Kampuni 4 Chipukizi Zinazotoa Huduma za Kifedha Afrika

Tafsiri:
en_US

Ndani ya kipindi cha muongo mmoja uliopita, Afrika imepiga hatua kutoka eneo lisilo na maendeleo na kuwa bara la kutazamwa kwenye mambo ya uchumi na jamii. Mojawapo ya sekta zinazovutia barani Afrika ni sekta ya teknolojia za kifedha.

Kufuatana na World Bank Global Findex, kiasi cha asilimia 60 ya wakazi wa nchi za ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika hawana akaunti za benki. Kwahiyo miradi midogo midogo ya teknolojia ya fedha imekuwa na faida katika kuendeleza uchangamano wa kifedha barani Afrika.

Teknolojia za Kifedha Afrika

  • Tangu mwaka 2017, programu za tarakilishi zinazosaidia au kuwezesha mabenki na huduma nyingine za kifedha zimekua kwa asilimia 60.
  • Uuwekaji fedha kwenye mradi ya teknolojia hizi tangu mwaka 2015, umefikia dola za Kimarekani milioni 320.
  • Eneo la ukanda kusini mwa jangwa la Sahara ndilo linaloongoza duniani kwa matumizi ya pesa mtandaoni. Kwa mfano, sekta ya pesa mtandaoni, ni mara 13 zaidi ya benki za kawaida.

Kwa takwimu hizi kichwani, makala hii itabainisha kampuni 5 chipukizi bora Afrika za teknolojia za Kifedha za kuangaliwa sana mwaka 2021.

1. Bitpesa

fintech africa

BitPesa ambayo hivi karibuni ilibadilisha muundo wake na kuitwa AZA Group, ni teknolojia ya kufanyia malipo na sarafu za kidijitali. Inawawezesha wateja kununua au kuuza Bitcoin kwa kutumia sarafu za Kiafrika. Teknolojia yake pia inashirikisha mahamisho ya kibenki pamoja na malipo kupitia simu. Madhumuni yake ni kuwawezesha wateja wake kufanya biashara ya kigeni kwa urahisi.

BitPesa inafanya kazi nchini Ghana, Nigeria, Kenya, Uganda, Senegal, Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo na Tanzania. Mwaka 2018, iliinunua kampuni ya TranferZero, kampuni ya utumaji pesa kidijitali kutoka Hispania. Fedha za kampuni hii ni kutoka kwa wawekezaji 12 ambao ni pamoja na Sompo Holdings na Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini. Imejipatia fedha zenye thamani ya dola milioni 30 katika raundi sita za kuchangisha fedha. Raundi yake ya mwisho ilikuwa ni ya kulipia deni ambayo ilifanikiwa kuchangisha dola milioni 15.

Takwimu hizi ni kielelezo cha umuhimu wa Bitpesa. Mazingira ya fedha mtandao barani Afrika ni makubwa na yanatarajiwa kukua zaidi kadri watu wengi wanavyotegemea simu zao kuhifadhi fedha na kufanya miamala ya kibiashara au kulipia bili.

Huku BitPesa ikiwa na fedha za kutosha na muundo mpana baada ya kuinunua kampuni ya TansZero, inatarajiwa kunufaika kutoka kwenye fursa hii ya soko. Kwa kuongezea, kampuni hii ni mojawapo ya kampuni imara ya kubadilishia pesa za kidijitali. Huku pesa za kidijitali zikizidi kuchukua umaarufu barani Afrika, mradi huu mdogo wa kijasiriamali, unatarajiwa kufikia kiwango kikubwa cha ukuaji. Kwa hakika, ni mradi kuangaliwa sana mwaka 2021.

2. Cellulant

fintech africa cellulant

Cellulant ni kampuni chipukizi yenye huduma zote za malipo ambayo ilianzia Kenya. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004, imetanuka hadi kwenye nchi 33 za Afrika ambazo ni pamoja na Uganda, Zambia, Nigeria, Ghana na Botswana. Kupitia muundo wake makini, imefanikiwa kuunganisha idadi kubwa ya wateja, wafanya biashara, wafanyakazi wa mitandao ya simu na mabenki.

Sababu kuu inayoongoza shughuli za Cellulant na ufafanuzi wa ukuaji wake ni urahisi, kanuni inayoaminika katika ulimwengu wa kisasa. Kama ilivyo kwenye nchi zilizoendelea ulimwenguni kote, asilimia kubwa ya watu kwenye mataifa ya Afrika wanavutiwa na teknolojia ziwawezeshazo kulipia bili na kuhamisha fedha kutoka majumbani mwao au maofisini bila kuwa na haja ya kwenda benki.

Kampuni hii chipukizi inahudumia asilimia 12 ya malipo yote ya kidijitali barani Afrika. Wateja wanaweza kununua, kulipia huduma, kufuatilia matumizi yao, kuifadhi fedha na kujipatia mikopo kirahisi kwa njia hii. Ufanisi na uaminifu wake unapimwa kutokana na ukweli kwamba ina wateja wengi kama vile Multichoice na JamboJet Airlines. Imeshirikiana pia na serikali ya Nigeria kupitia skimu ya kusaidia uendelezaji wa ukuaji.

Kampuni ina fedha kiasi cha dola milioni 54.5. Wawekezaji wake ni pamoja na The Rise Fund, Velocity Capital Private Equity na Satya Capital. Fedha hizi zinatarajiwa kuipandisha kwenye vilele vya juu zaidi. Kwa kuzingatia nafasi yake ya sasa na umuhimu wake, Cellulant ni mojawapo ya kampuni chipukizi za kutazama mwaka 2021.

3. Jumo

fintech africa jumo

Jumo ni kampuni chipukizi inyosaidia au kuwezesha mabenki na huduma nyingine za kifedha iliyoko nchini Afrika Kusini. Shughuli zake zinaunganisha watoa huduma za simu za mkono, biashara ndogo na za kati na wananchi wengine wote. Kupitia utumizi wake mpana wa sayansi ya data, kampuni ina bidhaa nzuri za akiba na mikopo. Inafanya kazi pia na watoa huduma za bima kutoa aina mbalimbali za bima kwa watu binafsi na wafanyabiashara.

Kampuni hii imepanua wigo kwenye nchi nyingine za Afrika kama Ghana, Rwanda, Zambia, Tanzania, Kenya na Uganda. Licha ya hayo, imekuwa ndiyo kampuni chipukizi ya kwanza kutoka Afrika Kusini kuchaguliwa na Google Inc kwa programu iitwayo ‘the Launchpad Accelerator.’ Huu ni uthibitisho kuwa umuhimu wake sio tu unaonekana kwenye macho ya Afrika bali pia kutoka kwenye upeo mpana wa dunia ya tecknolojia.

Tangu uanzishwaji wake mwaka 2014, imetoa huduma zake kwa zaidi ya wateja milioni 7.5. Ukuaji wake pia unaonekana kupitia kutanuka kwake kwa nguvu kazi yake. Kwa sasa, imeajiri watumishi karibia mia tatu kutoka saba wakati ilipoanza. Raundi zake nane za michango ya fedha zimevuna dola milioni 91.7 za Kimarekani. Ina jumla ya wawekezaji 10 wakiwemo Goldman Sachs, Odey Asset Management na Finnfund. Kwa sapoti hii ya kifedha na nafasi yake nzuri kwenye sekts, Jumo inatarajiwa kukua kwa uhakika katika miaka ijayo.

4. Yoco

fintech africa yoco

Yoco ni uzao mwingine wa Afrika Kusini ambao unastahili kuangaliwa sana mwaka 2020. Sehemu ya wafanyabiashara wadogo na wa kati wa Afrika Kusini ambao wanapokea malipo ya kadi ni asilimia 10 tu. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2015, kampuni imejikita kwenye kubadili hali.

Kwa kuanzisha programu inayowawezesha watumiaji kufanya malipo kwa kupitia simu zao za mkononi, Yoco imetoa huduma kwa zaidi ya wafanyabiashara wadogo na wa kati zaidi ya 50,000. Kati ya wateja hawa, asilimia 75 hawajawahi kufanya malipo kwa kadi. Takwimu hizi zinathibitisha kwamba kampuni ina uwezo wa kutanua wigo wa wateja kwenye sekta hii na hata nchi nyingine za Afrika.

Ukuaji wake makini unachagiwa zaidi na sapoti ya kifedha inayopokea kutoka kwa wawekezaji wake. Ina jumla ya wawekezaji 15 ambao ni pamoja na Futuregrowth Asset Management, Partech na Quona Capital. Imekuwa na raundi tano za uchangishaji wa fedha, raundi zilizozalisha dola milioni 23 za Kimarekani. Kwa msingi huu, mbingu tu ndicho kikomo kwa kampuni hii chipukizi ya teknolojia za fedha.

Hitimisho Kuhusu Kampuni za Huduma za Kifedha

Kwa miaka kadhaa, Afrika imetajwa sana kwa sababu za mambo mabaya kama vile vita, njaa, n.k. Hata hivyo, muongo mmoja uliopita, maendeleo katika sekta mbalimbali kumepelekea ulimwengu kulitatazama bara hili kwa mwanga tofauti. Kuanzishwa kwa kampuni mbalimbali za teknolojia yz kifedha, ni miongoni mwa maendeleo hayo. Mikakati na nafasi ya makampuni yaliyotajwa kwenye makala hii, yanafafanua uchangamano wao kwenye orodha ya makampuni chipukizi ya teknolojiz za kifedha ya kutazamwa mwaka 2021.