Jinsi ya Kusajili Kampuni Tanzania

Usajili wa jina la biashara na kampuni nchini Tanzania unahusisha taratibu kadhaa, nyaraka na taasisi za kiserikali. Hii ndio hatua ya kwanza ya jinsi ya kufungua kampuni. Kwahivyo, nia ya makala hii ni kukuonyesha namna ya kusajili kampuni.

BRELA Ni Nini?

Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ni taasisi ambayo inahusika na usajili wa makampuni Tanzania. Mwaka wa 2018, BRELA ilikamilisha uzinduzi wa Mfumo wa Usajili kwa Njia ya Mtandao (BRELA ORS). Mfumo huu utawawezesha wateja kupata huduma zote za BRELA online popote walipo, wakati wowote wa siku bila kutembelea majengo ya BRELA. Katika makala hii tutakuonyesha jinsi ya kujisajili BRELA.

Tanzania imeorodheshwa katika nafasi ya 144 kati ya mataifa 190 katika urahisi wa kufanya biashara, kulingana na Benki ya Dunia.

Jinsi ya kufungua kampuni.
Biashara ya utengenezaji wa matofali Songea, Tanzania.

Gharama za Kusajili Kampuni

Usajili wa kampuni BRELA sio bure. Huu ni muhtasari wa gharama za kusajili kampuni BRELA.

AINA YA HUDUMAGHARAMA KATIKA TZS
Usajili wa jina la biashara5,000
Usajili wa KampuniKuanzia 95,000
Nambari ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN)Haitozwi
Cheti cha Usajili337,200
Leseni ya biashara400,000
Usajili wa Mamlaka ya Usalama na Afya Kazini (OSHA)600,000

Hatua za usajili wa kampuni ya Tanzania ni kama ifuatavyo:

Usajili wa Jina la Biashara

 1. Kwanza, unahitajika kufanyia utafiti wa jina la biashara kwa kutuma maombi ya mapendekezo na kwa kuwasilisha majina matatu ili kuhakikisha mapendekezo ya majina ya biashara yako hayajasajiliwa tayari.
 2. Ukifanikiwa, unaweza kulihifadhi jina kwa ajili ya matumizi ya baadaye au kuisajili kampuni moja kwa moja.
 3. Biashara inaweza kuendeshwa kama jina la kibiashara (mmiliki wa pekee) bila ya kusajiliwa kama kampuni.

Usajili wa Makampuni ya Biashara Tanzania (Makampuni ya Ndani)

 1. Maombi ya cheti cha usajili hufanywa na Wakala ya Usajili wa Biasharana Leseni (BRELA)
 2. Mkuu wa idara, mteja au katibu wa kampuni lazima awasilishe yafuatayo kwa Msajili wa Makampuni: fomu 14a, fomu 14b na Malengo na Katiba ya Kampuni.

Usajili wa Kampuni (Makampuni ya Kigeni)

 1. Matawi ya makampuni ya kigeni yanatakiwa kuwasilisha nakala iliyothibitishwa ya mkataba na makala ya chama kwa kampuni kuu.
 2. Ilani ya kuonyesha eneo la ofisi na nchi iliposajiliwa kampuni hiyo.
 3. Orodha ya wakurugenzi na majina ya wawakilishi nchini Tanzania.

Baada ya kupata cheti usajili unahitaji yafuatayo:

 1. Nambari ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN).
 2. Leseni ya biashara.
 3. Nambari ya utambulisho wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT).
 4. Hazina ya Fidia ya Wafanyakazi.
 5. Usajili wa Hifadhi ya Jamii.
 6. Usajili kwa Mamlaka ya Usalama na Afya Kazini (OSHA)

kufungua kampuni brela

Jinsi ya Kupata TIN Number (Nambari ya Utambulisho wa Mlipa Kodi)

Baada ya kupata hati ya usajili, unahitaji kutuma maombi ya cheti cha TIN number ya biashara kutoka Mamlaka ya Ushuru ya Tanzania (TRA).

 1. Nakala zilizothibitishwa za hati ya usajili na Malengo na Katiba ya Kampuni yataambatanishwa na maombi ya TIN number.
 2. Maombi ya TIN kwa kila wanahisa / wakurugenzi. Kama mkurugenzi yeyote tayari alishapata vyeti vya TIN kwa matumizi mengineyo, hawezi kufanya maombi upya kwani nambari hiyo (TIN) ya awali bado itatumika.
 3. Angalau, mmoja wa wakurugenzi wa kampuni lazima awepo katika ofisi za ushuru ili kwa ajili ya kuiandaa data za kibiometriki. Vilevile, lazima utembelee ofisi za TRA ili kuchukua namba ya TIN mwenyewe.
 4. Nakala za pasipoti na picha za wakurugenzi / wanahisa.
 5. Kampuni inatakiwa kutangaza makadirio ya mapato au mauzo ili ipate tathmini ya kodi kwa mwaka wowote ule.

Leseni ya Biashara

Maombi ya leseni ya biashara hufanyika katika Wizara ya Biashara na Viwanda au Serikali za Mitaa. Hatua hii inachukua hadi siku 3 za kazi.

Nyaraka zinazohitajika

 1. Ushahidi wa ufaafu wa majengo ya kampuni.
 2. Nakala zilizoidhinishwa za Nambari ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN).
 3. Nakala zilizoidhinishwa za Malengo na Katiba ya Kampuni.
 4. Nakala zilizoidhinishwa za cheti cha usajili.
 5. Nakala zilizoidhinishwa kutoka Mamlaka ya Ushuru ya Tanzania (TRA).
 6. Nakala zilizoidhinishwa za mkataba wa kukodisha (ushuru wa stempu na kodi kulipwa) ofisi za kampuni.
 7. Nakala za pasipoti za wakurugenzi / wanahisa.

Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)

VAT hupokezwa kutoka Mamlaka ya Ushuru ya Tanzania (TRA) na kwa madhumuni ya kupata VAT lazima uweze kutimiza mahitaji yafuatayo:

 1. Wafanyabiashara wa Tanzania wenye mtaji wa milioni 50 kwa miezi sita ya kwanza ya biashara au milioni 100 katika mwaka wa kwanza wa biashara wanatakiwa kujisajili kwa kodi ya ongezeko la thamani.
 2. Kujisajili kwa ajili ya VAT, unahitaji kwenda katika ofisi za TRA au kujiandikisha kwenye mtandao.

Nyaraka Zinazohitajika

 1. Nakala zilizoidhinishwa za Nambari ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN).
 2. Nakala zilizoidhinishwa za cheti cha kibali cha kodi
 3. Nakala zilizoidhinishwa za leseni ya biashara.
 4. Nakala zilizoidhinishwa za Malengo na Katiba ya Kampuni.
 5. Nakala zilizoidhinishwa za cheti cha Usajili.
 6. Ununuzi wa Mtambo wa Kifedha wa Kielektroniki (EFD).
 7. Nakala zilizoidhinishwa za Mkataba wa kukodisha ofisi za kampuni.
 8. Nakala za pasipoti za wakurugenzi / wanahisa.

Hazina ya Fidia ya Wafanyakazi (Workers Compensation Fund)

Hazina ya Fidia ya Wafanyakazi hutoa mbadala wa mshahara na faida za kimatibabu kwa wafanyakazi iwapo watajeruhiwa katika harakati za kazi yao. Kujiandikisha kwa ajili ya hazina hii, waajiri wanahitaja kufanya yafuatayo:

 1. Kusajili pindi tu kampuni inaanza kuwaajiri wafanyakazi na kabla ya kampuni kuanza shughuli zake rasmi.
 2. Kujaza fomu ya Fidia Mapendekezo ya Fidia ya Wafanyakazi kwa Hazina ya Fidia ya Wafanyakazi (WCF) na Mamlaka ya Udhibiti wa Bima ya Tanzania (TIRA).
 3. Waajiri wanaweza kuchagua kuchukua sera ya bima badala ya fidia ya wafanyakazi.

Hifadhi ya Jamii (National Social Security Fund)

 1. Kila mwajiri katika sekta rasmi anahitajika kujiandikisha kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya Taifa.
 2. Mfanyakazi ana haki ya kuchagua mpango wa lazima atakaopendelea kujiandikisha nao.

Usajili kwa Mamlaka ya Usalama na Afya Kazini (OSHA)

 1. Ni lazima kujiandikisha na Mamlaka ya Usalama na Afya Kazini (OSHA) kwa kujaza fomu ya maombi na kutoa nyarakaza usajili wa kampuni.
 2. Maafisa wa OSHA watazitembelea sehemu za kazi kabla hujatuma maombi ya ukaguzi na usalama wa afya.

Hitimisho la Hatua za Kufungua Kampuni

Kila sekta ina leseni yake ya ziada. Unahitaji kujua mahitaji ya leseni katika sekta yako.

Makampuni ambayo yalisajiliwa kabla ya uzinduzi wa Mfumo wa Usajili kwa Njia ya Mtandao (ORS) Februari 1, 2018 lazima zilinganishwe na maafisa wa Msajili kabla kusajiliwa kupitia ORS. Makampuni hayo yataandaliwa upya na kisha kupakiwa kwenye ORS na wakurugenzi wa makampuni au makatibu wa kampuni.

Unapaswa kuhakikisha kwamba kampuni yako inakidhi viwango vilivyowekwa kwa kuyatambulisha mapato ya mwaka ya kampuni, kulipa kodi ya kampuni na VAT pale ambapo inahusika, kodi ya mapato kwa wafanyakazi na kutoa mchango kwa usalama wa jamii kwa ajili ya wafanyakazi.

Hivyo, ukifuata mwongozo huu wa taratibu za kufungua kampuni au jinsi ya kusajili biashara/jinsi ya kuanzisha kampuni na ukalipa gharama za kufungua kampuni, utaweza kuanza kuendesha biashara yako mara moja.