Jinsi ya Kujiunga na Biashara Zilizoshirikishwa (Franchise) Katika Afrika

Tafsiri:
en_US

Biashara zilizoshirikishwa (franchise) ni leseni ya kibiashara ambayo inaruhusu mtu au biashara nyingine kuuza bidhaa au kutoa huduma kwa kutumia nembo na kitambulisho cha biashara nyingineyo.

Kuna aina mbili za kushirikishwa: muundo wa biashara na bidhaa na jina la kibiashara. Ushirikishwaji wa muundo wa biashara ni maarufu katika sekta kama vile mali isiyohamishika, maduka ya kisasa, huduma ya magari, na biashara ya mikahawa na hoteli. Biashara inayoshirikishwa hupata huduma maalum na bidhaa kutoka kwa biashara asilia inayodhibiti shughuli za kibiashara.

franchise business africa
The Fish & Chip Co, kampuni shirikishi ya Afrika Kusini.

Huduma zinazotolewa na kampuni asilia ni pamoja na:

 • Utambulisho wa biashara kwa njia ya nembo na alama za kibiashara.
 • Mfumo mpana wa shughuli za biashara.
 • Usaidizi wa kuchagua mahali pa kuweka biashara, kubuni mpangilio wa duka, kuajiri na kutoa mafunzo ya wafanyakazi, kupata pembejeo zinazohitajika, na kufanya shughuli za matangazo.

Katika mbinu ya kushirikishwa kupitia bidhaa na jina la biashara, biashara inayoshirikishwa inatarajiwa kununua kwa upekee bidhaa fulani kutoka kampuni asilia. Tofauti na aina nyingine ya kushirikishwa, mfumo huu hautozi ada ya mara kwa mara. Mbinu hii ni ya maarufu kwa biashara za bidhaa kama petroli, soda, na usambazaji wa bidhaa za gari. Hata hivyo, biashara nyingi zinazohusishwa zinahamia kwenye mfumo wa biashara kwa vile zina faida zaidi.

 

Ushirikiano Huu Una Faida Gani kwa Biashara Iliyohusishwa?

 • Kupunguzwa kwa hatari ya hasara za kibiashara. Kuna msaada wa muda mrefu kutoka kwa kampuni asili pamoja na kutumia mbinu na mikakati ya uendeshaji biashara ambayo imejaribiwa hapo awali katika maeneo mengineyo.
 • Mfululizo wa wateja. Kwa kupata ushirikiano kupitia bidhaa za biashara maarufu, pana ukubalifu kutoka kwa umma ikilinganishwa na jinsi biashara hiyo ingepokelewa iwapo ni biashara inayoanzishwa tu.
 • Wafanyakazi bora na mahiri. Kampuni asili hutoa mafunzo ya awali na hata kuyaendeleza na hivyo kuibua wafanyakazi wenye ujuzi ambao unahitajika ili kutimiza malengo ya kampuni.

Ushirikiano Huu Una Hasara Gani kwa Biashara Iliyohusishwa?

 • Kuna ubunifu mdogo. Biashara kuu hutoa mwelekeo wa jinsi biashara tanzu zinafaa kuonekana na kufanya kazi. Masharti haya hayawapi wajasiriamali kuuhususha ubunifu na upekee wao.
 • Kwa kuwa biashara hii inawakilishwa na biashara tanzu mbalimbali, sifa ya biashara asili inaweza kuathirika vibaya kutokana na matokeo mabaya ya shirika mojawapo linalotumia kitambulisho chake.
 • Makubaliano yanaihitaji biashara iliyohusishwa kugawanya faida zake na kampuni kuu.

 

Jinsi ya Kujiunga na Biashara za Kushirikishwa Barani Afrika

Katika hatua hii, inatarajiwa kwamba una mtaji wa kutosha na ujuzi muhimu wa biashara. Kisha, utahitajika kuchuja orodha yako ya biashara unazotaka kujishirikisha nazo na kufanya utafiti kwa kila moja kabla ya kuamua ni ipi haswa unayolenga kujiunga nayo. Baada ya kutimiza mahitaji hayo ya kimsingi, unahitaji kufuata hatua zifuatazo kujiunga na biashara hizo barani Afrika.

Wasiliana na Kampuni Kuu

Ili kutoa taarifa kwa kampuni asili kuhusu haja yako ya kujiunga nao, unaweza kutembelea tovuti yao ili kupata fomu ya maombi. Mara tu baada ya biashara hiyo kupata ombi lako, wanaweza kuwakaribisha kufanya mawasilisho ya kushindana na biashara nyinginezo zinazotaka kushirikishwa au kukutumia katalogi kwa ukaguzi. Iwapo eneo unalopendelea tayari lina biashara iliyokwishahusishwa, unaweza kuwekwa katika orodha ya kusubiri au kushauriwa kuanzisha biashara katika eneo tofauti.

Kukamilisha Hatua za Maombi zilizoainishwa

Katika jaribio la kutathmini uwezo wa biashara tanzu tarajiwa, kampuni asili huweza kuhusisha tathmini ya kimawazo na kiakili, ujazwaji wa dodoso, na uchambuzi wa rekodi yako ya mikopo. Kwa kawaida, biashara asilia hutia maanani kutambua:

 • Uzoefu wa kibiashara wa kampuni inayolenga kujiunga.
 • Sababu zako za kutaka kujishirikisha na kampuni hiyo na iwapo una ufahamu wa jinsi kampuni hiyo huendesha shughuli zake.
 • Ujuzi wako wa kuongoza shughuli za biashara pamoja na ujuzi wako wa maswala ya kifedha.
 • Eneo lako unalolipendelea na iwapo una nia ya kuyafikiria maeneo mengine.
 • Uwezo wako wa kusimamia ukubwa fulani wa idadi ya wafanyakazi.

Hasa, mengi ya mahitaji yanayoangaziwa katika fomu ya maombi yanahusiana na uwezo wa kifedha wa anayetuma maombi. Kampuni kuu itatakuuliza kuhusu madeni na mali yako ili kutathmini kama bado unaweza kuendesha biashara vizuri iwapo patajiri changamoto zisizotarajiwa za kifedha. Kutathminiwa kwa fomu yako kunaweza kuchukua muda kwani kampuni hiyo kuu inahitaji muda wa kutosha ili kukagua kila swala kwa undani.

Dadisi Kuhusu Kampuni Inayonuia Kukushirikisha

Sasa, kwa kuwa tayari umewasilisha taarifa zote zinazohitajika na maombi yako yamekubaliwa, ni nafasi yako kuikagua kampuni hiyo. Hii ni nafasi yako ya kuuliza wasimamizi wa kampuni swali lolote ulilo nalo kuhusu kampuni. Unaweza hata kuwasiliana na biashara nyinginezo zinazojihusisha na kampuni hiyo na hata kutembelea biashara zao ili kuelewa aina ya misaada inayotolewa na kampuni kuu pamoja na mwenendo wa mauzo. Baadhi ya maswali ambayo yatakusaidia kujua kampuni kuu vizuri ni:

 • Idadi ipi ya biashara tanzu nyinginezo ambazo zimefunguliwa katika eneo hilo katika mwaka uliopita?
 • Je, ni mafanikio yapi ya kibiashara yanayodhihirika katika kampuni hizi tanzu katika eneo unalolenga na hata zaidi?
 • Ni majukumu yapi yanayokidhiwa na kampuni asili katika hatua za kuchipuka kwa biashara na baadaye?

Tafuta Sehemu Inayofaa Shughuli Za Biashara Inayoshirikishwa

Katika biashara yoyote, mahali inapowekwa ni kigezo muhimu cha mafanikio. Kwa bahati nzuri, mashirika asili husaidia biashara tanzu kutambua sehemu bora kulingana na utafiti wao. Kupata mahali mwafaka kunaweza kuchukua muda lakini ni hatari kuanzisha biashara katika eneo lisiloafiki.

Tafuta Ufadhili wa Ziada wa Kifedha

Kuna njia mbalimbali za kupata fedha zinazohitajika. Kwa mfano, unaweza kupata asilimia 40-50 ya fedha kama inavyotakiwa na mabenki zaidi na kisha kupata kuongezea kwa njia ya mkopo kutoka taasisi za fedha. Kwa kuwa mara nyingi mashirika asili hutoa mwongozo katika kila hatua, huenda utapata msaada wao katika kuandaa mpango wa biashara na kutimiza mahitaji mengineyo jinsi yalivyoainishwa na benki.

Soma na Ufahamu Maelezo Yote ya Mkataba

Kabla ya kutia saini mkataba halisi wa kushirikishwa katika biashara, kampuni asili itakupa hati ya kutoa taarifa. Waraka huu huwa una maelezo ya kina kuhusu kampuni ikiwa ni pamoja na makubaliano ya kutoa taarifa na hatua za kisheria zinazoweka kuchukuliwa. Ni muhimu kutafuta usaidizi wa mwanasheria ambaye ana welewa na masuala hayo kabla ya kusainiwa mkataba. Lazima pia uhakikishe kuwa unachukua angalau wiki 2 ili kupitia mkataba huo.

Huku baadhi ya mataifa ya Afrika yakiwa na mahitaji ya kipekee katika sheria zinazowalinda watumiaji wa bidhaa, kuna baadhi ya masharti ya kimsingi kuhusiana na mikataba ya ushirikishwaji huu wa kibiashara. Kwa mfano, sheria hii inatambulisha kipindi ambayo cha siku 10 baada ya kusaini mkataba ambacho kampuni iliyotaka kushirikikishwa inaweza kujiondoa katika mkataba huu bila adhabu yoyote.

Fanya Maandalizi Yanayohitajika ili Kuanzisha Biashara Iliyoshirikishwa

Hakikisha kuwa maelezo yote ya duka ni sahihi kabla ya kuifungua milango kwa wateja wako. Hii ni pamoja na kuweka zana za dukani, kuhifadhi bidhaa na vitu vyote muhimu, na kuwaajira na kuwapa mafunzo wafanyakazi wa kutosha. Kwa kuangazia maswala haya yote, upo tayari kuendesha na kupanua biashara yako iliyoshirikishwa barani Afrika.

https://www.youtube.com/watch?v=FA5G6c-GRqc&feature=youtu.be

 

Hitimisho

Mojapo ya njia ya kufanikiwa katika biashara za Afrika ni kwa kujishirikisha na biashara nyingine iliyonawiri. Kama ilivyo na shughuli yoyote ile ya kibiashara, kuna baadhi ya faida na hasara ya kujiunga na biashara nyingine iliyonawiri barani Afrika. Hatua muhimu inayofaa katika mchakato huu ni pamoja na kufanya utafiti kuhusu kampuni au biashara hiyo, kuhakikisha unakidhi mahitaji ya kushirikishwa na kampuni hiyo, na kuhakikisha kwamba maelezo yaliyomo katika mkataba ni ya manufaa kwako.