Jinsi HouseAfrica Imerahisisha Uwekezaji wa Mali Isiyohamishika Kupitia Blockchain

Tafsiri:
en_US

HouseAfrica ni chombo kinashughulikia mali isiyohamishika ya gharama nafuu kwa kutumia teknolojia ya blockchain katika kununua na kuuza mali kwa gharama ya chini kwa mbinu salama na rahisi.

Lengo la House Africa ni kutoa ufumbuzi wa matatizo ya kimakazi barani Afrika kwa kuhakikisha kuwa watu wanaufurahia ukodishaji (wa makazi). Maombi ya kukodisha na mikataba ya taratibu ya kukodisha inafanywa mtandaoni kwa kutumia mikataba stadi/ mikataba erevu inayoharakisha michakato na pia kuifanya ya moja kwa moja.

Jinsi HouseAfrica Inatatua Matatizo ya Afrika

Unaweza kuwekeza katika HouseAfrica kwa kununua hisa ambazo zitakupa faida ya juu. Kwa kutumia teknolojia ya blockchain, HouseAfrica huuza kiwango fulani cha mradi wa nyumba kwa wawekezaji. Vilevile, wanawezesha ongezeko la kasi la upatikanaji wa nyumba katika Afrika. Kuanzisha biashara ya mali isiyohamishika inaweza kuwa ghali sana, na mara nyingi kuchukuliwa kuwa ni ya matajiri tu. Hata hivyo, HouseAfrica imeibua ufumbuzi wa tatizo hili kwa kuelekeza fedha zaidi katika maendeleo ya mali isiyohamishika. Kampuni hii inapokea malipo kwa njia ya kadi za benki, akaunti ya benki na hata Bitcoin.

Mali isiyohamishika ni biashara yenye faida kubwa ikiwekezwa. Kuna uhaba mkubwa wa makazi barani Afrika unaosababisha gharama kubwa za maisha na viwango duni vya maisha. HouseAfrica inaendeshwa na ari yake ya kiteknolojia ili kurahisisha uwekezaji katika biashara ya mali isiyohamishika. Mbali na hilo, wana timu ambayo ina ujuzi na uvumbuzi sahihi wa kufanya mabadiliko yanayofaa katika mali isiyohamishika.

Timu ya HouseAfrica.

Kumbuka kwamba,Fifi tuna wasiwasi dhidi ya maneno yana yanayoonekana kuvutia kama blockchain na mikataba erevu (smart contracts). Watu wengi wamelaghaiwa fedha zao wakati wa kuwekeza katika miradi inayotumia maneno yanayonata kama haya. Blockchain ni mfumo tu wa data iliyosambazwa na hutumia mbinu kadhaa kuhakiki. Teknolojia hii pekee haiwezi kutatua mengi ya masuala ambayo Waafrika wanakumbana nayo kuhusu mali isiyohamishika.

Jinsi Mapato ya HouseAfrica Hufanya Kazi

HouseAfrica inawapa wawekezaji watarajiwa uwezo wa kujibunia mtiririko wa fedha kwa njia ya mapato ya kila mwaka. Unapowekeza katika mali, utapata kiasi cha hisa ambacho kitakulimbikizia mapato kila mwaka. Uwekezaji wa mali isiyohamishika huzalisha aina mbili za mapato; ongezeko la thamani na mapato. Wawekezaji hupata faida kulingana na hisa wanazomiliki. Kwa mfano, kama kuna wawekezaji wawili ambapo mmoja ana hisa 100 huku yule mwingine ana hisa 1000, aliye na hisa 1,000 atapokea mapato zaidi ikilinganishwa na mwenye hisa 100. Mwekezaji anaweza kuchagua kuuza hisa zake kwa kuangazia thamani bei ya iliyopo ya hisa hizo. Kwa kufanya hivyo, atapata faida ya mitaji au ongezeko la thamani.

Jinsi ya Kupata Gawio Katika HouseAfrica

HouseAfrica huchuma mapato yake kutokana na uwekezaji wa madeni na hisa zisizo na riba ya kudumu. Hata hivyo, kwa wakati huu, wanatilia mkazo zaidi katika uwekezaji wa hisa zisizo na riba ya kudumu.

Mapato ya Hisa Zisizo na Riba ya Kudumu

Awali, uwekezaji wa hisa zisizo na riba ya kudumu uliwapa wawekezaji baadhi ya haki (uwezo), kama haki ya mapato ya kodi ikiwa mali imekodishwa. Wawekezaji katika mali isiyohamishika wenye haki za hisa zisizo na riba ya kudumu hupata uwekezaji mkubwa kadri muda unavyoendelea. Mapato yao hutokana na malipo ya ukodishaji na faida ya mtaji mara tu wanapouza hisa zao.

Kwa kuwekeza katika HouseAfrica, unaweza kupata sehemu ya umiliki katika mali nyingi katika bara la Afrika. Mali hii isiyohamishika inaweza kuwa ya kimakazi au kibiashara. Kama mwekezaji ana umiliki wa haki wa hisa zisizo na riba ya kudumu, anaweza kukusanya mapato kutoka kwa wapangaji wanaomiliki mali hiyo.
Makampuni yenye Malengo maalum (Special Purpose Vehicle) huundiwa wawekezaji wenye hisa zisizo na riba ya kudumu, na kisha huhifadhiwa na mwekezaji katika Kampuni Mdhamini. Kampuni hizi huwa ni taasisi za kibiashara ambayo huundwa ili kukidhi malengo yaliyotambulishwa vizuri.

Ugavi wa Mapato Katika HouseAfrica

HouseAfrica husambaza mapato kwa njia ya asilimia 90 ya mapato yanayopaswa kutozwa kodi kwa wanahisa kila mwaka. Malipo haya hupewa kwa wawekezaji kitaslimu, kulingana na mafanikio yao kutokana na kusanyiko (kwa hisa zao) katika mwaka mzima. Mwekezaji anaweza kuchagua kuzitoa pesa kwa njia ya akaunti ya benki au kuziwekeza tena na HouseAfrica. Malipo ya mapato hayategemei thamani ya hazina ya hisa zako. Ili kupata gawio, si lazima kuuza hisa zako. Mara tu baada ya kununua hisa, huna haja ya kufanya kitu kinginecho. Utahitajika tu kukaa na kusubiri mapato na faida bila juhudi yoyote ya ziada.

Hitimisho

Ni muhimu kutambua kuwa tofauti na gawio ambalo hulipwa kila mwaka, ongezeko la thamani huafikiwa kwa njia tofauti. Njia mojawapo ya kuafikia ongezeko la thamani ni kutokana na mauzo ya mali. Mali isiyohamishika huweza kuuzwa kwa Thamani ya Bei Iliyopo (Current Price Value), ambapo katika hali hii majengo huwa na ongezeko la thamani. Pia, ongezeko la thamani huafikiwa kupitia Thamani Halisi ya Hisa (Net Share Value—NSV) ambayo huongeza baada ya kipindi fulani muda. Hata hivyo, kulingana na aina ya mali isiyohamishika unayomiliki, utapokea ongezeko la thamani wakati unauza hisa zako. Kwa kuwa sasa unajua jinsi HouseAfrica hufanya kazi na jinsi ya kupata faida, fikiria kununua na kuwekeza hisa za HouseAfrica.