Jinsi ya Kupata Pesa Mtandaoni Kupitia Upwork

Tafsiri:
amen_USes_ESfr_FRnl_NLuk

Upworkni tovuti ya kazi za kujitegemea mtandaoni. Je, unaweza kujikimu kifedha kwenye intaneti kupitia Upwork? Jibu la dhahiri ni, ndiyo! Ikiwa unataka kujichumia pesa kupitia Upwork kama mfanyakazi wa kujitegemea (freelancer), hatua ya kwanza ni kujifungulia akaunti ya Upwork. Kufungua akaunti yako ni bure.

Je, Upwork ni nini?

Tovuti za kazi za kujitegemea, Elance na Odesk, ziliunganishwa kuunda Elance-Odesk mwaka wa 2013. Mwaka wa 2015, kampuni hiyo ilibadili jina na Upwork ilianzishwa. Kampuni hiyo inawaunganisha wateja walio na kazi na wateja wanaotafuta kazi za kujitegema (freelancers) kote ulimwenguni. Upwork hutoza ada kwa kila kazi iliyokamilishwa kwenye jukwaa hilo. Katika miaka ya hivi karibuni, kampuni hiyo imeshuhudia ukuaji mkubwa. Kwa sasa ina thamani ya zaidi ya dola bilioni 1.98. Ina wateja zaidi ya laki nne kila mwaka na watafuta kazi zaidi ya milioni 12.

Jiunge na Upwork Upate Kazi Mtandaoni

Mbona Utumie Upwork?

Licha ya Upwork kutoza ada ya juu, ukweli ni kwamba ni jukwaa linaloweza kukusaidia kujipatia pesa kama mfanyakazi mtandaoni. Hii ni kwa sababu kadhaa:

  • Zaidi ya ujuzi 5000. Hii ina maana kwamba unaweza kupata pesa kutokana na moja ya ujuzi 5,000. Mifano ya ujuzi huu ni uandishi wa kiubunifu, huduma za SEO, uhasibu, kutafsiri na kupogramu kompyuta kati ya nyingine nyingi.
  • Washindani wachache. Sababu moja kuu inayofanya Upwork ifanikiwe ni kwamba kampuni ambazo zinashindana nayo ni chache mno na haziwezi kukulipa pesa nyingi.
  • Kampuni tajika. Kampuni hii ni maarufu na inayojulikana katika jumuiya wafanyakazi wa kujitegemea.
  • Kuaminiwa na kampuni nyingine kubwa. Kampuni nyingi kubwa kama Dropbox, Facebook, Zendesk, na Microsoft hutumia Upwork kuajiri wafanyakazi wa kujitemea kwenye intaneti (online freelancers).
  • Vifaa vya ziada. Jukwaa hili linatoa vifaa vya kiziada kwa wafanyakazi wa kujitegema kama vile usalama wa malipo, Ppwork Time Tracker, na vifaa za mawasiliano salama.

Jinsi ya Kufanikiwa kama Freelancer wa Upwork

Upwork

Ili kuwa na ufanisi kama mfanyakazi wa mtandaoni wa Upwork, unahitaji kufanya yafuatayo:

Tambua Ujuzi Wako

Kwa vile Upwork ina ujuzi zaidi ya 5000, ni muhimu kwako kutambua ujuzi wako bora. Hii ni kwasababu utaweza kutoa huduma bora kwa wateja wako huku ukijifurahisha kwa kufanya kazi.

Tengeneza Profile (Wasifu) Nzuri

Baada ya kutambua ujuzi wako bora, unapaswa kuunda profile nzuri ya Upwork. Wasifu (profile) huu ni muhimu kwa sababu itakuwa jambo la pili wateja wako wanaona baada ya kutuma maombi ya kazi. Kwa kifupi, profile nzuri ya kazi inapaswa:

  • Kuwa na picha yako nzuri
  • Kuwa rahisi na wazi katika kuelezea kile unachofanya.
  • Kueleza sifa zako za kitaaluma na kiakademia.
  • Kuwa na kitambulisho (anwani) cha kitaaluma.
  • Kuwa na video ya kuitambulisha inayoipa profile yako uzito.
  • Kuunga kazi nyinginezo ulizofanaya kwenye wasifu yako.

Onyesha/Tambulisha Kazi Yako

Katika wasifu wako, unapaswa kuongeza kazi zako nyinginezo. Hii inajumuisha baadhi ya kazi ya awali ambazo umezifanya. Kwa mfano, kama wewe ni msanidi wa programu (app developer), unapaswa kuonyesha baadhi ya programu ulizoziunda. Ikiwa wewe ni mwandishi, unapaswa kutoa viungo kwa baadhi ya kazi zako za zamani. Unahitajika kufanya vivyo hivyo hata kwa makundi mengine yote.

Maombi ya Kazi

Baada ya kuunda wasifu wako, unapaswa sasa kuanza kuomba kazi zinazofikia sifa zako. Ili kufanya hivyo, unahitaji kuhakikisha kwamba:

  • Maombi yako yanaelezea ujuzi wako bora.
  • Inaonyesha kwa nini wewe ni bora kuliko waombaji wengine.
  • Inaonyesha baadhi ya kazi zako za zamani.
  • Ina vifungo vinavyoonyesha kazi yako ya zamani.
  • Wewe ni miongoni mwa watu wachache wa kwanza kuomba.
  • Umeyasoma maelezo yote ya kazi.

Kazi Yenyewe

Ikiwa utabahatika kupata mteja, unapaswa kufanya kazi ya hali ya juu. Ikiwa huna uhakika kuhusu chochote, unapaswa kuhakikisha kupitia mteja. Vilevile, unapaswa kuwasilisha kazi kwa wakati. Ikiwa mteja anaomba marekebisho, unapaswa kuyafanya haraka iwezekanavyo.

Baada ya kukamilisha kazi, unapaswa kumwomba mteja akutolee maoni mazuri na akutuze ifaavyo. Wateja daima watampendelea freelancer mwenye kutolewa maoni mazuri na aliye na kiwango cha juu cha tuzo.

Jambo la Ziada

Ili kufanikiwa kama freelancer wa Upwork, lazima ufuate miongozo iliyowekwa na kampuni. Ikiwa utashindwa kufanya hivyo akaunti yako inaweza kufutiliwa. Baadhi ya ukiukwaji wa kawaida unaopaswa kuepuka daima ni:

  • Kuomba malipo nje ya jukwa hili. Licha ya kwamba hii inaweza kukusaidia kuepuka kutozwa ada kubwa, inaweza kukufanya upoteze akaunti yako.
  • Kushindwa kutekeleza mikataba yako. Ikiwa utafanya hivyo, wateja wanaweza kulalamika kwa upwork, na kukusabababishia kupoteza akaunti yako.
  • Upwork haikuruhusu kutuma anwani zako za kibinafsi kwa wateja.
  • Maneno ya unyanyasaji au usumbufu kwa wateja

Ninapataje Malipo Kutoka kwa Upwork?

Upwork huwa na uchaguzi kadhaa wa jinsi ya kupokea fedha zako. Unaweza kutoa/kupokea fedha moja kwa moja kwenye akaunti yako ya benki au kutumia mawakala kama vile PayPal, Payoneer na Mpesa nchini Kenya.

Upatikanaji wa mbinu za malipo hutofautiana miongoni mwa nchi. Chaguzi za malipo zinazopatikana kwako zitaonyeshwa kwenye akaunti yako wakati unapoongeza njia ya malipo.

Ada ya Upwork

Unaweza kuwa na unajiuliza, “Ni vipi Upwork hulipa pesa?”
Hutozwi ada ya kujiunga na kuunda wasifu wako kwenye upwork. Hata hivyo, kama mfanyakazi wa kujitegemea, unatozwa ada (sliding fee) kulingana na malipo yako ya maisha kwa kila mteja asiye na biashara. Malipo ya huduma ni sawa hata kama mikataba ni ya saa, bei maalum, au ya kimiradi. Ada hii ni kama ifuatavyo.

  • Kati ya dola 0 – dola 500: Utalipa asilimia 20
  • Kati ya dola 500.01 – dola 10,000: Utalipa asilimia 10
  • Kati ya dola 10,000.01 au zaidi: Utalipa asilimia 5

Jinsi ada za Upwork zinavyofanya kazi: Katika mradi wa dola 600 na mteja mpya, ada yako ya huduma itakuwa asilimia 20 kwa dola 500 na asilimia 10 kwenye dola 100 iliyobaki. Mapato yako baada ya ada yatakuwa dola 490.

‘Sliding fees’ haitozwi kwa mikataba yenye wateja wanaoitwa ‘Enterprise clients.’ ‘Enterprise clients’ wa Upwork hujumuisha biashara chipuzi (startups) zinazokua kwa haraka na hata kampuni kubwa za kimataifa. Upwork hujadili mikataba binafsi na kampuni hizi kwa kuangazia upekee wake. Kwa ujumla, mikataba ya wateja wenye biashara ina ada funge ya huduma ya asilimia 10.

Ikiwa wewe ni mfanyakazi wa Upwork aliyeoredheshwa kama bora (Top Rated) au mwenye talanta inayoinuka (Rising Talent) aliyeajiriwa kwa kazi za kipekee (Featured Jobs) utalipa ada ya huduma iliyopunguzwa (discount). Kazi za kipekee huwa ni zile ambazo mteja amelipa ili kuzifanya zionekana za kipekee ikilinganishwa na zingine (sawia).

Je, Upwork ni Halali?

Ndiyo, Upwork ni jukwa la kikazi halali la mtandaoni. Hata hivyo, mara kwa mara, kunaweza kuwa na matapeli (scammers) kwenye jukwaa hilo. Lakini kampuni inayomiliki jukwaa hili ni halali na yenye kuaminika. Utapata kulipwa baada yako na mteja kuipitia na kuihakiki kazi. Kwa bahati nzuri, upwork ina mchakato wa kushughulikia migogoro ikiwa haukulipwa kwa kazi uliyofanya.

Majukwaa mbadala ya Upwork

Mbali na Upwork, kuna majukwaa mengineyo maarufu kama vile:

Jiunge na Upwork Upate Kazi Mtandaoni

Hitimisho

Kwa miaka mingi sasa, Upwork imejijengea umaarufu na uwezo unaowaunganisha freelancers duniani kote na biashara na watu binafsi. Matokeo yake ni kuwa, watu wengi sasa hujipatia mamilioni ya dola kila mwaka kama wafanyakazi wa kujitegemea. Kwa kufuata hatua tulizotaja hapo juu, wewe pia unaweza kufanikiwa katika hili.

Makala Zaidi ya Jinsi ya Kujipatia pesa kwenye Intaneti