Jinsi ya Kuweka Akiba

Tafsiri:
en_US

Kila mtu anataka kuwa na maisha ya starehe na kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya wategemezi wake. Msingi wa uimara kama huu wa kifedha ni usimamizi mzuri wa fedha. Kwa vile matumizi ya teknolojia ya kisasa yamekita mizizi yake katika Afrika, kuna njia nyingi za kidijitali ambazo mtu anaweza kutumia ili kutimiza malengo yake ya kifedha.

Njia moja ni matumizi ya programu za kifedha, ambazo hufanya kazi kama zana za kuwezesha kuweka akiba na kuwekeza kwa njia ya busara. Ingawa orodha ni ndefu, baadhi ya prgramu bora za fedha za kibinafsi katika Afrika zinazoweza kukusaidia kuhifadhi na kuwekeza fedha ni pamoja na:

Mint

https://www.youtube.com/watch?v=JPfI6iOAbbI

 

Mint ni programu ya fedha za kibinafsi ambayo inayowawezesha watumiaji kuangazia bajeti zao kwa urahisi. Kwa njia ya teknolojia hii, wateja wake wa Afrika wanaweza kuhifadhi fedha ili waweze kununua bidhaa wanazotaka, kulipia bili mara moja, na pia kuweza kudhibiti alama yao ya mikopo. Pia, ni chombo madhubuti kwa ajili ya kufuatilia utendaji wa uwekezaji mbalimbali pamoja na kuwatahadharisha wateja kuhusu shughuli yoyote isiyo ya kawaida kwenye akaunti zao.

Ili kupata huduma bora ya Mint, unahitaji kuunganisha akaunti yako. Utaratibu huu unahitaji:

  • Jisajili kupitia programu ya Mint au kwenye tovuti ya Mint kwa kutumia barua pepe yako. Ingiza nywila ili kuwa salama na faragha.
  • Fuata maagizo ili kuunganisha mint na akaunti kama vile PayPal, mikopo na kadi za benki, na rehani. Vipengele vya usalama vya programu hii ni dhabiti sawia zile za benki, na hivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi.
  • Andaa bajeti. Unaweza kufanya marekebisho kama vile makundi ya bidhaa za kununuliwa, kubinafsisha jinsi ya kuarifiwa, na kuweza kugawanya gharama.

YNAB

 

Hii ni programu nyingine ya fedha za kibinafsi katika Afrika. YNAB (You Need A Budget) ni sawa na mbinu ya jadi ya bajeti ya bahasha. Programu inadai kuwa watumiaji wake wana uwezo wa kuhifadhi zaidi ya dola 6,000 katika mwaka wao wa kwanza wa kutumia mpango huu. Inatoa muda wa bure wa majaribio ya siku 34, na baadaye mtu anahitajika kulipa dola 11.99 kwa mwezi au dola 83.99 kwa mwaka. Mpango huo una makocha, uwezo wa kupiga soga, mazungumzo yaliyorekodiwa, na rasilimali nyinginezo za kuwasaidia zaidi watu binafsi kuhusu bajeti zao.

Kanuni za matummizi ya YNAB ni:

  • Gawanya malipo yako kwa makundi maalum ya gharama kabla ya kutumia fedha zako.
  • Tenga baadhi ya fedha kwa matumizi yasiyo ya kila mwezi kama njia ya kujiandaa kwa ajili ya malipo hayo.
  • Mambo huweza kuwa magumu, kwa hivyo tenga fedha ya kutosha ili kukidhi vitu ambavyo una uwezekano wa kugharamika zaidi kuvinunua.
  • Jitahidi kutumia mapato ya mwezi uliopita kwenye matumizi mwezi wa sasa, na pia kuhakikisha matumizi yako yako chini ya mapato yako.

Kutumia programuu hii ya bajeti ya YNAB, unahitaji:

  • Kujisajili kwa kwenye tovuti.
  • Kufuata maagizo ili kukuwezesha kuiunganisha kwa akaunti yako ya benki.
  • Kuamua juu ya kiasi cha fedha unachotaka kufanyia bajeti ya mwezi na kugawa kwa makundi yanayokufaa.

Cinch Financial

 

Cinch Financial ni mojawapo ya programu bora za fedha za kibinafsi unayoweza kutumia barani Afrika, ambayo inafanya kazi kwa kufanya tathmini ya matumizi ya mtu pamoja na tabia zake za kuweka akiba. Taarifa hizi zitawezesha programu hii kupendekeza uboreshaji wa kuweka akiba na kwa ujumla, uimara wa kifedha. Kuna nguzo nne za kimaadili zizoongoza katika shughuli zao. Hii ni pamoja na:

  • Mtiririko wa matumizi. Cinch hufuatilia mapato yako, bajeti na matumizi. Hatimaye, hukupa taarifa kuhusu kiasi ambacho lazima uwe nacho ili uweze kutimiza gharama maalum.
  • Madeni na mikopo. Chombo hiki cha usimamizi wa fedha hukusanya madeni yako ikiwa ni pamoja na mkopo wako wa elimu, gharama ya deni ya kadi ya benki, na mikopo mingineyo. Hii hufanya kazi kama ukumbusho wa majukumu yako ya kifedha.
  • Bima. Kwa kuwa bima huwa muhimu kwa utulivu wa kifedha, programu hii kutathmini madeni yako, wategemezi, na mapato yako ili kuamua kama bima yako ni ya kutosha.
  • Hazina ya Akiba. Cinch huonyesha kiasi cha fedha unachostahili kuweka kando kwa ajili ya gharama isiyotarajiwa na hata kutoa mwongozo wa iwapo unahitajika kuongeza kiasi hiki.

Ili kujisajili kwenye programu hii, unahitajika kufuata hatua hizi:

  • Maelezo ya kibinafsi. Jibu maswali yaliyowasilishwa kuhusiana na wategemezi wako, bima, umiliki wa nyumba na gari, na mapato ya nyumbani.
  • Wasifu wako wa mikopo. Utaruhusu programu kukusanya taarifa zaidi kuhusu mkopo.
  • Kuunganishwa kwa akaunti. Utahitajika kuunga Cinch kwa akaunti yako ya fedha
  • Maelezo ya mwisho. Jibu maswali yaliyowasilishwa kuhusu tabia yako ya kifedha.

Albert

 

Programu hii ya fedha za kibinafsi ni sawa kwa kiasi fulani na Cinch Financial ingawa inaongeza mguso wa kibinadamu kwa mpangilio wake. Albert haitozwi ada na inawawezesha watumiaji wake kuambatana na mpango wao wa akiba walivyoainisha. Baada ya kuamua kiasi ambacho unaweza kuweka akiba bila shida katika mwezi, kiwango hiki kitahamishwa moja kwa moja kwa akaunti yako ya akiba ya Albert. Mbinu hii pia husaidia kufuatilia matumizi yako kama njia ya kuepuka matumizi yasiyo ya lazima. Pia, ina kipengele cha ziada kinacholipiwa kiitwacho Albert Genius, ambacho kinatoa huduma kama vile malengo ya akiba, na ushauri wa kitaalam wa kifedha.

Ili kutumia programu hii ya fedha za kibinafsi, unahitaji:

  • Kupakua programu hii ni na ufuate maelekezo.
  • Kuanzisha akaunti yako ya akiba ya Albert. Aidha unaweza kutumia chaguo la akiba smart au kuamua kuhusu kiasi mahsusi cha kuweka akiba kila wiki.

Acorns

Acorns ni mojawapo ya programu za fedha za kibinafsi unayoweza kutumia kuwekea akiba na kuwekeza fedha. Inafanya hivyo kwa kuzifanya jumla salio ya kila kadi ya mikopo au kuangalia shughuli za akaunti na kuwekeza kiwango cha ziada. Ingawa si bidhaa maalum kwa ajili ya malengo ya muda mrefu kama vile kuweka akiba kwa ajili ya kustaafu, ni nzuri kwa ajili ya vijana wa kisasa na makundi mengine ya watu ambao hawana uwekezaji mkubwa. Pia, ina sifa za ziada za kusaidia kuhusu mpango binafsi wa akiba.

Ili kuanza, unahitaji:

  • Pakua programu Acorns au jisajili katika tovuti.
  • Tumia anwani yako ya barua pepe ili kupokea taarifa muhimu mara kwa mara.
  • Ingiza maelezo yako ya benki ya mtandanaoni pamoja na akaunti na nambari ya kuelekezewa huduma. Utahitajika pia kutoa anwani yako ya mahali halisi.
  • Jaza maelezo ya jumla ya wasifu ikiwa ni pamoja na kazi yako, mapato, na malengo ya kifedha.

Hitimisho

Msingi wa uimara wa kifedha ni kuongeza mapato yako kwa kuwekeza kwa njia ya busara na kupambana na kutumia zaidi ya mapato yako. Katika enzi hizi za kisasa, teknolojia imeonekana kurahisiha shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na usimamizi wa fedha. Mbinu zilizojadiliwa katika makala haya ni baadhi tu ya programu bora za fedha za kibinafsi katika Afrika zinazoweza kukusaidia kuweka akiba na kuwekeza fedha zako.

This post is also available in en_US.