Mwongozo wa Mipango ya Mafao ya Pensheni Nchini Kenya

Tafsiri:
en_US

Watu hujiandaa kwa uzee na kustaafu kwa njia tofauti. Baadhi huwekeza kwa watoto wao kama namna ya kujikimu wazeekapo wakati wengine huwekeza kwenye mafao. Mafao ya pensheni ni muhimu, hususani kwa waajiriwa wanaostaafu wakati wafikishapo umri wa kustaafu.

Kujiandaa kwa uzee wako, ni kitu muhimu wakati unapokuwa na nguvu za kufanya kazi, huku ukitunza fedha kwa ajili ya familia yako. Mafao ya pensheni huwa na riba kwa muda na ufikapo muda wa kustaafu, utakuwa umejilimbikizia fedha za kutosha kuendeshea maisha.

Mfumo wa Mafao ya Pensheni Nchini Kenya

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii unatoa ulinzi wa kifedha kwa mafao ya Wakenya pindi wanapostaafu. Mfumo unafanya kazi kutokana na michango inayokusanywa kutoka kwa wanachama na zaidi umejikita kwenye sekta ya ajira rasmi.

Sheria mpya ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii inasema asilimia kumi na mbili ya mshahara wenye mafao, utawasilishwa kwenye mfuko kama mchango. Asilimia 12 hugawanywa mara mbili, asilimia sita kutoka kwa mwajiriwa na asilimia sita kutoka kwa mwajiri. Hata hivyo, sheria hii, bado haijaanza kutumika kutokana na kesi mbalimbali dhidi yake.

Sheria ya zamani ya mfuko bado inaendelea kutumika ambapo kila mwajiriwa anapaswa kulipa shilingi 200 za Kenya (karibu dola 2 za Kimarekani) pamoja na kiasi hicho hicho kutoka kwa mwajiri. Ni muhimu kufahamu kuwa mafao, sio jambo la lazima kwa waajiri kwa vile wako huru kuanzisha mifuko yao ya hifadhi ya waajiriwa.

Mishahara, Mafao ya Pensheni na Sheria za Kazi Nchini Kenya

Kifungu namba 189 cha Sheria ya Mafao ya Pensheni, kinatoa udhibiti sahihi wa mafao ya pensheni, kiinua mgongo na posho kwa watumishi wote wa umma walio chini ya serkali nchini Kenya. Watu wafanyao kazi kwenye sekta binafsi, wanaweza pia kuwasilisha michango yao.

Mamlaka ya mafao ya ustaafu (RBA) ilianzishwa ili kudhibiti, kusimamia na kuhamamsisha mipango ya mafao ya ustaafu ambayo kimsingi, iko kwa waajiriwa walio kwenye sekta rasmi. Ibara ya tisa na ya kumi ya sheria ya ajira ya mwaka 2007, inasema kila mwajiriwa, ataajiriwa chini ya mkataba. Mkataba ambao utajumuisha mafao ya pensheni na mipango ya mafao ya pensheni. Hii inamaanisha kuwa waajiriwa watahusishwa kwenye mipango ya mafao ya pensheni.

Pension schemes support one's family upon retirement or death.
Mafao ya pensheni ni muhimu kwa wategemezi pindi mwajiriwa anapofariki.

Faida za Mafao ya Pensheni

Mafao ya pensheni yana faida nyingi sana kwa mtu binafsi na kwa familia yake aidha anapofariki au anapostaafu. Wategemezi wake hupata kiasi fulani cha mafao. Tutaangazia mafao ya pensheni kwa mwajiriwa anapofariki na mafao anayoyapata.

Mafao ya Pensheni kwa Familia ya Mwajiririwa Aliyefariki

Ibara ya 17 ya sheria ya mafao ya pensheni inasema wategemezi wa mwajiriwa, watapokea mafao baada ya kifo chake. Yaweza pia kuwa baada ya kustaafu kwake endapo amefanya kazi kwa miaka kumi au zaidi. Mtu aweza kupewa mafao ya pensheni kwa mkupuo au kwa aina ya mafao. Iwapo marehemu hakubainisha wapaswao kulipwa au wategemezi, hapo wadhamini kwa ridhaa yao, wataamua kuwapatia mafao wategemezi.

Mafao ya Pensheni kwa Mwajiriwa Ambaye Ajira Yake Imesitishwa

Kwa bahati mbaya, nchini Kenya, hakuna mafao kwa wasio na ajira. Hata hivyo, mtu aweza aweza kupata mafao ya pensheni pindi ajira yake inapositishwa. Ibara ya sita ya sheria ya mafao ya pensheni inaruhusu malipo ya pensheni, mafao na posho pindi ajira ya mtu inapositishwa.

Mwajiriwa anapaswa kulipwa malipo ya ajira iliyositishwa, ambayo si zaidi ya siku 15 kwa kila mwaka kamili aliofanya kazi kwa mwajiri yule yule. Hata hivyo, iwapo mkataba wa ajira iliyositishwa ni kutokana na utovu wa nidhamu, anapaswa kulipwa malipo ya ajira inayositishwa. Sheria ya ajira inasema mwajiriwa atalipwa marupurupu kwa kazi iliyofanywa kabla ya ajira kusitishwa, malipo ya likizo ya mwaka na cheti cha utumishi.

Ukokotoaji wa Malipo ya Pensheni

Sheria ya zamani ya mfuko wa hifadhi ya jamii, inadai asilimia kumi ya mapato ya mwajiri kama mchango. Hata hivyo kuna malipo yanayojumuishwa ya hela ‘kilemba’ ya shilingi 400 za Kenya. Hata hivyo sheria mpya ya mfuko wa hifadhi ya jamii inataka asilimia 12 ya mchango, asilimia 6 toka kwa mwajiriwa na asilimia nyingine 6, toka kwa mwajiri.

Sheria mpya ya mfuko wa hifadhi ya jamii ina aina mbili za michango. Aina ya kwanza imejikita kwenye malipo ya pensheni yaliyo chini ya kiwango cha mshahara kilichowekwa. Aina ya pili imejikita kwenye mapato ya mafao ya pensheni yapitayo kiwango cha chini cha mshahara. Kiwango cha chini cha mshahara kimepangwa kuongezeka kutoka shilingi za Kenya 6,000 kwa mwaka wa kwanza na shilingi 7,000 kwa mwaka wa pili hadi wa tano. Katibu wa Baraza la mawaziri kisha ataangalia kwenye michango ya kila mwezi kwakuzingatia kiwango cha chini kitakachofikiwa.

Mfumo wa Kodi kwa Malipo ya Pensheni

Malipo ya pensheni yana kodi inayodhibitiwa na ibara ya 8 ya sheria ya kodi ya mapato. Mafao yapatikanayo kwa njia ya pensheni, yanatozwa kodi. Hata hivyo, wanachama wanaweza kuomba msamaha wa kodi na kulipwa kwa mkupuo shilingi 60,000 za Kenya wakati wa kustaafu kwa kila mwaka wanaoendelea kuwa watumishi hadi wafikishe kiasi cha shilingi za Kenya 600,000.

Mafao yafuatayo, yanatozwa kodi. Malipo ya kwanza yalipwayo kwa mkupuo shilingi za Kenya 60,000, michango chini ya shilingi 20,000 za Kenya kwa mwezi au asilimia thelathini chini ya mshahara wenye pensheni na pia mapato yatokanayo na vitega uchumi.

Hitimisho

Mafao ya pensheni ni muhimu kwa wategemezi na mwajiriwa pindi anapofariki au anapostaafu. Kwahiyo ni muhimu kuwa mwanachama wa mpango wa pensheni nchini Kenya.