Jinsi Ya Kufungua Akaunti Ya Benki Nchini Kenya Kwa Mtu Aliye Ughaibuni

Tafsiri:

Watu wengi kutoka Kenya wanafanya kazi nje ya nchi na mara nyingi wangependa kuhifadhi fedha zao kwenye mabenki nchini Kenya, kuwekeza au kutuma pesa nyumbani. Kwa sababu hizi, wanaweza kufungua akaunti ya benki ya mtu aliye ughaibuni ili kuitumia kwa matumizi ya kibenki akiwa nje au nchini Kenya.

fifi-diaspora-1.jpg
Co-operative Bank of Kenya Diaspora Banking.
  • Ono la Kenya 2030 linautambua mchango wa wakaao ughaibuni kama kiwezesho kikubwa cha ukuaji wa uchumi wetu na hatua muhimu ya mafanikio kamili ya ushindani kidunia na ustawi wa Kenya kufikia mwaka 2030.
  • Idadi ya Wakenya walio nje, inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni tatu na inaendelea kuongezeka.

Akaunti Ya Benki Ya Mtu Aishiye Ughaibuni Inafanyaje Kazi?

Akaunti benki ya mtu aishiye ughaibuni inatofautiana kutoka benki moja na nyingine. Hata hivyo, mabenki mengi yana mameneja uhusiano ambao huwaongoza watu jinsi ya kufungua akaunti za benki za waishio ughaibuni na kuwekeza nchini Kenya. Pia wanawasaidia kutumia vyema fedha zao. Kando ya hayo, baadhi ya mabenki hutoa mikopo ya mali zisizohamishika kwa wateja wa akaunti za benki za washio ughaibuni.

Yahitajikayo Ili Kufungua Akaunti Ya Aishiye Ughaibuni

Ufunguaji wa akaunti ya benki ya mtu aishiye ughaibuni, unatofautiana kati ya benki moja na nyingine. Kwa ujumla, yafuatayo ni baadhi ya yahitajikayo:

  • Kadi ya utambulisho.
  • Picha ndogo ya pasipoti.
  • Bili ya matumizi.
  • Ushahidi wa ukaazi.
  • Uthibitisho wa nyaraka zako zote kupitia mwanasheria au afisa ubalozi wa Kenya.
  • Unatakiwa pia kujaza fomu mtandao ya habari zako binafsi kama vile majina yako kamili, nambari ya simu ya mkononi na anuani ya barua pepe.

Vipi Ni Vipengele Vya Akaunti Ya Mtu Aishiye Ughaibuni?

Vipengele vya akaunti za waishio ughaibuni, pia vinatofautiana kutoka benki moja na nyingine. Hata hivyo, vifuatavyo ndivyo vipengele vikuu:

  • Baadhi hazina tozo za kila mwezi.
  • Akaunti zinapatikana katika aina tofauti tofauti za fedha.
  • Nyingi hutoa nafasi ya kuwasiliana na mameneja uhusiano.
  • Kadi ya Debit hutolewa.
  • Baadhi hutoa mikopo baada ya mtumiaji kuitumia akaunti kwa miezi sita.
  • Waweza kufanya miamala kupitia programu au mtandao wa kibenki.
  • Wengi wao hujipata riba katika fedha za ndani na za kigeni.

Akaunti nyingi za benki za waishio ughaibuni hutoa huduma zote za kibenki na pia huruhusu mtu kutuma pesa kwa haraka sana. Waweza kudhibiti na kuifadhi fedha zako ukiwa nchini Kenya au nje. Fedha zako zaweza kuwa katika aina mbalimbali za fedha, hali inayorahisisha uchukuaji pesa katika nchi yoyote uliyopo. Hii ni nafuu kwa vile huhitaji kulipia gharama za ubadilishaji kila mara uhitajipo kutoa fedha. Pia ipo huduma kwa wateja siku zote za wiki na benki kwa njia ya intaneti.

Iwapo uko nje ya nchi, waweza kutuma nyaraka kwa kupitia huduma ya watuma vifurushi na barua kimataifa au kwa barua pepe. Vivyo hivyo, baadhi ya mabenki yana huduma ya usajili mtandaoni, hivyo kufikiwa zaidi. Nyingine, hutuma wakala mahali ulipo kuchukua saini na nyaraka zako.

fifi-sw-diaspora-2.jpg

Mikopo Kwa Wenye Akaunti Za Waishio Ughaibuni

Mabenki nchini Kenya hutoa huduma za mikopo kwa wateja wao waishio nje ya nchi. Baadhi ya mikopo itolewayo inajumuisha:

1. Mikopo ya mali zisizohamishika pamoja na ujenzi. Mkopo huu waweza kutumika kujenga makazi au jengo la biashara.
2. Mkopo wa malipo na mali. Mkopo huu waweza kutumika kununua mali kwa ajili ya biashara zako kama vile samani au mashine.
3. Mikopo binafsi. Yaweza kuwa kipo salama au isiyo salama. Inatolewa kwa watu binafsi kwa kutegemeana na mikataba ya ajira zao.
4. Mikopo ya biashara. Waweza kuutumia mkopo huu kwa mahitaji mbalimbali ya kibiashara. Inawezekana kutumika kwenye mchakato wa kupatia hati dhamana kwa biashara yako.
5. Mkopo ya ununuzi wa eneo. Waweza kuutumia mkopo huu kununulia ardhi au eneo.

Baadhi ya mabenki amabyo yanatoa mikopo kwa wenye akaunti za waishio ughaibuni nchini Kenya ni pamoja na:

Equity Bank
Cooperative Bank
CBA
Barclays Bank
Gulf African Bank
I&M Bank
Chase Bank
Family Bank
Credit Bank
NIC Bank
Kenya Commercial Bank
Diamond Trust Bank

Zingatia kusoma yahitajikayo kwa kila benki, huduma wazitoazo kupitia akaunti za waishio ughaibuni na vipengele vya akaunti zao.

This post is also available in en_US.