Njia 10 za Kujipatia Bidhaa za Bure Barani Afrika

Tafsiri:
en_US

Inapofika wakati wa kuhifadhi fedha, kila mtu hutaka ajipatie bidhaa za bure. Kuna njia nyingi ambazo waweza kupata bidhaa za bure barani Afrika kutoka kwenye vyumba vya hoteli, mikahawa na tiketi za sinema. Waweza kupata bidhaa za bure kupitia mtandao au hata kutoka ujirani ndani ya jamii yako. Baadhi ya bidhaa zitolewazo bure hutolewa na makampuni yanayotangaza biashara zao au watu binafsi ambao huona hawazihitaji.

Waafrika Kusini huhifadhi mabilioni ya randi kwa kujisajili kwenye programu za uaminifu (loyalty) kwenye maduka makubwa ya rejareja kama vile Pick n Pay.

Wawezaje kupata bidhaa za bure barani Afrika?

1. Tazama Kutoka Maeneo ya Karibu na Ulipo

Waweza kuangalia matangazo ya bidhaa za bure mtandaoni au kwenye maeneo mengine kama Facebook. Waweza pia kuuliza kwa watu jirani yako kama kuna sehemu uwezayo kupata bidhaa za bure. Waweza kupata vitu vitolewavyo bure kama samani na vyombo vya nyumbani.

2. Bidhaa za Mfano

Maduka hutoa bidhaa za mfano wakati wanapozitangaza. Waweza kuziona bidhaa mpya kama zile za urembo na manukato na kuendelea kufuatilia ni lini kampuni itatoa bidhaa za bure za mfano. Kama huwezi kuzipata hizo bidhaa za mfano, waweza pia kuangalia kutoka kwa watengenezaji kupitia mtandao. Baadhi ya wazalishaji hutoa bidhaa za mfano kwa majaribio au kwa mapitio.

3. Jisajili na Program ya Uaminifu

Waweza kujisajili kupata zawadi kutoka migahawani na kwa wafanya biashara wadogo wadogo walioko jirani na wewe. Mara nyingi wanatoa zawadi maalum kwa wanachama wao wakati wa matukio kama siku ya kuzaliwa, kutegemeana na manunuzi yako kwao. Unaweza kabisa kujipatia tiketi ya bure ya sinema, chakula, kadi ya zawadi au hata bidhaa.

Kwa mfano, watumiaji nchini Afrika Kusini wanatunza mabilioni ya randi kupitia programu za uaminifu. Kwa mujibu wa Truth Loyalty White Paper mwaka 2018, maduka ya dawa na ya bidhaa za urembo nchini Afrika Kusini yanaongoza linapokuja suala la programu za uaminifu. Maduka sahihi zaidi kwa program za uaminifu nchini Afrika Kusini ni Clicks Clubcard, Pick n Pay Smart Shoppers and Dis Chem Benefit Programme.

4. Jihusishe na Sherehe za Taifa za Chakula

Kwa watu wanaojishughulisha sana na mitandao ya kijamii, waweza kuona kuna sherehe za maadhimisho ya vyakula vingi. Waweza kuuona mgahawa au sehemu iuzayo chakula karibu nawe ambayo inashiriki kwenye matukio hayo na waweza kujipatia kinywaji au chakula cha bure. Kwa mfano, wakati wa siku ya kimataifa ya kahawa, ambayo ni tarehe 1 ya mwezi wa kumi, migahawa mingi huwapatia wateja wao kikombe cha bure cha kahawa.

5. Jisajili na Matumizi ya Bure ya Majaribio

Waweza kujipatia runinga ya bure au chombo cha nyumbani kwa kujisajili na matumizi ya bure ya majaribio. Kwenye huduma nyingine za mtandaoni, makampuni mengi hutoa mwezi mmoja wa matumizi bure. Kwa hiyo, kwa upande wa programu, waweza kupata mwezi mmoja bure wa huduma kwa kujisajili na kampuni hiyo. Mara muda wa bure unapomalizika, waweza kusitisha huduma ili kuzuia gharama zaidi.

6. Shiriki Kwenye Mashindano

Kwa kushiriki kwenye mashindano na matukio mengine, inawezekana kujishindia zawadi nono. Kwa mfano, vituo vingi ya redio Afrika Mashariki, hutoa zawadi maridhawa kwa watu wanaoshiriki kwenye shindano. Kando ya hayo, waweza kuzawadiwa kwa mapitio ya tangazo.

7. Badili Kadi za Credit kuwa Zawadi:

Je, una kadi ya Credit, kama una pointi zitokanazo na matumizi ya kadi za Credit, waweza kuzibadilisha kwa zawadi za kupanda ndege au hata mapumziko. Baadhi ya kadi za Credit zina zawadi maalum kama vile kuwezeshwa kwenye huduma za bima za usafiri na uingiaji kwenye veranda za viwanja vya ndege. Tafiti ni aina zipi za zawadi uwezazo kuzipata na ulipe kwenye kadi ya Credit ili kuzipata zawadi hizo.

8. Shiriki Katika Tafiti za Mitandaoni

Waweza kabisa kujipatia kadi ya zawadi au fedha kwa kujibu tu maswali kadhaa. Inachukua dakika chache kujibu maswali hayo na waweza kujipatia muda wa bure wa maongezi au tiketi za kuingilia sehemu mbali mbali. Waweza kuangalia hapa kuona tafiti za mtandaoni zinazopatikana nchini mwako na ujisajili ili kufikiriwa kwa tafiti zijazo. Endapo upo kwenye nchi ambayo M-Pesa inapatikana kama vile Kenya Uganda na Tanzania, waweza kushiriki kwenye huduma hizi za tafiti za mtandaoni na kulipwa kupitia M-Pesa.

Tafiti nyingi za mitandaoni sio halisi na hawalipi kama wanavyoahidi kwenye tovuti zao.

9. Tumia Kuponi

Ni rahisi kupata punguzo kutoka maduka na chapa mpya karibu yako. Mara nyingi, unaponunua bidhaa, unapewa nyingine bure. Waweza kupata kuponi kutoka maduka ya mtandaoni au kwenye masoko makubwa karibu yako. Waweza pia kupata kutoka tovuti za kuponi nchini Kenya, Tanzania, nk. Soma vigezo na masharti ya duka ili kuona kama unakidhi kupata kuponi.

10. Angalia Kutoka Kwenye Mashamba Karibu Yako

Mashamba mengi ya jamii, hutoa sehemu ya mazao pindi wapatapo mavuno mengi au kuwa wameshapanga mazao kwa kulingana na ubora wake. Unachotakiwa kufanya ni kuyatambua mashamba yamilikiwayo kwa ujima na kuyafuatilia nyakati wanapotoa nafaka za bure au aina nyingine ya mazao. Hii ni njia bora sana ya kujipatia chakula cha bure.

Jaribu baadhi ya njia zilizotajwa hapo juu and waweza kujipatia chakula cha bure, safari ya bure au zawadi maalum kama runinga. Kumbuka kufuatilia ili kujua muda nafasi hizo zinapopatikana.

This post is also available in en_US.