Nchi Zenye Huduma za Afya kwa Wote Duniani

Tafsiri:
en_US

Huduma za Afya kwa Wote ni mpango wa serikali wa kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wote bila kuangazia uwezo wao wa kugharamia tiba. Mwaka wa 1948, Shirika la Afya Duniani lilitangaza afya ya msingi kama ya haki za binadamu na kutokea wakati huo pamekuwa na ongezeko la kutafutwa kwa huduma hizi za afya. Kiwango kikubwa cha ufadhili wa huduma za afya kwa wote hutokana na kodi na ushuru unaotozwa mapato na mishahara. Baadhi ya nchi, inawalazimu wananchi kununua bima ya afya. Katika nchi nyingi, huduma za afya zinafadhiliwa na njia zaidi ya moja.

#### Aina ya Huduma za Afya kwa Wote. Utofauti baina ya nchi unaweza kuwa mkubwa sana.

– Nchi kama vile Uingereza, Norway, Italia na sehemu za Uhispania zina huduma za afya za bure kwa wananchi. Huhitaji kuwa na bima ya afya ya kibinafsi ili uweze kuhudumiwa na daktari au hospitali. Watu wana uhuru wa kuchagua na kuongeza bima ya afya ya kibinafsi ya kupata huduma za afya binafsi.
– Katika nchi kama vile Canada, Australia, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Singapore na Uswisi, serikali husaidia kufadhili huduma za afya zinazotolewa na mashirika ya kibinafsi. Nchi hizi zimetekeleza mfumo wa bima ya afya unaohusisha huduma kwa umma na kibinafsi kwa tiba ya kimsingi.
– Bima ya Afya nchini Marekani hupokea ruzuku kutokana na Obamacare na kufikia mwaka wa 2019 iliwajibishwa.
– Baadhi ya nchi kuchanganya huduma za afya na mifumo mingine kama vile kulipia tu unapopokea matibabu, malipo ya mapema na bima binafsi ili kuleta ushindani na hivyo kupungua kwa gharama ya serikali.

Wakati serikali inagharamia huduma za afya, inahakikisha kwamba hospitali na madaktari wanatoa huduma bora kwa gharama ya chini. Serikali inaweza pia kutumia uwezo wa kununua ili kuhakikisha watoa huduma wanatoza bei nafuu.

Ramani ya huduma za afya duniani na ChartsBin.com.

Hii ni orodha ya nchi barani Afrika, Amerika na Ulaya zinazotoa Huduma za Afya kwa Wote.

Afrika

Algeria

Algeria ina huduma za afya kupitia mtandao mpana wa hospitali, kliniki na zahanati. Huduma hizi za afya huafadhiliwa na usalama wa kijamii. Hata hivyo, bado watu kulipa kiwango fulani cha gharama kwa sababu ruzuku ya serikali hulipia asilimia ndogo tu. Maskini Watu wenye kipato cha chini hupata huduma za bure za afya ilhali matajiri wenye uwezo wa kifedha hujilipia.

Botswana

Serikali inasimamia asilimia 98% ya vituo vya afya. Wananchi wote hupata huduma za matibabu bure. Wao hulipa ada ndogo ya BWP 70 ($ 6.60) kwa ajili ya huduma nyingine za afya mbali na huduma za kupunguza makali ya virusi kurefusha maisha na afya ya uzazi ambayo hutolewa bure.

Burkina Faso

Nchi hii hutoa afya kwa wote kupitia Bima ya Afya kwa Wote (AMU). Raia na vikosi vya kijeshi husimamia huduma hizi.

Misri

Wizara ya Afya inafanya kazi katika hospitali za umma na kuwasaidia wananchi kupata huduma za afya bure. Hata hivyo, wale wenye uwezo wa kulipia huduma za afya wako huru kufanya hivyo.

Ghana

Nchi ina Bima ya Afya na wananchi hutozwa malipo kulingana na kipato chao. Huduma za kiafya huendeshwa na Wizara ya Afya au Huduma ya Afya ya Ghana.

Mauritius

Huduma za afya ni bure bila malipo kwa wananchi wake wote.

Morocco

Serikali inasimamia asilimia 85 ya sekta ya afya ya umma. Huduma zao hasa huwazingatia maskini wasiojiweza katika jamii ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za huduma za kibinafsi za afya. Mpango huu unafadhiliwa na Hazina ya Kitaifa ya Jamii inayogharamia asilimia 16 ya idadi ya watu.

Rwanda

Ina mfumo wa bima ya afya ya jamii ambapo watu hutozwa ada kulingana na mapato yao kuelekea mfuko wa bima ya afya. Wenye kipato cha juu hulipa zaidi wakati wale wenye kipato cha chini hupata misamaha ya malipo lakini kuhitajika kulipa asilimia fulani ya gharama za matibabu.

Ushelisheli

Serikali inaendesha shughuli zote za vituo vya afya na hivyo hutoa matibabu ya bure kwa wananchi.

Afrika Kusini

Afya ya umma ambayo hutoa huduma za matibabu kwa wananchi wengi haina wahudumu wa kutosha wala fedha za kutosha. Hata hivyo, kuna mfumo wa kibinafsi ambao unawahudumia tu matajiri kwani pana vifaa na huduma bora zaidi.

Tunisia

Afya ya umma inaendeshwa kupitia Bima ya Afya ya Kitaifa. Wananchi wanapata huduma za matibabu katika vituo vinavyomilikiwa na serikali kwa kulipa ada ya chini kwa ushirikiano wa malipo na serikali. Wale walio na mapato ya chini hupokea misamaha ya ushirikiano wa malipo.

Amerika

Argentina

Huduma za afya hutolewa kwa njia ya ushirikiano kati ya wafanyakazi na vyama vya wafanyakazi kupitia mipango ya kufadhiliwa, bima ya serikali, hospitali za umma na mipango ya bima ya kibinafsi. Huduma hii inatolewa kwa wote.

Bahamas

Baada ya kuidhinishwa Agosti, Sheria ya Bima ya Afya ya Kitaifa inatoa huduma za afya za msingi na hata kuenea kwa huduma maalum.

Brazil

Huduma za afya kwa wote ilipitishwa mwaka 1988 ingawa huduma za afya bado zilikuwa zinapatikana miaka mingi kabla. Marekebisho ya mwaka wa 1969 ya katiba ilikubalisha kodi ya asilimia 6 ya mapato yote kwa ajili ya huduma za afya.

Canada

Sheria ya Afya ya ilipitishwa mwaka wa 1984 kuharamisha hospitali na madaktari kutoza ada ya ziada juu kwa wagonjwa. Kwa njia ya ufadhili wa umma, mfumo huu unatoa huduma zaidi katika hospitali za kibinafsi. Madaktari hawapokei mishahara ya kila mwaka. Badala yake, wao hukusanya ada inayotokana na huduma. Asilimia 29 ya huduma ya afya ya Canada innagharamiwa na watu binafsi. Wengi wa wananchi wa Canada wana bima za kibinafsi kupitia waajiri wao na huwezesha gharama zote.

Chile

Serikali inatoa huduma za afya kupitia FONASA, Hazina ya Taifa ya afya na bima za kibinafsi. Wafanyakazi na wastaafu huchangia asilimia 7 ya mapato yao kwa ajili ya bima ya afya isipokuwa wastaafu maskini wasiojiweza kiuchumi. FONASA hutoa huduma kwa wanawake wajawazito, wategemezi wa wafanyakazi walio na bima, watu masikini, watu wanaoishi na ulemavu na wenye matatizo ya kiakili.

Colombia

Mageuzi ya mfumo wa afya yalifanywa ili kutoa huduma bora ambazo ni endelevu zitakazohakikisha wananchi wote wananufaika.

Costa Rica

Huduma za afya kwa wote zinafadhiliwa kupitia mfumo wa bima ya kijamii kupitia wafanyakazi walioajiriwa. Huduma hii ilipanuliwa baadaye ili kuwajumuisha wategemezi wa wafanyakazi kati ya 1961 na 1975. Upanuzi zaidi ulichangia kuingizwa huduma za msingi, matibabu maalumu, huduma za malazi hospitalini na pia kutibiwa na kuruhusiwa kwend nyumbani kwa watu wanaoishi katika maeneo ya vijijini. Baadaye, iliweza kupanuliwa kujumuisha wakulima na wale wa mapato ya chini. Nchi imeepuka kutumia bima ya kijamii inayochangia kwa kutokuwa na usawa katika nchi nyingi. Kupitia mfumo wa Caja Costarricense de Seguro Social (CCSS), wananchi wa Costa Rica sasa wanaweza kufurahia huduma za matibabu za bure. Matibabu ya kibinafsi yanapatikana. INS hutoa huduma za afya ya kibinafsi kusaidia CCSS.

Cuba

Nchi hii ina Mfumo wa Kitaifa wa Afya unaogharamia wajibu wa kifedha na uendeshaji wa shughuli za afya ya wananchi wote. Hakuna hospitali ya kibinafsi kwani vituo vya afya vyote vinamilikiwa na serikali. Mfumo huu unashughulikia watu wengi, ila hauna fedha za kutosha na wahudumu wa kutosha. Serikali hupanga misioni kwa madaktari katika nchi nyingine.

Mexico

Huduma ya afya ya umma hufadhiliwa kikamilifu au kwa sehemu kulingana na hali ya mtu ya ajira. Wananchi wanastahiki kupokea huduma ya afya ya bure. Instituto Mexicano del Seguro Social (IMSS) inasimamia mipango ya afya kwa ajili ya watu walioajiriwa na wategemezi wao.

Hata hivyo, haitoi huduma kwa watu wanaofanya kazi katika sekta binafsi. Badala yake, wao hupata huduma kutoka Instituto de Seguridad y Servicios Sociales de los Trabajadores del Estado (ISSSTE). Pia kuna huduma za afya za bure na zilizoruzukiwa ambazo zinapatikana kwa wananchi wote.

Peru

Bima ya afya ya umma inalenga kuongeza ubora wa afya kwani inasisitizia afya ya uzazi na watoto. Pia, inakusudia kulinda maskini kutokana na kufilisishwa kifedha kutokana na gharama za ugonjwa. Watu wote ni wanalazimishwa kujiunga na bima za afya kwa wote.

Trinidad na Tobago

Trinidad na Tobago wana mfumo bima ya afya kwa wote ambao unatoa afya ya msingi ambayo inapatikana katika nchi nzima. Bimah ii hutumiwa na wananchi kutafuta msaada wa huduma ya matibabu kwa vile ni bure.

Marekani

Takribani asilimia 92 ya wananchi wana bima ya afya. Massachusetts ilikuwa jimbo la kwanza kuanzisha bima ya afya kwa wote. Sheria ya Huduma ya Afya na Elimu ya Maridhiano ya 2010 ilipanua bima ili kuwafidia wakazi wote wa kisheria kufikia mwaka wa 2014. Hata hivyo, utekelezwaji wake kamili haukufanyika kwani baadhi ya Majimbo yalishindwa kutekeleza upanuzi wa Medicaid ulionuia kutoa ruzuku ya bima ya afya kwa watu wenye kipato cha chini.

Data ya huduma ya afya kwa wote ya WHO na Benki ya Dunia.

Ulaya

Ufaransa

Serikali inasaidia huduma ya afya kupitia bima ya afya ya taifa. Serikali inawajibikia asilimia 70 ya huduma ya matibabu na kati ya asilimia 35 na 100 ya dawa zinazotakiwa. Inaorodheshwa kama taifa bora katika dunia kwa maswala ya afya.

Ujerumani

Ni miongoni mwa bima za afya za kijamii kongwe, kutokea mwaka wa 1883. Waajiri huchangia nusu ya waajiri wao bima ya afya ilhali watu waliojiajiri hujilipia mchango mzima wao wenyewe. Karibu asilimia 90 ya wakazi wana mpango rasmi wa kisheria wa bima ya afya, ambao hushughulikia karibu hazina 100 za umma za magonjwa. Wananchi wengineo wana bima binafsi ambazo hasa hutumiwa na wafanyakazi wa kibinafsi na watu wenye mapato makubwa.

Ugiriki

Wizara huratibu huduma za matibabu kwa ajili ya Afya na Mshikamano wa Jamii huku Huduma ya Kitaifa ya Afya inatoa huduma za afya ya umma. Huduma za kiafya za Ugiriki zinaorodheshwa 14 kulingana na ripoti ya Shirika la Afya Duniani ya 2000.

Guernsey/Jersey

Wakazi wa visiwa wana huduma za afya kwa wote sawia na ya Uingereza. Wengi wa madaktari na wauguzi hupokea mafunzo kwa mtazamo wa afya ya Uingereza.

Iceland

Manispaa ya Mitaa hutoa huduma ya afya. Huduma za afya kwa umma hufadhiliwa na ushuru. Idadi yote ya wakaazi wa Iceland hupokea huduma za afya kwa kipimo sawa.

Ireland

Sheria ya Afya inadhibiti mfumo wa afya uliofanyiwa marekebisho mwaka wa 2004. The Huduma Tendaji ya Afya hutoa huduma za afya. Pia, kuna huduma za afya za kibinafsi. Asilimia 37 ya idadi ya watu wana kadi ya matibabu ambapo, mmiliki anaweza kupata huduma ya GP inayofadhiliwa na kodi ambayo inatoa € 2.5 kwa kila dawa zinazotakiwa.

Italia

Huduma ya afya ya umma inajulikana kama “Servizio Sanitario Nazionale” SSN katika Kiingereza; (Huduma za Afya ya Taifa). Huduma hii hufadhiliwa na ushuru na ni sawia na ya Uingereza. Huduma kama vile kuhudumiwa na daktari wa ujumla na elimu ya dharura ni bure ila huduma nyinginezo hutofautiana kwa njia ua ushirikiano wa malipo. Pia, kuna mifumo sambamba ya kibinafsi kwa huduma za meno na macho.

Uholanzi

Huduma za msingi na tiba zina bima ya lazima huku aina nyinginezo za huduma kama vile ile ya wazee, wagonjwa mahututi na wagonjwa wa kiakili kugharamiwa na bima ya kijamii. Bima hii ya kijamii hufadhiliwa kutokana na ushuru. Takribani asilimia 55 ya huduma ya afya hufadhiliwa moja kwa moja na serikali, na asilimia 45 inafadhiliwa na bima ya umma.

Watoa bima lazima wakidhi huduma za tiba na huduma za msingi na gharama zinazotokana na dawa. Ni kinyume cha sheria kwa wanaotoa bima kukataa au kutia vikwazo katika maombi ya matumizi ya bima ya afya au kukataa kugharamia matibabu yaliyopendekezwa na daktari. Mfumo huu unafadhiliwa na asilimia 50 kutoka malipo ya kodi (ya mishahara) inayolipwa na waajiri huku serikali ikitoa asilimia 5 ya ziada na asilimia 45 iliyosalia ya mchango hulipwa na watu binafsi waliochukua bima.

Kiwango cha ada inayotozwa kwa watu wazima ni karibu € 100 kila mwezi. Serikali husaidia watu wenye kipato kidogo ikiwa hawawezi kumudu. Kwa watoto wenye umri usiozidi miaka 18 wao hulipiwa gharama zote bila malipo ya ziada.

Norway

Huduma ya afya ya wote inafadhiliwa na ushuru na mfumo huo unaendeshwa kimajimbo. Ufadhili huu hutoka serikali za wilaya na manispaa. Huduma ya meno huwalipia watoto chini ya miaka 18, ilhali watu wazima pia hujumuishwa na kulipiwa baadhi maradhi. Norway ni miongoni mwa nchi zilizoorodheshwa kuwa na huduma bora za afya.

Ureno

Ureno imekuwa ikitoa huduma za afya inayojulikana kama Servico Nacional de Saúde (SNS) tangu 1979. Huduma hii inatolewa kwa wakazi Ureno na wa kigeni. Yeyote anaweza kujiunga na Taasisi ya Matibabu ya Dharura ya Kitaifa National Medical Emergency Institute (INEM) kwa kupiga 112.

Romania

Ina ukamilifu wa huduma ya matibabu ambayo inatoa uchunguzi wa kimatibabu, upasuaji na huduma za baada ya operesheni. Serikali hufadhili kliniki zote za umma na hospitali, huku huduma ya meno hazifadhiliwi na serikali. Hata hivyo, baadhi ya hospitali hutoa huduma ya meno bila ya malipo.

Uingereza

Nchi zote za Uingereza zina Huduama za Afya ya Kitaifa kwa wakazi wa kudumu. Ni mfumo unaofadhiliwa kwa ushuru. Awali mfumo huu ulikuwa umeundwa kuwa bure bila ya malipo lakini mabadiliko yalifanywa ili kukidhia malipo ya dawa na tiba ya meno. Hata hivyo, watoto chini ya miaka 16 na baadhi ya watu wanaopokea faida fulani bado wanaweza kupata huduma hizi. Lakini tangu huduma za afya kugatuliwa, kuna utofauti wa huduma za afya kulingana na nchi husika.

Uswisi

Huduma za afya zinadhibitiwa na Sheria ya Bima ya Afya ya Kitaifa ya mwaka 1994, kote inakopatikana. Wananch wote lazima wawe na Bima ya Afya ndani ya miezi mitatu baada ya kuchukua makazi yao ya Uswisi.

New Zealand

Mfumo wa afya unafadhiliwa kutokana na ushuru. Shirika la Afya Duniani lilitambulishwa kuwa asilimia 77.4 ya gharama za huduma ya afya hukidhiwa na serikali, huku watu binafsi wakifidia gharama za huduma za kibinafsi.

Hitimisho

Kulingana na Shirika la Afya Duniani, huduma za afya kwa wote ina maana ya kwamba watu wote wanapata huduma za afya wanazohitaji (kuzuia, kukuza, matibabu, ukarabati na huduma za kupunguza) bila ya changamoto za kifedha wakati wa kulipia huduma hizi.

Shirika hilo linabainisha kuwa huduma za afya kwa wote ina athari ya moja kwa moja juu ya afya na ustawi wa wananchi. Upatikanaji na matumizi ya huduma za afya utawawezesha watu kukuza uzalishaji wao na kuchangia vilivyo kwa ajili ya familia na jamii zao. Pia, itaweza kuhakikisha kwamba watoto wanaweza kwenda shule na kusoma. Wakati huo huo, watu watakuwa na usalama wa kifedha na kuwazuia kuingizwa katika umaskini kutokana na kugharamia huduma ya afya wao wenyewe.