Tangu ilipoanzishwa mwaka 1998, Soko la Hisa la Dar Es Salaam (DSE) ni moja ya chaguzi za uwekezaji zinazopatikana kwa raia na wageni nchini Tanzania.
Kulingana na Investment Safety Rankings, Tanzania iko katika nchi 127 kati ya 192 kwa ubora wa kuwekeza, na kuifanya iwe ni ya wastani ukilinganisha na nchi nyingine Afrika.
Yaliyomo
Nani Anaweza Kuwekeza kwa DSE?
Wote Watanzania na wageni wanaruhusiwa kuwekeza katika soko la hisa. Walakini, wageni wanaruhusiwa kuwekeza hadi asilimia 60 katika jumla ya hisa katika kampuni.
Je Ni Vyombo Vipi Vya Fedha Ambavyo Wafanyabiashara Wanaweza Kununua na Kuuza?
Wafanyabiashara kwenye soko la hisa wanaweza kununua na kuuza hisa, hundi za kampuni na za serikali, n.k.
Jinsi ya Kufanya Biashara Kwenye Soko la Hisa
Kwanza, watu wenye nia ya kufanya biashara kwenye soko hili wanatakiwa kufungua akaunti na mmoja wa mawakala 14 wenye leseni.
1. Jaza Fomu ya Ufunguzi wa Akaunti ya CDS
Dalali wako atakupa fomu ya maombi. Mara tu itakapojazwa, utapata nambari ya akaunti ya kwenye mfumo wa elektroniki uitwao Central Depository System (CDS). Biashara zako zote zitarekodiwa kwa DSE kwa kutumia nambari hii.
2. Jaza Fomu ya Ufunguzi wa Akaunti Kwa Dalali
Utahitaji kujaza fomu ambayo inahitaji maelezo ya kibinafsi kama nambari ya kitambulisho, anwani, upendeleo kwa ukusanyaji wa gawio na malipo ya ada. Utahitaji pia kupeleka nakala ya pasipoti yako au leseni ya udereva.
Kwa usajili wa kampuni kwenye soko utahitaji vifuatavyo:
- Nakala ya cheti cha kusajiliwa kwa kampuni
- Nakala za vitambulisho vya wakurugenzi wa kampuni
- Nakala ya katiba ya kampuni
- Fomu ya maombi ya Akaunti ya amana kwa mwili wa shirika
3. Tuma Fedha Kwa Akaunti ya Dalali Wako
Unahitaji kutuma fedha za kufanyia biashara kwenye soko kwenye akaunti ya dalali. Unaweza kufanya hivyo kupitia benki au njia nyingine yoyote rahisi ya kuhamisha pesa.
4. Peana Agizo la Biashara
Basi unahitaji kuwasiliana na dalali wako kubainisha hisa unayotaka kununua.
.
Kampuni Kubwa Zilizoorodheshwa
- Tanzania Breweries (TBL): kampuni kubwa kwenye la soko DSE na mtayarishaji / msambazaji mkuu wa vinywaji nchini Tanzania.
- East African Breweries (EABL): kampuni ni ya pili kubwa kwenye soko la DSE
- Acacia (ACA): moja ya wachimbaji wakubwa wa dhahabu nchini Tanzania
- Tanzania Cigarette Company (TCC): kampuni kubwa kabisa ya tumbaku nchini Tanzania
- Vodacom (VODA): kampuni kubwa zaidi ya simu nchini Tanzania
Kampuni Zilizoorodheshwa
Na. | Msimbo wa Kampuni Kwenye Soko | Kiungo |
---|---|---|
1 | ACA | Tazama Wasifu |
2 | CRDB | Tazama Wasifu |
3 | DCB | Tazama Wasifu |
4 | DSE | Tazama Wasifu |
5 | EABL | Tazama Wasifu |
6 | JHL | Tazama Wasifu |
7 | KA | Tazama Wasifu |
8 | KCB | Tazama Wasifu |
9 | MBP | Tazama Wasifu |
10 | MCB | Tazama Wasifu |
11 | MKCB | Tazama Wasifu |
12 | MUCOB | Tazama Wasifu |
13 | NICO | Tazama Wasifu |
14 | NMB | Tazama Wasifu |
15 | NMG | Tazama Wasifu |
16 | PAL | Tazama Wasifu |
17 | SWALA | Tazama Wasifu |
18 | SWIS | Tazama Wasifu |
19 | TBL | Tazama Wasifu |
20 | TCC | Tazama Wasifu |
21 | TCCL | Tazama Wasifu |
22 | TICL | Tazama Wasifu |
23 | TOL | Tazama Wasifu |
24 | TPCC | Tazama Wasifu |
25 | TTP | Tazama Wasifu |
26 | USL | Tazama Wasifu |
27 | VODA | Tazama Wasifu |
28 | YETU | Tazama Wasifu |
Hitimisho
Soko la Hisa la Dar Es Salaam ni mwanachama wa Chama cha Soko la Hisa la Afrika na Shirikisho la Masoko ya Hisa Duniani (WFE). Kwakuwa Tanzania ni sehemu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, DSE, Soko la Hisa la Nairobi na Soko la Hisa la Uganda hatimaye yatakuwa soko moja la hisa la Afrika Mashariki.
Ili kuwekeza katika soko hili, unashauriwa kufanya utafiti wa kina, uwe mwangalifu na uweke malengo ya muda mrefu na usambaze uwekezaji wako ili kupunguza hatari inayotokana na kuwekeza kwenye kampuni moja.

Ndesanjo ni mwanablogu mzoefu na mwandishi wa habari.