Kuna wakati unahitaji fedha kwa haraka ili kutatua jambo fulani. Unaweza kuomba msaada toka kwa marafiki au ndugu. Hata hivyo wanaweza wasiwe na uwezo wa kukusaidia. Kwa bahati nzuri, unaweza kuomba mkopo toka benki au kampuni ya mikopo mtandaoni. Ukiacha benki, hizi ni huduma nyingine unazoweza kutumia kwa mikopo binafsi au ya biashara nchini Kenya.

M-Shwari

M-Shwari ni huduma ya mkopo inayotolewa kupitia M-Pesa. Huduma hii ni ushirikiano kati ya Safaricom and Benki ya CBA iliyoanzishwa mwaka 2012. Kupata mkopo unatakiwa uwe na umri wa miaka 18, uwe tayari na akaunti ya M-Pesa kwa kipindi cha miezi 6.

Kiwango cha chini cha mkopo ni Ksh 100 na kiwango cha juu ni Ksh 20,000. Mkopo una kipindi cha siku 30 cha kulipa kwa riba ya 7.5%. Unaweza kulipa mkopo kupitia akaunti yako ya M-Pesa. Ikiwa siku 30 zimepita, malipo yatatolewa kwenye akaunti yako ya M-Shwari. Ukichelewa kulipa utatakiwa kulipa 7.5% ya kiwango kilichobaki kumaliza malipo.

KCB M-Pesa

Huduma hii ni ya ushirikiano kati ya Safaricom na Benki ya Kenya Commercial (KCB). Kiwango cha chini cha mkopo ni Ksh 50 na kiwango cha juu ni Ksh 1,000,000. Itakubidi uwe na KCB M-Pesa menu kwenye simu yako.

Kupata mkopo inakubidi uwe na miaka 18 au zaidi, uwe na akaunti ya M-Pesa kwa kipindi cha miezi 6, Historia yako ya akaunti ya M-Pesa ndio itakadiria kiwango cha mkopo utakachopewa.
img

MCo-op Cash

MCo-op cash ni huduma ya mkopo inayotolewa na Co-operative Bank of Kenya kwa kutumia "app". Kiwango cha chini cha mkopo ni Ksh 3,000 na kiwango cha juu ni Ksh 100,000.

Ili kupata mkopo toka MCo-op cash unahitajiwa kuwa mteja wa Cooperative Bank. Unahitaji pia kupata "app" toka the Google Play Store au the iOS Store. Mkopo wa binafsi mwezi mmoja una riba ya 1.166% wakati mkopo wa binafsi wa miezi mitatu una riba ya 3.498%. Mkopo wa biashara una riba ya 1.166% na mkopo wa bima wa miezi mitatu una riba ya 0.102%.

Eazzy Loan

Eazzy loan ni huduma ya Equity Bank. Unahitaji kuwa mteja wa Equity Bank. Unahitaji pia kuwa na kadi ya simu ya Equitel. Kuna aina mbili za mikopo toka Eazzy Loan: Mkopo wa Benki ya Equity na mkopo wa Eazzy plus. Toka Eazzy Plus unaweza kukopa hadi Ksh 3,000,000. Kiwango cha chini cha Mkopo wa Benki ya Equity ni Ksh 100 na kiwango cha juu ni Ksh 200,000.

Mkopo wa Benki ya Equity una kipindi cha miezi 12 cha kulipa wakati Eazzy Plus ni siku 30. Riba ya mikopo hii ni kati ya 2% na 10% ikijumisha malipo mengine ya benki, kodi, n.k.

Branch

Branch, ilianzishwa mwaka 2015 huko San Francisco ikiwa na ofisi Nairobi. Wakenya wengi wamekuwa wakitumia huduma hii kupata mikopo. Kupata mkopo toka Branch unahitaji kuwa mteja wa M-Pesa na uwe na akaunti ya Facebook yenye jina linalofanana na jina kwenye kitambulisho chako cha serikali.

Unatakiwa upate "" app"" ya Branch toka Google Play Store kisha uiunge na akaunti yako ya Facebook. Kisha weka maelezo yanayotakiwa kama vile namba ya simu. Kiwango cha chini cha mkopo ni Ksh 1000 na kiwango cha juu ni Ksh 50,000. Mkopo hutolewa kupitia M-Pesa na riba inategemea na kipindi cha kulipa mkopo wako.
img

Tala

Tala, iliyoanzishwa mwaka 2014, ilikuwa ikiitwa Mkopo Rahisi. Kupata mkopo toka Tala, unahitaji kuwa rekodi nzuri ya M-Pesa na pia uwe na simujanja. Kiwango cha mkopo kinategemea historia ya matumizi yako ya M-Pesa.

Unachotakiwa kufanya ni kupata ""app"" ya Tala toka Google Play Store kisha uiunge na akaunti yako ya Facebook kisha uweke maelezo yanayohitajika. Kiwango cha chini cha mkopo ni Ksh 500 na kiwango cha juu ni Ksh 50,000 ambapo riba ni 15%. Utalipa mkopo wako kwa muda wa wiki tatu kupitia M-Pesa.

Timiza

Timiza ni "app" ya Benki ya Barclays. Huduma hii inapatikana kwa yeyote mwenye simu. Sio lazima uwe mteja wa benki hii. Unaweza kutumia hii ""app"" kutunza fedha zako ili kuweza kupata kiwango cha juu cha mkopo hapo baadaye. Unaweza kutumia huduma hii hata kama huna simujanja kwa kupiga namba hii *848#.
img

mKey

Finserve Africa ilianzisha huduma ya mKey kama mapinduzi ya huduma za fedha zinazomjali mteja. Kwa kutumia "app" hii unaweza pia kutuma fedha kwenye huduma ya M-Pesa, Equitel Money na Airtel money. Unaweza pia kununua muda wa kuongoea toka kampuni za simu za Safaricom, Equitel, Airtel, Telkom na Faiba. Licha ya kukopa, unaweza kutumia huduma hii kulipa na kununua bidhaa na huduma.

Hitimisho

Kabla ya kuamua kutumia huduma zilizotajwa hapo juu, hakikisha kuwa unajua kiwango cha riba, muda wa kulipa na mashari ya kupata mkopo wa binafsi au wa biashara.