huwa na gharama ndogo ya ubadilishaji fedha. Inawafanya wafanyakazi wa kujitegemea kupokea pesa kidogo kuliko zile walizostahili kupokea.

Kwa sasa, PayPal inapatikana kwenye nchi 50 barani Afrika. Hata hivyo, nchi kama Zambia, mtu aweza kutuma pesa au kufanya malipo kwa bidhaa na huduma, lakini hawezi kupokea pesa.
 

Payoneer

Payoneer pia inatoa malipo kwa wafanyakazi wa kujitegemea. Inapatikana kwenye zaidi ya nchi 200 na katika fedha tofauti 150. Ni akaunti ya uhakika kwa vile wafanyakazi wa kujitegemea wanapokea pesa katika sarafu ya nchi zao. Inamaanisha kwamba, hawapaswi kulipia gharama za ziada kwa ubadilishaji wa fedha kama upo Ulaya, Amerika, Uingereza, China au Ujapani. Malipo ni haraka tofauti na pindi utumiapo wire transfer. Malipo yakishafanyika, pesa hupatikana kati ya saa 2 hadi 6.

Ada za Payoneer ziko wazi. Wafanyakazi wa kujitegemea hutozwa asilimia 3 kama hawatatumia mtandao na asilimia moja kama mteja atalipa kupitia Kadi ya Credit. Yapo malalamiko kuwa kampuni inachukua muda mrefu kuithibitisha akaunti. Hivyo kama mfanyakazi wa kujitegemea, fungua akaunti yako kwanza kabla hujaanza kudai malipo toka kwa wateja wako.

Payoneer inapatikana kwenye nchi nyingi za Afrika. Kwa mfano, unaweza kutuma fedha toka Payoneer kwenda Mpesa. Tafuta ni nchi zipi za Afrika zina huduma hii.

 

TransferWise

Kama unataka kufanya hamisho la kibenki, fikiria kutumia TranferWise. TransferWise, hivi sasa inajulikana kama Wise, imekuwepo tangu mwaka 2010. Ni chaguo zuri kwa wafanyakazi wa kujitegemea kwa vile wanapokea pesa moja kwa moja ikiwa kwenye sarafu ya nchi zao pasipo kuwa na gharama za ziada za ubadilishaji wa fedha.

Akaunti ina wepesi wa utumaji pesa ndani ya saa 10 kwa mfumo wa hamisho benki ACH, saa 12 kwa hamisho SWIFT na saa 36 kwa hamisho la benki. Ada hizi zinategemeana na benki unayotumia na kiasi kiachopaswa kulipwa na mteja wako.
 

Skrill

Skrill zamani ilikuwa inajulikana kama Moneybookers, ambayo waweza kutuma na kupokea malipo kwenye zaidi ya nchi 200 kwa sarafu mbali mbali arobaini. Ni njia salama na ya haraka ya kutuma pesa ulimwenguni kote.

Ni njia maarufu ya kutuma fedha Kenya na Tanzania. Kwa mfano, unaweza kupokea pesa akaunti yako ya Skrill nchini Kenya na kisha ukatuma fedha hizo kwenye akaunti yako ya Mpesa. Tazama jinsi ya kutuma toka Skrill kwenda Mpesa.

Kuanzisha akaunti ya Skrill ni bure na haraka na waweza anza kutuma na kupokea pesa mara moja. Waweza kutoa pesa kutoka akaunti ya Skrill kwenda akaunti yako ya benki. Waweza pia kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya Skrill kwenda akaunti ya benki.

Hakuna gharama kwa kupokea pesa kwenye akaunti yako. Hata hivyo, kutuma pesa kwa anuani ya barua pepe, kunagharimu asilimia 1.45 ya kiasi kitumwacho. Inachukua kati ya siku moja na tano kuzipokea pesa baada ya kuanzisha mchakato wa kuzitoa. Muda itakaochukua utaoneshwa pindi utakapoanza mchakato wa kuzitoa.

 

MoneyGram

Moneygram ni chaguo jingine kwa wafanyakazi wa kujitegemea barani Afrika kupokea malipo. Waweza kuitumia kwa mahamisho ya fedha ndani au nje ya nchi. Inapatikana kwenye nchi zaidi ya 200 na zaidi ya sarafu 45. Baadhi ya njia za malipo ni pamoja na kuchukua/kupokea pesa mkononi, kuhamisha kibenki, akaunti ya pochi ya mtandaoni na Kadi ya Debit.

Gharama za Moneygram zinajumuisha asilimia 2 kwa fedha juu ya dola 900, wakati miamala ya mtandaoni inagharimu dola 11. Hata hivyo, ada zinategemea nan chi zinazohusika na kiasi cha muamala kinachofanywa. Gharama za benki ni nafuu wakati kadi za debit na credit ni gharama ya juu.
 

Western Union

Western Union

Western Union inafanya malipo mtandaoni katika vituo zaidi ya laki tano duniani kote. Waweza kuitumia kuwalipa wafanyakazi wanaojitegemea ndani ya nchi au kimataifa. Huduma hii inapatikana kwenye nchi zaidi ya 200 na yaweza kufanya miamala ya sarafu zaidi ya 40.

Kwa uhamishaji pesa ndani ya nchi gharama ni dola 5, wakati malipo mtandao kwa benki yanagharimu dola 11. Kama unafanya muamala kwa kutumia Kadi ya Debit au Credit, gharama ni dola 49.99. Inachukua kati ya siku za kazi moja na tano kupokea pesa. Baadhi ya njia za malipo zinajumuisha kuchukua pesa mkononi, hamisho kibenki, Kadi ya Credit/Debit kupitia tovuti ya Western union.
 

Escrow

Escrow ni uwanja ambao unadhibiti fedha mara pindi mteja anapomuajiri mfanyakazi wa kujitegemea na kuziachia fedha hizo pale kazi inapokamilishwa na pande zote kuridhika. Inachukua siku za kazi kumi kwa kazi kuidhinishwa. Inapatikana kwenye nchi nyingi wakati sarafu zinazopatikana zinajumuisha dola ya kimarekani, dola ya Australia, euro na paundi ya Uingereza. Njia zake za malipo zinajumuisha PayPal, Kadi za Debit/Credit na hawala za fedha. Gharama zake ni asilimia 2.25 kwa kiasi kati ya dola 10 na dola 5,000 wakati kima cha chini ni dola 10. Kama kiasi ni kati ya dola 5,000 na dola 2,500 gharama ni asilimia 0.26 na ongezeko la dola 162.5. Iwapo kiasi ni zaidi ya dola elfu ishirini na tano, gharama ni asilimia 0.89 au asilimia 1.78 ya kiasi chote.
 

Hitimisho

Siku hizi kuna kazi nyingi za kujitegemea zinazopatikana mtandaoni. Ukiwa na ujuzi au maarifa fulani, unaweza kupata kazi online. Ukishapata kazi, unatakiwa kuna wa namna ya kupokea pesa online za malipo yako kwa kuwa anayekulipa anaweza kuwa anaishi nchi ya mbali. Njia tulizoorodhesha hapa ni moja ya njia bora unazoweza kutumia kupokea pesa mtandaoni.