Ufadhili wa Biashara Chipuzi Nchini Kenya

Tafsiri:
en_US

Kenya iliorodheshwa katika nafasi ya tatu bora katika Ripoti ya Uwekezaji ya 2018. Ripoti hiyo pia ilionyesha kuwa kulikuwa na ongezeko la asilimia 300 la jumla ya ufadhili kwa miradi ya kibiashara barani Afrika kati ya mwaka 2017 na 2018. Kuna ufadhili wa kutosha kwa ajili ya biashara chipuzi kutoka kwa serikali na wadau wengine katika sekta za kibinafsi. Zifuatazo ni baadhi ya mifano ya ufadhili inayoelekezewa katika miradi ya biashara chipuzi nchini Kenya.

Hazina ya Maendeleo kwa Vijana (Youth Enterprise Development Fund)

Huu ni mpango wa serikali wenye lengo la kuwawezesha vijana kujishughulisha na biashara. Pia, ni mojawapo wa nguzo muhimu ya kufikia Ruwaza ya Kenya ya 2030. Hazina hii ya vijana ilianzishwa mwaka 2006 kuwasaidia vijana kuanzisha biashara. Serikali inatumia mfumo huu kujaribu kupambana na hali ya ukosefu wa ajira miongoni mwa wahitimu na vijana kwa ujumla. Vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 wanaweza kupata fedha kutoka kwa hazina hii. Hata hivyo, mpangilio wa hazina hii umekuwa unakabiliwa na changamoto, hasa kutokana na ufisadi nchini Kenya kwa maafisa wanaohusika.

Hazina ya Uwezo (Uwezo Fund)

Uwezo Fund ni mradi ulioanzishwa mwaka wa 2013 kama njia ya kuwawezesha vijana. Kimsingi, mradi huu hasa unalenga kuwafaidi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Hazina hii inalenga kusaidia kuleta usawa wa kijinsia na kujikwamua kutokana na umaskini. Vilevile, kupitia mradi huu, wawekezaji hupata ushauri na mtaji kwa shughuli zao za kutarazaki. Unaweza kupata mkopo kuanzia shilingi 50,000 hadi 500,000 kwa wakati mmoja kutoka kwa hazina hii.

Hazina ya Mandeleo ya Wanawake (Women Enterprise Fund)

Wizara ya Jinsia ilianzisha Women Enterprise Fund kwa kuwalenga wanawake. Hazina hii hutoa mtaji wa kuanzishia biashara kwa wawekezaji wanawake. Pia, mradi huu unanuia kuwasaidi kutafuta soko kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa na wanawake. Kadhalika, mradi huu unakusudia kuwafanya wanawake waweze kujikimu kifedha na kuondoa utegemezi.

Mikopo ya Bitcoin kwa Biashara Ndogo

BitBond ni wakopeshaji wa kimataifa ambao wanatetea matumizi ya sarafu za kidijitali kama vile Bitcoin. Ukiwa na BitBond, unaweza kupata mkopo unaohusishwa na biashara ya Bitcoin. Inawezekana kupokea mikopo yenye kiwango sawa cha Bitcoin. Wafanyabiashara wa mtandaoni wanapendelea mikopo ya BitBond. Ni muhimu kufahamu kwamba hata biashara ndogo zinaweza kulipia mkopo wa BitBond.

Mwekezaji Malaika (Angel Investors)

Mwekezaji malaika ni mtu ambaye hutoa mikopo kwa ajili ya kuanzisha biashara. Fedha zinazotolewa zinaweza kuwa mtaji kwa biashara chipuzi, au zinaweza kuwa msaada unaoendelea kwa kipindi maalum. Wawekezaji malaika huangalia mpango wa biashara yako ili kujua iwapo biashara unayotaka kuanzisha ni ya kuaminika. Unahitaji kuwashawishi kwamba wazo lako la kibiashara litakuwa na mafanikio. Wana faida kuzidi benki na wakopeshaji binafsi kwa kuwa ni wavumilivu na wanaweza kutoa mtaji zaidi inapohitajika. Baadhi ya wawekezaji malaika unaoweza kuwaangazia ni Savannah Fund.

Mashindano ya Mipango wa Biashara

Huu huwa ni mradi wa mara kwa mara unaoendeshwa na mashirika na serikali. Mashindano huishia kwa kutoa fedha za haraka na huduma kama vile za uhasibu na kisheria kwa gharama iliyopunguzwa kwa washindi. Faida ya ushindani wa biashara ni kwamba unaweza kupata nafasi ya kupokea mawazo zaidi, kupokea ushauri na pia kujenga mahusiano. Baadhi ya mashirika ambayo hutoa mashindano hayo ni pamoja na Micro Small and Medium Enterprises (MSME) kupitia mradi wa Jitihada na Wizara ya Biashara, Viwanda na Ushirika.

Uwekezaji kwa Njia ya Mtaji (Venture Capital)

Uwekezaji wa mtaji huisadia kampuni kupata mkopo, ushauri na kujenga mahusiano ya biashara. Jambo la muhimu ni kuthibitisha kuwa wazo lako la biashara yako ni la kipekee na litachangia kutimiza malengo yako. Wawekezaji hawa huhitaji umiliki wa kiwango fulani wa biashara. Ni muhimu kuwa makini ili usitoe udhibiti mkubwa na umiliki wa biashara kwa ajili ya mtaji kwa njia hii. Mojawapo wa chaguo za mfumo huu wa uwekezaji ni Venture Capital for Africa.

Kukopa Kutoka Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (Saccos)

Bila shaka, Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo (SACCO) ni vyanzo vikuu vya mtaji wa kufadhili biashara chipuzi. Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo huwa na viwango vya chini vya riba kwa mikopo ikilinganishwa na benki. Ili uweze kupata mkopo wa biashara kutoka Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo, unahitaji wadhamini ili, iwapo hutaweza kulipa mkopo, watalipa kwa niaba yako. Kadhalika, unaweza kuwa kutoa dhamana ya kiasi cha mkopo iwapo huna wadhamini. Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo ni bora ikilinganishwa na benki kwa kuwa vinakupa muda zaidi wa malipo na pia kiwango chao cha riba ni cha chini. Hata hivyo, kabla ya kuomba mkopo kutoka Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo, unahitajika kuwa umefungua akaunti na wao na pia umewekeza nao kwa kipindi fulani.

Hitimisho

Kupata chanzo sahihi cha ufadhili wa biashara yako chipukizi ni muhimu kwani hapana mwekezaji atakayeanzisha biashara ambayo hatimaye itanadiwa. Tunakushauri kwamba uufanye utafiti wa kina kuhusu kampuni unatayoka kupata mkopo kabla kujishirikisha nayo. Isitoshe, hakikisha kuwa inakuwa na matumizi sahihi na uliyonuia ya fedha pindi unapozipokea.