Maeneo ya kazi ya kushirikiana ni mahali ambapo watu hukutana na kazi kwa kujitegemea. Wanaweza kufanya kazi katika vikundi au binafsi. Maeneo ya kazi ya kushirikiana yana vifaa sawia na ofisi za jadi. Miongoni mwa vifaa kwamba pata ni pamoja kuunganishwa kwenye mtandao, mashine za kupiga chapa, na kumbi za mikutano. Hata hivyo, tofauti kati ya maeneo ya kazi ya kushirikiana na ofisi ya jadi ni kwamba, ili kutumia maeneo ya kazi ya kushirikiana huhitaji kutia sahihi makubaliano ya muda mrefu ya kukodisha. Katika maeneo ya kazi ya kushirikiana, unaweza kuchagua kukodisha kwa kila siku, kila wiki, au kila mwezi.
Kenya imechapuza ukuaji wa biashara chipukizi katika sekta mbalimbali. Pameshuhudiwa ukuaji wa maeneo ya kazi ya kushirikiana, hasa jijini Nairobi. Baadhi ya maeneo bora ya kazi ya kushirikiana nchini Kenya ni pamoja na yafuatayo.
iHub
iHub ni biashara chipukizi bunifu ya kiteknolojia yenye malengo ya kutoa maeneo ya kazi ya kushirikiana kwa wajasiriamali, wabunifu, watengenezaji wa programu, watafiti na waandishi wa programu. Inapatikana Senteu Plaza iliyopo kwenye makutano ya barabara ya Galana / Lenana mjini Nairobi. Wao hutoza ada ya dola 2 kwa saa huku malipo ya kila mwezi yanaweza kuwa dola 700. Kituo hiki pia kinatoa ukumbi kwa ajili ya matukio na ufadhili wa mitaji ya miradi. Wao hushirikiana na mashirika mengine ambayo hufadhili wawekezaji.
Nailab
Nailab ni kituo cha kibiashara ambacho kinalenga mawazo mapya. Kilianzishwa mwaka 2011 na kiko mjini Nairobi. Kituo hiki kinatoa huduma za kupevusha na kuchapuza miradi na mawazo ya biashara. Vikundi na watu binafsi wanaweza kupata maeneo ya kazi ya kushirikiana kwani wana nafasi kwa ajili ya matukio inayoweza kukidhi hadi watu 100. Wao hutoza ada kati ya dola 10 na dola 100 kwa mwezi. Mafanikio ya Nailab ni dhahiri, hasa kutokana na ufadhili wa dola milioni 1.6 waliopokea kutoka Wizara ya Habari na Mawasiliano.
Foundry Africa
Foundry Africa ni kituo kinachotoa nafasi ya kufanyia kazi kwa biashara ndogo chipukizi, wafanyakazi huria na wabunifu. Miongoni mwa vifaa walivyonavyo kwa wateja wao ni pamoja na ofisi zinazofungika na madawati ya kufanyia kazi. Kituo hiki husaidia kujenga uhusiano, kushirikiana na ubunifu. Kituo hiki kiko Nelleon Place, kwenye barabara ya Rhapta, Westlands. Ada zao mbalimbali ni kati ya dola 200 na dola 350 kwa mwezi.
Hub Mint
Mint Hub ni biashara chipukizi inayotoa nafasi za kazi kwa wajasiriamali na wavumbuzi. Kituo hiki kinatoa huduma za ofisi za kisasa na ofisi za jadi. Miongoni mwa huduma nyinginezo zinazotolewa na kituo hiki ni pamoja na wajumbe, usambazaji wa mizigo na msaidizi wa kidijitali. Kituo hiki kiko kwenye jengo la Western Heights, Karuna Road eneo la Westlands, Nairobi. Ada inayotozwa kwa ofisi za kisasa ni dola 100 kwa mwezi, huku ofisi za kibinafsi ni dola 250 kwa mwezi.
Ikigai
Ikigai ni ofisi ya kazi kwa kushirikiana iliyopo katika maeneo ya mazingira mazuri ndani ya Nairobi. Wana matawi yao Westlands, Lower Kabete na Lavington. Kituo hiki kinatoa huduma za maeneo ya kazi ya kushirikiana ya ndani na nje kwa biashara na watu binafsi. Wao hutoa huduma mbalimbali, zikiwemo nafasi za ofisi, nafasi binafsi, nafasi za pamoja za kifanyia kazi na kumbi za kuendeshea matukio. Wao hutoza ada ya dola 100 kila mwezi.
Hive
Hive ni kituo kinachotoa nafasi ya kufanyia kazi kwa wajasiriamali, wafanyakazi huria, biashara chipukizi, wabunifu na watafiti. Kituo kinatoa huduma hizi kwa mazingira tulivu na ya kisasa ya kazi, na ambapo unaweza kujumuika na watu kutoka nyanja mbalimbali za kitaaluma na maisha. Kituo hiki kiko katika eneo la Westlands, Nairobi na wao hutoza ada ya kati ya dola 30 na dola 75 kwa mwezi.
Workstyle Africa
Workstyle Africa ni eneo jipya la kazi ya kushirikiana nchini Kenya. Baadhi ya huduma wanazotoa ni pamoja na ukaguzi na huduma ya ushauri, miongoni mwa nynginezo. Wanatoa huduma hizi kama ofisi za kibinafsi, mikutano na matukio na maeneo ya kazi ya kushirikiana. Unapata nafasi ya kufanya kazi, kukutana na watu wapya na kukuza biashara yako. Eneo hili liko Westlands. Wao hutoza ada ya dola 25 kwa siku na dola 400 kwa mwezi.
Hitimisho
Kama una biashara na ungependa kuikuza, ni swala la busara kujaribu kutumia maeneo ya kazi ya kushirikiana. Faida ni kwamba unapata kujumuika na watu wapya na kushirikisha mawazo mapya. Pia kupata huduma ya mtandao na madawati ya kufanyia kazi bila kuwa na haja ya kununua.