Orodha ya Masoko Online Afrika

Tafsiri:
en_US

Uwezo wa mawasiliano ya kimataifa kwa kompyuta umetoa nafasi kwa wauzaji wa Afrika kufanya biashara zao mtandaoni. Kuna mifumo mbalimbali ya mtandaoni barani Afrika ambayo husaidia wauzaji kuongeza wateja wao na mauzo bila ya kushirikiana ana kwa ana. Makala haya yataonyesha baadhi ya masoko online maarufu Afrika.

Faida za Kuuza Bidhaa Mtandaoni

Masoko ya mtandaoni huwapa wauzaji wa Afrika faida mbalimbali. Baadhi yazo ni:

  • Upatikanaji wakati wowote. Masoko ya mtandaoni barani Afrika yana muundo ambao unaruhusu watu binafsi kununua bidhaa wakati wowote, iwe mchana au usiku. Hivyo basi, una uwezo wa kuuza bidhaa zako hata wakati unapolala.
  • Uwepo wa soko kubwa. Wakati wa kuuza bidhaa kutoka duka la ana kwa ana, unaifikia idadi ndogo ya wateja. Masoko ya mtandaoni hutoa ufumbuzi mzuri kwa changamoto hii kwa kuwezesha kuuzia idadi kubwa ya watu ndani na nje ya eneo lako.
  • Usimamizi rahisi. Masoko ya mtandaoni kwa kawaida hufanya kazi kwa bidii kwa niaba yako. Hii ni pamoja na kutoa maagizo na uhusiano mwema na wateja baada ya kuuza. Unachohitaji kufanya ni kuwa na bidhaa bora na kuzipakia ipasavyo.

Afrikrea

Wavuti huu umeishia kuwa mojawapo wa masoko kubwa ya mtandaoni barani; swala linalothibitishwa na idadi yake ya wateja. Afrikrea ina zaidi ya maduka 5400 na imewahudumia wateja katika nchi 110 duniani kote. Zaidi ya hayo, tovuti hii ina takribani wageni 260,000 kila mwezi na imekuwa na zaidi ya maagizo ya bidhaa 66,000.

Soko hili hulenga wateja wanaopenda bidhaa zenye asili ya Afrika. Ina nia ya kufanya kazi na wabunifu ambao wanatumia miundo ya Afrika na mitindo ya bihaa ambayo inaweza kupata umaarufu kwa soko la kimataifa. Wauzaji wanaweza kuuza kitu chochote ikiwemo mapambo ya vito, mikoba, nguo, vitambaa, na mapambo ya sanaa.

Baadhi ya faida ya kuuza kwenye Afrikrea ni pamoja na uwepo wa usaidizi uliowekwa kusaidia kusimamia matangazo na orodha, malipo ya moja kwa moja kutoka kwa mteja, na orodha ya huduma zisizotozwa ada. Zaidi ya hayo, unatakiwa tu kulipa ada ya asilimia 10-15 baada ya kuuza bidhaa.

Ili kufaidika na Afrikrea kama muuzaji, unahitaji kufungua duka lako kwenye wavuti bila malipo. Mara tu baada ya mnunuzi kuagiza bidhaa yako, utapata taarifa kupitia ujumbe wa simu au barua pepe. Baada ya kupokea maagizo haya, una saa 48 ili kuthibitisha. Mara baada ya kuthibitishwa, utapokea fedha katika mkoba wako wa mtandaoni.

Ni muhimu kutambua kuwa muuzaji anawajibikia usafirishaji wa bidhaa.

 

Zando

Kama wewe ni mfanyabiashara nchini Afrika Kusini na unasaka jukwaa la masoko ya mtandaoni, Zando ni mojawapo ya chaguzi bora. Wauzaji wanaweza kuuza bidhaa zao zinazohusiana na mtindo, urembo, au vifaa vya nyumbani. Ina takribani wageni milioni 3.5 kila mwezi na zaidi ya bidhaa 800 zinazouzwa kwenye tovuti hii. Muuzaji anatarajiwa kushughulikia upatikanaji wa bidhaa na pia upakiaji. Baada ya hapo, Zando inachukua huduma ya usafirishaji wa bidhaa, huduma za baada ya mauzo, na mawasiliano na mteja.

Ili kuanza kuuza kwenye soko hili la mtandao, unahitaji kujiandikisha kwenye tovuti. Baada ya kufanya hivyo, sasa upo tayari kupakia bidhaa yako pamoja na maelezo husika. Ili kupakia picha halisi kwenye jukwaa hili la kibiashara, bidhaa hizi zinakaguliwa na kampuni kabla ya kuwekwa kwenye soko.

Faida za mfumo huu ni kwamba una uwezo wa kusimamia maagizo ya bidhaa na bidha zilizopo. Baada ya kupokea maagizo ya bidhaa, una masaa 36 kupakia bidhaa na kutuma kwenye ghala la Zando. Utapokea malipo kati ya siku 30 baada ya kuwasilishwa kwa bidhaa.

 

Konga

Konga ni mojawapo ya masoko ya mtandaoni maarufu nchini Nigeria. Unaweza kuuza bidhaa mbalimbali kwenye tovuti ikiwa ni pamoja na bidhaa za mitindo na urembo, mapambo ya nyumbani na hata vifaa vya kielektroniki. Mojawapo ya sababu ya kuwa mfumo wa biashara bora ni ufanisi wa muundo wa mawasiliano ambao unaruhusu kuzungumza na wanunuzi wako. Zaidi ya hayo, unaweza kupata kuamua kuhusu bei ya bidhaa zako na pia maelezo mengine muhimu kama vile njia unayopendelea ya kuwasilishia bidhaa na njia ya malipo. Konga hutoza ada ya asilimia 3 ya mauzo.

Ilii kuanza kuuza kwenye Konga, unahitaji kutembelea tovuti yao na kujaza fomu ya kujisajili. Kampuni hii hatimaye itathibitisha maelezo yako na kuhakikisha una taarifa sahihi kuhusiana na njia za mawasiliano na maelezo ya benki. Mara tu baada ya kampuni kuhakikisha maelezo, utapewa afisa wa kukusaidia wakati wowote kwa namna yoyote iwezekanavyo.

Utapewa akaunti ya SellerHQ; ambayo itakusaidia katika usimamizi wa soko na inakuwezesha kusimamia hesabu yako, kupakia picha za bidhaa unazokusudia kuuza, na hata kufuatilia mauzo na mapato. Kama majukwaa mengineyo ya kimtandao barani Afrika yenye nia ya kudumisha uhalali wao, Konga hukagua bidhaa zilizopakiwa kabla ya kuwekwa kwenye tovuti. Mara tu baada ya mteja anapoweka maagizo ya bidhaa, una masaa 24 ili kuthibitisha na siku 3 ili kusafirisha bidhaa hiyo. Malipo hutumwa kwa akaunti yako ndani ya siku 3 baada ya mteja kupata bidhaa alizoagiza.

 

Jumia

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012, Jumia imeishia kuwa mojawapo ya soko kubwa la mtandaoni barani Afrika. Kwa sasa inahudumu katika zaidi ya nchi 10 za Afrika zikiwemo Kenya, Nigeria, Uganda, na Tunisia. Unaweza kuuza vitu mbalimbali kwenye jukwaa hili ikiwa ni pamoja na nguo, vitabu, vifaa vya kielektroniki, afya na urembo, na mapambo ya nyumbani. Ni muhimu kutambua kuwa Jumia inaruhusu tu bidhaa ambazo ni mpya, halali, na zenye ubora wa kuridhisha.

Ili kujiandikisha kwenye Jumia, unahitajika kwenda kwa tovuti yao na kubonyeza ” start selling now”. Wakati wa kusajili, hakikisha kuwa na maelezo muhimu kama vile anwani yako, eneo la duka, na aina ya bidhaa. Kampuni itatuma barua pepe ikiwa na kiungo chao cha “Vendor Hub”. Kwenye ukurasa huu, utakuwa na aina mbalimbali ya habari kama sehemu ya mpango wao kimafunzo. Pia utapata kiungo chao cha ukurasa wa “Seller Center”. Kwa kutumia kiungo hiki utajaza akaunti yako ya benki, maelezo ya bidhaa, na habari nyinginezo muhimu.

 

Kilimall

Tangu kuanzishwa kwake, Kilimall ni moja ya masoko online Kenya. Soko hili la mtandaoni ni sawia kama Jumia na majukwaa mengine yaliotajwa kwenye makala haya. Kwa mfano, pana kitengo cha muuzaji ambacho kinawezesha wauzaji kutangaza bidhaa zao.

Ili kuanza kuuza kwenye Kilimall, unahitaji kujiandikisha kama muuzaji. Hii inaweza kufanyika kwenye mtandao au kupitia programu ya Kilimall. Unaweza kuchagua kujiandikisha ama kama muuzaji wa kimataifa au wa nchini. Mara baada ya kufungua duka, sasa ni wakati wa kuchagua kwa usahihi aina ya bidhaa, pamoja na maelezo ya muhimu, na kupakia picha sahihi. Kwa kukamilisha hatua hizi rahisi, utakuwa tayari kufanya biashara katika soko hili la mtandaoni barani Afrika.

 

Hitimisho

Nyakati za kuwa na duka halisi la kuuza bidhaa zako zimepitwa. Kuwepo kwa mtandao kumeruhusu watu binafsi kufungua maduka ya mtandaoni na kufikia soko kubwa. Kutathmini ubora na sera za kila taasisi itasaidia kutambua zaidi soko mwafaka la mtandaoni la kutumia barani Afrika.