Nini cha Kutarajia Baada ya Uchapishaji wa Fedha Mpya za Kenya

Tafsiri:
en_US

Kifungu cha 231(4) cha katiba ya Kenya kinatoa maelezo kuhusu kuunda, kuchapa na kusambaza fedha mpya. Tarehe ya mwisho ya utekelezaji wa kifungu hiki ilipita miaka mitatu iliyopita.

Noti mpya ya 1,000 ikiwa na picha ya rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta.

Baada ya kutolewa kwa fedha za kwanza, Benki Kuu ya Kenya ilifikishwa Mahakama Kuu kwa kukabidhi mkataba wa kuchapa fedha nyingine kwa kampuni hiyo hiyo. Kwa bahati nzuri, Mahakama Kuu iliamuru kuwa Benki Kuu ya Kenya haijakiuka kanuni yoyote katika utoaji wa mkataba huo. Kwa hivyo, Benki Kuu Kenya itaendelea kuchapisha na kutoa fedha mpya. Bila kujali ni nini kimetokea, Wakenya wanapaswa kutarajia yafuatayo kutokana na uchapaji na utoaji wa fedha mpya.

Mambo ya Kuvutia

  • Mtu yeyote aliye na zaidi ya shilingi milioni moja na hana akaunti ya benki atalazimika kutembelea Benki Kuu ya Kenya ikiwa anataka kuzibadilisha na fedha mpya.
  • Maelezo kwenye fedha hizi yameandikwa kwa rangi mbalimbali ili kuonyesha utajiri wa Kenya na watu wake.
  • Ujumbe wa noti ya Sh50 unahusu nishati ya kijani, noti ya Sh100 inahimiza kilimo, noti ya Sh200 inakuza huduma za kijamii, noti ya Sh500 inakuza utalii na noti ya Sh1, 000 ni ishara ya utawala.
  • Noti ya Sh1,000 ndio noti ya thamani kubwa zaidi nchini Kenya.

Udhibiti wa Uhalifu

Ni vigumu kukubali kuwa watu wengi nchini Kenya wananufaika na uhalifu wa kifedha. Fedha mpya itahakikisha uchumi unaostawi kwa kudhibiti uhalifu kama ukwepaji wa kodi, rushwa, utakatishaji fedha na fedha bandia. Kukomesha matumizi ya fedha moja kwa faida ya nyingine inamaanisha kuwa wale wanaomiliki fedha za zamani ambazo zilipatikana kwa uhalifu hawawezi kuzitumia.

Watu hawatakuwa katika nafasi ya kuziingiza fedha hizo kwenye mfumo kwa malipo. Hii ni harakati nzuri ukizingatia upotezaji mkubwa wa fedha za umma kila siku. Pamoja na matarajio ya juu kutoka kwa Wakenya kuona juhudi za serikali katika kupambana na uhalifu, sera hii peke yake ni zana bora.

Utoaji wa fedha mpya nchini Kenya ni tofauti na India, ambapo serikali iliuza sera ya kuondoa uhalali wa fedha zake ili kudhibiti uhalifu lakini iliishia kuvuruga sera ya fedha. Wahalifu waliolengwa na sera hii hawakupoteza utajiri wowote, lakini sera hiyo iliacha jamii imeathiriwa. Tangu wakati huo, wachumi wamekuwa wakifanya kazi ili kurejesha uchumi wa India.

Kukuza Matumizi ya Malipo Kwa Simu za Mkono

Watu wanaharakisha kubadilisha fedha zao kabla ya tarehe 1 Oktoba, siku ya mwisho ya kutumia fedha za zamani. Hii imesababisha watu kutumia njia za malipo kwa simu za mkono, haswa M-Pesa, ili kuzuia kushikilia sarafu za zamani. Kusudi la serikali ni kufuatilia mtiririko wa pesa. Fedha za dijiti ni kati ya njia ambazo zinatumiwa kufanikisha lengo la serikali.

Wafanyabiashara katika nchi jirani wamebuni njia za kuzuia kutumia fedha za zamani kupitia matumizi ya M-Pesa. Hii imesababishwa na hatari fedha bandia ambazo zimeambatana na sera hii. Malipo ya simu ya mkono husaidia biashara kujiepusha na hatari ya kukubali fedha bandia.

mpesa
M-Pesa ni huduma kuu ya malipo kwa simu za Mkono nchini Kenya.

Uimara wa Shilingi

Shilingi inaonekana kuwa imara tangu kuanzishwa kwa fedha mpya, tofauti na dola na fedha nyingine. Wachambuzi wanasema kwamba uimara wa shilingi umechangiwa na ukwasi wa uchumi wa Kenya. Kuna mahitaji makubwa ya dola kwa sababu watu wanajaribu kujilinda kutokana na kutokuwa na uhakika wa fedha mpya. Thamani ya shilingi ya Kenya kulinganisha na dola inaweza kuongezeka.

Uwezekano wa Mfumuko wa Bei

Benki Kuu ya Kenya ilisema kuwa karibu shilingi bilioni 25 ( mlioni za Kimarekani 241) za Kenya zimeibuka na ziko kwenye mzunguko wa fedha tangu kuanza kwa utoaji wa fedha mpya. Pia, kumekuwa na amana kubwa ya fedha za kigeni ndani ya benki. Wachambuzi wa kifedha wanasema kuwa watu wengi wanaoshikilia fedha kutoka kwa mapato haramu wanajitahidi kubadili kabla ya tarehe ya mwisho. Wanabadilisha fedha za zamani kuwa dola ambayo ni rahisi kubadilishana kwa fedha mpya. Kuongezeka kwa fedha katika mzunguko kunaweza kusababisha mfumko wa bei kwani watu wanakimbilia kutumia fedha za ziada kabla ya tarehe ya mwisho.

Kwa muhtasari, uchapishaji na utoaji wa fedha mpya na Benki Kuu ya Kenya una upande mzuri na mbaya. Gavana wa Benki Kuu, Bwana Njoroge, alisema kwamba wamejifunza kutoka kwa kosa la India na serikali iko tayari kutokuharibu uchumi. Kwa bahati nzuri, wachambuzi wanasema kwamba ikiwa kuna athari mbaya za sera, zitakuwa za muda mfupi. Ikiwa taarifa zao ni za kuaminiwa, Kenya inapaswa kuzingatia sera hii na kukabiliana na athari za muda mfupi kwa faida ya muda mrefu.