Makampuni Haya Yanabadili Takataka Kuwa Fedha na Ajira Barani Afrika

Tafsiri:
en_US

Idadi kubwa ya Waafrika wamekuja na ubunifu ambao ni suluhisho kwa udhibiti wa takataka ili kutengeneza mazingira safi na yanayokalika na pia kutoa fedha na ajira.

Inakisiwa kuwa ni asilimia kumi tu ya takataka barani Afrika, ndiyo hufikishwa dampo na nchi tano za kiafrika ni miongoni mwa wachangiaji wakubwa duniani wa taka za plastiki baharini.

Udhibiti wa takataka kwenye nchi zinazoendelea, kwa yakini umetawaliwa na utupaji ovyo wa takataka, ambao mara nyingi huhusishwa na uchomaji ovyo takataka. Uchomaji huu wa takataka unachangia gesi chafu hasa uchomaji wa takataka za kikaboni ambazo zaweza kuchukua zaidi ya asilimia hamsini ya taka ngumu za manispaa.

Fifi Finance inaangalia jitihada chache kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Yo-Waste

Yo-Waste ni mradi wa kiteknolojia uliyoanzishwa nchini Uganda wa udhibiti wa takataka ambao unashughulikia takataka, inazichakata na kuwa suluhisho la usafi wa jiji kwa wafanyabiashara na kwa serkali. Mradi huo wa kijasiriamali unawaunganisha wakusanyaji takataka wa kienyeji, wafanyabishara ya uchakataji taka na wateja ambao wanahitaji huduma hiyo kwa kutumia programu kwenye simu ya mkononi au kwa tovuti yao.

Yo-Waste inawaruhusu wafanyabiashara kudhibiti wenyewe gharama na ukusanyaji wa takataka katika eneo moja. Kwa kutumia Yo-Waste, waweza ukapanga na kuomba huduma ya uzoaji wa takataka, kuanzisha malipo ya kurudiarudia na mengine mengi kwa kutumia bure program ya Yo Waste.

Kwa mfanyabiashara kuanza kutumia huduma ya Yo-Waste, unahitajika kutuma barua pepe kwenye kampuni. Timu ya Yo-Waste watapanga miadi nawe kuja kukagua biashara yako na kufanya unyambulifu wa takataka na kuona ni kwa vipi watakusaidia gharama za ukusanyaji wa takataka na kuzichakata baadhi yake. Baada ya makubaliano kwenye gharama, ambayo mara nyingi ni asilimia ishirini ya gharama ya nyuma uliyokuwa unatumia kwenye ukusanyaji wa takataka, utajaza mkataba na kuanza kutumia huduma zao.

EcoFuture

EcoFuture ni kampuni ya Kinigeria ya kuchakata takataka inayozipa kaya na wajasiriamali wadogo nafasi ya kujipatia kipato kutoka kwenye takataka za plastiki zilizochakatwa kila siku na huku wakisambaza vifaa vilivyosindikwa kwa viwanda vya uchakataji nchini Nigeria.

EcoFuture inazikusanya takataka za plastiki zilizokwisha chakatwa kutoka kwenye kaya na kituo cha biashara kilichoanzishwa kwa kupitia tovuti, program ya simu ya mkononi na ujumbe wa simu ya mkono.

Kwenye ukusanyaji, takataka kutoka kila kaya, zinapimwa kwenye mzani na ujazo huo unaingizwa kwenye hifadhi data. Kisha kaya hutuzwa pointi zinazogomboleka kwa kuzingatia ukubwa na kiwango cha takataka zilizochakatwa wanazotupatia.

Kwa vile kaya huzilimbikiza pointi kwa muda, wanaweza kuzigomboa pointi hizo kwa zawadi maalum kama vile vyakula, bima ya afya na pesa taslimu kutegemeana na kiasi na aina ya takataka wanazozichakata.

Mr Green Africa

Mr Green Africa ni kampuni ya Kikenya yenye makao yake mji mkuu Nairobi, ambayo imejenga mfano wa biashara ya udhibiti wa takataka ambayo kimsingi inakusudia kuwainua waokota takataka na jamii zao.

Mr Green Africa inawamotisha waokota takataka wa pembezoni na msingi wa wadau wa piramidi kwa kuwapatia bei ya malipo na mafao zaidi, kufanya usambazaji endelevu wa takataka zinachokatwa ambazo hutoa njia za kuondokana kwao na umasikini, sanjari na kuleta matokeo chanya ya mazingira.

Mr Green inasindika takataka zilizochakatwa kuwa malighafi yenye thamani na makapi yake kutengeneza mfumo wa usambazaji wa bidhaa za plastiki. Waokota takataka wanafaidika kutoka kwa programu mbalimbali aminifu za msambazaji na huduma nyingine kama ujuzi wa maisha na ujasiriamali, msaada wa huduma za afya na pia kuweza kupata mikopo midogo midogo. Faida nyingine zisizo za kifedha, ni pamoja na kupatiwa mavazi ya kujikinga kama glavu na buti pamoja na nyenzo kama simu za mikononi kwa nyakati fulani.

Mr Green Africa inawaona waokota takataka wasio rasmi kama mashujaa wasioonekana ambao wameminywa chini ya mfumo wa takataka kwa muda mrefu. Kuanzisha utaratibu ambao waokota takataka wasio rasmi wanafanya biashara moja kwa moja na Mr Green Africa kunawapa mashujaa hawa wasioonekana fursa adimu ya kuboresha maisha yao.

WeCyclers

Nchini Nigeria, WeCyclers hutoa huduma rahisi ya kuchakata takataka kwa kaya kwa kutumia baiskeli za mizigo za gharama nafuu ziitwazo WeCyclers.

Tunawezesha mabadiliko ya kijamii kwa kutumia mazingira kwa kuwaruhusu watu kwenye jamii za kipato cha chini, kujipatia thamani kutoka kwenye takataka zao.

Kampuni inahamasisha familia kuchakata chupa za plastiki, mifuko ya plastiki na makopo ya alumini. Takataka zikusanywazo kutoka kwenye kaya hupimwa kwa siku maalum za wiki. Familia hupewa pointi za WeCyclers kwa kila kilo ya takataka wazitoazo. Pointi hizo hugombolewa kupitia vitu kama simu za mikononi, vyakula muhimu na vitu vya nyumbani. Familia hupokea taarifa za kukumbushwa ukusanyaji na pia taarifa za zawadi moja kwa moja kwenye simu zao. Baada ya kukusanya, WeCyclers huzichanganya takataka ambazo huziuza kwa wasindikaji wa takataka wa maeneo yao.

Takataka Solutions

Takataka Solutions ni kampuni ya Kikenya inayodhibiti takataka. Inakusudia kuwabadilisha fikra Wakenya juu ya takataka. Kampuni inakusanya takataka kutoka kwenye kaya, sehemu za biashara na viwandani.

Tunazichukua takataka kwenda kwenye maeneo yetu maalum ya uchambuzi ambako tunazichambua takataka kuwa zaidi ya vijisehemu arobaini. Tunavundika takataka za kikaboni kuwa mboji ya kiwango cha hali ya juu, huku vitu vingine kama karatasi, plastiki, chupa, chuma ama tukivichakata sisi wenyewe au kwa kupitia washirika wetu. Hii inatuwezesha kufikia kiwango cha juu kabisa cha uchakataji takataka duniani- asilimia tisini na tano!

Asilimia sitini na tano ya takataka zinazokusanywa na kampuni yetu ni za kikaboni. Sehemu yake ndogo huuzwa kama chakula cha nguruwe na inayobaki hutengeneza mboji ya kiwango cha hali ya juu iitwayo “TakaSoil” ambayo hutumika kama dawa ya kurutubisha udongo ili kuuimarisha na kuujenga kwa kilimo na kwa bustani.

Repurpose Schoolbags

Repurpose Schoolbags ni jithada ya Rethaka Foundation ya Afrika Kusini. Jitihada hii inajumuisha uchakataji wa takataka, nishati ya jua na elimu.

Mifuko ya mgongoni inatengenezwa kwa asilimia mia moja na takataka za plastiki zilizochakatwa, ikiunganishwa na paneli ya nishati ya jua inayojichaji wakati wa mchana wakati mwanafunzi akienda shule. Hii kwa upande mwingine, inatumika kama chanzo cha stima kwa watoto wanapojisomea ana kufanya kazi za kufanyia nyumbani wakati wa giza.

Mabegi hayo yamebuniwa pamoja na michirizi inayoakisi kama hatua ya usalama, kuwafanya watoto waonekane wakati wakienda shuleni mapema asubuhi sana.

Plastiki iliyotumika kutengeneza mabegi hayo huchukuliwa majalalani na pia kwenye shule zinazoendesha kampeni kwa wanafunzi wao kuleta plastiki ili kuonesha upingaji wa utupaji ovyo takataka.

EcoPost

EcoPost ni biashara jamii ambayo inatoa suluhisho mbadala kwa udhibiti wa takataka ambalo ni moja ya tatizo kubwa la takataka nchini Kenya.

EcoPost inakusanya takataka za plastiki na kutengeneza bidhaa imara, rafiki kwa mazingira, nguzo za uzio, alama za barabarani na samani za nje.

Plastiki mara nyingi huoneshwa kama mhalifu wa uharibifu wa mazingira. Lakini haipaswi kuwa hivyo. EcoPost ni biashara jamii inayotanabaisha changamoto za udhibiti wa takataka mijini (uchafuzi hewa wa plastiki), tatizo sugu la ajira kwa vijana,ukataji miti na mabadiliko ya tabia nchi.

Eco Shoes

Eco Shoes ni shirika la biashara jamii lenye makao yake nchini Ghana ambalo linatumia vitambaa vilivyotumika, matairi yaliyotumika na sehemu ya viatu vilivyotumika kuwa viatu vizuri na vitu vya kiutamaduni au kihistoria.

Tunawaajiri wanawake wengi muhimu, vijana wa mitaani waliorekebika na watu wenye ulemavu ili kutengeneza msingi wa uzalishaji wetu. Tunaugusa uwezo binafsi wa watu hawa ambao vinginevyo, wangekuwa hawana ajira au kuishi chini ya mstari wa umaskini na kuuinua ujuzi wao kupitia mafunzo ya mara kwa mara.

Hitimisho

Ufumbuzi wa udhibiti wa takataka na jitihada barani Afrika zimetatua tatizo kubwa la ajira na fedha. Ukiondoa kodi kutoka kwenye viwanda vinavyochakata bidha za plastiki, kodi kwenye soko la dunia la udhibiti wa takataka, ilikisiwa kuongezeka kutoka dola za kimarekani 265.61 mwaka 2017 hadi dola za kimarekani 282.1 mwaka 2018.

Iwapo umeburudishwa na makala hii, tafadhali ‘ipe mabawa’ kwa kuisambaza kwa wengine.