Biashara za Mtandaoni Zinazolipa

Tafsiri:

Kutokana na ongezeko la matumizi ya simu za kisasa na intaneti, biashara za online zimepanuka. Kwa bahati mbaya, wajasiriamali wengi na watu wasio na ajira hawana taarifa za kutosha kuhusu jinsi ya kufanya biashara mtandaoni. Hivyo basi, makala haya yananuia kutoa maelezo muhimu kuhusu jinsi ya kufanya biashara za mtandaoni barani Afrika.

Soma makala haya kwa Kiingereza: How to start an online business in Africa

Manufaa ya Kuanzisha Biashara ya Mtandaoni

  • Gharama zake ni za chini ikilinganishwa na biashara zinazohitaji majumba/maduka.
  • Unaweza kuwafikia wateja wengi zaidi mtandaoni ikilinganishwa na nje ya mtandao. Ni njia mwafaka ya uendeshaji wa biashara saa 24 hata ukiwa umelala.
  • Sio lazima umiliki duka au jukwaa la biashara ya mtandaoni kwani unaweza kuuza bidhaa kwenye maduka kama vile Michongo na Zudua. Tazama orodha ya maduka mtandaoni Afrika unayoweza kutumia kuuza bidhaa mtandaoni na pia maduka ya biashara mtandaoni Tanzania.

Biashara ya Mtandaoni Inayolipa

Kuna orodha ndefu ya biashara za mtandaoni zenye faida barani Afrika. Baadhi yazo ni:

1. Bidhaa za Mapambo na Ulimbwende

online business ideas africa
OnCheck ni duka la mtandaoni liuzalo mitindo ya Kiafrika.

Katika ulimwengu wa kisasa, kila mtu anataka kuonekana vizuri na aingiane sawasawa na mitindo inayovuma. Unaweza kupata pesa kupitia dhana hii kwa kuuza bidhaa kama vile nguo, viatu, mapambo ya vito, bidhaa nywele, marashi, na mikoba. Kulingana na mtaji wako na wateja walengwa, unaweza kupata bidhaa mpya kabisa au hata zilizotumika kiasi.

2. Bidhaa za Uboreshaji Nyumbani

Watu wengi wana hamu ya kupata bidhaa ambazo zinaweza kubadilisha nyumba zao ziwe makazi bora zaidi. Ni dhahiri basi, kwamba pana soko kubwa la vyombo, bidhaa za mapambo ya makazi, na samani.

3. Bidhaa za Watoto

Wazazi wa kisasa wako tayari kugharamika hata ziada ili kuhakikisha kwamba watoto wao wana maisha mazuri. Vifaa bandia vya kuchezea, nguo za kimitindo pamoja na vifaa vinginevyo vya kuwalea watoto vimekuwa sasa mahitaji ya kimsingi, na wala si vya kifahari. Kwa hivyo, mtu anaweza kuwa na biashara yenye faida kwa kuziuza baadhi au nyingi ya bidhaa hizo mtandaoni.

4. Huduma za Ushauri wa Kibiashara

Hii ni mojawapo ya sekta kubwa ya huduma za kitaalamu duniani. Kuna kazi nyingi za ushauri ambazo mtu anaweza kuzishiriki kupitia teknolojia. Hizi ni pamoja na mahusiano ya umma (public relations), uongozi, mauzo (marketing), kazi, na ushauri wa kimawasiliano (communications consultancy). Hii ni biashara ya kufanya hata ukiwa nyumbani.

5. Kutoa huduma za Matukio na Sherehe

Tabaka la kati na juu katika Afrika linazidi kupanuka, na hivyo, watu wengi wananuia kuandaa matukio na sherehe za binafsi au kimashirika yatakayofana. Unaweza kujitoma katika shughuli hii kwa kutoa mahema, viti na vitu vinavyohusiana na sherehe, kukodisha uwanja wa matukio, huduma za upishi, au vifaa vya burudani. Huduma kama hizi zimepata sana uhitaji katika harusi, mazishi, sherehe za kumbukumbu za kuzaliwa, mikutano ya kampuni, na hata mikusanyiko ya kawaida ya familia.

6. Vyakula

Ukuaji wa miji na kuongezeka kwa idadi ya wataalamu ni baadhi ya mambo ambayo yamechangia kuongezeka kwa mahitaji ya maduka ya vyakula mtandaoni. Idadi kubwa ya waajiriwa katika miji ya Afrika iliyoendelea na hata inayoendelea hukosa muda wa kununua vyakula. Badala yake, unaweza kutoa uvumbuzi rahisi kwa kuhifadhi bidhaa zinazohitajika na kuwapelekea wateja wako kama vile kampuni ya Piki.

Namna ya Kufanya Biashara Mtandaoni

 

1. Isajili Biashara Yako

Katika hatua hii, unapaswa kuwa umefanya utafiti wa kina wa soko ili kuamua juu ya bidhaa au huduma unazokusudia kutoa pamoja na wateja wako walengwa. Baada ya hapo, hatua inayofuata ni kuisajili biashara hii ili upate leseni ya biashara online. Kwa kufanya hivyo, utaihalalisha biashara yako kisheria na hivyo kuongeza nafasi yako ya kupata ufadhili kutoka kwa wawekezaji binafsi au kupata mikopo kutoka kwa taasisi za fedha. Utahitaji pia kusajili jina la biashara.

2. Tambua Mbinu Mwafaka Mtandaoni

Kulingana na biashara ya online unayofanya, unaweza kuchagua kutumia soko la mtandaoni lililojengwa tayari (ecommerce platform), au kwa kujijengea tovuti yako mwenyewe, au utumie njia mseto. Masoko ya kimtandaoni ambayo unaweza kutumia kuuza biashara zako ni pamoja Zudua, Kilimall, na mengine mengi. Hata hivyo, kwa kutumia majukwaa kama haya, itakugharimu ada fulani.

Vilevile, unaweza kujijengea tovuti yako mwenyewe kupitia Shopify, WordPress, WooCommerce na BigCommerce. Mbinu hii itakuwezesha kudhibiti jinsi unavyotaka mwonekano wa tovuti yako uwe. Ni muhimu kutathmini kwanza jinsi tovuti mbalimbali zilivyo kabla ya kufanya uchaguzi dhahiri. Ili kupanua idadi yako ya wateja, unaweza pia kutumia mbinu mesto; ambayo inahusu kutumia soko la mtandaoni na pia tovuti yako binafsi.

 biashara za online
Unaweza kuuza kupitia duka la Afrikrea.

3. Amua Kuhusu Mkondo wa Malipo Unaokufaa

Unaweza kuchagua kupeana akaunti ya benki kwa wateja kuwekea amana ya malipo au kutumia njia hizi za mtandao za malipo kwa ajili ya biashara barani Afrika. Kwa kutegemea nchi ya Afrika unamohudumia, njia hizi za mtandao za malipo zinajumuisha malipo kwa pesa rununu, PayPal, n.k. Kama utakuwa unahitaji teknolojia ya kupokea malipo kwa njia ya kadi (debit card na credit card) basi utahitaji kutumia huduma za malipo mtandaoni kama vile MFS Africa, Flutterwave, PesaPal miongoni mwa nyingine.

4. Anza kuuza

Usisubiri hadi kila kitu eti kionekana kuwa kamilifu. Kama ilivyo kwa maduka halisi, biashara ya mtandaoni huchukua muda wa kufikia kiwango unachokitaka. Ili kufanikisha mauzo, unaweza kutumia mitandao ya kijamii, maonyesho, punguzo (discount), matukio muhimu, na hata mapendekezo kutoka kwa wateja wa awali. Uwezeshaji wa Kusaka Mtandaoni (Search Engine Optimisation) pia ni njia unayoweza kutummia ili kuwavutia watu zaidi kwenye tovuti au duka lako la mtandaoni. Tumia pia Google ili kupata miongozo mbalimbali ya jinsi ya kupata wateja mtandaoni au jinsi ya kutangaza biashara mtandaoni.

5. Uwasilishaji wa Bidhaa Unaoaminika

Kulingana na nchi unamoendeshea biashara, unaweza kutumia usafiri wa umma unaoaminika ili kufikisha bidhaa zilizonunuliwa. Pia, unaweza kuwasiliana na kampuni za kutuma mizigo na bidhaa kama vile Posta au kampuni chipukizi za usafirishaji haraka wa mizigo au huduma nyingineyo ili kuwafikia wateja wako.

6. Kupanua Biashara

Baada ya kuhakikisha kuwa biashara imestawi, unapaswa sasa kuangazia jinsi ya kuipanua na kuikuza hata zaidi. Utumiaji wa huduma za wataalamu ili kukidhi mahitaji yanayokua ni mojawapo ya njia bora za kufanya hivyo. Pia, ni muhimu kutathmini tabia za kimatumizi za wateja wako kama msingi wa kuanzisha, kuongeza, au kuondoa baadhi ya bidhaa.

Hitimisho la Biashara Mtandaoni

Sawa na mabara mengineyo, Afrika inapitia maendeleo makubwa ya kiteknolojia. Biashara ya mtandaoni ni mojawapo ya maendeleo hayo. Ukianzisha duka la mtandao na ukiwa unajua jinsi ya kuuza bidhaa mtandaoni au kutoa huduma mtandaoni, utapata fursa ya kuwafikia wateja wengi sana na kupata faida kubwa. Ikiwa utafuata hatua zilizojadiliwa katika makala haya, kama mwekezaji utakuwa umejihakikishia mafanikio ya biashara za online.

Soma Zaidi

This post is also available in en_US.