Unayohitaji Kujua Kuhusu Bima ya Afya Nchini Kenya

Tafsiri:
en_US

National Hospital Insurance Fund (NHIF) hutoa bima ya afya kwa watu katika sekta rasmi na sekta isiyo rasmi. Kwa watu katika sekta rasmi, NHIF ni huduma ya lazima. NHIF huwawezesha watu kupata huduma za kimatibabu kwa wakati wowote bila ya kuwa na wasiwasi kuhusu gharama.

Bima hii ya matibabu kwa sasa inakimu mahitaji ya watu katika sekta isiyo rasmi, kuhakikisha kuwa Wakenya wote wanaweza kupata bima hii. NHIF inahudumia vikundi vyote nchini Kenya kama vile watumishi wa umma na ina mpango mwingine unaowaangazia wenye mapato duni (maskini), watu wazee na wale wanaoishi na ulemavu.
gharama za kujiunga na nhif

Je, Faida za Uanachama wa NHIF ni zipi?

Kuna faida nyingi ambazo wanachama wa NHIF waliosajiliwa hupokea. Baadhi yazo ni pamoja na yafuatayo:

  • Kugharamia tiba mke/mume aliyetambulishwa pamoja na wategemezi, iwapo watakaa hospitalini kwa kipindi watakapokuwa wakitibiwa.
  • Utoaji wa huduma za afya kwa wanachama na wategemezi.
  • Vituo mbalimbali vya afya vimewekewa bima na NHIF kiwa ni pamoja na baadhi ya hospitali za binafsi.

Sifa Tanzu za NHIF

Mpango huu wa bima ni nafuu na una sifa zifuatazo:

  • Haibagui kuhusishwa kwa aina yoyote ya matibabu ila tu matibabu ya kiuraibu au kimapambo.
  • Haina upeo wa kiumri.
  • Haimzuilii yeyote kwa mujibu wa idadi ya wategemezi aliowatambulisha.

Usajili wa NHIF

Unaweza kujiandikisha kwa NHIF mtandaoni na kwa kutembelea (binafsi) ofisi mbalimbali nchini. Wale wanaoruhusiwa kujiunga na mpango huu wa NHIF ni wale waliofikia umri wa miaka 18 na kuwa na mapato ya shilingi 1,000 kwa mwezi na shilingi 12,000 kwa mwaka kutokana na mishahara au kwa kujiajiri wenyewe. Unaweza kukagua michango na ada yako ya kila mwezi.

Mahitaji ya Usajili wa NHIF

Wakenya wanahitajika kuwasilisha stakabadhi zifuatazo wakati wa usajili wa NHIF:

  • Nakala ya kadi ya kitambulisho cha kitaifa ikiwa ni pamoja na ile ya mke/mume pale inapohitajika.
  • Picha za rangi za pasipoti za mke/mume na wategemezi pale inapohitajika.
  • Vyeti asilia vya kuzaliwa vya wategemezi pamoja na nakala zake.
  • Nakala ya barua ya ajira kutoka kwa mwajiri (isipokuwa wale wa waliojiajiri wenyewe).

Wakaazi wa kigeni pamoja na wanafunzi wanahitajika kuwasilisha stakabadhi zifuatazo wakati wa usajili:

  • Nakala za pasipoti na kibali cha kazi pale inapohitajika.
  • Picha za rangi za pasipoti zikiwemo za mke/mume na wategemezi pale inapohitajika.
  • Kama utatumia mfumo usiohitaji mtandao, unatakiwa kupakua na kujaza fomu ya uanachama kutoka kwa tovuti ya NHIF. Hatimaye unatarajiwa kuiwasilisha fomu iliyojazwa pamoja na ada inayohitajika kwenye matawi yake yanayopatikana kwa urahisi kote nchini.

Kwa wale wanaonuia kusajili mtandaoni, fuata hatua hizi rahisi.

  • Tembelea tovuti ya NHIF.
  • Bonyeza jisajili mtandaoni (register online).
  • Itafute na ubonyeze sehemu ya “mwajiri, mfanyakazi au umejiajiri mwenyewe” (“Employer, Employee or Self Employed”) kutoka kwa orodha iliyopo.
  • Chagua iwapo wewe ni Mkenya au mgeni.
  • Jaza sehemu zote zinazohitajika.
  • Ambatisha nakala ya kitambulisho / pasipoti / kitambulisho cha ugeni na picha za pasipoti picha yako.
  • Kama umeoa au umeolewa, ambanatisha nakala ya cheti chako cha ndoa.
  • Bonyeza Hifadhi (Save) ili kutuma maombi ya usajili.

Jinsi ya Kuiwezesha Tena Akaunti ya NHIF

Kuiwezesha tena akaunti yako, unahitajika kutuma shilingi 1,500 kwa njia ya M-Pesa, nambari ya Paybill 200222. Tumia nambari yako ya kitambulisho kama nambari ya akaunti. Utakuwa umeuwezesha uanachama wako na utaanza kufurahia faida baada ya miezi miwili.

Gharama za Bima ya Afya NHIF

Gharama za kujiunga na NHIF hutofautiana kutokana na sera ya bima uliyonayo. Kwa mfano, Supa Cover ndio bima kubwa zaidi. Gharama za bima hii ni shilingi 500 kwa mwezi kwa mwenye bima na wanaomtegemea.

Je NHIF Inafanya Kazi Vipi?

NHIF inajizatiti kuhakikisha kuwa Wakenya wote wanafurahia kwa kina matibabu kutokana na hali yoyote isiyotabirika na gharama za matibabu. NHIF inaelewa kuwa Wakenya wengi wanazuiliwa katika hospitali kwa kukosa fedha za kulipia gharama zao za matibabu. Wengine wanalazimika kuuza mali zao ili kupata kiasi cha fedha ili kuweza kulipia gharama zao za matibabu.

Watu katika sekta zisizo rasmi wana hiari ya kujiunga na mpango huu wa bima ya NHIF kwa kuchangia shilingi 500 kila mwezi kwa kila mwanachama. Wanachama wa NHIF hupokezwa kadi ya uanachama ambayo wanatarajiwa kuwasilisha endapo wanatembelea hospitali ambazo zimeidhinishwa kwa matumizi ya NHIF. Madaktari watakuhudumia na utaweza kupata huduma ya matibabu hadi utakapoondoka hospitalini. Ni jukumu la hospitali kuidai NHIF ili kupata fidia kwa gharama uliyotumia kupata matibabu.

Kuna zaidi ya vituo vya afya 400 vilivyoidhinishwa na kukubaliwa nchini Kenya. Hi ina maana kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwamba NHIF inakubalika katika hospitali utakayoitembelea. NHIF ina upekee wake ikilinganishwa na bima nyinginezo kwa vile haina ubaguzi kwa mujibu wa magonjwa yanayoweza kugharamiwa nayo; inajumlisha magonjwa yote. Vilevile, ikiwa wagonjwa watazitembelea hospitali za binafsi, wanaweza kuigawa gharama ya matibabu na NHIF.

Hitimisho Kuhusu Bima ya Afya ya NHIF

Hakikisha ya kwamba umeweza kujiandikisha kwa bima hii ili uweze kunufaika na faida zote za kiafya. Utakuwa umekingwa kutokana na hali ya afya isiyo na uhakika wowote na majanga ambayo hayatabiriki.

Habari Zaidi