Jinsi ya Kuuza Kupitia Shopify

Tafsiri:
amen_USes_ES

Je, unakusudia kuanzisha biashara ya mtandaoni lakini hujui jinsi ya kufanya hivyo? Siku hizi, kuna watumiaji mabilioni wa mtandao ulimwenguni kote. Hii inamaanisha kuwa fursa ya kupata pesa online kwa kulenga watumiaji hawa ni bora ajabu. Wakati huo huo, mchakato wa kuanzisha biashara ya mtandaoni umefanywa kuwa rahisi kutokana na majukwaa mbalimbali ya ecommerce.

Baadhi ya majukwaa haya ni kama WooCommerce, Wix, Weebly, na Squarespace. Hata hivyo, jukwaa bora ambalo linajumuisha kila kitu unachohitaji kuendesha duka la ecommerce ni Shopify. Hii ni kampuni ya dola bilioni 31 ambayo ilianzishwa mnamo mwaka wa 2006. Makala haya yataelezea hatua rahisi za jinsi ya kuuza kupitia Shopify.

Manufaa ya Kuanzisha Biashara ya Mtandaoni

 • Gharama zake ni za chini ikilinganishwa na biashara zinazohitaji majumba/maduka.
 • Unaweza kuwafikia wateja wengi zaidi mtandaoni ikilinganishwa na nje ya mtandao. Ni njia mwafaka ya uendeshaji wa biashara saa 24 hata ukiwa umelala.
 • Sio lazima umiliki duka au jukwaa la biashara ya mtandaoni kwani unaweza kuuza bidhaa kwenye maduka kama vile Shopify.

Shopify ni nini?

Shopify tanzania

Hapo awali, ilikuwa vigumu kuanzisha duka la e-commerce kama Amazon. Ulihitajika kuwa na wabunifu wa wavuti wenye uzoefu, ambao walitoza maelfu ya dola. Waanzilishi wa Shopify waliona fursa katika haya yote kwa kuunda jukwaa ambalo mtu yeyote anaweza kuunda duka lake la mtandaoni kwa muda mfupi na bila haja ya kuwa na maarifa ya ubunifu wa wavuti (website design). Kufikia sasa, jukwaa hili limeibua programu inayoweza kutekelezwa na unaweza kuzindua duka lako kwa kipindi kifupi. Pia ina soko ambapo unaweza kununua vifaa vya kuboresha duka lako la mtandaoni kama vile usindikaji wa malipo (payment processing), muundo wa fomu, na uuzaji.

Jinsi ya Kuuza Mtandaoni Kupitia Shopify

Kuwa na Wazo

Unahitaji kujua kuwa maduka mengi ya Shopify hufeli pia. Mengi yayo hufeli hata kabla ya maadhimisho ya mwaka wao wa kwanza. Sehemu ya sababu inayoweza kufeli ni kwamba mara nyingi biashara hizi huwa hazipewa mawazo bora. Kwa hivyo, unahitaji kufanya utafiti na kupata wazo la kibiashara linalofaa. Unapofanya hivi, unapaswa kupata majibu ya maswali yafuatayo:

 • Wazo hili ni la kipekee?
 • Ninaweza kujaza maagizo (orders) ya bidhaa?
 • Watu wanahitaji aina hii ya bidhaa kweli?
 • Soko ninalolena ni lipi?
 • Washindani wangu ni akina nani?

Kabla ya kuteua wazo fulani, unashauriwa kuwauliza watu jinsi wanavyohisi kuhusu wazo hilo. Hii itakupa mwongozo kuhusu ikiwa bidhaa unazonuia kuuza ni muhimu au la.

Jitayarishe Kupata Pesa Kupitia Shopify

Baada ya kuamua juu ya biashara unayotaka kuzindua, unahitaji kujiandaa. Jambo la kwanza unalohitajika kufanya ni kuunda nembo (logo) ya biashara yako. Ili kuwasaidia wajasiriamali kwa hili, Shopify ina zana ya kuundia nembo bila gharama inayoitwa Hatchful ambayo itakusaidia kuunda nembo yako kwa muda mchache. Nembo hii inapaswa kuwa na jina la kampuni yako. Kwa kawaida, jina linapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

 • Fupi.
 • Yenye kuvutia
 • Rahisi kukumbukwa
 • Iliyo na maana inayohusiana na bidhaa unazouza

Baada ya haya, unapaswa kushughulikia suala la hesabu za bidhaa (inventory). Unashauriwa kupata wauzaji wa bidhaa wa jumla wa kigeni, ambao watakuuzia bidhaa kwa bei nzuri na nafuu ili uweze kupata faida utakapouza kwenye duka lako la Shopify. Ili kufanya hivyo, unaweza kujadiliana na wauzaji wa Kichina au Kivietinamu kupitia majukwaa kama Alibaba.

Baada ya kuwa na kitambulisho cha jina na kufanya “inventory” tayari, unahitaji kuanza kukuza duka lako la e-commerce. Hatua ya kwanza ni kujiandikisha na uchague kifurushi (package/plan) unachohitaji.

Ada ya Shopify

Kifurushi cha msingi (Basic) kinagharimu $29 kwa mwezi. Kifurushi (plani) cha Shopify hutozwa ada ya $79 na Advanced ni $299 kwa mwezi. Kama biashara chipukizi (startup), unashauriwa kuanza na kifurushi cha msingi kwa sababu kina huduma zote unazotaka.

shopify tanzania

Kama huna uwezo wa kulipa kila mwezi, unaweza kutumia jukwaa la Ecwid ambalo lina plani ya bure. Ingawa jukwaa hili lina plani zenye ada, plani ya bure (basic) itakuwa ni ya bure daima.

Baada ya kuchagua kifurushi unachotaka, sasa unapaswa kuchagua moja ya themes nyingi za bure za kujenga duka lako online na uanze kuweka bidhaa zako. Unapofanya hivi, unapaswa kuhakikisha kuwa unafanya yafuatayo:

 • Kuwa na picha za hali ya juu kwa bidhaa yako.
 • Eleza bidhaa zako vizuri.
 • Chunguza maneno yako makuu (keywords) vizuri.
 • Hakikisha kuwa picha zako zote zinapangwa na zinaelezewa vizuri .

Mwishowe, unapaswa kuhakikisha kuwa una sheria na masharti sahihi, sera, na miongozo ya kurudisha bidhaa zilizonunuliwa. Kumbuka, unapaswa kuanza shughuli tu ukishamaliza kujenga mtandaoni duka na bidhaa zako tayari.

Mbali na kuwa na bidhaa halisi, unaweza pia kutumia mkakati wa usafirishaji wa bidhaa hizi (drop shipping). Huu ni mkakati ambapo, haumiliki bidhaa lakini badala yake unawaelekeza watu kwa kampuni nyinginezo. Huu ni mkakati usiohitaji rasilimai nyingi ambao watu wengi hutumia siku hizi. Kwa kuongezea, kwa kutumia zana kama Printful, unaweza kujitengenezea shati zako mwenyewe na miundo mingine inayoweza kuchapishwa bila kujishughulisha na usafirishaji.

Tambulisha Bidhaa Zako Sokoni

Baada ya kujenga duka lako la mtandaoni, sasa unahitajika kuzitambulisha ili kuziuza. Njia bora ya kufanya hivyo ni kwa kuunda kampeni ya PR, ili kuzipa sifa bidhaa zako hata kabla ya kuzindua. Unaweza kutumia tovuti maarufu katika sekta yako ili kukuza wavuti wako. Baada ya hayo, unaweza kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, na Twitter ili kupigia debe bidhaa zako. Licha ya hatua hii kuwa yenye gharama ya juu, itakuwa ya thamani sana wakati unapoanza kupata pesa. Unaweza kufuata mikakati ifuatayo:

 • Hakikisha kuwa duka lako la mtandaoni limeboreshwa vizuri kwa ajili ya SEO.
 • Ingiza kitufe cha kununua kwenye Instagram.
 • Tumia pesa kwa kulipia mitandao ya kijamii na mikakati ya utaftaji (search strategies).
 • Washirikishe online influencers.
 • Unda viral videos zitakazokusaidia katika utambulishaji wa bidhaa zako

Hitimisho

Shopify ni jukwaa bora ambalo kampuni nyingi hutumia. Jukwaa hili ni dhabiti sana kiasi kwamba wakati Amazon ilipoamua kufunga shughuli zake, ilielekeza wateja wake kwenye Shopify. Vidokezo hivi vitakusaidia jinsi ya kupata pesa kupitia Shopify na kuwa mjasiriamali aliyefanikiwa. Walakini, kama nilivyosema hapo awali, wakati mchakato wa kuanza duka utakuwa rahisi, kufanikiwa katika shughuli hizi haitakuwa rahisi tu hivyo. Utalazimika kukesha usiku mwingi ukijiandaa kwa haya na kutumia pesa kufanikiwa.