Orodha ya Forbes ya watu tajiri zaidi ulimwenguni imejaa watu ambao walianzisha kampuni zao wakiwa vijana. Watu kama Mark Cuban, Bill Gates, na Michael Dell walijijengea utajiri wao kabla ya miaka 20. Hii inaashiria umuhimu wa miaka ya ujana kwa mtu yeyote yule. Hata hivyo, inasikitisha kuwa vijana wengi wanapoteza miaka yao ya ujana kwa kufanya makosa kadhaa. Katika makala haya, tutayaangalia makosa haya ya vijana ili uweze kuyaepuka.
Nikiwa mdogo, wazazi wangu waliniambia, “Maliza chakula chako, kuna watu wengine kwingineko wana njaa.” Mimi huwaambia binti zangu, “Maliza kazi yako ya nyumbani (homework). Kuna watu wengine kwingineko wanatamani sana nafasi kama yako” Thomas Friedman
Makosa ya Pesa ya Vijana
Ujana ni pacha na kutokuwa na uzoefu. Kwahiyo kuna makosa mengi ya pesa ambayo vijana hufanya kutokana na umri mdogo. Tutaangalia makosa haya tukiamini kuwa vijana wakitambua makosa yao, wataweza kuwa na utamaduni bora wa kutunza pesa.
Kuchagua Kozi Isiyofaa
Watu wengi huanza masomo ya chuo kikuu katika miaka yao ya ujana. Kwa bahati mbaya, hii ni hatua ambapo watu wengi hufanya makosa mengi. Utafiti unaonyesha kuwa vijana wengi husomea kozi ambazo hazina thamani sana katika soko la kazi. Mfano wa kozi ambazo hazipendekezwi sana ni pamoja muundo wa mitindo (fashion design), historia, sayansi ya maktaba, na drama.
Kuna sababu tatu zinazofanya kozo hizi zisipendelewe sana. Kwanza, kozi hizi hazihitajiki kwa sana katika soko la kazi. Pili, kozi hizi haziwapi wanafunzi ujuzi halisi wa kutumika ikiwa hawatapata kazi kutokana na kozi hiyo waliyosomea. Tatu, kozi hizo hazilipi vizuri sana. Kwa mfano, mwanasayansi wa maktaba hupata chini ya shilingi milioni 4 kila mwaka. Isitoshe, idadi ya maktaba zinazid kupungua. Hii inamaanisha kuwa kampuni zinazohitaji maktaba zina haja kubwa ya usambazaji zaidi kuliko mahitaji yake.
Jinsi ya kuzuia kuchagua na kusomea kozi isiyofaa kinyakati
Ili kuzuia kosa hili, tunapendekeza ufanye yafuatayo:
- Wasiliana na wataalamu ili kupata habari juu ya mustakabali wa kazi.
- Angalia karibu na wewe na upate fursa ambazo zitakuwa faafu kikazi katika siku zijazo.
- Kabla ya kuisomea kozi, fikiria jinsi sekta hiyo ya ajira itakavyokuwa katika siku zijazo.
Kutokamilisha Masomo
Vijana wengi wanajulikana kwa kutokamilisha elimu yao. Utafiti umeonyesha kuwa watu ambao hukamilisha masomo yao ya vyuo vikuu hupokea pesa nyingi kuliko wale ambao wanaachia masomo katika kiwango cha shule ya upili. Sababu kuu ni kwamba kazi nyingi zinazolipa mshahara mkubwa zinahitaji watu wenye masomo ya chuo kikuu. Yeyote aliye na shahada ya Masters atapata malipo ya juu ikilinganishwa na yule mwenye digrii ya kwanza au hata yule asiye na digrii.
Kwa hivyo, ikiwa wewe ni kijana ambaye anafikiria kuacha shule, tunapendekeza ufikirie tena kuhusiana na hili. Kupuuza haya kutakuletea kujuta kwa maisha yako yote.
Kukosa Kuanzisha Biashara
“Si kila mtu anaweza kufanya biashara.” Kauli hii inamaanisha kuwa sio kila mtu anayeweza kufanikiwa kama mjasiriamali. Wakati mzuri wa kujua ikiwa unaweza kuwa biashara yenye mafanikio au la ni katika miaka yako ya ujana. Kama ilivyoelezwa hapo juu, historia imeonyesha ya kuwa mabilionea na mamilionea wengi walianzisha kampuni zao wakati wa ujana wao.
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kukuvutia ili kuzingatia unapoanzisha biashara yako kama kijana:
- Huna majukumu mengi.
- Una uhuru wa kufeli kutokana na majaribio. Ukifeli, bado unaweza kutafuta ajira nzuri.
- Una muda mwingi ambao unaweza kuutumia ili kuendesha biashara.
- Itakusaidia kuanza kuweka akiba iwapo utastaafu mapema maishani.
Kukosa Mipaka ya Kifedha (Being Extravagant)
YouTube, Facebook, Snapchat, Instagram, na Tiktok ni mitandao ya kijamii ambayao imesaidia pakubwa kuunda kasumba ya ununuzi. Majukwaa haya yanaonyesha watu ambao wanaishi maisha bora zaidi. Kwa sababu ya haya, kampuni zimeanza kuwalenga vijana katika kampeni zao za uuzaji. Kwa mfano, kampuni kama Apple na Microsoft zimewaajiri influencers kuuza bidhaa zao.
Yote hii imefanya vijana wengi wajiingize katika uraibu wa kununua vitu hivi vinavyosifiwa na ma-influensa. Vijana hawa wanalazimika sasa kutaka kununua iPhone ya hivi karibuni na vifaa vya hivi karibuni vya Microsoft Surface. Hii yote imesababisha kuongezeka kwa madeni miongoni mwa vijana. Kuwa na bajeti nzuri kunaweza kusaidia kuzuia hali hii.
Kwa bahati mbaya, vijana ambao wanajiingiza kwenye madeni ya aina hii ni nadra kufanikiwa maishani. Hii ni kwa sababu kiasi kikubwa cha mapato yao huenda kuyashughulikia madeni yao. Kumbuka kuwa, pindi unapoingia kwenye madeni, unaishia kuwa mtumwa wa madeni. Baadhi ya vitu vinavyoweza kukuingiza kwenye madeni, unavyopaswa kuepuka kama kijana ni kama:
- Bidhaa mpya kama vile simu za iPhone na Apple Watch.
- Kujisajili kwenye DSTV, Netflix na intanenti ya kulipiwa kila mwezi.
- Bidhaa za mitindo ya kisasa na ya gharama ya juu kama Gucci na Prada.
- Migahawa ghali
Kuosa Akiba ya Uzeeni (Unapostaafu)
Makosa ambayo vijana wengi hufanya ni kufikiria kuwa hawatastaafu. Wanafikiria kuwa kipindi cha kustaafu ni mbali sana. Hili ni kosa kubwa ambalo vijana hawa wanaishia kujuta. Ikiwa uko chini ya miaka 20, ni jambo la busara kwako kuanza kufikiria kuhusu kustaafu kwako. Kwa mfano, ikiwa utaanza kuweka akiba ya Shilingi elfu 2 tu kila mwezi ukiwa na miaka 15, utakuwa na zaidi ya shilingi milioni moja – pamoja na riba – unapofikia umri wa miaka 60.
Ikiwa utaanza kuweka akiba ya Shilingi elfu 2 kila mwezi wakati una miaka 30, utakuwa na zaidi ya shilingi laki 7 utakapofikia umri wa miaka 60. Pia, kumbuka kuwa unaweza kuishi kwa zaidi ya miaka 15 baada ya kustaafu kwako. Kwa hivyo, tunapendekeza uanze kuweka akiba kwa mujibu wa kustaafu kwako wakati wa miaka yako ya ujana. Unaweza kufanya hivyo kwa kujishughulisha na kazi za muda kama vile graphic design na uundaji na ukarabati wa wavuti.
Kutojifunza Ujuzi Mpya
Kama kijana, rasilimali kubwa ambayo unayo ni wakati. Una wakati mwingi ambao unaweza kutumia kuendeleza taaluma yako. Hivyo basi, hata wakati uko chuoni, tunapendekeza uanze kuwekeza katika ujuzi mpya. Kwa bahati nzuri, kuna majukwaa mengi ambayo yatakusaidia kuanza kujifunza ujuzi mpya. Hii ni pamoja na majukwaa kama:
- Udacity
- Coursera
- Skillshare
- Khan University
- EDX
Muhtasari
Kipindi cha ujana ndicho muhimu zaidi kwa kila mtu. Ni pale msingi wa maisha yao umeanzishwa. Pia ni kipindi ambacho unaruhusiwa kufanya makosa. Kwa hivyo, unaweza kujiwekea msingi mzuri kwa maisha yako ya ujana kwa kuyakwepa makosa haya na kuwekeza kataika kujijenga na kujiinua. Utakuja kutambua kwamba inavutia zaidi kuwa na furaha katika miaka yako ya uzeeni kuliko wakati wa ujana wako.