Nafasi za Kukuza Startup Afrika

Uchumi wa Afrika kwa kiasi kikubwa huendeshwa na biashara ndogo na za wastani (SMEs). Hata hivyo, biashara chipukizi mara nyingi zinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kibiashara ikiwa ni pamoja na uhaba wa mtaji, ukosefu wa ujuzi wa kutosha wa kibiashara na maarifa kwa wajasiriamali, na mikakati duni ya mauzo. Matatizo haya husababisha biashara nyingi kutonawiri katika mwaka wa kwanza au ndani ya miaka 5 ya awali.

Ikiwa una watu wanaoweza kukuelekeza, unaweza kuepuka baadhi ya changamoto hizi. Vituo vya biashara vya kukuza biashara chipukizi hushughulikia hali kama hii barani Afrika. Makala haya yataonyesha baadhi ya vituo maarufu vinavyojihusisha na kukuza biashara zinazochipuka.

business incubators africa

Anza (Tanzania)

Anza ni kituo kinachonuia kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini kwa kuzisaidia startup Tanzania ambazo shughuli zake zinalenga kuboresha maisha ya wananchi moja kwa moja au kwa njia nyingineyo. Inayalenga mashirika katika sekta za afya, kilimo, elimu, maji, usafi wa mazingira na usafi, au sekta ya nishati safi.

Inatimiza majukumu yake ya kusaidia biashara chipukizi nchini Tanzania kwa kujengea uwezo, uanzishwaji wa jamii, kuwezesha upatikanaji wa ufadhili, na kukuza mazingira ya ujasiriamali. Kwa mujibu wa kujenga uwezeshaji, Anza huendesha mpango wa miezi 8 unaohusisha mafunzo ya biashara na kutoa ushauri. Pia, huwaunganisha wajasiriamali na wataalamu ambao huwasaidia kuendeleza biashara zao. Biashara chipukizi pia zinaweza kupata mkopo ambao riba yake ni ndogo kuliko ile ya benki za kawaida. Vitovu vya Anza ni maeneo yanayopokea watu kupitia sehemu zake za ushirikiano wa kikazi. Hii ni njia nyingine ambayo Anza huweza kuwasaidia wajasiriamali kujumuika na kupunguza gharama zinazohusiana na kuanzisha biashara.

 

Nailab (Kenya)

Nailab imekuwepo tangu mwaka 2010 kupitia ushirikiano kati ya Nailab Limited na 1% CLUB. Lengo lake muhimu ni kupunguza vikwazo vya kuanzisha biashara vinavyokumba startup Kenya katika sekta ya Teknolojia Habari na Mawasiliano. Sam Gichuru, ambaye ni mwanzilishi wa kituo hiki kinachokuza wajasiriamali alisema,

Tunataka kuweka mazingira ambayo wajasiriamali wa biashara chipukizi wanaweza kujiinua kimaarifa, kiteknolojia na kupata fursa za kiufadhili ili kutatua kero zinazohusishwa na masoko mapya.

Kutokana na mazingira yake yanayohusisha wawekezaji, watengenezaji wa programu, sekta binafsi, washirika wa kimaendeleo, na wajasiriamali, Nailab imesaidia zaidi ya biashara chipuzi 500 katika upatikanaji wa fursa za uwekezaji na pia kupokea maelekezo. Washirika wake ni pamoja na Jack Ma Foundation, Close the Gap, na UNFPA. Mojawapo ya miradi yake mashuhuri ni programu ya ujasiriamali ambayo huendeshwa kwa miezi 6. Katika kipindi hiki, walengwa hupata ujuzi muhimu kuhusu jinsi ya kuendeleza bidhaa na upatikanaji wa soko.

 

Wennovation Hub (Nigeria)

Hii biashara chapuzi kwa biashara chipukizi iliyoanzishwa mwaka 2010 na imeongeza athari kwa idadi kubwa ya wajasiriamali wanaochipuka nchini Nigeria. Inatoa huduma hizi katika miji ya Lagos, Ibadan, Abuja, na Kaduna. Kama njia ya kuboresha mazingira yake, kitovu cha Wennovation kinalenga biashara chipukizi zinazohudumu katika viwanda vyenye athari za kijamii kama vile miundombinu ya kijamii, nishati safi, huduma za kiafya, elimu, na kilimo. Shughuli zake zinafanywa kwa nyanja tatu: jisi ya kuanzisha biashara, kuimarisha mazingira ya biashara chipukizi, na fursa ya kupokea ushauri.

Uwezo wake wa kutoa msaada kwa biashara chipukizi katika eneo hilo umeimarishwa kwa njia ya ushirikiano na taasisi zenye mafanikio kama vile Bill na Melinda Gates Foundation, United Nations Foundation, Total, na Chuo Kikuu cha Lagos. Hadi sasa, biashara hii chapuzi imesaidia zaidi ya biashara chipukizi 300. Imewawezesha vijana zaidi ya vijana 6,000 kwa kuyafadhili mawazo yao ya kibiashara kwa takribani dola milioni 2.5.

Mbali na msaada wa kifedha, mafunzo na mipango ya maelekezo, na kuendelezwa kwa jamii, kitovu cha Wennovation kina nafasi ya kufanya kazi kwa kushirikiana ambayo inaruhusu wafanyabiashara kupunguza gharama zao za uendeshaji biashara huku wakikuza mahusiano na mitandao na wenzao wenye maono sawia ya kiujasiriamali.

 

Injini (Afrika Kusini)

Kama mojawapo wa biashara zinazosaidia kukuza biashara chipukizi katika Afrika, Injini inalenga sekta ya teknolojia ya elimu. Mipango yake kwa kawaida ni pamoja na maelekezo na ushauri, warsha, ufadhili, na msaada katika mchakato wa kujikuza. Sehemu hizi zina faida kwa wajasiriamali chipukizi ambao wanataka kuboresha sekta ya elimu barani Afrika kwa njia ya teknolojia.

Kawaida, Injini huchagua biashara chipukizi kutoka nchi mbalimbali za Afrika na kuzihusisha kwa miezi 5 ya ukuzaji wa kibiashara kabla ya kutoa ufadhili wa dola 50,000 kwa kila moja ili kuendeleza shughuli zao. Baadhi ya biashara chipukizi ambazo zimefaidi kutokana na kukuzwa na Injini ni pamoja na M-SHULE, Quillo, na Syafunda.

 

Technology Innovation and Entrepreneurship Center (Misri)

Kituo hiki cha kukuza biashara nyinginezo, ambacho kinajulikana kama TIEC, kinahusishwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Misri. Kilianzishwa kwa nia kuu ya kukuza uvumbuzi wa Teknolojia Habari na Mawasiliano na hatimaye kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa kitaifa. Ina programu kadhaa za ukuzaji kama vile Innovation Cluster, InnovEgypt, BEST, NTL, na TIEC-IA. Miradi yote hii ina lengo la kusaidia wajasiriamali chipukizi katika sekta ya Teknolojia Habari na Mawasiliano nchini humo.

Sawia na biashara nyinginezo za ukuzaji wa biashara chipukizi zilizotajwa barani Afrika, TIEC inatoa maelekezo na ushauri, mafunzo, na kujenga mahusiano yenye manufaa kwa walengwa wake. Aidha, biashara chipukizi zilizochaguliwa hupata ufadhili wa hadi dola 13,500 (paundi 120,000 za Misri) mwishoni mwa mwaka mmoja wa mpango wa ukuzaji ili kuongeza biashara zao. Pia, husaidia biashara chipukizi kupunguza gharama zao za kuhudumu kwa kutoa nafasi nafuu za ushirikiano za kikazi. TIEC imesaidia kukuza kampuni kama Bey2ollak na Ta2heal.

TIEC Egypt
TIEC nchini Misri.

Hitimisho Kuhusu Kukuza Startup

Shughuli za ujasiriamali zinaweza kuwa zenye changamoto kwa biashara chipukizi. Ili kuweza kustahimili na kufanikiwa katika sekta lengwa, unahitaji mwongozo na msaada wa mshirika mwenye uzoefu na mwenye mipangilio bora. Ukiyafahamu hayo, baadhi ya taasisi zilizojadiliwa katika makala haya ni baadhi ya zile zinaoweza kuikuza biashara chipukizi barani Afrika. Mashirika haya hutoa mafunzo muhimu ya ujasiriamali na maelekezo na ushauri, kukutambulisha kwa mazingira ya wawekezaji na washauri, na kutoa msaada wa kifedha unaohitajika.