Jua Kali – Sekta Isiyo Rasmi Inayonawiri Nchini Kenya

Tafsiri:
en_US

Jua kali ilibuniwa wakati wa ukoloni kwakuwa kazi ya jua kali ilifanywa hasa na wale waliokuwa wameacha shule. Wafanyabiashara wengi wa kazi za ufundi hufanya kazi kando ya barabara na hutumia sehemu kubwa ya siku kufanya kazi chini ya jua kali. Walakini, kazi za ufundi ni biashara inayoongezeka nchini Kenya.

Jua kali ni sekta isiyo rasmi ambayo inaajiri Wakenya zaidi ya milioni 14 wanaowakilisha asilimia 83 ya kazi nzima nchini Kenya kulingana na ripoti ya Uchunguzi wa Uchumi wa Kenya wa 2014. Sekta hiyo inajumuisha ujuzi na utaalam mbali mbali wakati wa kukuza kazi ya kujiajiri.

Bidhaa za Jua Kali Nchini Kenya

Kuna bidhaa na huduma mbalimbali kutoka kwa sekta ya jua kali. Bidhaa hizi hujumuisha viwanda vikubwa vya kisasa hadi kwa vifaa vidogo vya ubunifu vya zana za mikono. Baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na mafundi wa jua kali ni pamoja na fanicha ya hali ya juu, vitanda vya springi na masanduku ya chuma. Huduma zinazohusiana na sekta ya jua kali ni pamoja na mafundi wa viatu, ukarabati wa gari na baiskeli, ukarabati wa nguo zilizoraruka na kuchomelea na kuuza kwa nguo za mitumba.

Idadi kubwa ya mafundi wa jua kali hufanya kazi ya kuchomelea. Wanaunda milango ya hali ya juu na maridadi, madirisha na paa. Serikali ya Kenya kupitia mpango yake wa Ajenda Nne ambao unajikita katika kutoa nyumba za bei nafuu ni jukumu muhimu katika kukuza biashara ya kuchomelea. Mafundi wa jua kali wanapata wanapata oda za kutengeneza milango, mageti na paa. Licha ya hayo, mashule mengi yanahitaji wanafunzi kutumia sanduku za chuma na ndoo kwani zinadumu kwa muda mrefu, hii inahimiza ukuaji wa sekta ya jua kali.

Washona viatu pia wanachangia jukumu muhimu katika uchumi wa Kenya kupitia utengenezaji wa viatu vya hali ya juu. Kazi yao inahitaji ubunifu mwingi na utaalamu kwani wao huweza kushonesha viatu kutoka kwa matairi ya gari. Licha ya hayo wao pia wanashonesha mikanda ya hali ya juu kutoka kwa ngozi ya wanyama na inadumu kwa muda mrefu.

Washonaji wa nguo wanafaidika pia kutokana na ukuaji wa sekta ya jua kali. Hii ni kwa sababu wao hushonesha nguo za hali ya juu ambazo hutumika nchini na zingine husafirishwa ugenini. Ni kawaida kuona watalii wakinunua shanga na nguo za kimasai. Watalii wananunua bidhaa za mavazi kama zawadi na kama mapambo. Nguo za jua kali zinaonyesha ubunifu wa hali ya juu ambao unahimiza utangamano na uhusiano wa tamaduni tofauti za jamii za Kenya.

Umekanika pia hujumuisha sekta ya jua kali. Bidhaa zao ni bora na wa hali ya juu na zinapendelewa ikilinganishwa na bidhaa zilizoingizwa nchini kutoka ugenini. Mekanika wana majukumu muhimu katika ukarabati wa baiskeli, magari na pikipiki. mitambo yao ni ya ubora wa juu ukilinganisha na zinazotoka ng’ambo. Wanatumia mashine zilizotengenezwa kwa mikono kutengeneza sehemu za mitambo na pia katika ukarabati wa sehemu zilizovunjika.

Maendeleo ya Jua Kali Nchini Kenya

Sekta ya jua kali imenawiri kwa nyakati mgumu tangu enzi ya ukoloni. Serikali ya Kenya imehimiza ukuaji wa sekta ya jua kali kupitia mpango ya kubuni ajira kwa vijana wa Kenya. Wale walio tayari kuwekeza katika jua kali wanapaswa kuwa na mtaji wa kutosha, wajifunze kuzoea mazingira ya uhasama wa kibiashara, wajifunze masomo na kuwa imara haraka. Hata hivyo, katika siku za karibuni, kutokana na kutambua na kuthamini sekta hii ya jua kali watu wengi wanajitoza katika sekta.

Serikali ya Kenya imeunda masoko ya mafundi wa jua kali kama Soko la Masai, Soko la Gikomba na Soko la Kisumu ni miongoni mwa masoko bora ya mafundi wa jua kali. Serikali pia inatoa mikopo kwa vijana walio katika vikundi iliwawekeze kwenye biashara ndogo ndogo.

Kuna mipango mingine kama wafanyikazi wa Jua Kali Workforce, ambayo inawezesha fursa za kuunganisha wateja na wafanyakazi wenye ujuzi kutoka sekta isiyo rasmi na bidhaa za jua kali.

Changamoto Zinazokabili Sekta ya Jua Kali

Sekta ya jua kali ilipigwa na nyakati ngumu za uchumi na kutakiwa kuwa na mtaji mkubwa wa kuanzisha biashara. Hata hivyo, pia imestahili upinzania kwani ilihusishwa na watu walioacha shule. Kati ya changamoto kubwa zinazokabili sekta hii ni mazingira magumu ya kufanya kazi. Mafundi wengi wa jua kali wanakosa maduka madhubuti na kuwalazimisha kufanya kazi katika maeneo ya wazi chini ya jua kali.

Sekta hii pia inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa biashara zilizoanzishwa hapo awali. Wawekezaji katika jua kali wanashindwa kutoa matangazo ya kutosha kwa ukosefu wa fedha. Pia wanakabiliwa na unyanyasaji kutoka mamlaka hasa kutoka miji na halmashauri za manispaa. Serikali za kaunti pia zinatoza ada kubwa za leseni za kufanya kazi ambazo zinachangia kudorora kwa ukuaji wa talanta za Wakenya.

Uuzaji katika sekta ya jua kali unaathiriwa sana na mikasa ya moto mara kwa mara. Soko la Gikomba limekuwa likiathirika zaidi kutokana na kuzuka kwa moto. Wamiliki wa biashara wanapoteza mamilioni ya pesa na mali. Inachukua juhudi kubwa kujenga tena kile wamepoteza kutokana na mikasa ya moto.

Kuhitimisha, sekta ya jua kali hutoa fursa nzuri ambayo haihitaji kiwango cha juu cha elimu. Kuanza, unachohitaji ni talanta, ubunifu na motisha. Hili ni wazo nzuri kuwekeza zaidi kwa vijana wa Kenya wasio na ajira.