Venture Capital for Africa (VC4A) inawaunganisha wajasiriamali wa biashara chipukizi wa Afrika na ujuzi, mipango ya usaidizi, washauri na wawekezaji wanaohitaji ili kufanikiwa. VC4A ilianzishwa kwenye mkutano wa kila mwaka wa African Venture Capital Association mjini Dakar, Senegal mwaka wa 2007.
Wajasiriamali waliopo kwenye VC4A wanaweza kuorodhesha biashara zao chipukizi, kupata washirika na hata kupata mtaji. Unapata fursa ya kuungana na kundi la wataalamu wa kimataifa ambao watakaokupa ushauri bila malipo. Unaweza pia kufuatilia maendeleo yako ya kutafuta ufadhili na kuungana na wawekezaji zaidi ya 5000. Hakuna ada ya siri!
Yaliyomo
Huduma Zinazotolewa na VC4A
- Wajasiriamali wanapata fursa ya kitengo cha mafunzo cha VC4A, kupokea mawaidha na maelekezo na uwezo wa kupata mitaji.
- Washirika wa miradi wanaweza kuwashirikisha wanachama katika mipango yao ya ujasiriamali, mashindano na kutoa huduma.
- Wawekezaji wanaweza kugundua kampuni kubwa, kutafiti kuhusu fursa na kuwafuatilia waanzilishi moja kwa moja.
- Washauri wanaweza kupitia na kukagua maombi ya ushauri na kuungana na waasisi wa biashara chipukizi na kuwasaidia katika safari yao.
Kuchagisha Mtaji
Kama una mradi wa biashara chipukizi uliosajiliwa kwenye VC4A, una uwezo wa kuibua mtaji. Kusajili wasifu wa mradi unahusisha hatua nne rahisi. Hakuna ada ya siri au gharama inayohusishwa.
- Tayarisha mapendekezo ya mradi wako
- Sajili nia yako
- Washirikishe wawekezaji watarajiwa ili kubuni mtaji
- Hitimisha kwa kuingia katika mkataba
Kitengo Cha Mafunzo Cha VC4A (VC4A Startup Academy.)
Kitengo hiki cha mafunzo kinaongoza kwa rasilimali za mtandaoni kwa ajili ya waanzilishi wa biashara chipukizi. Unaweza kupata ufahamu wa kisasa wa sekta husika, zana za biashara chipukizi na kujifunza kutokana na wataalamu 78 waliopo katika mazingira ya biashara chipukizi barani Afrika.
- Kozi ya kwanza inaitwa, “Anza biashara yako”, na inakuelekeza katika hatua za kuanzishwa biashara yako chipukizi.
- Kozi ya pili ni “Kuza biashara yako”, na inashughulikia kinachohitajika baada ya biashara yako chipukizi ipo tayari kutanuka.
- Kozi ya tatu ni “Fadhili biashara yako”, ambapo utajifunza jinsi ya kuvutia miradi ya ufadhili. Katika kila moja ya sura hizi utapata maelezo mengi mengineyo yatakayokuwezesha kuchagua maeneo maalum ya kuzamia.
- Kozi ya nne inaitwa “Masuala yako ya kisheria”, kwa lengo la waasisi ambao wanataka maelezo zaidi kuhusu athari ya kisheria ya kuanzisha biashara zao na kupata shughuli hizi kufadhiliwa.
- Mwisho wa kozi utapata cheti cha kipekee cha VC4A Startup Academy.
Kutoa Mawaidha na Maelekezo
Lengo la mpango huu wa kutoa mawaidha na maelekezo ni kusaidia wajasiriamali wenye mustakabali mwema kuzalisha kampuni kubwa. Tunafanya hivyo kwa kuwalinganisha washauri wenye tajiriba na wajasiriamali wenye mustakabali mwema.
Wajasiriamali wa Afrika wenye biashara chipukizi zilizosajiliwa kwenye VC4A wana fursa ya kuwasilisha ombi la kupokea msaada wa mawaidha na maelekezo. Baada ya kuyawasilisha maombi haya na kukaguliwa na kuchapishwa ni jukumu la mmoja wa washauri wa VC4A kujitokeza na kutoa msaada unaohitajika.
Miradi na Mipangilio
Kwenye wavuti wa VC4A, una uwezo wa kuchunguza mipango iliyopo na ijao na matukio kwa wajasiriamali watarajiwa, waanzilishi wa miradi na washirika mbalimbali.
Hitimisho
Biashara Chipukizi za Afrika na wajasiriamali Waafrika wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile mtaji, ujuzi, na uwezo wa kujitanua ili kujulikana. VC4A ina malengo ya kutoa mawaidha na maelekezo, kitengo cha mafunzo na ufadhili. Kutokana na haya pamesababishwa mafanikio mengi katika nchi kama vile Ghana, Afrika Kusini, Tanzania, Zambia, Kenya, Nigeria, Uganda, Misri, Somalia na Cameroon.
Viungo vya Kusoma Zaidi
- Habari za mafanikio, sekta na mataifa yanayoongoza
- VC4A kwenye LinkedIn
- VC4A kwenye Twitter
- VC4A kwenye Facebook
This post is also available in en_US.