Biashara Chipukizi Zenye Ufadhili Mkubwa Nchini Kenya

Tafsiri:
en_US

Kenya ni mojawapo ya nchi zinazoongoza katika uvumbuzi wa kiteknoljia katika Afrika. Hii ndiyo sababu mazingira yake ya kiteknolojia nchini humo ni maarufu kwa jina la Silicon Savannah. Mbali na wawekezaji binafsi, serikali ya Kenya, kama njia ya kupunguza umaskini na ukosefu wa ajira hasa miongoni mwa vijana, inatoa ufadhili wa biashara mpya kupitia Mfuko wa Maendeleo kwa Vijana (Youth Enterprise Development Fund.)

Zifuatazo ni baadhi ya biashara chipukizi zenye ufadhili mkubwa nchini Kenya.

Cellulant

Cellulant, iliyoanzishwa mwaka 2004, ni miongoni mwa biashara chipukizi bora za kifedha kupitia teknolojia nchini Kenya. Inatoa huduma za malipo za kidijitali kwa Waafrika ambayo huwaunganisha wanaotoa huduma za fedha na biashara. Jukwaa hili limewasaidia watu kutoka sekta mbalimbali ili kupata huduma za fedha. Tangu uzinduzi wake, imekuwa na uwezo wa kuchangisha zaidi ya dola milioni 55.

CarePay

CarePay, iliyozinduliwa mwaka 2015, ina makao yake makuu mjini Nairobi. Ni mfumo wa kutoa huduma ya afya kwa njia ya teknolojia kwa kushirikiana na kampuni nyingine ili kutoa huduma bora za afya. CarePay ni mpango wa kifedha wa afya ambao unaweza kutuma, kuhifadhi na kutumia kwa ajili ya huduma za afya kwa njia ya M-Tiba. Mfumo huu umeshirikiana na watoa huduma ya afya ili kutoa tiba bora na kwa gharama nafuu. Kampuni hii imeweza kukusanya zaidi ya dola milioni 45 kutoka kwa wawekezaji wake.

M-Kopa

M-Kopa, iliyozinduliwa mwaka 2012, ni biashara chipukizi ambayo imevutia wawekezaji wengi ili kutoa nishati safi ya jua. Lengo la biashara hii chipukizi ni kuwapa watu binafsi wenye kipato cha chini nishati safi. Baadhi ya wawekezaji wake ni pamoja na CDC Group na LGT Venture Philanthropy, zikiwa na jumla ya ufadhili wa dola milioni 38. Mradi huu huhusisha vifaaa vya nishati ya jua, balbu za LED, tochi za kushindiliwa na redio. Pia ina uwazi wa USB kwa ajili ya kushindika simu za mkono. Hii ni njia kubwa ya kuongeza upatikanaji wa nishati katika maeneo ambayo hakuna muunganisho wa nguvu za umeme.

Copia Global

Copia Global ni huduma tamba ya kibiashara (mobile commerce) ambayo inaweza kufikiwa na Waafrika wa kawaida, bila kujali kipato chao. Jukwaa hili linatoa huduma za ununuzi kwa kuwezesha bidhaa na huduma kukufikia hadi ulipo. Ina makao yake makuu mjini Nairobi na imeweza kuibua zaidi ya milioni 6 kutoka kwa wawekezaji wake.

Africa’s Talking

startups funding kenya

Africa’s Talking ni biashara chipukizi yaani iliyoanzishwa kwa ushirikiano wa Sam Gikandi na Eston Kimani mwaka wa 2010. Makao yake makuu yapo mjini Nairobi. Biashara hii chipukizi imeweza kuzindua zaidi ya dola milioni 8.6 kutoka kwa wawekezaji wake. Miongoni mwa wawekezaji yake ni IFC, Orange Digital Ventures, Better Ventures na Social Capital. Ukumbi huu unatoa mawasiliano kwa njia ya sauti na jumbe fupi (SMS) na huduma za malipo.

Twiga Foods

Twiga Foods, iliyozinduliwa mwaka 2014, ni jukwaa linalolenga kuziba pengo kati ya wakulima na uhakika wa chakula. Hii ni huduma ya simu ambayo inaruhusu utoaji wa mazao ya kilimo kwa kuwaunganisha wakulima na wanunuzi. Mradi hu ulibuni zaidi ya dola milioni 44.6. Baadhi ya wawekezaji wake muhimu ni pamoja Google Launchpad Accelerator na TLCom Capital. Kwa kufanya kazi pamoja na zaidi ya wakulima 17,000, mradi huu unatafuta njia za kupanua shughuli zake nje ya Kenya.

Branch

Branch ni huduma za fedha zinazohusishwa na Facebook na kuwaruhusu watumiaji kukopa fedha. Huduma hii ni inapatikana tu kupitia malipo ya huduma ya Safaricom ya M-Pesa. Mradi huu umeweza kuzindua zaidi ya dola milioni 4.9 kutoka kwa wawekezaji wake, ikiwa n pamoja na Centum Investments. Branch inahudumu nchini Kenya, Tanzania, Nigeria na California.

Sendy

startups in kenya

Sendy ilizinduliwa mwaka 2014 kuziba pengo kati ya wafanyabiashara na madereva wa aina mbalimbali za magari. Biashara zinaweza kuhamisha kwa urahisi bidhaa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Unapotumia Sendy, unapunguza gharama za usafiri na pia kuongeza ufanisi. Mradi huu umeweza kuzindua zaidi ya doal milioni 12 kutoka kwa wawekezaji wake, ikiwemo Safaricom, KenAfric, Unilever, Bidco na Chandaria Industries Limited.

Hitimisho

Kenya ni taifa linalotoa nafasi kwa biashara chipukizi na hivyo kupendelea ukuaji wa biashara. Kwa bahati nzuri, kama una wazo bora la biashara na huna fedha ya kuanza, unaweza kupata ufadhili kwa urahisi nchini Kenya. Pia, pamoja na serikali kuingilia kati ili kutoa fedha, ni rahisi kuzindua biashara chipukizi.