Mwongozo wa Kupata Mkopo wa Ununuzi wa Mali Isiyohamishika Nchini Kenya

Tafsiri:
en_US

Mkopo maalum kwa ajili ya ununuzi wa mali isiyohamishika, inazidi kupatikana kwa urahisi nchini Kenya. Mikopo hii mara nyingi mkopo wa nyumba au mkopo wa ardhi. Kwahiyo wanunuzi wamekuwa wakiitumia mikopo hii ili kuwasaidia kujipatia eneo au maeneo. Wakopeshaji wengi nchini Kenya, wanahitaji mkopaji alete hati ya umiliki wa mali kama dhamana ya mkopo kwake.

Kufikia mwezi Desemba mwaka 2017, idadi ya wakenya waliokuwa wamechukua mikopo ya aina hii, ilikuwa 27,000. Idadi hii inatarajiwa kuongezeka kwani watu wengi wanachagua aina hii ya mkopo kwa uwekezaji. Mkopo huu wa ununuzi wa mali isiyohamishika, unapatikana kiurahisi, hasa kutoka kwa taasisi nyingi za kifedha. Ni vizuri kufahamu kuwa mkopo huu una riba.

Hatua za Kupata Mkopo wa Ununuzi wa Mali Isiyohamishika

Zifuatazo, ni hatua zitumiwazo na wakopeshaji ili kutoa mkopo:

  • Jinsi ya kuomba mkopo wa ununuzi wa mali isiyohamishika: Yakubidi ufike kwa mkopeshaji unayempenda kwa ajili ya kukuthibitisha. Mkopeshaji ataangalia kipato chako kwa mwezi ili kuona unastahili kupewa kiasi gani. Kipato chako, pia kitatumika kuona ni kiwango gani utapaswa kulipa kama marejesho ya mkopo. Mkopeshaji pia ataangalia hali yako ya nyuma ya kifedha ili kujiridhisha na ukopaji wako. Miongoni mwa mambo mengine atayoyaangalia mkopeshaji pia ni umri wako. Kadri ulivyo kijana, na ndivyo urefu wa urejeshaji wa mkopo wako utakavyokuwa.
  • Utolewaji wa mkopo: Mkopeshaji akijiridhisha kuwa unakopesheka na kwamba unao uwezo wa kulipa mkopo, basi taratibu za kuidhinisha ombi lako huanza. Mchakato huhusisha wewe mkopaji kuleta nyaraka mbalimbali za benki, makubaliano ya mauzo, barua ya ofa na ripoti ya tathmini.
  • Utoaji wa ofa: Mchakato ukamilikapo, mkopeshaji atampatia mwombaji barua ya ofa. Barua hiyo huwa na masharti pamoja na vigezo vya mkopo. Mkopaji anapaswa kukubaliana na masharti na vigezo hivyo, kisha mkopeshaji huendelea na uhalisia wa mali.
  • Uhakiki wa mali: Pindi mkopaji akubalipo vigezo na masharti ya mkopo, mkopeshaji huendelea na uhakiki wa mali. Hii ni hatua ambayo mkopaji hutoa taarifa za mali iliyowekwa kama dhamana kwa mkopo wake. Mkopeshaji atampatia mnunuzi hati ya mali ili kumalizia uhamisho wa umiliki. Kisha mkopeshaji huchukua hati ya umiliki pamoja na nyaraka nyingine za usajili na kuandika malipo.
  • Malipo: Usajili ukamilikapo, malipo hufanyika. Mkopeshaji humpatia aidha mkopaji au mnunuzi kiasi kilichokopwa. Mchakato huu waweza kuchukua siku kati ya 90 hadi 180. Mchakato huenda kasi kutegemeana na upatikanaji haraka wa nyaraka muhimu. Pia kasi ya usajili wa mali kwenye mamlaka husika, huchangia kujua mchakato utachukua muda gani.

Nyaraka Muhimu Wakati wa Uombaji wa Mkopo wa Ununuzi wa Mali Isiyohamishika

Nyaraka mbalimbali huhitajika wakati wa kuomba mkopo. Hata hivyo, nyaraka hizi hutofautiana kutokana na aina ya mkopo. kwa mfano, kukopa ili kununua gari, ujenzi au kununua kutoka kwa mwendelezaji.

Mkopo wa Ununuzi wa Nyumba

  • Hati ya umiliki wa ardhi.
  • Hati ya kibali cha thamani ya ardhi.
  • Barua ya ofa au makubaliano ya mauzo.
  • Hati ya kibali cha ardhi.

Mkopo kwa Ujenzi wa Nyumba:

  • Hati halisi ya umiliki wa ardhi.
  • Hati ya kibali cha thamani ya ardhi.
  • Michoro iliyoidhinishwa.
  • Hati ya kibali cha kukodi.
  • Andiko mradi lioneshalo malipo kwa mradi.

Mbinu za Kupata Mkopo Nafuu wa Ununuzi wa Mali Isiyohamishika

Biashara ya ardhi au majengo, imevamiwa na wimbi kubwa la udanganyifu. Hivyo ni vyema kufanya uchunguzi yakinifu na kusaka kupitia msajili wa ardhi kabla ya kuchukua hatua yoyote. Kusaka ni muhimu ili kubaini umiliki wa mali na kujiridhisha kuwa mali hiyo, haina mtu mwingine anayedai kuimiliki.

Tafiti thamani ya mali ili kujiridhisha kuwa thamani iliyotolewa na muuzaji ni sahihi. Gharama ya ardhi au jengo, huamuliwa na mahali lililoko, ukubwa wake, huduma zipatinakanazo na hali yake. Kisha hakikisha una mwanasheria ambaye atazihifadhi nyaraka muhimu kwa msajili wa nyaraka.

Hati ya umiliki wa ardhi au nyaraka nyingine zihusianazo na umiliki wa ardhi au mali, hubakia kwa mkopeshaji hadi pale utakapokamilisha malipo ya deni lako lote. Waweza pia kuhitajiwa kulipa malipo ya awali ambayo mara nyingi ni asilimia kati ya tano hadi ishirini ya gharama ya mali. Ukilipa malipo makubwa ya awali, unapunguza gharama ya mkopo wako. Pia zipo gharama ziambatanazo na mkopo kama vile ada za kisheria, ada za tathmini, ada ya uthaminifu, ada ya uhamisho na usajili wa ardhi au jengo. Gharama ya jumla inakaribia asilimia kumi ya bei ya mali husika.

Hitimisho

Iwapo unakusudia kujenga nyumba au kupata ardhi au jengo, fikiria kuchukua mkopo wa ununuzi wa mali isiyohamishika. Lakini hakikisha unafanya uchunguzi yakinifu wa mali hiyo na pia hakikisha masharti ya mkopeshaji ni nafuu.