Ushauri wa Jinsi ya Kutunza Pesa

Tafsiri:
amen_US

Kuzingatia na kuendeleza mpango wa bajeti ni uamuzi muhimu kwa usimamizi wa mapato na gharama zako za kifedha. Kutayarisha mpango wa bajeti ni hatua ya kwanza ya kutunza pesa, kufanya akiba na kuyaweka maisha yako ya kifedha chini ya udhibiti. Kuunda mpango wa bajeti haipaswi kuwa shughuli ngumu. Mpango rahisi tu wa bajeti unaweza kuwa na athari kubwa kwenye tabia yako ya kifedha.

Hali hii imetufanyikia sisi sote: kuishi kwa malipo ya mshahara tu (paycheck to paycheck), tukishangaa ikiwa tutakuwa na pesa za kutosha kukidhi mahitaji yetu. Lakini kama msemo wa zamani unavyotukumbusha, “penye nia, pana njia”. Ikiwa umeyafikia makala haya, tayari umegundua kuwa unahitaji kuanza kutayarisha bajeti yako. Utajifunza pia jinsi ya kutengeneza mpango wa kuweka akiba na hatua za kujibidiisha kushikamana na hatua hizo.

Kukusanya Ushahidi

Kutumia pesa zaidi ya mapato mara nyingi huja kwa sababu tunakosa kuwajibika tunavyotumia pesa zetu. Kawaida, tunagundua hali hii tu wakati mapato tayari yamekamilika na malipo (mshahara) yanayofuata bado hayajaonekana. Unachohitaji kufanya ni kuamua ni pesa ngapi unanuia kutumia na kile unacholenga kugharamia. Hatua ya kwanza ya kujua ni wapi unapoweza kuokoa pesa ni kujua pesa zako zinaenda wapi, na zinatumika vipi.

Mbinu maarufu ya kuweka kumbukumbu za gharama ni kwa kuziandika. Unaweza kufanya hivyo kwenye spreadsheet, kwenye daftari, au kutumia programu ya bajeti. Chaguo ni lako. Ni muhimu kufanya hivyo angalau mwezi mmoja kabla ya kuandaa mpango wako wa bajeti.

Anza kwa Utafiti

Mara tu ukizifuatilia gharama zako za kila mwezi, ni muhimu kuandaa orodha ya gharama zako muhimu zaidi na zisizo muhimu zaidi. Ili kuamua ni vitu gani vinaenda kwenye kila orodha, zingatia kwanza aina tofauti za gharama.

  • Gharama zisizohamishika – hizi ni zile ambazo hazibadilika kila mwezi, kwa mfano: kodi, bima, ada ya benki, ulipaji wa deni.
  • Gharama zinazoweza kubadilika – hizi ni zile ambazo hutofautiana kila mwezi, kwa mfano mboga, vitu vya utunzaji wa kibinafsi, mafuta ya gari, mavazi, zawadi.
  • Gharama za dharura – Zinazotokana na hali zisizotabirika, kwa mfano Huduma ya afya, kukarabati simu au laptop iliyoharibika. Kwa kawaida, pesa hizi zinafaa kutoka kwenye akaunti yako ya akiba ya dharura.
  • Gharama za ziada au za kipekee – Gharama zote ambazo sio muhimu, kwa mfano: kula kwenye mikahawa, kwenda kwenye sinema, kulipia ada ya Netflix, na kadhalika

Kwenye orodha yetu, gharama ya vitu muhimu zaidi, kama vile Kodi na ulipaji wa deni, imewekwa juu kwenye orodha.

Vipi Unaweza Kustahimili Msukosuko wa Kifedha

Mara nyingi huwa ni vigumu kuacha vitu kwenye orodha yako. Labda huenda huhitaji kikombe hicho cha kahawa cha gharama ya juu sana asubuhi, lakini unapokinunua utapata utulivu siku nzima.

Ili kuamua ni kiasi gani unaweza kuacha kutumia, unastahili kuzipa gharama zako kipaumbele. Anza kwa kutenganisha gharama zako kuu kutoka kwa gharama zako za kila siku. Hii itakusaidia kuibua mpango wako wa bajeti na kutambulisha asilimia sahihi ya matumizi ya mambo fulani fulani.

Kwa mfano, anza kwa kutengeneza chati. Ongeza gharama zako kadri unavyozipokea na kuziweka katika makundi. Unaweza kufanya hivyo kwenye karatasi au kutumia spreadsheet au hata mojawapo ya programu za bajeti ya rununu. Chini yake, weka jumla kwa kila kitu au sehemu (ya matumizi), ambayo utalinganisha na mapato yako.

Mfano wa Mpango wa Bajeti Unaoweza Kutumika

Hebu tumtazame Alice mwenye mapato ya shilingi elfu 145 (takriban laki moja na nusu). Baada ya miezi 3, anagundua kuwa overdraft yake imeongezeka kwa shilingi elfu 45 katika miezi iliyopita. Je, hii ingewezaje kutokea? Hana habari kuhusu hili kwa sababu alikuwa akiamini kuwa hakutupitiliza kiwango chake cha matumizi. Lakini mara tu unapoiandika, unagundua haraka kuwa kweli alikuwa akitumia pesa nyingi kuliko mapato yako.

KitengoMatumizi ya kila mwezi
Kodi ya Nyumba75000
Vyakula45000
Usafiri15000
Burudani25000
Jumla160000

Kwa hivyo, Alice hutumia shilingi elfu 15 kwa mwezi. Baada ya miezi mitatu, deni lake litakuwa limeongezeka hadi shilingi elfu 45. Sasa huu ni wakati mwafaka kwake wa kubadilisha tabia zake na kuchunguza tena mtindo wake wa matumizi. Kwa hivyo, Alice anaibuka na mpango mpya wa jinsi anavyotaka kutumia pesa zake. Mpango huu mpya ni pamoja na kulipa deni lake la shilingi elfu 45, na kuhakikisha kuwa jumla ya matumizi yake hayazidi shilingi elfu 145.

KitengoMatumizi ya kila mwezi
Kodi ya Nyumba75000
Vyakula35000
Usafiri15000
Burudani12500
Ulipaji wa Madeni7500
Jumla145000

Baada ya miezi 6, Alice atakuwa amelilipa kabisa deni lake. Alice haibadilishi bajeti yake mpya. Anatenga shilingi 7,500 kwa mwezi ili kufanya akiba. Ataweka shilingi elfu 5 katika akaunti ya akiba na shilingi 2,500 katika akaunti ya uwekezaji.

Bajeti ya Moja kwa Moja(Automatic budget)

Kwa watu wengi, ni kawaida kupokea pesa zao zote kupitia kwa akaunti moja. Hivyo basi hawafahamu sana kuhusu gharama zao. Kwa sababu hii, ni muhimu kuwa na amana kadhaa za akiba au kuwa na akaunti za benki tofauti. Kwa mfano, unaweza kuwa mbunifu kwa kutenganisha akaunti za muda (fixed accounts) kutoka kwa zile za gharama za mara kwa mara (expenses). Unaweza kufikia malengo haya kwa kuhamisha kiasi fulani kila wiki, au mara moja kwa mwezi, kuelekea kwa akaunti tofauti ya matumizi. Hii itakuhakikisha kuwa hautumii pesa nyingi kwenye vyakula, gharama za mavazi na hata burudani.

Zindua Sheria za Bajeti

Kuendeleza mpango wa bajeti na kuwa na mtazamo wa kijumla mzuri wa gharama za kifedha ni jambo moja, na kuweka bajeti ni jambo tofauti kabisa. Hali hii inaweza kufikiwa kwa urahisi iwapo utajitungia na kufuata sheria kadhaa za bajeti za kibinafsi.

Mojawapo ya sheria bora za bajeti zinazotumika mara nyingi ni ya 50/30/20. Hii inafanyaje kazi? Mpango huu rahisi wa bajeti hukuhimiza kutumia asilimia 50 ya mapato yako kulipia mahitaji, asilimia 30 kwa mahitaji yako na kuweka akiba ya asilimia 20 iliyosalia. Sheria hii ni nzuri kwa sababu hukuruhusu kuweka akiba ya (humusi) moja juu ya tano ya pesa yako bila kuwa mbanifu sana wa matumizi. Tambua zaidi juu ya  sheria hii ya bajeti.

Mbinu tofauti za Kuandaa Bajeti

Kuishi kwa kutumia bajeti haimaanishi kuwa sasa utaacha kufurahia maisha. Ina maana tu kuwa sasa una udhibiti wa maisha yako ya kifedha na kwa mambo yale unayoyawekezea pesa zako.

Ikiwa bajeti inakuzuia zaidi kuliko inavyokusaidia, unaweza kujaribu mbinu nyingine tena. Kwa mtazamo unaofaa na uvumilivu, una uhakika wa kuwa na uwezo wa kufikia malengo yako yote.