Huduma za benki za Kiislamu au fedha kwa mujibu wa Uislamu ni jumla ya shughuli za benki au fedha ambazo zinaambatana na Sharia (sheria ya Kiislamu) na Hadith, maneno yaliyorekodiwa na matendo ya Mtume Muhammad.
Maelezo ya Haraka Kuhusu Benki za Kiislamu barani Afrika
- Ivory Coast inaongoza kwa utoaji wa dhamana kwa kuangazia misingi ya Kiislamu.
- Sudan ina sekta kubwa ya benki za Kiislamu.
- Kuna zaidi ya taasisi 80 za fedha za Kiislamu katika Afrika.
- Benki ya Kiislamu ya kwanza kwa vigezo vya sasa, Mit Ghamr Akiba Bank, ilianzishwa mwaka 1963 katika Mit Ghamr, Cairo, Misri.
Yaliyomo
Huduma za Benki za Kiislamu Barani Afrika
Kwa mujibu wa kampuni ya masuala ya fedha duniani, Moody, tangu mwaka wa 2014, dola bilioni 2.3 ya dhamana zinazofungamana na Sharia zimetolewa katika Afrika. Shirika hili pia lilitambulisha kwamba kumekuwa na ongezeko la idadi ya leseni kwa taasisi za Kiislamu za kifedha na kupanda hadi kwa zaidi ya 80 katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Baadhi ya taasisi za fedha katika nchi kama vile Afrika Kusini, Senegal na Nigeria hutoa “afueni ya Uislamu,” ambayo ina maana kwa huduma za kifedha zinazotolewa na benki za kawaida ila kwa kuzingatia kanuni za Kiislamu.
Kufuatia ongezeko la huduma za benki kupitia simu katika Afrika kama vile M-Pesa, Safaricom na benki ya Kiislamu ya Gulf African Bank walitangaza mipango ya uzinduzi wa M-Sharia, huduma inyozingatia Sharia kwa njia ya M-Pesa.
Kanuni za Benki ya Kiislamu
- Sharia inapiga marufuku riba au ushuru, faida zinazopatikana kupitia dhuluma au unyanyasaji katika biashara.
- Uwekezaji katika biashara ambazo zinatoa bidhaa au huduma zinazoangaziwa kuwa kinyume na mafundisho ya Kiislamu (kwa mfano nyama ya nguruwe, kamari au pombe) ni “haramu” (kwa kuwa ni dhambi, na marufuku).
- Benki ya Kiislamu inahusisha kugawana kwa faida na hasara. Benki hupata faida kwa njia ya kushirikishwa ambapo inamhitaji anayekopa pesa kuigawia benki faida atakayopata (pamoja na hasara) badala ya kulipa riba.
Manufaa ya Benki ya Kiislamu
- Kupunguza hatari ya hasara. Benki za Kiislamu hufanya uchambuzi wa kina wa hatari. Hivyo basi benki hizi hazifadhili kampuni zenye hatari. Hii inasababisha uthabiti wa kifedha na uwekezaji.
- Kupunguza bidhaa, huduma na mazoea hatari. Kanuni za benki za Kiislamu hupiga marufuku shughuli zozote haramu katika Uislamu kama vile kamari, pombe, ukahaba, uvumi, nk.
- Huduma zinazoambatana na Sharia. Benki za Kiislamu zinaruhusu Waislamu wacha Mungu kuwekeza na benki na taasisi hizo huku wakiheshimu maadili ya Kiislamu.
- Haki za kifedha. Benki za Kiislamu zimejengwa kwa msingi wa kugawana faida / hasara na hatari zinazoshirikishwa kati ya benki na wateja kwa njia sawia.
Hasara ya benki ya Kiislamu
- Gharama ya juu. Fedha za taasisi za Kiislamu huhusisha gharama kubwa. Kila shughuli ya kibiashara inahitaji mkataba zaidi ya moja, ambayo huweza kuwa na gharama kubwa sana.
- Mseto wa kinga na ukuaji. Ubashiri na kununua rasilmali kama kinga ya wakati wa kushuka kwa thamani ya fedha ni marufuku. Kwa hiyo, uwezekano wa chukua tahadhari ya hasara ni mdogo sana. Benki za Kiislamu hazijishughulishi na uwekezaji hatari. Wawekaji amana wanazuiwa kuwekeza katika mifumo ya uwekezaji yenye hatari zaidi, ambayo inaweza kuwa na faida kubwa.
- Kuhatarishwa kwa wawekaji amana. Kupitia mfumo wa kugawana faida na hasara, ina maana kuwa kuna ongezeko la hatari ya hasara kwa wale wanaoweka fedha kwenye benki. Wateja wa benki hawawezi kufuatilia kikamilifu sera na maamuzi ya benki kwani wao si sehemu ya usimamizi wa benki hiyo.
- Tatizo la mtanziko wa kisera. Mkazo mkuu unatiliwa kuhusu jinsi shughuli zinaendeshwa kwa mujibu wa Sharia kupitia bodi ya Kiislamu. Bodi ya Sharia huteuliwa na mabenki. Kunaweza kuwa na migogoro ya nia iwapo wajumbe wa bodi watajaribu kudumisha uhusiano na benki hiyo inayolipa ada zao. Isitoshe kudhibiti bodi hii ni ghali.
- Uhaba wa ugavi na utoshelezaji wa kifedha. Huduma za benki ya Kiislamu bado si chaguo la kimsingi la benki katika nchi nyingi.
Benki Zinazozungatia Sharia Katika Shughuli Zake Barani Afrika
Baadhi ya taasisi za kifedha na benki za kawaida ambazo mtu anaweza kutumia kwa ajili ya huduma za benki zenye misingi ya Kiislamu barani Afrika ni pamoja na:
Nchi | Benki |
---|---|
Algeria | Al Baraka Bank of Algeria |
Chad | Ecobank Chad |
Djibouti | Saba Islamic Bank |
Misri | National Bank of Egypt, Al Baraka Bank, Faisal Islamic Bank of Egypt |
Ethiopia | Hijra Bank, Somali Microfinance Institution (SMFI) |
Ghana | Ghana Islamic Microfinance |
Gambia | Arab Gambian Islamic Bank |
Guinea | Banque Islamique de Guinee, ICB Islamic Bank of Bangladesh |
Kenya | First Community Bank of Kenya, Dubai Islamic Bank, Gulf Bank, Sharjah Islamic Bank |
Morocco | Ma Banque islamique |
Nigeria | Sterling Bank Plc, FinBank, Jaiz Islamic Bank, Stanbic IBTC Bank, Keystone Bank |
Niger | Banque Islamique Du Niger, Niamey |
Senegal | Banque Islamique Du Senegal |
Somalia | Salaam Bank, Dahabshil Bank, Salaam Somali Bank |
Afrika Kusini | Absa Bank, Al Baraka Bank, Jordan Islamic Bank |
Sudani | Al Shamal Islamic Bank, Faisal Islamic Bank, Al Salam Bank, Al Tadamon Islamic Bank, Al Baraka Bank Sudan |
Tanzania | Amana Bank |
Tunisia | Banque Zitouna, Al Baraka Bank Tunisia |
Uganda | National Islamic Bank of Uganda |
Hitimisho
Sekta ya Benki za Kiislamu inatarajiwa kukua kwa zaidi ya dola trilioni 3 kufikia mwaka wa 2020. Benki ya Dunia inaamini kwamba benki hizi zenye misingi ya Kiislamu zina uwezo wa kupunguza umaskini.
Kwa mujibu wa Utafiti wa Pew, idadi ya Waislamu duniani ambao wanaishi barani Afrika itaongezeka kutoka asilimia 15.5 mwaka wa 2010 hadi asilimia 24.3 mwaka wa 2050.
This post is also available in en_US.